Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo Wapinga Matokeo, Wataka Uchaguzi Urudiwe, pia NEC na ZEC zivunjwe

Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo Wapinga Matokeo, Wataka Uchaguzi Urudiwe, pia NEC na ZEC zivunjwe

Niandamane kisa aliekuwa mbunge wa Hai kapoteza Jimbo

Niandamane kisa aliekuwa mbunge wa Kawe kapoteza Jimbo

Niandame kisa Mgombea wa uraisi kupitia Chadema kaikosa ikulu, na kampeni zake za kufoka tu kwa kujitegeza akimalizia na neno SAWA SAWA. Sasa Kama sio kushindwa wao walitaka ashindwe nani?

Mzee wa ubwabwa katulia hana neno na mtu. Atae andamana ahakikishe na bima yake ya afya iko active asije kuomba michango ya matibabu.
 
Hapo ni sasa na kufunga goli wakati refa keshamaliza mpira.
 
Tamko la Chadema na ACT

1. Kurudiwa kwa uchaguzi.

2. Kuvunjwa kwa NEC na ZEC.

3. Maandamano yasiyokuwa na kikomo kuanzia tarehe 2/11/2020.

Ngazi ya kata maandamano yataekelezwa kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi katani.

Ngazi ya jimbo maandamano yataekelezwa kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo.

Sambaza ujumbe huu.

Reporter: EmmanuelKasomi
 
Kwa hatua tuliyofikia sasa watanzania kutoka kila kona ya nchi tuko teyari kupigania ukombozi wa taifa hili kutoka kwa mkoloni mweusi CCM.

Itakumbukwa mwaka 2019 katika uchaguzi wa serikali za mitaa dhuruma ya haki na demokrasia za watanzania zilinyang'anywa kama ilivyo hivi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Mwaka jana tulisubiri sana kusikia viongozi kutoka kambi ya upinzani watoe go ahead na wawe msitari wa mbele katika kupigania demokrasia ya nchi hii lakini waliufyata licha ya watanzania kuwa teyari.

Pia viongozi hao waliwahi kukwepa maandamano ya amani yaliyokuwa yameandaliwa na Mange Kimambi, yalikuwa yamefikia hatua ya kuingia barabarani tu lakini siku ya tukio hawakuweza kuonekana. Siku ile ilikuwa ndio yenyewe kabisa ya kuanza harakati za kuingoa serikali ya CCM

Katika uchaguzi huu, haikuhitaji kusubiri siku ziende kiasi hiki wala kusikiliza ushauri.

Walipoanza kutangaza matokeo tu ingetosha palepale kuitisha press na watanzania wote tupinge huu ubinywaji wa haki na demokrasia hapa nchini.

Nachelea kusema kwamba, viongozi mnatukwamisha katika harakati hizi za ukombozi.

Siku ya kesho nitakuwa wa mwisho kuingia barabarani endapo tu nikiiona safu yote ya uongozi wangu ikiwa frontline.
 
Kwa hatua ilipofikia Sasa nchi yetu hii inafaa kuwaombea (KIFO) hawa Viongozi wetu Waovu.

Kupanga Maandamano Ni jambo moja na kuandamana ni jambo lingine mkiona njia hiyo pia imeshindikana inabidi mtumie njia mbadala zaidi.

Najua watanzania wengi wanaandamishwa na familia zao kucha kutwa Baba anataka hiki Mama anataka kile Mke Nae Watoto Pia, Huwezi kuandamana Kama Huna Hata akiba ya kilo 10 za unga ndani.

Njia Mpadala Ni Kuwaombea Tu Mungu awapende Zaidi Basi Maana ni jambo aliitaji hata Muda Sana Na Waweza lifanya hata Peke Yako Ndani.

🦻[emoji2533].
 
Kwa hatua tuliyofikia sasa watanzania kutoka kila kona ya nchi tuko teyari kupigania ukombozi wa taifa hili kutoka kwa mkoloni mweusi CCM.

Itakumbukwa mwaka 2019 katika uchaguzi wa serikali za mitaa dhuruma ya haki na demokrasia za watanzania zilinyang'anywa kama ilivyo hivi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Mwaka jana tulisubiri sana kusikia viongozi kutoka kambi ya upinzani watoe go ahead na wawe msitari wa mbele katika kupigania demokrasia ya nchi hii lakini waliufyata licha ya watanzania kuwa teyari.

Pia viongozi hao waliwahi kukwepa maandamano ya amani yaliyokuwa yameandaliwa na Mange Kimambi, yalikuwa yamefikia hatua ya kuingia barabarani tu lakini siku ya tukio hawakuweza kuonekana. Siku ile ilikuwa ndio yenyewe kabisa ya kuanza harakati za kuingoa serikali ya CCM

Latika uchaguzi huu, haikuhitaji kusubiri siku ziende kiasi hiki wala kusikiliza ushauri.

Walipoanza kutangaza matokeo tu ingetosha palepale kuitisha press na watanzania wote tupinge huu ubinywaji wa haki na demokrasia hapa nchini.

Nachelea kusema kwamba, viongozi mnatukwamisha katika harakati hizi za ukombozi.
Siku ya kesho nitakuwa wa mwisho kuingia barabarani endapo tu nikiiona safu yote ya uongozi wangu ikiwa frontline.
 
Kuna watu wengi wamedai kuwa Rais Magufuli na serikali yake walitaifisha kampuni binafsi na viwanda kadhaa ikiwemo kiwanda kimoja cha kuzalisha dawa za binadamu kisha wakaweka uongozi na usimamizi wa kijeshi ambao wameishia kudhulumu haki za wafanyakazi, unyanyasaji na kuachisha wengi kazi. Hawa wameapa kushiriki maandamano ya kuanzia kesho na siyo wanasiasa.

Kufumba na kufumbua Rais Magufuli atarajie kuwa maandamano yanayoitwa ya kisiasa kuanzia kesho yatafanikiwa sana na kupata uungwaji mkono wa juu kwakuwa yamejumuisha wengi walioumizwa kutoka nyanja mbalimbali.

Tutarajie matamko ya serikali zenye nguvu za kuwalinda waandamanaji kwakuwa wanajua siyo wanasiasa pekee watakao andamana. In fact wanaisasa ndani ya maandamano haya ni wachache sana! Wengi wa watakaoandamana ni walioumizwa na huu utawala katili wa John Magufuli.

Trend inaonyesha kuwa kwa vyovyote vile Tanzania itabadilika sana na ni dhahiri kuwa sasa inaelekea kuwa moja ya nchi zisizo na usalama duniani.

Angalia mfano kusini mwa Tanzania, sasa serikali inapambana na kikundi cha ugaidi. Watu wamepoteza ajira na vipato. Ufukara umetawala kwenye familia. Kwa muktadha huu serikali haikupaswa kamwe kuvuruga uchaguzi mkuu. Kufanya hivyo kumetoa pumzi ya makundi mengi kupumua. Serikali makini na inayoona yaliyokuwa yakiendelea nchini, ilipaswa kutumia uchaguzi huu kumaliza nguvu ya makundi mengi ila badala yake imeutumia kuwaongezea nguvu. Hakika yajayo ni ya tofauti.

Tutacheka cheka humu na kujifanya kuwa wanaongea tuu ila ukweli zama zimeenda kubaya. Waumizwaji ni wengi na nchi imegawanyika sana. Udhaifu wowote ule wa kisiasa ulipaswa kuepukwa kipindi hiki kuliko zama zozote zile katika historia ya nchi yetu.

Nimemaliza!
 
wa TZ Bana sisi ni hodari sana wa mdomo kuliko vitendo tena ukikaa vibaya unaweza ukapigwa biti na mbongo ukasema huyu jamaa ananimaliza leo hahaha dah. ila niseme kwakweli vitendo ni muhimu kuliko maneno wale waliokuwa tayari kuandamani wajitokeze tu wakaungane na wenzao kuleta mabadiliko ila mm siko tyr kwakweli.
 
Serikali ikiwekewa vikwazo, ikashindwa kufanya miradi ya maendeleo, unakuwa umemkomoa Magufuli au unaumiza ndugu zako?
Kwenye miaka ya themanini kulikuwa na shinikizo kali kuwa Afrika Kusini iliyokuwa chini ya utawala wa makaburu iwekewe vikwazo vikali vya kiuchumi.

Dunia nzima kasoro Marekani na Uingereza waliunga mkono wazo hilo. Sasa pamoja na kwamba wananchi waliumia lkn matokeo yake utawala wa kibaguzi uliporomoka.

Sasa na sisi chini ya huu utawala wa kiimla ni kweli vikwazo vitatuumiza lkn mwisho wa siku azma itatimia tu. Hakuna marefu yasiyokuwa na mwisho.
 
Zimbabwe imewekewa vikwazo kwa miaka 20 sasa umeona wapinzani walifanikiwa kuchukua nchi?

Hebu jiulize, wananchi wakishajua kuwa maisha yao yanaanza kuwa l magumu kwa sababu ya vikwazo vilivyoombwa na wapinzani unafikiri watakuwa upande gani?
Zimbabwe wapinzani hawajachukua nchi sio kwa sababu wananchi wanakiunga mkono Zanu PF bali ni kwa sababu ya vote rigging inayofanywa na Zanu PF ktk kila uchaguzi, ni kama hapa tu.

Sasa kwa kipindi chote ambacho wamekuwa kwenye vikwazo hao Zanu PF wameisaidiaje nchi hiyo, jiulize Zimbabwe leo iko katika hali gani.
 
Back
Top Bottom