Kwa hatua tuliyofikia sasa watanzania kutoka kila kona ya nchi tuko teyari kupigania ukombozi wa taifa hili kutoka kwa mkoloni mweusi CCM.
Itakumbukwa mwaka 2019 katika uchaguzi wa serikali za mitaa dhuruma ya haki na demokrasia za watanzania zilinyang'anywa kama ilivyo hivi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Mwaka jana tulisubiri sana kusikia viongozi kutoka kambi ya upinzani watoe go ahead na wawe msitari wa mbele katika kupigania demokrasia ya nchi hii lakini waliufyata licha ya watanzania kuwa teyari.
Pia viongozi hao waliwahi kukwepa maandamano ya amani yaliyokuwa yameandaliwa na Mange Kimambi, yalikuwa yamefikia hatua ya kuingia barabarani tu lakini siku ya tukio hawakuweza kuonekana. Siku ile ilikuwa ndio yenyewe kabisa ya kuanza harakati za kuingoa serikali ya CCM
Katika uchaguzi huu, haikuhitaji kusubiri siku ziende kiasi hiki wala kusikiliza ushauri.
Walipoanza kutangaza matokeo tu ingetosha palepale kuitisha press na watanzania wote tupinge huu ubinywaji wa haki na demokrasia hapa nchini.
Nachelea kusema kwamba, viongozi mnatukwamisha katika harakati hizi za ukombozi.
Siku ya kesho nitakuwa wa mwisho kuingia barabarani endapo tu nikiiona safu yote ya uongozi wangu ikiwa frontline.