CHADEMA na CUF waungana kipinga nyongeza ya posho bunge la katiba

CHADEMA na CUF waungana kipinga nyongeza ya posho bunge la katiba

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,455
Baadhi ya vyama vya siasa, wanaharakati na wananchi wa kawaida wameshangazwa na maombi hayo ya posho, wakisema wajumbe wamesahau kilichowapeleka bungeni na kukimbilia kutetea masilahi yao.

Vyama vya Chadema na CUF kwa nyakati tofauti, vilisema kuwa vitaanzisha juhudi za kuwataka wabunge wao ambao ni wajumbe wasusie agenda yoyote inayotaka kuongezwa kwa posho hizo.

Tamko la vyama hivyo limetolewa huku Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho wajumbe wake ndio wanaodaiwa kupigia debe mpango huo, kikisema kitatoa ufafanuzi juu ya hoja hizo baada ya kupata ‘taarifa rasmi’.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema jana kuwa wajumbe hao hawakupaswa kudai nyongeza ya posho kwa vile hawakutumwa kwenda Dodoma kudai marupurupu ya fedha.

Alisema kuanza kujadili suala la nyongeza ya posho badala ya kuzungumzia hoja za msingi zilizopo kwenye Rasimu ya Katiba, ni sawa na kuwapuuza wananchi ambao wanasubiri kupata Katiba Mpya.

“Wametoka kwenye hoja na kutupeleka kwenye mambo mengine ambayo hayana msingi wowote. Sisi kama Chadema tunapinga na tunataka wabunge wetu watambue hilo,” alisema.

Alisema wale wanaolalamika kwamba Sh300, 000 hazitoshi wanajaribu kupindisha ukweli, kwani kuna baadhi ya watumishi wa Serikali wanalipwa kiasi hicho ikiwa ni mshahara wao wa kila mwezi.

Alisema Chadema kimewataka wabunge wake kutojiingiza kwenye malalamiko hayo badala yake wazingatie kile walichotumwa na wananchi kwenda Dodoma.
 
Unafiki wa wanasiasa Dr.W.Slaa acha unafika usirukie ili jambo anza kwanza na wabunge wako bungeni kila siku wanachukua posho.
 
Last edited by a moderator:
Unafiki wa wanasiasa Dr.W.Slaa acha unafika usirukie ili jambo anza kwanza na wabunge wako bungeni kila siku wanachukua posho.

Unaharibu sasa mkuu acha hili lipite ili tuje tuwahoji vizuri kama huo mji unabadilika maisha kipindi cha bunge!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Acheni Unafiki, Mbowe yumo kwenye Kamati ya wanaodai Posho pamoja na kina Lukuvi halafu mnasema Eti CUF na Chadema wanaipinga? Au mbowe mshamvua uanachama? Nassari nae yupo CCM? angalau Zitto pekee hata kama mnafiki amejitofautisha na wengine kwa kusema hata ikiongezwa hatoichukua, Kama Chadema na CUF mnayoongea yanatoka kwenye Mioyo yenu tangazeni kutochukua nyongeza ikiongezeka.
 
SLAA amwambie MBOWE ajitoe kwanza kwenye timu ya watu 6 iliyoundwa kufuatilia ongezeko hilo, la sivyo watakuwa wanatuchuuza tu.
 
Nahisi hili swala la POSHO ni mpango MAHUSUSI wa kupoteza uelekeo wa hili BUNGE. Haiwezekani hadi Mwenyekiti wa muda Mh. Pandu Kificho kuanza kulishughulikia hili wakati halipo kabisa kwenye HADIDU ZA REJEA za kwenye hili BUNGE la KATIBA.
 
Acheni Unafiki, Mbowe yumo kwenye Kamati ya wanaodai Posho pamoja na kina Lukuvi halafu mnasema Eti CUF na Chadema wanaipinga? Au mbowe mshamvua uanachama? Nassari nae yupo CCM? angalau Zitto pekee hata kama mnafiki amejitofautisha na wengine kwa kusema hata ikiongezwa hatoichukua, Kama Chadema na CUF mnayoongea yanatoka kwenye Mioyo yenu tangazeni kutochukua nyongeza ikiongezeka.

Mimi mwenyewe namshangaa SLAA, badala amwambie MBOWE ajiengue kwanza kwenye hiyo timu ya watu 6 anapiga kelele zisizo na maana.
 
Cybercrime...ile ni kamati iliyoundwa kuhusiana na hayo madai..kuwa mjumbe wa kamati haimaanishi unaunga mkono hoja
 
Kwa mtu mwenye maono ya mbele, hapo wala hakuna katiba mpya, ni kupoteza pesa na muda, na kama ikitoka itakuwa katiba yenye muundo wa kichama zaidi...maana awliyo jazana humo bungeni ni makada na wabunge wa chama cha kifisadi...katiba mpya ya kweli itapatikana baada ya 2015
 
Nahisi hili swala la POSHO ni mpango MAHUSUSI wa kupoteza uelekeo wa hili BUNGE. Haiwezekani hadi Mwenyekiti wa muda Mh. Pandu Kificho kuanza kulishughulikia hili wakati halipo kabisa kwenye HADIDU ZA REJEA za kwenye hili BUNGE la KATIBA.

Ulafi tu wa wabunge.
 
Acheni Unafiki, Mbowe yumo kwenye Kamati ya wanaodai Posho pamoja na kina Lukuvi halafu mnasema Eti CUF na Chadema wanaipinga? Au mbowe mshamvua uanachama? Nassari nae yupo CCM? angalau Zitto pekee hata kama mnafiki amejitofautisha na wengine kwa kusema hata ikiongezwa hatoichukua, Kama Chadema na CUF mnayoongea yanatoka kwenye Mioyo yenu tangazeni kutochukua nyongeza ikiongezeka.

Mnyika ameshatoa msimamo kwamba haungi mkono nyongeza ya Posho.Pengine Mbowe kuwepo huko atapendekeza zisiongezwe au zifutwe kabisa kwa wabunge wa bunge la jamhuri isipokua zibaki laki 3 kwa wale walioteuliwa na Rais
 
Hizi ni gelesha za kijinga kupinga posho mchana usiku wanazitafuta kwa tochi.

Nashukuru kuwa mjumbe wa bunge la katiba sasa nimejua rangi halisi za wanasiasa siyo watu ni madudu kabisa.

Hiyo kupinga kwenye tv na redio ni geresha tu sitaki hata kuwasikia kwa sababu nimeyaona kwa macho.
 
Acheni Unafiki,
Mbowe yumo kwenye Kamati ya wanaodai Posho pamoja na kina Lukuvi halafu
mnasema Eti CUF na Chadema wanaipinga? Au mbowe mshamvua uanachama?
Nassari nae yupo CCM? angalau Zitto pekee hata kama mnafiki
amejitofautisha na wengine kwa kusema hata ikiongezwa hatoichukua, Kama
Chadema na CUF mnayoongea yanatoka kwenye Mioyo yenu tangazeni
kutochukua nyongeza ikiongezeka.

akili yako imemezwa na posho kiasi hujui kama hiyo kamati sio wote wanaunga mkono posho, haya mama jipange watawaongezea
 
Mnyika ameshatoa msimamo kwamba haungi mkono nyongeza ya Posho.Pengine Mbowe kuwepo huko atapendekeza zisiongezwe au zifutwe kabisa kwa wabunge wa bunge la jamhuri isipokua zibaki laki 3 kwa wale walioteuliwa na Rais
Bora ukae kimya tu huna unachokijua nakuonea huruma kabisa.
 
Mnyika ameshatoa msimamo kwamba haungi mkono nyongeza ya Posho.Pengine Mbowe kuwepo huko atapendekeza zisiongezwe au zifutwe kabisa kwa wabunge wa bunge la jamhuri isipokua zibaki laki 3 kwa wale walioteuliwa na Rais
Utamuua njaa Lema
 
Back
Top Bottom