Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani CUF wamevunja ndoa na ccm?
Baadhi ya vyama vya siasa, wanaharakati na wananchi wa kawaida wameshangazwa na maombi hayo ya posho, wakisema wajumbe wamesahau kilichowapeleka bungeni na kukimbilia kutetea masilahi yao.
Vyama vya Chadema na CUF kwa nyakati tofauti, vilisema kuwa vitaanzisha juhudi za kuwataka wabunge wao ambao ni wajumbe wasusie agenda yoyote inayotaka kuongezwa kwa posho hizo.
Tamko la vyama hivyo limetolewa huku Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho wajumbe wake ndio wanaodaiwa kupigia debe mpango huo, kikisema kitatoa ufafanuzi juu ya hoja hizo baada ya kupata taarifa rasmi.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema jana kuwa wajumbe hao hawakupaswa kudai nyongeza ya posho kwa vile hawakutumwa kwenda Dodoma kudai marupurupu ya fedha.
Alisema kuanza kujadili suala la nyongeza ya posho badala ya kuzungumzia hoja za msingi zilizopo kwenye Rasimu ya Katiba, ni sawa na kuwapuuza wananchi ambao wanasubiri kupata Katiba Mpya.
Wametoka kwenye hoja na kutupeleka kwenye mambo mengine ambayo hayana msingi wowote. Sisi kama Chadema tunapinga na tunataka wabunge wetu watambue hilo, alisema.
Alisema wale wanaolalamika kwamba Sh300, 000 hazitoshi wanajaribu kupindisha ukweli, kwani kuna baadhi ya watumishi wa Serikali wanalipwa kiasi hicho ikiwa ni mshahara wao wa kila mwezi.
Alisema Chadema kimewataka wabunge wake kutojiingiza kwenye malalamiko hayo badala yake wazingatie kile walichotumwa na wananchi kwenda Dodoma.
Good !
Mnyika ameshatoa msimamo kwamba haungi mkono nyongeza ya Posho.Pengine Mbowe kuwepo huko atapendekeza zisiongezwe au zifutwe kabisa kwa wabunge wa bunge la jamhuri isipokua zibaki laki 3 kwa wale walioteuliwa na Rais
hii ndiyo siasa posho kwanza mengine yatafuataHizi ni gelesha za kijinga kupinga posho mchana usiku wanazitafuta kwa tochi.
Nashukuru kuwa mjumbe wa bunge la katiba sasa nimejua rangi halisi za wanasiasa siyo watu ni madudu kabisa.
Hiyo kupinga kwenye tv na redio ni geresha tu sitaki hata kuwasikia kwa sababu nimeyaona kwa macho.
Mimi mwenyewe namshangaa SLAA, badala amwambie MBOWE ajiengue kwanza kwenye hiyo timu ya watu 6 anapiga kelele zisizo na maana.