CHADEMA na CUF waungana kipinga nyongeza ya posho bunge la katiba

Mwenye dhamira ya kweli ktk kupinga ongezeko hilo kwa muono wangu ni KANGE E. LUGOLA jamaa huwa anamaanisha anachoongea magamba wengne na baadhi ya wapinzani kama Nassari mmmh! Majanga tupu
 

Good !
 

Swali. Je yale makubaliano ya dk slaa wkt anagombea urais kuwa alipwe sawa na mbunge endapo atakuwa ameshindwa kwenye uchaguzi. Ina maana hata hizi posho za bunge la katiba nazo atakuwa analipwa????
 
hebu angalia wabunge hawa walio kwenye kikao, cha kwanza walichokumbuka ni kudai posho eti laki 3 kwa ck haitoishi, subiri kidogo alafu jiulize, ungekuwepo kwenye lile bunge ungukuwa upande gani? usinijibu ila jiulize 2 na baada ya hapo uwe na sababu ya kuwapinga au kuwasaporti, mimi ningekuwepo ninge... kumbe sitakiwi kutoa majibu, ila sidhani kama kuna mzalendo wa kweli nchi hii wengi wetu ni wabinafsi sana.tubadirike watanzania, tanzania mbele mambo mengine baadae, unaweza kuthubutu kweli bila aibu mchana kweupe mbele ya watanzania wasio na uwezo wa hata kulipa nauli ya 400 eti laki tatu kwa siku haikutoshi kweli? Eh MUNGU ponya mioyo ya urafi kwa waonaopata nafasi katika nchi hii
 
siasa bila dictatorship, haiendi!

pure democracy haiwezi kuleta maendeleo hata kidogo!

kama rais hawezi kufanya maamuzi mwenyew mazito bila kuwasikiliza hawa, hakika politics will be politics as always.

sikudhani kabisa ari ya 2005 ingetufikisha hapa tulipo sasa..

kutoka shs 600 mpaka 1300? this is a very high inflation just for few years.
 
Mnyika ameshatoa msimamo kwamba haungi mkono nyongeza ya Posho.Pengine Mbowe kuwepo huko atapendekeza zisiongezwe au zifutwe kabisa kwa wabunge wa bunge la jamhuri isipokua zibaki laki 3 kwa wale walioteuliwa na Rais

Pengine.. hiyo ni njia moja ya kuwa na hisia zenye kuleta hali chanya kupunguza mtafaruku ?? Kwa upeo wako unadhani Tume ile iliundwa kwa ajili ya nini ??

Na historia inatuonesha Mbowe ni mtu wa aina gani.. sembuse ni wote wapo hivo hivo tu katika chama chenu, kinachofanyika ni kung'ata na kupuliza..
 
hii ndiyo siasa posho kwanza mengine yatafuata
 
wenye akili tulishajua hakuna jipya bunge la katiba zaidi ya posho na ngono nawaonea huruma wazazi wenye mabinti udom, cbe
 
Huo ni uzandiki na unafiki mtupu, Mbona Slaa alipotaka kugombea Urais alitoa sharti la kulipwa kama mbunge? tena alidai stahili mbalimbali ambazo analipwa hadi leo? Kwa vile yeye hayuko kwenye bunge la Katiba ndiyo maana anadai hakuna haja ya kulipwa au kudai zaidi ya Tshs 300,000/= . Sisi tulioko hapa Dodoma ndiyo tunaofahamu jinsi maisha yalivyo juu, vyumba hadi 120,000 vya mitaani, chakula 25,000 hadi 30,000 mlo mmoja, usafiri Taxi town tripu 15,000 hadi 20,000. kwa siku matumizi ni zaidi ya 330,000. Hivyo kumbuka kuwa hakuna kazi isiyokuwa na faida. Slaa akumbuke hata sisi tuliokuja Dodoma ni sehemu ya Watanzania na sisi Katiba inatuhusu. Hivyo kudai posho inayokidhi maisha ni moja ya haki zetu kikatiba tusiangalie kazi iliyotupeleka peke yake. Nasisi ni watu. Slaa acha kutunyanyapaa.
 
Mimi mwenyewe namshangaa SLAA, badala amwambie MBOWE ajiengue kwanza kwenye hiyo timu ya watu 6 anapiga kelele zisizo na maana.

Dr Slaa amewaagiza wabunge wa Chadema including Mbowe.
Hivi nyie Nyumbu wa Lumumba mkoje ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…