CHADEMA: Namba ya simu ya Brenda Rupia iliyokuwa ikitumika kuchangisha michango imefungiwa na kampuni ya Airtel

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinauarifu umma kuwa namba ya simu ya Mrugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chadema, Mhe. Brenda Rupia 0789160733, iliyokuwa ikitumika kuchangisha michango kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa chama, imefungiwa na kampuni ya Airtel Tanzania tangu tarehe 19 Januari 2026.

Baada ya kufanya mawasiliano na uongozi wa Airtel, wamegoma kueleza kwanini wameifungia namba hiyo badala yake wamesema wanamtaka muhusika kufika katika ofisi zao popote nchini.

Hatua ya kumtaka mtu kufika kwenye ofisi zao inashangaza kwani kampuni hiyo imekuwa ikihamasisha huduma za kidijitali kwa wateja wake, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kupunguza msongamano wa watu katika matawi yao.

Chadema inalani vikali kitendo hiki na kuitaka Airtel Tanzania kuacha kujihusisha au kutumiwa na mifumo ya kisiasa kukandamiza demokrasia na kukiuka haki za raia.

Aidha, tunasisitiza umuhimu wa kampuni hiyo kulinda faragha na haki za watumiaji wa huduma zake.

Pili, tunaitaka Airtel Tanzania kufungua mara moja akaunti hiyo ya Airtel Money, kwani kuchangisha michango kwa uwazi kwa madhumuni halali si kosa.

Taifa linafahamu vyema lengo la michango hiyo na hakuna sababu ya msingi ya kuzuia shughuli hiyo ya kidemokrasia.

Chadema itaendelea kupigania haki, uwazi na demokrasia bila woga wala kuyumba.

1769085338827.png
 
Hii nchi ingekua na mahakama zenye kueleweka hawa jamaa ni kuwaburuza mahakamani ili wakalipishwe faini ya mabilioni. Huu utoto wa kujiingiza kwenye siasa nashangaa tume ya ushindani (FCC) ipo kimya kabisa.

Refusal to supply service ni kosa kwenye fair competition, mteja lazima alindwe.

Hata vodacom ilitumika kufanikisha utekaji wa kabendera.

Kuna taasisi inabidi katiba mpya na sheria zake izifute tu moja wapo ni hii FCC.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinauarifu umma kuwa namba ya simu ya Mrugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chadema, Mhe. Brenda Rupia 0789160733, iliyokuwa ikitumika kuchangisha michango kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa chama, imefungiwa na kampuni ya Airtel Tanzania tangu tarehe 19 Januari 2026.

Baada ya kufanya mawasiliano na uongozi wa Airtel, wamegoma kueleza kwanini wameifungia namba hiyo badala yake wamesema wanamtaka muhusika kufika katika ofisi zao popote nchini.

Hatua ya kumtaka mtu kufika kwenye ofisi zao inashangaza kwani kampuni hiyo imekuwa ikihamasisha huduma za kidijitali kwa wateja wake, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kupunguza msongamano wa watu katika matawi yao.

Chadema inalani vikali kitendo hiki na kuitaka Airtel Tanzania kuacha kujihusisha au kutumiwa na mifumo ya kisiasa kukandamiza demokrasia na kukiuka haki za raia.

Aidha, tunasisitiza umuhimu wa kampuni hiyo kulinda faragha na haki za watumiaji wa huduma zake.

Pili, tunaitaka Airtel Tanzania kufungua mara moja akaunti hiyo ya Airtel Money, kwani kuchangisha michango kwa uwazi kwa madhumuni halali si kosa.

Taifa linafahamu vyema lengo la michango hiyo na hakuna sababu ya msingi ya kuzuia shughuli hiyo ya kidemokrasia.

Chadema itaendelea kupigania haki, uwazi na demokrasia bila woga wala kuyumba.

Aya makampuni yamezidi upumbavu , waburuzwe mahakamani
 
Kwanini Spokesperson wa Chama anatumia mtandao wa Airtel ambao uko owned 49% na Serikali?

Mitandao Ina Comply na standards za Regulator ambae ni TCRA ila hao Kabacholi Airtel ni Kutii maelekezo tu Bila haya
 
kuna mtandao hauko chini ya TCRA?
NIsome Tena Vizuri, Regulator yupo kote isipokuwa Kuna mitandao ni ngumu Kufanya twisting kwasababu majority wako owned na Kampuni kubwa za nje ambazo Kuna namna Fulani hata TCRA hawezi kuwazingua kama atakavyomzingua Airtel, TTC au Zantel
 
Back
Top Bottom