Pre GE2025 CHADEMA ni Wakati wa Kwenda na Lissu. Msisite, nina sababu…

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Je Unajua Ipo CCM yaweza toka madarakani hata kwa Katiba hii hii?
Yes, inawezekana kabisa, lakini siyo kwa kupitia chaguzi za kisiasa.

Tambua kwamba CCM kuendelea kubaki madarakani au kushinda katika Uchaguzi wa Siasa haitegemei kupigiwa Kura na mtu yoyote yule ktk Uchaguzi wa Siasa hapa Tanzania.
Kwakuwa Katiba inaweza kuwa hata nzuri ila wa kuilinda wakawa waoga

Watanzania ni waoga sana kwenye haki zao sijui kwanini !
 

Attachments

  • 5781825-51775523b226d8414338068b2d50cfec.mp4
    3 MB
Kuvutia watu kukusikiliza siyo sifa ya uongozi. Hata Diamond Plutnamz ana mvuto sana wa kusikilizwa. Lakini sifa za uongozi kwa nchi kama Tanzania ni za ziada.
 
Watamlipa nini akiukosa?
 
Sidhani kama hili linahitaji mjadala.

Kuna Mdau mmoia alilete uzi humu ukafutwa ndani ya dakika mbili. Alisema 2025 Urais wa JMT Tundu Lissu Njia ni nyeupe.

Sikujua kwa nini Uzi ulifutwa kwa kasi ile.
 
Tundu Lisu anatosha...tena uandaliwe mdahalo na kizimkazi tuone yale macho kama hayatadondoka chini!
 
Naunga mkono hoja Lissu agombee, na mgombea mwenza atafutwe mwanamke msomi na mwenyekuweza kujenga hoja
Ngoma ibaki kama ilivyokua 2020 ,lissu na mgombea mwenza wa 2020, Mwalim kwa nini nasema hivi

1.Mwalim 2020 nafasi yake kama Mgombea mwenza aliitendea haki sana mara 50 ya mgombea mwenza wa ccm kipindi kile
2. Mwalim tiyari ni mzoefu kakika purukushani za kampen, anajua ni mapungufu gani ya 2020 ya kurekebisha , yupo na ushawishi pia anajua kumiliki jukwaa, uyu anafahamika tiyari kwa watanzania na bado kijana pia. Hapa haitakiwi fanya makosa katika hili.


3. Mwalim geographia ya tz tiyari anaifaham , kwa histori chadema 2015 wagombea wote walikua wanaume na walifanya vizuri sana, pia 2020 Wagombea walikua wanaume na walifanya vizuri sana mpaka mwendazake aka kwapua uchaguzi.

Kwa vigezo tajwa hapo juu kama Tundu anasimama kama Mgombea urais kwa tiketi ya chadema , Mwalim abaki kua Mgombea, hakuna sababu ya kuja na mtu mpya kwa nafasi ya Mgombea mwenza , uchaguzi ujao ni muhim sana kama ukifanyika, no time to confuse our peoples.

All in all nimpogeze mleta mada
 
Huyo Mwamba wanamuogopa mno,yaani akishinda Lissu Sidhani kama atatangazwa maana atawafunga watu wengi sana kwa ufisadi!
 
Naunga mkono hoja Lissu agombee, na mgombea mwenza atafutwe mwanamke msomi na mwenyekuweza kujenga hoja
Wewe unataka kuturudisha kwa Mama Abdul endapo litatokea la kutokea.Kikombe ichi kitupishe kwa kweli!!
 
 

Attachments

  • Screenshot_2024-08-16-13-49-12-189_com.whatsapp.jpg
    279.4 KB · Views: 1
..Tundu Lissu kama mwanasiasa ana uwezo kuliko Samia Suluhu.

..kwanza, Lissu ni msomi mwenye uelewa wa mambo mengi ya kisiasa, kiutawala, kiuchumi, na kijamii, kuliko Samia.

..Pili, anao uwezo wa kufikisha ujumbe, kuhamasisha, na kuunganisha wananchi, kuliko Samia.

..Tatizo litakalomkwamisha Lissu ni kama atakuwa na fedha na rasilimali za kutosha kufanya kampeni nchi nzima, na kila mahali ambapo Ccm itafika.

..Vilevile kikwazo kingine ni vyombo vya habari kama havitatishiwa ili visusie kampeni za wapinzani na kutoa habari za Samia peke yake.

..Vyombo vya ulinzi na usalama hao waachwe tu, wakiona maji yamewafika shingoni CCM, hawatawasaidia.
 
Acheni mizaha ya kijinga..!
 
Lissu anaweza kushinda uchaguzi. Samia hakubaliki, tazama hata nguvu anayotumia. Lakini hatuna tume ya kutangaza upinzani
 
Wapenda haki wote tumekuelewa, tumelipokea na tunaliunga mkono.
 
Sio ataleta changamoto tu bali atachukua ndoo
 
Naiunga mkono CDM kulingana na kwamba CCM kimegawa raslimali zetu huku tukibaki bila ajira na maendeleo yanaenda kidokidogo sana. Ufisadi wa kufa mtu.

Ila simuungi mkono Lissu.
Wala Lisu hataki umuunge mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…