Mwizukulu wa Buganda
Member
- Nov 19, 2024
- 94
- 307
Tundu Lissu amesema hayo baada ya kuwasili kwenye ofisi ya Makao Makuu ya CHADEMA tokea achaguliwe kuwa mwenyekiti wa Chama hicho.
Tundu Lissu amesema kuwa tuna uchaguzi Mkuu Oktoba, na tuna No Reform No Election. Hayo mambo mawili hayaendi pamoja, kiswahili chake ni Hakuna Mabadiliko, Hakuna Uchaguzi. Siyo hatutasusia Uchaguzi.
Hatujazungumza Boycott, hakuna uchaguzi. Tuone tutawezaje kwenda nayo mbele, either kwa pamoja kama inawezekana au tuamue lipi muhimu zaidi. Tunaenda kujifungia ili tuijadili hii na chama, haitakuwa ni uamuzi wa Tundu Lissu, itakuwa ni uamuzi wa chama.
Inabidi tuzungumze lugha pekee anayoweza kuzungumza Rais Samia, na ataizungumza kwasababu nani anayetaka uchaguzi kama wa mwaka jana(Serikali za Mitaa - 2024), Uchaguzi wa 2020, uchaguzi wa 2019? No reform No Election. Na Tutazungumza lugha ambayo Samia ataielewa, na tutazungumza hii habari na kila mtu mchana kweupe, hatuna chochote cha kuficha, hatuna ajenda ya siri.
Pia soma