CHADEMA njia pekee ya kushika dola 2030, unganisheni nguvu na team Magufuli

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,340
Reaction score
4,659
Miaka takribani 2 imepita toka afariki Hayati Rais wa awamu ya tano John Pombe Magufuli na juzi tarehe 17/03/2023 tumeazimisha miaka miwili ya kifo chake kwa masikitiko makubwa.

Baada ya kufariki kiongozi wa awamu ya 5 nchi imepitia vipindi tofauti ambavyo vimethibitisha na kudhihirisha aina ya siasa yetu kama nchi.

Kukosekana kwa misimamo,chuki na hasira zimekithiri zidi ya siasa za Rais alopita na hata safu yake ya uongozi imeonekana kuwa ni butu hadi kupelekea watu aliowaamini ni dhaifu na hawawezi kwenda pamoja kwenye serikali iliyopo.

Katika kumbukumbu zangu kuna majina mengi yaliondolewa kwenye orodha ya serikali hii ya 6 akiwemo Ndugu Polepole, Bashiru pamoja na wengineo.

CCM imejisahaulisha kuwa imepitia kipindi hicho cha mpito dhidi ya watu hawa ambao waliopenda na kuzoea mfumo uliopita wa Rais Magufuli pia ni dhahiri bado hakuna maelewano mazuri kati ya pande hizo mbili mpaka sasa.

CCM imejisahaulisha Zaidi kwa kuingia makubaliano dhidi ya chama cha upinzani ambacho kilichoharibu sifa za awamu iliyopita kwa kuonekana mbaya kwenye Taifa kuliko awamu zote sababu hiyo tu,inatosha kuwafanya CHADEMA kuungana na CCJ ili kujivika taji la nchi ifikapo mwaka 2030.


Binafsi naona mafanikio makubwa ya CHADEMA kwenye CCJ kuliko CCM hili litadhirika ifikapo 2024 kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na 2025 kwenye uchaguzi mkuu wa Taifa.

Salamu.
 
Awamu ya nne hamkuteseka?au kisa mlizoea kumtukana JK akawachekea basi mkawa mnaona kila Rais ni mjomba wenu. Punguza unonko
Aibu ipi?. Yeye kuwatesa CHADEMA kwenye utawala wake ni sahihi?. Punguza unafiki. Yule ibilisi Hana lolote ndio maana hakumaliza hata miezi mitatu awamu ya pili, akafa kwa aibu.
 
Vyama vyote ni kama makampuni makubwa yanayomilikwa na wachache
Shares zinakuwa kubwa kama mko Directors kidogo

Sasa waongezeke wengine tena
Hilo ndio wanaangalia zaidi MASLAHI TU

Hawawazi hata siku moja kuwaza watavukaje hapa tunapoona watoto wanaenda na MAJIVU shuleni kama ubao?

Hivi mnawaaminije watu wanaoona umeme unakata miaka na miaka, shule hazina madawati na waalimu wa kutosha, hospital zisizokuwa na huduma nzuri
Ajali zisizokuwa na suluhu
Ni mambo ya ajabu sana

Naona tuweke sanduku kama msikini au kanisani kulichangia taifa kama sadaka
Maana hela zinapigwa na watu wanashangilia tu

Hakuna faida ya kuungana wala nini ni sisi wenyewe tuungane kama nchi na kuwakataa majizi
 
Aibu ipi?. Yeye kuwatesa CHADEMA kwenye utawala wake ni sahihi?. Punguza unafiki. Yule ibilisi Hana lolote ndio maana hakumaliza hata miezi mitatu awamu ya pili, akafa kwa aibu.
kufa kila mtu anakufa acha kumsemea vibaya, kila binadamu ana mazuri yake na mapungufu yake
 
CDM hawawezi kuunganisha nguvu na JPM remnants hilo halipo wametumika sana kumdhalilisha tena kwa sherehe hapo hakuna mariadhiano.
 
Team Maguful au Genge S sio kabisa, ni afadhali CHADEMA kusubiri miaka mingi ujayo kuliko kujiunga na hili genge. Humo ndani kuna ukabila, ukanda, chuki, dhuluma, visasi, wizi, uchawi nk. Hapana.
 
Wazo lako ni zuri sana lakini sisi furaha yetu ni pale kikundi haramu cha Magufuri empire kinaposambaratishwa na ccm wenzie basi sisi kwetu ni faraja kwa sababu wahanga wakubwa wa jpm ni CHADEMA.
 
Awamu ya nne hamkuteseka?au kisa mlizoea kumtukana JK akawachekea basi mkawa mnaona kila Rais ni mjomba wenu. Punguza unonko
Ile awamu nakumbuka kuna watu walipigwa mabom arusha na mashumbusi .wa dr. Slaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…