Miaka takribani 2 imepita toka afariki Hayati Rais wa awamu ya tano John Pombe Magufuli na juzi tarehe 17/03/2023 tumeazimisha miaka miwili ya kifo chake kwa masikitiko makubwa.
Baada ya kufariki kiongozi wa awamu ya 5 nchi imepitia vipindi tofauti ambavyo vimethibitisha na kudhihirisha aina ya siasa yetu kama nchi.
Kukosekana kwa misimamo,chuki na hasira zimekithiri zidi ya siasa za Rais alopita na hata safu yake ya uongozi imeonekana kuwa ni butu hadi kupelekea watu aliowaamini ni dhaifu na hawawezi kwenda pamoja kwenye serikali iliyopo.
Katika kumbukumbu zangu kuna majina mengi yaliondolewa kwenye orodha ya serikali hii ya 6 akiwemo Ndugu Polepole, Bashiru pamoja na wengineo.
CCM imejisahaulisha kuwa imepitia kipindi hicho cha mpito dhidi ya watu hawa ambao waliopenda na kuzoea mfumo uliopita wa Rais Magufuli pia ni dhahiri bado hakuna maelewano mazuri kati ya pande hizo mbili mpaka sasa.
CCM imejisahaulisha Zaidi kwa kuingia makubaliano dhidi ya chama cha upinzani ambacho kilichoharibu sifa za awamu iliyopita kwa kuonekana mbaya kwenye Taifa kuliko awamu zote sababu hiyo tu,inatosha kuwafanya CHADEMA kuungana na CCJ ili kujivika taji la nchi ifikapo mwaka 2030.
Binafsi naona mafanikio makubwa ya CHADEMA kwenye CCJ kuliko CCM hili litadhirika ifikapo 2024 kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na 2025 kwenye uchaguzi mkuu wa Taifa.
Salamu.