Pre GE2025 CHADEMA peke yake haiwezi kamwe kuitoa CCM madarakani...

Pre GE2025 CHADEMA peke yake haiwezi kamwe kuitoa CCM madarakani...

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kwanza hakuna mjadala kuwa CCM inatakiwa kutolewa madarakani kwa njia yoyote ile.

Pia hakuna mjadala kuwa mpaka sasa hakuna jinsi nyingine ya kuwa na chama kingine nje ya CHADEMA cha kupambana na CCM.

Ni ukweli kwamba CHADEMA ni chama bora cha siasa kuliko vyama vyote vya siasa nchini CCM ikiwemo.

Baada ya CHADEMA kwa ubora, inafuatia CCM na vyama vingine kama vile ACT na vinginevyo viko kwenye fungu (bundle) moja.

Lakini kuitoa CCM madarakani pamoja na udhaifu wake,inataka jamii ya watanzania kwa uhalaiki wake ( amassed) kujua nini kifanyike ili kuitoa CCM madarakani.

Kuishutumu CCM kwa uovu wake ni jambo la zamani kwa sasa. Kati ya watanzania 100 watanzania 60 wanaujua uovu wa CCM kwa undani sana.

Hakuna asiyejua kuwa CCM ndiyo inaifilisi nchi hii. Watanzania wote wanajua maisha yao yanaharibiwa na CCM kuwepo madarakani.

Lakini asilimia tisini (90%) ya watanzania hawapo tayari kushiriki kwenye harakati za kuitoa CCM madarakani.

Watanzania wengi wanadhani kazi ya kuitoa CCM madarakani ni ya CHADEMA peke yao.

Kila siku wanalaumiwa ni kwa nini hawaitoi CCM madarakani. Cha kushangaza watu wengi wanaogopa kuiudhi CCM.

Huwezi kuta wafanyakazi Serikalini, wafanyabiashara, wakulima na watu wa kawaida wakipambana hadharani na CCM.

Kwa mazingira haya huwezi tarajia CHADEMA peke yao kuitoa CCM madarakani.

Kutegemea CHADEMA peke yake kuitoa CCM madarakani, ni kutarajia muujiza.
 
Kwanza hakuna mjadala kuwa CCM inatakiwa kutolewa madarakani kwa njia yoyote ile.

Pia hakuna mjadala kuwa mpaka sasa hakuna jinsi nyingine ya kuwa na chama kingine nje ya CHADEMA cha kupambana n

Kwa mazingira haya huwezi tarajia CHADEMA peke yao kuitoa CCM madarakani.

Kutegemea CHADEMA peke yake kuitoa CCM madarakani, ni
Dhumuni kuu la huu uzi nini?
 
Sina ushabiki wa vyama vya siasa ila upinzani bado sana kupambana na ccm.

Ili kupambana nao ni kwenda jino Kwa jino nao ila sasa upinzani kazi yao ni kulalamika tuu kwenye kila jambo analofanya ccm.
 
Kwanza hakuna mjadala kuwa CCM inatakiwa kutolewa madarakani kwa njia yoyote ile.

Pia hakuna mjadala kuwa mpaka sasa hakuna jinsi nyingine ya kuwa na chama kingine nje ya CHADEMA cha kupambana na CCM.
kawaida wakipambana hadharani na CCM.

Kwa mazingira haya huwezi tarajia CHADEMA peke yao kuitoa CCM madarakani.

Kutegemea CHADEMA peke yake kuitoa CCM madarakani, ni kutarajia muujiza.
Ili ccm itoke kwa mfumo huu inatakiwa wazee wengi wafe kwanza. Yaani kwa hali ilivyo ni miaka 20. Ccm itatoka pale ambako idadi ya vyama itadhibitiwa kimfumo. Yaani vyama view na itikadi kama vile socialist, capitalist na mlengo wa kati. Hapo kutahitaji rais mwenye kujali nchi kuliko chana chake ambaye kwa utashi wake aishawishi jamii kufanya haya mageuzi.
 
Sina ushabiki wa vyama vya siasa ila upinzani bado sana kupambana na ccm.

Ili kupambana nao ni kwenda jino Kwa jino nao ila sasa upinzani kazi yao ni kulalamika tuu kwenye kila jambo analofanya ccm.
Upinzani tulionao ni wa hovyo mno.

Akitokea mtu ananyoosha mambo wanampinga.

Hawaeleweki wanachokitaka.

Hakuna mtu makini atawaunga mkono watu wasiojielewa.
 
Wanaweza ila shida ipo kwanini wanakwama .
1. Wanawasifia ccm
2. Wapo kindaki ndaki na ccm
3.wa wanawapigia debe ccm ili waishi
Hawana backup plan so wakizingua wanafunzwa adabu sasa huoni ccm ndio chama hapa nchini .
 
Upinzani tulionao ni wa hovyo mno.

Akitokea mtu ananyoosha mambo wanampinga.

Hawaeleweki wanachokitaka.

Hakuna mtu makini atawaunga mkono watu wasiojielewa.
CCm wamegawa pikipiki mkoa mmoja tuu wanaanza kulialia ety mama amepata wapi pesa za kugawa pikipiki mikoa yote ya Tanzania, yani utadhani wao wamepigwa marufuku kutumia pesa zao kuwapa wananchi.
 
Back
Top Bottom