KANU ilikuwa na watu Toka ndani ya KANU!!
CCM itakuwa hivyo hivyo 2025🔥
Tatizoni kuwa Watanganyika jambo la kijinga linasambaa haraka kuliko jambo la akili na maarifa.
Kuna jambo limeshajengeka kwenye akili za watu kuwa wale wanaohamia upinzani ni wasaliti na mamluki wanaotumwa na CCM.
Tena wanakuambia kabisa kuwa wale ni wasaliti wametumwa na CCM msiwapokee wametumwa kuhujumu Chama . Ujinga mtupu. Wakati huo huo CCM inawakaribisha na kuwapa madaraka wale wanaotoka upinzani!
Hali hii inawafanya wale wanotoka CCM na kujiunga na upinzani kuishi maisha ya shida sana ndani ya Chama na kutengwa sana na kukejeliwa kwenye mitandoa hasa pale wanapojaribu kugombea nafasi za uongozi kama haki yao ya kuomba ridhaa kwa ajili ya kukijenga chama ili waweze kuzidi kuwavuta wengine . Badala yake wanakejeliwa na kuitwa wasaliti ,mamluki wa CCM n.k ,hatimaye kujiona wapweke sana hivyo kuamua kurudi CCM. Kule wakirudi CCM kama kawaida yake inawapokea kwa vingi'ora na mbwembwe kubwa ili tu kuhakikisha watu wengi wanaona ni bora wafie ndani ya CCM kwani heshima zao ndani ya Chadema zinadhiliwa na hata wakifa hawazikwi kwa heshima inayostahili badala yake watu wanaona ni bora wazike Mbwa kwa heshma kwa sababu tu ni mbwa wa wanaedhani kuwa ni mwenzao kutokana na kuwa ni lini alianza nao harakati.
Bado upinzani haujajua kuwa Lengo la watanzania ni kuwa na Katiba mpya inayoweka maslahi ya umma mbele na sio vyama na kuwafanya watanzania wote kuwa huru kisiasa ,kijamii na kiuchumi.
Mfano kwa sasa ni wazi kuwa kuna Watu ndani ya CCM wanapaswa kuwa Wapinzani nje ya CCM halikadhalika kuna Wapinzani hasa Chadema wanapaswa kuwa kwenda CCM mana nia zao na fikra zao zinafanana sana na za kina Bashe na Mwigulu. Ni watu kwenye majukwaa wanajinadi kama watetezi wa wanyonge lakini wamejaa tamaa kubwa sana ya fedha na mali. Hawa wanaonekana kila baada ya uchaguzi wanarudi CCM au wanaanzisha chokochoko ili wapate uteuzi.
Mfano Mtu kama Mpina , hata wale Covid 19 ni majembe sana. Hata ukiwasikiliza bungeni . Wakirudi Chadema wakubaliwe kwa sababu walitumia demokrasia na uhuru tunaoutaka kufika walipofika.
Walitumia mwanaya na ubovu wa katiba kuingia bungeni kinyume na katiba ya chama chao na katiba ya nchi lakini wamejipatia kazi kutokana na nguvu ya Serikali na Ikulu na nguvu ya Bunge na mahakama lakini pia wamecheza na akili ya siasa kuwa kuna haki fulani zimekiukwa ndani ya chama chao wakapata loop hole japo ni kweli kuwa baadhi yao hawaipendi CCM na hawana chembe ya falsafa za CCM. Wakirudi kukipigania chama chao ili kuingia CCM basi wapokelewe. Lengo ni kuitoa CCM na kuisambaratisha kwanza kisha kuleta katiba mpya itakayomfanya mtanzania yeyote kuwa huru kufanya kazi ya siasa ,au biashara au kazi nyingine ya umma bila kuingiliwa na CCM kama ilivyo sasa.
Huku kuwabagua na kuwapa majina mabaya wale wanaotoka vyama vingine kuja Chadema imewafanya mpaka wapinzani wengine kuona kuwa kwenda chadema ni hatari zaidi kuliko kurudi CCM. Mfano Zito Kabwe na wengi ndani ya Chama chake wapo tayari kuungana na CCM kuliko Chadema kwa sababu wanatulanwa na kudhalilishwa zaidi na wanachadema kuliko wanaCCM . Hii sio maana ya Demokrasia. Huu ni uhuni unaotakiwa kupingwa sana.
Hili linatakiwa liachwe mara moja ili Chadema kiwa chama chenye Nia hakisi ya kuongoza dola. Mnaweza msiwateue au kuwapa nafasi ndani ya chama lakini mnaweza kuwatumia k2a heshma kubwa kwenye kampeni bila kuwakejeli au kuwatukana kwenye mitando. Kukaa kimya wakati mwingine ni hekima kubwa.
Hivi mtu kama Dr. Slaa ni mtu wa kupuuza na kumwita msaliti na mamluki wakati tangu akiwa CCM mpaka sasa amesimamia msimamo wake wa kupinga kuuzwa kwa rasilimali za umma na ufisadi ndio maana alikataa kumuunga mkono Lowasa . Na ule ulikua ni msimamo usio na unafiki na akaondoka nchini bila kuhamia CCM kwa imani yake kubwa aliyokua nayo ndani ya chama chake akaona ni bora akae pembeni kuliko kushika silaha na kuigeuzia Chadema kwenye Kampeni. Alitumia hekima Kubwa sana.
Dr.Slaa anapaswa kuenziwa ndani ya Chadema na sio kutukanwa.
Mambo ya kutukana wale wanaopingana kwa hoja yalifanyika wakati huo wa chama kimoja na sio sasa. Kwa sasa mnatakiwa muweke mdahalo mjenge hoja juu ya umoja wetu ,sera zetu za uchumi na maendeleo ,vita dhidi ya ufisadi n.k.
CCM hawana cha kutuambia tena mana wamezuia mitandoa na vyombo vyote vya habari ili waseme wao lakini wamekosa cha kusema na hawaamniki tena. Sasa kwenye kampeni watatumia nini tena kutuhadaa au wataahidi kipi ambacho hawajawahi kukiahidi?
Mpaka sasa Rais peke yake kuelekea 2025 ametumia mabilioni ya pesa kununua pikipiki kuhofia upinzani. Yaani CCM wana hofu kuliko wapinzani. Hata Lisu hajawahi kusema kuwa atagombea tangu ameanza maandamano . Nimemfuatilia sana . Kwa maana hiyo Lisu bado hajaanza kampeni kwa mujibu wa sheria . Samia alishaanza kabla ya muda wake hivyo kikanuni hawezi kupitishwa na tume labda wabadili kanuni. Hana sifa ndani ya CCM na pia kwenye tume ya uchaguzi hana sifa mana alianza kampeni kabla ya wakati.
Anapaswa kuenguliwa mapema ili kuondoa aibu kubwa kwa taifa kuweka mgombea asiyefuata kanuni.
Kwa hiyo kama wapinzani wapo siriasi kuiondoa CCM madarakani ni lazima wawashawishi wale wanaoona kuwa wanaendana nao kimisimamo toka ndani ya CCM , ACT , CUF na NCCR mageuzi ili washinde uchaguzi. CCM ikishindwa itasambaratika mana hakuna atakayeweza kubaki kwenye chama bila kuwa na uteuzi. Wasomi wote wataikimbia CCM . Harakati za CCM ndani ya vyuo itakoma ,Watoto wadogo wanaoitwa Chipukizi watakoma na kurudi kusoma mana sheria hairuhusu watoto chini ya miaka 18 kuijihusisha na siasa.
Wafanyabiashara wa madawa na magendo na wakwepa kodi watakimbia . Ugaidi utapotea mana pesa wanazopokea toka nje zitahojiwa kuwa zinakwenda wapi !! Siasa za udini ,ukabila zitaondoka na kubaki siasa za hoja na ushawishi wa sera. Jeshi litajiimarisha katika sayansi na teknolojia badala ya Siasa. Polisi watafanya kazi zao kwa amani na kwa wepesi kwasababu watakua hawana mashinikizo ya kisiasa. Adui wa polisi watakua ni wahalifu na sio wanasiasa.
Nchi itakua na furaha kuu.