Pre GE2025 CHADEMA peke yake haiwezi kamwe kuitoa CCM madarakani...

Pre GE2025 CHADEMA peke yake haiwezi kamwe kuitoa CCM madarakani...

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Haki ina gharama! Watanzania tunaogopa kuhesabu gharama za demokrasia.
 
Haki ina gharama! Watanzania tunaogopa kuhesabu gharama za demokrasia.
Kabisa. Na CCM wanajua watanzania wanaogopa kulipa gharama ya ukombozi wao.

Kwa mfano vitisho vinavyotolewa hapa wakati Fulani na jeshi la polisi huwezi kusikia vinatolewa na polisi wa Kenya.

Polisi wa Kenya wanajua wakenya linapokuja suala la haki zao, hawana hofu ya kulipa gharama yake ili walipate.
 
Tafsiri ya maneno yako ndiyo iko hivyo. Kama CCM wangeweza kupika watu wao wenyewe kulikuwa na haja gani kusubiri wapikwe na CHADEMA ili waende "wakale" vyeo CCM!?

Kitendo cha kusema wanaenda CCM kula vyeo ni kiashiria kimojawapo ni kwa nini CCM kumejaa watu walaji wa rasirimali za Taifa.

Kwa CCM cheo ni ulaji.
Mkuu utaongea sana na sarakasi nyingi lakini unatakiwa ujue Tanzania ni nchi ya chama kimoja ndani ya mwamvuli wa vyama vingi 😂️😂️😂️😂️

Vyama vyote including Chadema na CCM wako bega kwa bega kuhakikisha Wakoloni na Watu Kama wewe wanaendelea kuamini kuwa Tuna mfumo sahihi wa Vyama vingi.

Fuatilia post zangu naiponda CCM sana sana lakini hii fact ichukue ili usipate kiharusi siku ukikutana na usiyoyatarajia.
 
Futilia post zangu naiponda CCM sana sana lakini hii fact ichukue ili usipate kiharusi siku ukikutana na usiyoyatarajia.
Usitakatifushe (Dogmatize) mawazo yako. Hizo post zako za kuiponda CCM hazihalalishi hoja yako hii kwamba CHADEMA na CCM ni chama kimoja.

Hii ni nadharia njama (conspiracy theory) isiyo na mashiko inayotumiwa na CCM kuwakatisha tamaa watanzania wasiwe na Imani na CHADEMA.

Mwenendo wa CCM kwa CHADEMA hauashirii kwa namna yoyote ile kuwa CHADEMA na CCM ni chama kimoja.
 
Sawa ni hiari yako kukataa au kukubali nadharia.
 
Na akili hizo zenu mkig'ang'ania madaraka mtaendelea kuwafanya warz masikini

Unafikiri Kila mtamzania mzalendo anayepost Habari njema hapa jf ni mwanasiasa?
Wengine ni tuna shughuli zetu halali hatuna mfungamano na siasa
Kwanini usemee mioyo ya wengine kila mmoja ana shughuli!
 
Kwanza hakuna mjadala kuwa CCM inatakiwa kutolewa madarakani kwa njia yoyote ile.

Pia hakuna mjadala kuwa mpaka sasa hakuna jinsi nyingine ya kuwa na chama kingine nje ya CHADEMA cha kupambana na CCM.

Ni ukweli kwamba CHADEMA ni chama bora cha siasa kuliko vyama vyote vya siasa nchini CCM ikiwemo.

Baada ya CHADEMA kwa ubora, inafuatia CCM na vyama vingine kama vile ACT na vinginevyo viko kwenye fungu (bundle) moja.

Lakini kuitoa CCM madarakani pamoja na udhaifu wake,inataka jamii ya watanzania kwa uhalaiki wake ( amassed) kujua nini kifanyike ili kuitoa CCM madarakani.

Kuishutumu CCM kwa uovu wake ni jambo la zamani kwa sasa. Kati ya watanzania 100 watanzania 60 wanaujua uovu wa CCM kwa undani sana.

Hakuna asiyejua kuwa CCM ndiyo inaifilisi nchi hii. Watanzania wote wanajua maisha yao yanaharibiwa na CCM kuwepo madarakani.

Lakini asilimia tisini (90%) ya watanzania hawapo tayari kushiriki kwenye harakati za kuitoa CCM madarakani.

Watanzania wengi wanadhani kazi ya kuitoa CCM madarakani ni ya CHADEMA peke yao.

Kila siku wanalaumiwa ni kwa nini hawaitoi CCM madarakani. Cha kushangaza watu wengi wanaogopa kuiudhi CCM.

Huwezi kuta wafanyakazi Serikalini, wafanyabiashara, wakulima na watu wa kawaida wakipambana hadharani na CCM.

Kwa mazingira haya huwezi tarajia CHADEMA peke yao kuitoa CCM madarakani.

Kutegemea CHADEMA peke yake kuitoa CCM madarakani, ni kutarajia muujiza.
sawa ila bado tunaimani na misemo ya wazee chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho
 
CCM inaweza Ikatolewa madarakani endapo Chadema wataweza kuijua nguvu ya umma kiuchumi na kisiasa na kijamii.

Nimeshangaa mpaka leo Wanachama wa Chadema wameshindwa kufikisha mili. 400 ya kumnunulia Makamu wa Mwanyekiti wao Gari.

Hapa kuna shida ,Chama chenye wanachama zaidi ya mil.5. kushindwa kuchanga mil. 400 ni tatizo kubwa sana. Hii ni kutokana na chama kukosa Ofisi na umoja.
Ilikua ni rahisi sana kukusanya pesa hizo kwa wanachama . Iko hivi wanachama laki nne wakitoa elfu mona kila mmoja Jumlla ni Tsh. 400,000,000/- (400,000 xTsh.1000/-)
Nguvu ya Elfu moja .

Mfano pia kuna wazazi walipoteza ndugu zao. Lakini zile familia bado ni hazijawahi kuwezeshwa na chama.
Kuna shida gani kuwahamasisha Wanachama kuchanga kwa ajili ya familia za watu waliokipigania chama ?
(Labda kuna watu hawajui kuwa Marehemu Ndesamburo alikua ndiye nguzo kubwa sana ya uchumi ndani ya Chadema na sio Mbowe kama wengi wanavyofikiri.
Ndesamburo angekuwepo angeweza akamnunulia Lisu gari mpya kwa pesa zake. Yule alikua ni bilonea aliyekipenda Chama na kulinda heshma ya Chama.
Ndesamburo ndiye aliyekua anatumia pesa zake kuwalipa mawakala na kurudisha pesa kwa wale waliokua wananunuliwa na CCM.
CCM walikua wanajua nguvu ya Ndesamburo ndani ya Chadema . R.I.P Ndesa mapesa. )

Kwa Hali ngumu ya kiuchumi ilivyo sasa kila Familia ikipewa mil. 20 itaamsha morali mkubwa sana na hamasha kwa wananchi kuona kuwa chama kipo kwa ajili ya watanzania na sio kutafuta madaraka.
Pesa ni sabuni ya roho. Hata magaidi wanajitoa muhanga kwa sababu ya pesa za kukamilisha misheni zao. Sasa Wapinzani wakibaki kuhamasisha tu bila kujali familia za wahanga ni kosa kubwa sana.

CCM imeshakosa ushawishi kwenye jamii. Wamebaki kutisha na kuangamiza watu kwa sababu wanaona wapinzani hawana habari na wale wanaouawa au kuteswa.
Nilimsikiliza kiongozi mmoja wa CCM wa wanafunzi wa vyuo Kule Singida. Alijiita kiongozi wa wasomi wa mkoa wa Singida. Alikua anatoa kauli ya kumuonya Tundu Lisu. Yaani ni mweupe pee kichwani . Anatoa vitisho badala ya kujibu hoja za Lisu. Ndio watu CCM inaowategemea kushinda uchaguzi .
Uchaguzi wenyewe upo kwenye wakati ambao vyombo vya Dola hasa polisi inajaribu kurudisha uhusiano wake na jamii.
Ni wazi kuwa polisi watakua kwenye wakati mgumu kutumia nguvu kupora kura na kupiga watu wakati wanahamasisha polisi kuwa karibu na jamii na kufanya kazi kwa haki na busara kubwa kuzingatia sheria za nchi ikiwemo sheria za Uchaguzi.

Inawezeka kabisa CCM kushindwa kwa katiba iliyopo na ikatumika kukiua kabisa kisionekane tena kwenye historia ya Dunia kama Ilivyokuwa KANU.
Chadema ni lazima ijipange kiuchumi na sio kugombana na vyombo vya dola kwa sasa kwani ushindi wa CCM ni mdogo sana kwa sasa.

Kama JPM alipelekwa puta na Lisu mpaka wakawa wanazuia mikutano yake nadhani kwa Huyu Mzanzibari hawezi hata kupata kura nusu ya Zile za JPM kwa sababu Wakulima na Wafugaji wote nchini hawawezi kuruhusu Maeneo yao yakauzwa kwa wageni ili wajenge mahoteli na kufanya uwindaji wa wanyama hai na kujenga viwanja vya ndege vya kutorosha wanayama ili hali Ngombe wao wanakamatwa na kutaifishwa. Uatajiri wa Wagogo,wakurya,Wasukuma,Wamasii ,Wambulu,Wasonjo ,Wanyiramba ,Wanyaturu , Wanyamwezi n.k ni Mifugo.
Wanyakyusa ,Wahehe, Waha, wamanyema n.k wanategemea ardhi kuishi na sasa ardhi yao inauzwa usiku na mchana tena kwa kusafiri kuwafuata wananunuzi huko Uarabuni na ulaya ,hawa kamwe hawawezi kukubali kumrduisha tena madarakani kwa sababu hata ile ndogo waliyobakiwa nayo itauzwa na watoto wao watakuwa manamba kwenye mashamba ya Wageni kama wakati wa mkoloni . Na sio hivyo tu bali hata hizo kazi za manamba watazikosa mana wageni wataweka roboti kufanya kazi mashambani.

CCM ijiandae kisaikolojia kuwa Chama kikuu cha upinzani.
Ripoti ya Mpina imeibua mengi sana yanayofanywa na serikali ya Samia kwa mgongo wa kuziba masikio kama Chura na kutowasikiliza wananchi.

Yale mambo ya kusema CCM isinifie mikononi mwangu yamepitwa na wakati .

Sasa ni wananchi wasife kwa njaa na umaskini mikokono mwa CCM.
 
1000 digits umeandika hoja yenye kina kirefu Sana...

Kuhusu pesa kwa asilimia mia Moja (100%) nakuunga mkono. Hakuna siasa bila pesa. Harakati ni pesa.

Kuna mahali kama chama kuna ulegevu wa kuweka uratibishaji wa ukusanyaji na utumiaji wa fedha ndani ya chama.

Kanuni ya fedha ya chama haijulikani kama ipo ama haipo...
 
Tume huru ya uchaguzi na katiba mpya ndio hatua za mwanzo kuitoa ccm
 
Na haiwezekani watu wote wawe kwenye ajira!
Kabisa... Lakini angalau kati ya watu 10 basi watu 9 wawe na ajira rasmi.

Hapa bongo kati ya watu kumi ni watu watatu tu ndiyo wapo kwenye ajira rasmi. Hapo changanya ajira rasmi na isiyo rasmi
 
na mission ya Chadema Sio kuitoa CCM mafarakani. Hilo ulijue tangu leo Kama ulikua bado gizani.

Upo sahihi
TZ hakuna vyama vya upinzani, wanasiasa wa upinzani wote ni mamluki wa ccm ktk kisiasa
 
Back
Top Bottom