Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Hili mada ya ushauri wa bure kwa Chadema, nimesoma humu kuwa wamesusia mkutano wa kesho wa vyama vya siasa kule Dodoma kwa hoja mpaka kesi inayomkabili Mwenyekiti wao ifutwe. Nawashauri ndugu zangu Chadema, wasisuse unless wana uhakika, kwa kususa kwao, kuna something tangible, they wish to achieve na kwa kususa huko they will, achieve, lakini huku kususa tuu just for the sake ya kususa, ili kuonekana ni mashujaa, wanaweza sana kususa, lakini kwa kususa huko, they won't achieve, anything, nawashauri Chadema, wasisuse, wahudhurie mkutano wa kesho, waende na hoja zao, mkononi, wasiwazilishe mezani, zitamfikia Rais Mama Samia, kwasababu tayari Rais Samia, ameishaonyesha kwa kauli na matendo, ana nia njema ya dhati to heal the nation, na tusonge mbele kwenda kwenye maendeleo ya kweli ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.


Kuhusu Hii Tabia ya Kususa Sasa
kuhusu tabia ya kususa, kisiasa, huu mtindo wa kuzira au kususa susa, kususia kila jambo usilokubaliana nalo, sio tabia za kike hizi?, au sio tabia za kitoto?!. Mtu unasusia jambo fulani la kisiasa, ili upate nini?. Kususia jambo lolote la kisiasa bila kupiga hesabu ya what do you want to achieve na kususa huko, sio political suicide?.

The Motive Behind Kususa.
Jee ni nini the motive behind kususa jambo fulani, una susa ili uachieve nini, na baada ya kususa, jee hao wasusaji huwa wanakipata kile walichokusudia?!. Kususa jambo fulani bila malengo, sio tuu ni utoto, bali ni ujinga, kwa sababu ni sawa na kumsusia ngedere shamba la mahindi!, utayavuna mabua!.


My Take. (Maoni Yangu).
Kususia kushiriki mkutano huo sio suluhisho, huku ni kujiua kabisa kisiasa, dawa ni kujenga hoja madhubuti na kukaa mezani kuzungumza, vingine tuitumie mahakama yetu kuzifumua sheria kandamizi za uchaguzi ili zituletee uchaguzi huru na wa haki.

1. Tume yetu ya Uchaguzi NEC, japo sio inclusive lakini ni Tume Huru, licha ya kuteuliwa na rais ambaye ni Mwenyekiti wa chama kimojawapo, kwa uhuru ule ule wa Mahakama zetu ambazo majaji huteuliwa na rais huyo huyo ambaye pia humteua Mtendaji Mkuu wa Bunge letu. Kama Bunge limeweza kuwa huru kwa mfumo huu, na Mahakama ni huru, hata Tume pia ni huru, ila ionekane kuwa huru, something more needs to be done kwenye Tume Hii.

2. Sheria yetu ya uchaguzi, ina mapungufu makubwa yanayohitaji kufanyiwa marekebisho ili kutoa ushindani wa haki. Tusiilaumu Tume kwa chochote kinachotokea kwa sababu Tume inatekeleza sheria zilizopo, kama ni sheria kandamizi, ni kosa la sheria na aliyezitunga na sio kosa la mtekelezaji.

3. The political game playing field is not level, we need to create a level playing field ili kupata ushindani wa haki. Hili nalo ni tatizo la kikanuni, mfano uchaguzi wa 2020, kuna mgombea mmoja anaingia kwenye kinyanganyiro na vingora, msafara, media, na wasaidizi kibao, huku budget yake is fully footed by state, ashindane na makapuku!, unategemea nini?. Tangu tumeanza uchaguzi wa vyama vingi, kuna chama dola kinashindana na vyama makapuku!.

4. Now it's high time vyama vya siasa, vianze kutake responsibilities kwa matokeo ya utendaji wa vyama vyetu kwenye chaguzi mbalimbali, kwa kukubali kushiriki uchaguzi katika mazingira haya, na tukishindwa kihalali kwenye sanduku la kura, katika uchaguzi huru na wa haki, tukubali matokeo, na sio kutafuta visingizio.

5. Lazima tufike mahali, kwa pale ambapo uchaguzi ulikuwa huru na wa haki licha ya kasoro za hapa na pale, ambazo hazitaathiri, matokeo ya jumla ya uchaguzi huo, tujifunze kukubali matokeo na kushindwa kihalali, asiyekubali kushindwa sio mshindani. Kisha turudi nyuma kujitathmini where did we go wrong. Tulipaswa kufanya nini ili kupata ushindi katika mazingira kama haya.

Conclusion.
The bitter reality kwa wapenda demokrasia wa kweli wa mfumo wa vyama vingi nchini, mimi nikiwemo, tumeshuhudia hali hii ndio uwezo wa ushindani kwa vyama vyetu vya upinzani nchini Tanzania ndio umefikia hapa baada ya miaka 30 ya vyama vingi, naweza kusema kuwa this is the peak ya upinzani Tanzania, upinzani Tanzania, ndio imefika mwisho wake sasa!. Sasa tuanze kujiuliza, jee kama hali ni hii sana, je hali itakuwaje kwa uchaguzi wa 2025?. Kama wapinzani hawatabadili mbinu na strategies, za namna ya kushindana na CCM kwenye ushindani usio sawa kupitia sanduku la kura, then, uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, kuna hatari kubwa kwa CCM, kuendelea kuyashikilia majimbo yote ya uchaguzi yaliyokuwa yanashikiliwa na lile jimbo moja la ngama la upinzani, nalo likarudishwa CCM, hivyo kuirudisha Tanzania kuwa ni nchi rasmi ya chama kimoja cha siasa, something which is not healthy at all to true modern democracy!.

Tanzania kama taifa, tujipe pole kwa gharama kubwa za chaguzi hizi, ila tuombe sana Mungu alisaidie taifa letu kama gharama hizi za uchaguzi wa kinachoitwa demokrasia ya uchaguzi huru na wa haki, zinajumuisha, machozi, jasho na damu za Watanzania, kwa kugharimiwa na damu na roho za Watanzania, hakuna namna nyingine yoyote ya fidia kwa damu za watu na roho za watu, zaidi vya karma!, kwa wanaojua the karma operatives, wanajua kilichotokea, tumsaidie rais wetu Mama Samia na nchi yetu Tanzania, tutende haki kwa wote, kuiepuka hii karma isiendelee kututafuna!.

Nawatakia Jumatano Njema na kesho Mkutano Mwema.

Wasalaam.

Paskali
Update
Kususa huku kumeleta matokeo chanya kwa kesi ya Mwenyekiti Mbowe kufutwa na Chadema na CCM wakafanya mazungumzo ya maridhiano na kukubaliana kitu kinachoitwa kugawana nusu mkate, ila makubaliano haya bado hayajatangazwa rasmi, ila M/Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, hakuwa sehemu ya mazungumzo haya, kwasababu anaishi nje ya nchi, hivyo aliporejea na kuyakuta makubaliano hayo ya kugawana nusu mkate, aliwashangaa wenzake na angalia anavyowaita Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?
P.

Rejea za kuhusu Kususa.
Baada ya uchaguzi wa 2010, Chadema ilisusia matokeo na kujidai kuwa hawamtambui JK, ila bunge tuu lilipoanza, niliibua mjadala huu
Chadema Yakubali Yaishe! Yamtambua Rais!, Yampongeza Rais!.

Matokeo ya Chadema Kususia Hotuba ya JK na Kuapishwa kwa Pinda

Media Kususia Habari za Fulani: Jee Tanzania Tuna Independent Media Yenye Jeuri Hiyo?.

Uchaguzi wa 2015 Ukawa wakadai Lowassa ndie mshindi, hivyo wakajifanya kususa, na kutomtambua Magufuli, mimi niliwapa ushauri ufuatao
Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali ya Magufuli ni Serikali Haramu. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!.

Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa kimya, Mungu ndiye akupiganie!

CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake - JamiiForums

Hatimaye CUF 'Wameridhia' Rasmi, Kushiriki Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar!. - JamiiForums

Japo umegharimiwa kwa machozi, jasho na damu, ulikuwa huru na wa haki!. Hongera CCM, CHADEMA poleni!. Mungu saidia Tz - JamiiForums

Ujio wa Lowassa CHADEMA: Kuna kundi wamesusa, wanapanga kurejea CCM! - JamiiForums
 
Kuwasafishia njia maharamia ni kushiriki na kushirikishwa kwenye kuhalalisha haramu, huku tukiyapa nguvu zaidi matendo yao haramu dhidi yetu,dhidi ya wengine, dhidi ya wapenda haki na dhidi ya watanzania, 🤔.
 
Hoa magaidi mnawabembeleza nn ,chama jinai

USSR
 
Ngoja nikuiite Kaka mkubwa kwa heshima yako jukwaani. Lakini nina swali dogo kwako. Uoni Mtesi wako kukuita kwenye kikao chake ni kumuonyesha anachokifanya Ni sahihi?. Nianavyo Mimi wako sahihi wasiende hakuna Mwenye Nia njema na wapinzani wa kweli nchi hii. Mkuu nchi hii hata wasema kweli tunapoelekea watateseka sana. Mfano Ni polepole
 
Paschal CHADEMA waliomba kuonana na Rais bana hayo mengine ni zugazuga tuuu.

Rais apate AUDIENCE nao. From there milango mingine itafunguka.
 
Kwa nini mtoto mdogo anasusa, kumbe ni kufikisha ujumbe kukataa kuonewa na kukataa kunyimwa haki ya utu wake,japo baba au mama hatafanyia kazi kwa ujeuri wake tu lakini nafsi itaendelea kumsuta daima na ipo siku huyo mtoto haki yake atapewa. Kumbe kususa banadamu anazaliwa nako ikiwa ni njia sahihi ya kudai haki yake dhidi ya watesi wake. Tutende haki ili mioyo yetu iwe na amani kwa pamoja TUPINGE UONGO NI DHAMBI.
 
Mkuu Mayalla Chadema shida yao ni majadiliano na Mh Rais sio kuhutubiwa na Rais, ndio maana hata msajili amesema kikao na Rais bado ila huu ni mkutano wa wadau wa siasa utakao funguliwa na Mama Samia.

Sasa kwenye majadiliano wanakuepo Chadema,ACT,TADEA,CUF, NCCR mageuzi watajadili nini bila mhusika mkuu ambaye ndio Rais hayupo.
 
Mbona NCCR Mageuzi wamekataa mualiko? Mbona vyama kibao vya upinzani vitakuwepo ikiwa pamoja na CUF na ACT Wazalendo? Mbona kuna majadiliano yatakayoongozwa na chama mahiri cha upinzani cha ADC? Kutokuwepo kwa Chadema hakuna athari yeyote.

Amandla...
 
Mayalla nia ya uzi wake ni kutaka kuiponda Chadema kuwa siyo Chama makini. Yaani Mayalla ni antiChadema.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
AAAAAAAAAAAAAAHHHHHHHHH WAPI BHAAAAANAAAAAAA!
 
Kaka paskal mayalla unayo hoja ya msingi kwamba katika kususa hakuna tija ikiwa waliosusa hawajabainisha lengo mahususi la kususa kwao.

Kubwa ni moja tu kutoka kwa wasusaji. Mkutano hauna lengo la mjadala wa kisiasa wa kutafuta ufumbuzi wa hali ya mtanziko wa kisiasa nchini, kinyume chake mkutano umekuwa kama picnic.

Mkutano ulipaswa kuweka nafasi ya wadau wa siasa nchini kutema nyongo zao mbele ya kipaza sauti na mbele ya makamera ya video dhadhir shahili dunia nzima ikisikia.

Hii ya kuwasilishwa kwa maandishi haina uwazi juu ya kilichowasilisha na ahadi za utekelezaji kutoka kwa aliyewasilishiwa.
 
Athari ipo. Chadema ni chama kikuu cha upinzani nchini believe it or not, kutokuwepo kwake kuna madhara ya moja kwa moja kwa sura ya nchi kisiasa kimataifa. Na kutokuwepo kwake kuna wasilisha malalamiko ya mpangilio mbovu na nia mbaya ya mkutano husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…