Wanabodi,
Hili mada ya ushauri wa bure kwa Chadema, nimesoma humu kuwa wamesusia mkutano wa kesho wa vyama vya siasa kule Dodoma kwa hoja mpaka kesi inayomkabili Mwenyekiti wao ifutwe. Nawashauri ndugu zangu Chadema, wasisuse unless wana uhakika, kwa kususa kwao, kuna something tangible, they wish to achieve na kwa kususa huko they will, achieve, lakini huku kususa tuu just for the sake ya kususa, ili kuonekana ni mashujaa, wanaweza sana kususa, lakini kwa kususa huko, they won't achieve, anything, nawashauri Chadema, wasisuse, wahudhurie mkutano wa kesho, waende na hoja zao, mkononi, wasiwazilishe mezani, zitamfikia Rais Mama Samia, kwasababu tayari Rais Samia, ameishaonyesha kwa kauli na matendo, ana nia njema ya dhati to heal the nation, na tusonge mbele kwenda kwenye maendeleo ya kweli ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. la mahindi!, utayavuna mabua!.[/SIZE]
My Take. (Maoni Yangu).
Kususia kushiriki mkutano huo sio suluhisho, huku ni kujiua kabisa kisiasa, dawa ni kujenga hoja madhubuti na kukaa mezani kuzungumza, vingine tuitumie mahakama yetu kuzifumua sheria kandamizi za uchaguzi ili zituletee uchaguzi huru na wa haki.
1. Tume yetu ya Uchaguzi NEC, japo sio inclusive lakini ni Tume Huru, licha ya kuteuliwa na rais ambaye ni Mwenyekiti wa chama kimojawapo, kwa uhuru ule ule wa Mahakama zetu ambazo majaji huteuliwa na rais huyo huyo ambaye pia humteua Mtendaji Mkuu wa Bunge letu. Kama Bunge limeweza kuwa huru kwa mfumo huu, na Mahakama ni huru, hata Tume pia ni huru, ila ionekane kuwa huru, something more needs to be done kwenye Tume Hii.
2. Sheria yetu ya uchaguzi, ina mapungufu makubwa yanayohitaji kufanyiwa marekebisho ili kutoa ushindani wa haki. Tusiilaumu Tume kwa chochote kinachotokea kwa sababu Tume inatekeleza sheria zilizopo, kama ni sheria kandamizi, ni kosa la sheria na aliyezitunga na sio kosa la mtekelezaji.
3. The political game playing field is not level, we need to create a level playing field ili kupata ushindani wa haki. Hili nalo ni tatizo la kikanuni, mfano uchaguzi wa 2020, kuna mgombea mmoja anaingia kwenye kinyanganyiro na vingora, msafara, media, na wasaidizi kibao, huku budget yake is fully footed by state, ashindane na makapuku!, unategemea nini?. Tangu tumeanza uchaguzi wa vyama vingi, kuna chama dola kinashindana na vyama makapuku!.
4. Now it's high time vyama vya siasa, vianze kutake responsibilities kwa matokeo ya utendaji wa vyama vyetu kwenye chaguzi mbalimbali, kwa kukubali kushiriki uchaguzi katika mazingira haya, na tukishindwa kihalali kwenye sanduku la kura, katika uchaguzi huru na wa haki, tukubali matokeo, na sio kutafuta visingizio.
5. Lazima tufike mahali, kwa pale ambapo uchaguzi ulikuwa huru na wa haki licha ya kasoro za hapa na pale, ambazo hazitaathiri, matokeo ya jumla ya uchaguzi huo, tujifunze kukubali matokeo na kushindwa kihalali, asiyekubali kushindwa sio mshindani. Kisha turudi nyuma kujitathmini where did we go wrong. Tulipaswa kufanya nini ili kupata ushindi katika mazingira kama haya.
Conclusion.
The bitter reality kwa wapenda demokrasia wa kweli wa mfumo wa vyama vingi nchini, mimi nikiwemo, tumeshuhudia hali hii ndio uwezo wa ushindani kwa vyama vyetu vya upinzani nchini Tanzania ndio umefikia hapa baada ya miaka 30 ya vyama vingi, naweza kusema kuwa this is the peak ya upinzani Tanzania, upinzani Tanzania, ndio imefika mwisho wake sasa!. Sasa tuanze kujiuliza, jee kama hali ni hii sana, je hali itakuwaje kwa uchaguzi wa 2025?. Kama wapinzani hawatabadili mbinu na strategies, za namna ya kushindana na CCM kwenye ushindani usio sawa kupitia sanduku la kura, then, uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, kuna hatari kubwa kwa CCM, kuendelea kuyashikilia majimbo yote ya uchaguzi yaliyokuwa yanashikiliwa na lile jimbo moja la ngama la upinzani, nalo likarudishwa CCM, hivyo kuirudisha Tanzania kuwa ni nchi rasmi ya chama kimoja cha siasa, something which is not healthy at all to true modern democracy!.
Tanzania kama taifa, tujipe pole kwa gharama kubwa za chaguzi hizi, ila tuombe sana Mungu alisaidie taifa letu kama gharama hizi za uchaguzi wa kinachoitwa demokrasia ya uchaguzi huru na wa haki, zinajumuisha, machozi, jasho na damu za Watanzania, kwa kugharimiwa na damu na roho za Watanzania, hakuna namna nyingine yoyote ya fidia kwa damu za watu na roho za watu, zaidi vya karma!, kwa wanaojua the karma operatives, wanajua kilichotokea, tumsaidie rais wetu Mama Samia na nchi yetu Tanzania, tutende haki kwa wote, kuiepuka hii karma isiendelee kututafuna!.
Wasalaam.
Paskali