Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.

The simple truth is, wanaweza kwenda wasisikilizwe pia kama ambavyo hawasikilizwi wasipoenda.

Uwepo wa kesi ya Mbowe mahakamani bado unaonesha kuna visasi kati ya hizi pande mbili, na kwasababu Chadema walishaonesha utayari wa maridhiano toka awamu iliyopita lakini bado wakatendwa...

Naona sasa ni zamu ya serikali kuanza kuonesha utayari kwa upande wao, na utayari wenyewe ni either waifute kesi ya Mbowe, au atleast waruhusu mikutano ya siasa, ndio mazungumzo yao yaanzie hapo, kinyume na hapo ni ubabe tu ndio utaendelea kati ya pande mbili.
 
Kususa siyo lazima uachieve something immediately .... wanapeleka ujumbe.

Hivi wao kwenda pale kupokea viongozi wa CCM, kuhutubiwa nao na kupiga picha kunawasadia nini zaidi ya kupoteza muda na resources.
 
Wataziwasilisha vipi wakati hawatapewa nafasi ya kuongea ?
 
Hakuna mwenye akili ndani ya CHADEMA anayeweza kuhudhuria huu mkutano wenye unafiki na hila ndani yake. Na wala hakuna mwenye akili timamu asiye mnafiki anayeweza kuwashauri CHADEMA kuhudhuria mkutano wa namna hiyo.

Hata makaburu hawakuwahi kufanya hila na ghiliba kama hizi za Samia. Fredrick de Clerk alivyotaka kujenga Afrika Kusini mpya, cha kwanza alionesha hiyo dhamira kwa kumwachia Mandela ambaye makaburu hawa walimfunga jela kwa kumwonea.

Baada ya kutoka jela, Mandela naye akiwa na dhamira njema, alienda kwenye mjadala na Serikali juu ya Afrika Kusini mpya.

Huu uwendawazimu wa hapa kwetu hakuna mwenye akili anayeweza kuukubali. Umemsingizia Mbowe na kumbambikia kesi, umemweka ndani, halafu unasema unaenda kwenye mjadala, unaenda kujadiliana na nani wakati kiongozi wa hao unaotaka kujadiliana nao umemweka ndani kwa kumwonea, tena ukisisitiza kwa uwongo mkubwa kuwa alitoroka nchi! Huu kama siyo ushetani, uhayawani na unafiki wa hali ya juu, utauita ni nini?

CHADEMA wasishiriki dhalimu. Hata kama ni miaka 10 au 20, wasimame katika haki, wasikubali kuingizwa kwenye huu uchafu wa siasa za unafiki na ulaghai. Ulaghai abakie nao Samia na watu wake. Watu wanaoipenda Tanzania, wabakie katika njia ya haki, iliyonyoka.
 
Mkutano is a one way traffic, ingekuwa kikao na Rais labda kungekuwa na tija...

Huo mkutano inaonekana kama ni K.P.I tu ya watu/mtu fulani pengine ili kuonesha kuna demokrasia au uwanja wa wanasiasa kukutana...

Halafu je kuna usawa gani kwa vyama vya siasa vingine, kukutana na Rais ambaye kwa kofia nyingine ni mwenyekiti wa CCM??
 
CHADEMA endelezeni harakati zenu kukijenga chama kimya kimya. Wenyewe wanaotaka CHADEMA isiwepo, kuringana na wanavyoibana,watajua haipo. Lakini mioyoni mwa watu mupo kwa kiasi kikubwa.

Huu ushauri wa kushiriki vikao kuharalisha uharamia na ujanja ujanja wa walio kwenye nafasi msijaribu kuufuata. Hayo maigizo yao waachie wao waigize. Achaneni kabisa na hayo maigizo
 
Vyama makini haviwezi kushiriki kubariki dhambi, kutakatisha dhurma !!
1. Uchaguzi ulikuwa feki ambao ulizaa viongizi ambao hawakutokana na wananchi.
2. Viongozi wengi wa upinzani wapo magelezani kwa kesi mbalimbali za michongo baada ya uchaguzi mkuu
3. Shughuli za kisiasa zimekuwa kwenye katazo kwa miaka 7ambavyo ni kimyume na Katiba na Sheria za nchi... yaani ubabe mtupu.
4. Madai ya katiba mpya yamegeuka kosa la Jinai, Ugaidi na uhujumu uchumi.

Haya yote yamekuwepo na hakuna anayejali - leo hii kuongea na watu hao wa lipi hasa? kuna geni hapo ndugu au kushoshana tu.
 
Nawapongeza sana CHADEMA na NCCR kwa kugomea ushiriki kwenye kikao hiki haramu cha kuwasafishia njia watesi.

Nchi imevimba toka 2015. Hakuna nafasi ya kupumua kwa wapinzani. Nia njema ya mama Samia ilipaswa kuonekana mwanzo kabisa kwa kukutana na Wapinzani kama Agenda yake ya mwanzo kabisa.

Kama hakupata nafasi,kikao hiki hakiweza kuwa cha kufungua tu na kupiga picha pekee na wapinzani wakati hajawasikiliza. Hii ni dharau, huku ni kuwapuuza.

Kama yeye hawapi umhimu wala kipaumbele, kwanini wapinzani wajione wanyonge kwa kufanywa ruber stamp kwenye udhalimu??
 
Umemaliza yote mkuu,ambaye hatakuelewa basi huyo ni msukule na hatakaa aelewe chochote hapa duniani.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Zab 1:1-6

Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa. Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki. Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea
 
Ya JPM asiyoyapenda anayapindua, ila yale yanayomfaidisha yeye na chama chake cha wahuni anayakumbatia kama lile la kuendelea kuwabana wapinzani hata kuzuia vikao vyao.

Aamue moja. Asiwe vuguvugu, awe au moto au baridi.
 
Paskali Mbona unaumia sana chadema kususia mkutano? Wewe si mwanaccm wewe? Unaweza kweli kumtakia adui yako mema? We chadema waache hizo ni mbinu zao za vita kama zile za wizi wa kura na vitisho zilivyo za chama chako cha ccm
 
Una jipya wewe mwanaccm mfu ulie enda ccm kwa upepo wa mwendazake Yani unepoteza mvuto kabsa mi nikikuonaga naisi hata kutapika haukujua thamani Yako kabla ya kujiunga ccm ndio maana Sasa watapatapa.una jipya.unless otherwise ujiondoe ccm
 
Haka kamkutano ni kamchongo cha ofisi ya msajili kupiga fedha.
Hakuna lolote zaidi ya hilo
Malalamiko yapo mengi ofisi ya msajili wa vyama vya siasa inapelekewa hawayafanyiwi kazi.
Vyama vya siasa vinakatazwa kufanya mikutano na polisi kinyume kabisa na sheria ya vyama vya siasa inavyoelekeza
Msajili ambaye ndiye msimamizi mkuu wa sheria yupo kimya
Afanyie kazi malalamiko hayo ndio awaite wadau waje kuzitafuna posho hizo vizuri.
Any way ndio mfumo unaoendelea kupungua kidogokidogo kwa Africa
Ambapo waliopo madarakani wanajiona wao tu na watu wao wa karibu ndio wanastahili kutawala wengine.
Hivyo wanatumia mianya ya mifumo mibovu ya katiba au ikibidi kubadilisha katiba ili waendelee kutawala wao wakiwaahidi kuwaletea maendeleo wananchi wao ambao % kubwa ni maskini.
Viongozi hao wa Kisiasa wanachagua watu wao wa kusimamia mifumo mbalimbali ili waendelee kula keki ya taifa huku wananchi wao wakiwa wengi ni maskini tena wa kutupwa.
Watu kama akina mtungo ni aina hiyo.

Hakuna haja ya hilo kongamano sijui kikao hicho.
Masuala ya kisiasa hapa tz ikiwemo kero,changamoto zinajulikana wazi pamoja na solution zake.

Kikao hicho ni mchongo tu wa kufanya matumizi ya hela za ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, pamoja na kuwapa takrima washiriki ili kutowafikiria vibaya kwamba wanakula wenyewe kasungura
Hii ofisi watumishi wake wanapiga pesa zao kupitia viwarsha na vimkutano kama hivi, tena kimewekwa mwisho wa mwaka ili wamalize mwaka vizuri
 

Hili kitu linafik Sana; kwamba Samia hajui hizo hoja?
 
Kwani kwenye ratiba iliyowekwa Humu kuna Kipengele cha kuwasilisha hoja? Labda iwe ratiba feki.
 
Hoja zote nini Chadema wangekaa mezani na kuzungumza zilishawakilishwa kitambo Ikulu, so kuwepo kikao maalum ,sio ichi Cha wadau wa democracy, Mtungi kafafanua vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…