Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.

Mkuu Pasko Tunashukuru kwa mada yako yenye hoja zilizoshiba lakini Nina maswali kidogo ,Je Mama Samia ni kweli ana Nia njema na nchi yetu hasa kuketa Maafikiano ya kisiasa?
Mbona ni kama haonyeshi hivo Yani maneno yake ni tofauti na matendo yake?
Na mbona Rais Mama yetu Samia ni kama kaanza kuwa na kibri Cha madaraka ukimcheki vizuri ni kama anasema Mimi ndo Rais hamna Cha kunifanya Zaid namuona anataka kama vile aabudiwe?
Zaidi ya hapo naweza kuhitimisha kwamba haya yote yanatokea ili yake maneno ya unabii yaweze kutimia kuhusu nchi yetu kwamba inapitia gizani na ipo siku wale wote walioipitisha gizani hakika watajuta,Maana ni ngumu kuamin katika Hali ya kawaida Yani nchi kwa miaka 6 ipo kwenye sintofaham kwa chuki za kisiasa ,watu kuumizwa,kupoteza maisha na Kila aina ya dhurma Leo anakuja Rais mwingine Badala ya kuitoa nchi shimoni anaendelea tu na Hali hiyohyo .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna haja ya kikao kutekeleza matakwa ya katiba, uwezi kukaa huku mambo ya wazi yasiyo ya haki yakiendelea, unatakiwa kuacha dhambi ndio unajiweka safi ndio mnazungumza!
 

CDM wao sio wadau wa Siasa na hicho kikako hakiwahusu....Kama wanajua hapo Rais ni mgeni rasmi tu na sio sehemu ya kikao shida yao ni nini?
 
Huyo Samia Leo ameshuka kutoka sayari nyingine Hadi asijue matatizo ya vyama vya siasa? Au Jaji Mtungi hajamwambia matatizo ya ofisi yake?

Wakati mwingine ficha upumbavu wako.
 
Maskini hawakukusikiliza ila Zitto amewaombea msamaha ili kiongozi wao asamehewe.
 
KUSUSA NI TABIA YA KIKE? Halafu tunaongozwa na Rais mwenye jinsia ya kike, unatoa picha gani?
 
Mayalla mtizamo wako ni wa kisiasa zaidi ambao hauwezi kuponya jeraha, ili uponye mfarakano achana na madai yako yote yaliyopo anza upya, unataka ukutane na Chadema huku viongozi wake hautaki wakafanya mikutano! Vyama ni vya wanachama. Mayalla haujawahi kulalamika kitendo cha wanaccm kufanya mikutano kila siku na kila mahali nchini, jana huko Njombe Mkuu wa Wilaya aliwahutubia UWT na kuwaambia serikali imetoa fedha wakopeshwe akina mama wa UWT! Pesa za wananchi zinakopeshwa wanachama wa chama kimoja, ukisema unaitwa unavurugu!
Waachie wote usiowapenda ili ukae nao meza moja muanze upya kulingana na katiba ya nchi na si hisani au hiari ya mtu, kesho
Samia akiondoka mtaanza kukamatana tena.
 
Paskali upo kwenye game siku nyingi.Nchi zilizokuwa za kijamaa ni ngumu sana kukubali mabadiliko na maridhiano angalia urusi ,Azerbaijan .Vyombo vya usalama na Chama tawala ni wamoja.Samia hana maamuzi yoyote wenye maamuzi ni wenye chama chao kama walivyojitabainisha wenyewe kuwa kiroboto chama kina wenyewe.
 
Jitahidi neema yako IPO njiani,Siku usiyoijua itqkufikia.Ila hiyo neema inakataza watu kufanya ubaya,wapate kuishi kwa kiasi na haki nk

Hofu yangu ni kwamba ukishateuliwa utafanana kwa asilimia kubwa na wao.

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Unatetea uovu, Samia na genge lake linadai heshima wasiokuwa nayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…