Uchaguzi 2020 CHADEMA, TBC TV wanawaharibia kampeni ya mgombea Urais wenu Tundu Lissu; chukueni hatua sasa na haraka kabla hawajaharibu zaidi!

Acheni unafki, lini mmeanza kuangalia TBC? si huwa mnaiita tbccm
baada ya kukutanishwa na kuzungumza pamoja tulidhani wamebadilika kumbe ni walewale TBCCM hovyo sana labda tuseme hawana waandishi na wapiga picha mahiri kama siyo fitina,tbccm bado wana hasira na CHADEMA. Alicho sema mwandishi ni sahihi kabisa hiyo siku na mimi nilishuhudia baada ya bibi mkubwa kuweka hako ka chanel saa 2 usiku tulipoishiwa na kifurushi,kwa hasira kesho yake nikakopa hela kununua kifurushi angalau nione ka ITV bwana
 
Ukiona. TBC Wanaomba suluhu ili warushe vipindi ujue faida Ni ya CCM. Hadi tume ikashiriki ujue Kuna hila
 
Mbowe alikuwa sahihi sana kuyafukuza Matbccm.. uzuri watanzania Wa Leo sio Wa mwaka 47
 
Mnaanza kutafuta pa kuangukia...

Sera zenu ni nyomi

Kwio
 
Kwa kuwa mlishatoa tahadhari hata Watazamaji huwa tunaangalia kwa tahadhari.
 
Naunga mkono
 
Sijaona shida kwa ITV, Mabele Makubi anafanya vizuri sana kwenye mikutano ya CDM

Of course, hata mimi sijaona tatizo kwa ITV...

Na kiuhalisia, hata TBC kama taasisi huru inayojitegemea haina tatizo...

Shida ni kuwa ni mali ya serikali na wote tunaijua serikali ya sasa iliyo chini ya CCM ya Magufuli..

Wanalazimishwa watende wanayoyatenda. Wanalazimishwa wakiuke miiko ya taaluma yao kwa manufaa ya kisiasa ya aliyeko ikulu...!

Kwa kifupi hata vyombo vya habari vyote kabisa kuanzia TVs, Radio stations, blogs, online TVs nk haviko huru 100% na vingine watendaji wakuu wao wamenunuliwa ili waandike ama watangaze kile tu atakacho dikteta....!

Na kama tasnia ya habari ina akili na inaangalia maslahi mapana na ya muda mrefu ya vyombo vyao, basi ni lazima sana washirikiane na wananchi kumfukuza Ikulu huyu dikteta Magufuli aondoke madarakani...!!

Hii ndiyo njia pekee ya ku - regain Uhuru wao walioupoteza kwa kulazimishwa kufanya mambo unethical and unprofessional kwa ajili ya mtawala dikteta huyu....
 
Mnaanza kutafuta pa kuangukia...

Sera zenu ni nyomi

Kwio

Asante kwa kushiriki kutoa maoni ktk hoja yangu...

Hata hivyo, umeelewa vibaya. Ngoja nijaribu tena kukupa elimu ya siasa kidogo....

1. Moja ya vigezo vya kukubalika kwa mgombea uongozi ni idadi ya watu wanaomuunga mkono....

2. Kwenye kampeni za uchaguzi huu, ni idadi ya watu wanaokuja kukusikiliza kujua MAONO na SERA zako iwapo watakuchagua....

3. Tundu Lissu na CHADEMA kwa Tanganyika ndiye anayeungwa mkono na watu wengi zaidi kwa HIARI yao si kwa ushawishi wa RUSHWA ya fedha ama USAFIRI kuwatoa makwao kwenda kwenye mikutano ya kampeni kama wanavyofanya CCM....

Hili ukatae ama ukubali, lakini huu ndiyo UKWELI WA MAMBO....

4. Sasa kinachofanywa na TBC ni kuugeuza UKWELI huu kupitia chombo hiki cha habari ili watu wa maeneo ya mbali ambao hawakuhudhuria mkutano fulani wanaouripoti wapate picha "hasi" tofauti na uhalisia....

Hata ujumbe unaoripotiwa ni tafauti kabisa na kilichozungumzwa na mgombea....;!!
 
Ivyoivyo poa ilimradi jina la CHADEMA litajwe tu
 
🤣🤣🤣 Nyie jamaa bana.... Kama watoto yatima. Ni kulalama tu
 
Ukiona. TBC Wanaomba suluhu ili warushe vipindi ujue faida Ni ya CCM. Hadi tume ikashiriki ujue Kuna hila
alieomba suluhu ni Mbowe baada ya kuona kuna mgomo baridi wa waandishi
 
TBC ni kama panya
 

TV stations zipo nyingi....Kwani mnalazimishwa kuangalia TBC1?
 
Angalau ITV wanajitaidi tofauti na TBC na STAR TV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…