Vyama vya upinzani na viongozi wao waliopo wakubali hawawezi kuitoa CCM madarakani kwa mbinu wanazotumia.
Pamoja na kwamba tuna miaka 25 tangu vyama vingi virudishwe bado vyama hivyo vimeshindwa kujijenga toka chini.
Wako na matawi ambayo hayana impact yoyote , hawawajui wapiga kura wao ni wakina inawezekana asilimia kubwa ya wasioenda kupiga kura ninwatu wasioipenda CCM ila kwa sababu hawana mizizi chini wameshindwa kuwatambua na kuwashaeishi wakapige kura.
Wameshindwa kusimamia hoja za msingi zinazowagusa watanzania kama watu kukosa malipo ya pensheni na kukazania mambo ambayo wapiga kura hayamgusi kwa haraka.
Wameshabikia sana Marekani na nchi za Ulaya na kutoa kauli za vitisho huku wakisahau wapiga kura wapo Tanzania.
Ni watu wasiojali wanachama wao wanataka nini ndiyo maana walimtoa mgomea aliyepitishwa wakamweka mgombea wanayemtaka wao.
Kushabikia mambo ambayo ni kinyume na utamaduni wa mtanzania ili mradi wapate support toka Ulaya