CHADEMA tuliwaambia kazi kubwa ni kujenga chama matawini ndio utafute kushika dola mkadharau

CHADEMA tuliwaambia kazi kubwa ni kujenga chama matawini ndio utafute kushika dola mkadharau

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,900
Reaction score
52,056
Wapiga kura hupatikana chini kwenye matatu mitaaani na vijijini.

CHADEMA walikuwa na resources zote hasa kipindi cha Slaa na Lowasa. MATAJIRI wengi walikuwemo chadema wangeweza kujenga ofisi Nzuri na za makao makuu na za matawi nchi nzima bila hata kutumia ruzuku Bali michango tu ya wanachama na wafadhili wa nje.

Lakini golden opportunity ile wakaipoteza.

Sasa uchaguzi huo mstaei matupu hayana watu wengi yalishafungwa siku nyingi mijini na vijijini kwa sababu mbalimnali ikiwemo kutolipa kodi nk.

CHADEMA badala ya kujenga branch network wakabwetela na kura za Lowasa ambaye alitumia branch network ya CCM kujijienga na kujulikana akiwa waziri mkuu akawa nchi nzima wanamjua kupitia CCM branch network.

Dharau hizi za kutojenga matawi imara kote nchi nzima kwaweza igeuza chadema kuwa hoi kama NCCR.

NCCR Mageuzi kilishakuwa chama miguu cha upinzani lakini sasa kiko hoi.
 
Chadema imeenea nchi nzima na kila mahali , hapa nilipo ni kijijini Ngyeke, ndani kabisa maporini lakini kampeni yetu imekuwa rahisi sana kwa vile kila mahali ni CHADEMA NI MSINGI, vijiji vyote huku ni chadema kasoro wachawi wachache sana
 
Chadema imeenea nchi nzima na kila mahali , hapa nilipo ni kijijini Ngyeke , ndani kabisa maporini lakini kampeni yetu imekuwa rahisi sana kwa vile kila mahali ni CHADEMA NI MSINGI , vijiji vyote huku ni chadema kasoro wachawi wachache sana
Endelea kujidanganya. Nipo kwenye Kata moja maarufu sana hapa Jijini Mwanza. Wapiga kura wengi wanadhani Mgombea Udiwani wa CCM kapita bila kupingwa kwasababu hawamjui mgombea yeyote zaidi ya wa CCM. Sipati picha uko vijijini hali ikoje!
 
Mnawekewa hadi video lakini bado hamuamini ! basi nendeni Geita kwenye malori na matrekta ya kukusanya wananchi
CCM chama cha waopendana sana mwenye Lori,trekta,bus au pikipiki bajaj au baiskeli kupeana lift kwenda mikutanoni kawaida

Ni solidarity ndani ya Chama inayowaunga pamoja wenye nacho na wasio nacho kuhakikisha CCM mikutano yake inafanikiwa na ushindi unapatikana
 
Mlivyokuwa mnaipa promo NCCR na Mbatia miezi michache iliyopita tuliwaonya NCCR kuwa mnawatumia tu na muda si mrefu mtaawatema!Ona sasa mmewatema na kuwasahau kabisa na sasa mnawakashifu!

Nways,CDM inapendwa tu hivyo hivyo!Nimekuja huku kijijini msambara,kata ya msambara wilaya ya kasulu!Hakuna ofisi ya CDM ila watu wanakwambia wanakwenda na Lissu!

Jioni huwa naenda kwenye vijiwe vya kahawa ambapo huwa tunapata fursa ya kuangalia taarifa ya habari kwa muuza kahawa!Mjadala ni mkubwa baada ya taarifa,sijaamini mpaka vijijini sasahivi watu wanajadili masuala ya nchi yao japo wajinga hawakosekani!
 
Wapiga kura hupatikana chini kwenye matatu mitaaani na vijijini.

CHADEMA walikuwa na resources zote hasa kipindi cha Slaa na Lowasa. MATAJIRI wengi walikuwemo chadema wangeweza kujenga ofisi Nzuri na za makao makuu na za matawi nchi nzima bila hata kutumia ruzuku Bali michango tu ya wanachama na wafadhili wa nje...
Wangekuwa hawajaenea mngekuwa mnawateka?
 
Mnawekewa hadi video lakini bado hamuamini ! basi nendeni Geita kwenye malori na matrekta ya kukusanya wananchi
Mfano chadema matawi HAMNA hivi mtu hata akupe Lori au trekta au basi bure utaenda kubeba hewa?CCM matawini kuna watu ukituma gari ukiwaambia niwakute tawini utawakuta kibao na nguo zao za CCM wamevaa tayari kupanda trekta au Lori au basi
 
Nilikuwa naona chadema tunaenda kubeba.ndoo lakini kwa upepo wa magufuri uko vijijini inatisha njiani tu akuna msanii yoyote lakini anajaza.xijaona picha ya mgombea wetu akipita vijijini na akajaza...kingne kilichonimaliza.nguvu..yani vijijini wagombea wa vyama pinzani awafahamiki...yanii kweli upinzani tuna safari ngumu sana...Dah
 
Chadema imeenea nchi nzima na kila mahali , hapa nilipo ni kijijini Ngyeke , ndani kabisa maporini lakini kampeni yetu imekuwa rahisi sana kwa vile kila mahali ni CHADEMA NI MSINGI , vijiji vyote huku ni chadema kasoro wachawi wachache sana
Aisee we ndio mwanamke mwanamke wa kuoa maana ni mvumilivu halafu mbishi sana
 
Waacheni watoto wetu waende shule na watumishi wa umma kwenye Halmashauri zetu msiwalazimishe wafunge ofisi waende kwenye kampeni za mgombea wenu.

Mmeongea miaka 5 na watanzania wameshawaelea sasa hofu yote hii ni ya nini?
 
Mfano chadema matatu HAMNA hivi mtu hata akupe Lori au trekta au basi bure utaenda kubeba hewa?CCM matawini kuna watu ukituma gari ukiwaambia niwakute tawini utawakuta kibao na nguo zao za CCM wamevaa tayari kupanda trekta au Lori au basi
Aina ya watu wanaokusanywa umeiona lakini ?
IMG-20180405-WA0006.jpeg
 
Back
Top Bottom