Sasa sijui sisi tunao wahimiza CHADEMA wafanye kazi kwa niaba yetu kutusaidia kuondoa uovu huu chini ya CCM, tuyaseme vipi, na mara ngapi haya tunayo washauri ili wapate kuyafanya!
Haya yote unayo yaandika humu mkuu 'Grahams'; wengine tulianza takribani miaka mitano iliyo pita kuwahimiza CHADEMA wajipange na kuwa tayari kwa hii 2025. Tumeshauri njia mbalimbali za kukifanya chama kuwa hai, tokea huko mitaani; kila ngazi hadi makao makuu ya chama..., ilikuwa ni kazi ya kuwaiga tu hao hao CCM kimuundo; lakini naona CHADEMA wao walitumia muda wao kivingine.
Sasa tupo hapa, pamoja na kwamba Magufuli hayupo kufanya yaliyo fanyika 2019/2020; lakini Samia yupo, ambaye yeye kaamua kutumia njia ya pesa, badala ya maguvu. Matokeo yatakuwa ni yale yale.