Mgombea urais wa Chadema alipopewa adhabu ya kutofanya kampeni kwa kukiuka maadili ya uchaguzi kama ilivyokawaida yake aliropoka kuwa ataendelea na kampeni. Hii ni kwa sababu yeye anajiona yupo juu ya sheria na haogopi sababu tu kuna mabeberu na watu kama akina Amsterdam wapo nyuma yake. Kamati Kuu Chadema imemdhibiti ili atii sheria.
Lissu anasahau kuwa Tanzania ni dola huru ambayo haiwezi kuingiliwa na mabeberu anaowategemea katiaka masuala ya ndani,ili mradi hakuna uvunjifu wa sheria za nchi. Hivyo Lazima atii sheria za nchi.
Kamati kuu ya Chadema imechelewa kumdhibiti Lissu kuropoka hovyo na hili limesababisha kuwauzi watanzania na kwa namna moja au nyingine hawatampigia kura yeye na wagombea wengine wa Chadema.
Lissu aliwatukana watanzania kuwa hawajui kiingereza, na inafikia hatua akiwa huko Ubelgiji huwa anaona aibu anaposikia Watanzania wanaongea Kiingereza. Hii ni Lugha mbaya sana kwa mgombea anaeomba kura, kamati kuu ilitakiwa kumdhibiti mapema lakini ilifeli.
Kamati kuu imechelewa kumdhibiti Lissu ili ajikite muda mwingi kunadi sera za chama chake, lakini amekuwa akitoa tuhuma za yeye kupigwa risasi na vyombo vya dola huku rafiki yake Ansbert Ngurumo akitoroka kwenda Ulaya. Lissu alipaswa adhibitiwe na kamati kuu mapema, hizi tuhuma ni mbaya sana, zitamletea matatizo.
Mbaya zaidi ni kuwatukana watumishi wa umma kuwa rais anawaokota majalalani,hili linakwenda kumnyima Lissu na chama chake kura,maana huwezi kuwaita watumishi wa umma kuwa wanaokotwa majalalani huku wewe ukitarajia kuwa boss wao. Kamati kuu imechelewa kumdhibiti Lissu kufahamu namna ya kutumia jukwaa kuomba kura.