Uchaguzi 2020 CHADEMA: Tutaishinda CCM jinsi ilivyo. Ng'ombe huyu mara hii hageuziwi Kibla, anachinjwa alivyolala

Uchaguzi 2020 CHADEMA: Tutaishinda CCM jinsi ilivyo. Ng'ombe huyu mara hii hageuziwi Kibla, anachinjwa alivyolala

"Serikali inayoogopa watu, serikali inayoishi kwa uongo haiwezi kushinda kura. Na mimi niwaambie na hiyo meseji iwafikie. Uchaguzi huu tunaenda hakuna wa kujitoa. Tunaenda tunajua hakuna Tume Huru ya Uchaguzi. Tunajua wanatunga sheria zozote wanazotunga," Mhe. Kigaila, NKMB

Tumeamua tuwaache watunge sheria yoyote. Kusiwe na Katiba au Tume Huru, uchaguzi tunakwenda kushindia kituoni. Wanataka hawataki, watatutangaza. Nani anawadanganya kwamba hamtatangazwa? Toka lini CCM na serikali yake walipanga kuwatangaza wapinzani?," Mhe. Kigaila Benson, NKMB.

Haijawahi kuwa nao, hawana, hawatakuwa nao. Tutawashida hivyohivyo. Ng'ombe huyu mara hii anachinjwa alivyolala. Akilala kifudifudi tunachinja kuanzia mgongoni, akilala kiubavu tunachinja kiubavu. Huyu tunachinja alivyolala. Tutawashinda wanapenda hawapendi," Mhe. Kigaila, NKMB
Endeleeni kukariri!
 
Hamasisheni Wananch wawapigie kura pomoni la sivyo ccm tutawanyoosha na vyombo vyetu vya dollar
 
Hahaha, tatizo CHADEMA imebaki mitandaoni tu huku field hawapo kabisa.
For your iformation CCM vijijini hamna chenu kabisa, kama huamini zama huko au muulize ndgyo akwambie!!
Sukari kijijini Tshs 3200/= kg moja.
Mbaazi ilikuwa Tshs 250,000/= hadi Tshs 300,000/=.
Kwa sasa ni Tshs 50,000/=.
Ni kichaa gani achague watu wa kuwauwa kiuchumi na kihalisia??
Polisi na Watendaji wawasaidie kuiba mabox, vinginevyo mmekwisha!!
 
Serikali za mitaa hamkushiriki sababu hakuna tume huru, ila kwenye huu uchaguzi mnashiriki hivyohivyo?
 
tindo , Salary Slip , Retired , Erythrocyte kama mna kumbukumbu nzuri huu ndiyo ulikuwa ushauri na msimamo wangu kamwe CHADEMA wasisusie uchaguzi na kuwapa washindani wao ushindi kwenye sahani ya fedha (not to give or serve CCM everything on a silver platter).

Kususia uchaguzi Tanzania ni sawa na kujimaliza kisiasa, matokeo tumesha yaona kule Zanzibar na huku Tanganyika kwenye chaguzi za kujaza nafasi kwenye majimbo na udiwani na kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa...
Mawazo yako ni mazuri sana. You have a point to ponder! Kama Kigaila alivyosema jana Serengeti kuwa wataingi katika uchaguzi bila tume huru, Katiba etc kwa vile tangu 1995 hawajawahi kuingia kwenye uchaguzi na ridhaa ya watawala. Akataja very nicely and inspiring mafanikio waliyoyapata katika chaguzi hizo! Lakini kumbuka mazingira yakisiasa ya nyuma NI TOFAUTI KABISA NA SASA! Dictatorship huko nyuma ilikuwa 10% or less!

Leo dictatorship is almost 100%. Kuna uwezekano ikatoka amri kuwa DED wote wawatangaze wagombea wa CCM come whay may! Unafanyaje? Umepata 99% of votes anatangazwa wa NCCR/CCM! Unafanyaje? This is my concern! Unasemaje tindo Salary Slip Erythrocyte
 
For your iformation CCM vijijini hamna chenu kabisa, kama huamini zama huko au muulize ndgyo akwambie!!
Sukari kijijini Tshs 3200/= kg moja.
Mbaazi ilikuwa Tshs 250,000/= hadi Tshs 300,000/=.
Kwa sasa ni Tshs 50,000/=.
Ni kichaa gani achague watu wa kuwauwa kiuchumi na kihalisia??
Polisi na Watendaji wawasaidie kuiba mabox, vinginevyo mmekwisha!!
Mwananchi gani wa kijijini ana shida na hayo masukari?

Hayo makitu mnayapapatikia nyie wa mjini kule kijijini wanajilia vyakula natural siyo hayo matakataka mnayobugia huko mjini na kuishia kulazwa muhimbili.
 
Mawazo yako ni mazuri sana. You have a point to ponder! Kama Kigaila alivyosema jana Serengeti kuwa wataingi katika uchaguzi bila tume huru, Katiba etc kwa vile tangu 1995 hawajawahi kuingia kwenye uchaguzi na ridhaa ya watawala. Akataja very nicely and inspiring mafanikio waliyoyapata katika chaguzi hizo! Lakini kumbuka mazingira yakisiasa ya nyuma NI TOFAUTI KABISA NA SASA! Dictatorship huko nyuma ilikuwa 10% or less! Leo dictatorship is almost 100%. Kuna uwezekano ikatoka amri kuwa DED wote wawatangaze wagombea wa CCM come whay may! Unafanyaje? Umepata 99% of votes anatangazwa wa NCCR/CCM! Unafanyaje? This is my concern! Unasemaje tindo Salary Slip Erythrocyte
Mbowe hawezi kuruhusu kususia uchaguzi, maana anajua hatakuwa na mbunge hata mmoja wa kumpa ruzuku na hivyo atakufa njaa!
 
Hatuna namna kwa hili, lazima watatungaza tu..wakileta za kuleta nikudeal na mtu Kama mtu (DED ) na ikibidi hadi ndg zao kokote waliko

Wakati una deal ma DED utakuwa bado umelewa faru John au itakuwa imekuisha kichwani?
 
Poleni.mmepoteza miaka 5.
Subirini mingine iishe.
1.mkuu wa majeshi anachaguliwa na mwenyekiti wa ccm
2.mkuu wa polisi anachaguliwa na mwenyekiti wa ccm
3.JAJI mkuu n.k anachaguliwa na mwenyekiti wa ccm
4.mwenye kiti wa NEC anachaguliwa na mwenyekiti wa ccm
5.wakurugenzi wa kusimamia uchaguzi wanachaguliwa na mwenyekiti wa ccm
"KAZI KWENU CHADEMA."
 
Watanzania tungekuwa wajanja, huu ndio wakati wa kuwaadhibu Madikteta na watu wengine waliozoea kula migongoni mwetu huku hawafanyi lolote la maana kwa miaka 60 sasa. Jamani tuondokane na ccm!
 
Tutengeneze base ya kura,let's say million moja,tukatumia hiyo base kushawishi wapiga kura kumi kwa wapiga kura milioni.Hapo utaona namna ilivyo rahisi kuwapiga mapema.Wale wapiga kura million moja Mara kumi,wakihakikisha wanahamasisha wapiga kura hats wawili kila moja,halafu tukalinda hizi kura,sioni jinsi watapona.

CHADEMA+ACT Wazalendo wanayo hiyo base,andaeni mikakamikakati ya pamoja.Watanzania Wanataka mabadiliko,tutengeneze mikakati chanya maana ni wepesi kuliko.Wanajimwambafy ila wanafahamu nguvu ya Wananchi.
 
Naomba Makamanda tukashitaki kwa pompeo
Duh hawa watu niwakuonea huruma tuu. Unanikumbusha Kuna mmoja alikimbilia kule WB kuzua pesa za kusaidia elimu kisa kuna jamaa yake kazi yake kuwajaza mimba watoto wa shule, ili kuwaokoa anataka serikali ikubaliane na upuuzi wake wa kufanya shule za tanzania ziwe na cliniki na muda wa kupata break ya kunyonyesha watoto, hii ingekuwa kama drive force ya watoto kuchukulia poa ngono zembe na uvunjifu wa maadili ya utanzania kwa watoto chini ya miaka 18. Hapo hata mimi ninawakubalia makamanda waende kwa pombeo wakashitaki
 
Tatizo walilizalisha upinzani wenyewe,Mh kikwete alitoa baraka zote mchakato wa katiba mpya lakini cha kushangaza wapinzani wakatoka nje ya bunge eti kwa sababu wametofautiana muundo wa serikali,hatimae kukwamisha mchakato.Narudia tena upinzani ndo tatizo
 
Kweli kabisa! Kuliko CCM ichukue ushindi mezani bora kupambana nayo.Ni vizuri kushiriki uchaguzi ili wakiiba wajulikane wameshinda kwa wizi.
 
Serikali inayoogopa watu, Serikali inayoishi kwa uongo haiwezi kushinda kura. Na mimi niwaambie na hiyo meseji iwafikie. Uchaguzi huu tunaenda hakuna wa kujitoa. Tunaenda tunajua hakuna Tume Huru ya Uchaguzi. Tunajua wanatunga sheria zozote wanazotunga," Mhe. Kigaila, NKMB

Tumeamua tuwaache watunge sheria yoyote. Kusiwe na Katiba au Tume Huru, uchaguzi tunakwenda kushindia kituoni. Wanataka hawataki, watatutangaza. Nani anawadanganya kwamba hamtatangazwa? Toka lini CCM na serikali yake walipanga kuwatangaza wapinzani?," Mhe. Kigaila Benson, NKMB.
Hizi ndizo kauli za kutoa kwa sasa. Masuala ya kubembelezana wakati watu hawataki ustaarabu hapana. Na kwa hii kauli naona CHADEMA imejipanga vilivyo kupambana na mazingira waliyopo. Kwa staili hii uchaguzi huu wa oktoba 2020 utakuwa mgumu sana
 
Mwananchi gani wa kijijini ana shida na hayo masukari?

Hayo makitu mnayapapatikia nyie wa mjini kule kijijini wanajilia vyakula natural siyo hayo matakataka mnayobugia huko mjini na kuishia kulazwa muhimbili.
We jamaa kwani wananchi wa kijijini wasipende sukari wamekua mazuzu mbona humewadhalilisha ndugu zetu wa kijijin?not fair
 
Back
Top Bottom