Uchaguzi 2020 CHADEMA: Tutaishinda CCM jinsi ilivyo. Ng'ombe huyu mara hii hageuziwi Kibla, anachinjwa alivyolala

Uchaguzi 2020 CHADEMA: Tutaishinda CCM jinsi ilivyo. Ng'ombe huyu mara hii hageuziwi Kibla, anachinjwa alivyolala

Tutengeneze base ya kura,let's say million moja,tukatumia hiyo base kushawishi wapiga kura kumi kwa wapiga kura milioni.Hapo utaona namna ilivyo rahisi kuwapiga mapema.Wale wapiga kura million moja Mara kumi,wakihakikisha wanahamasisha wapiga kura hats wawili kila moja,halafu tukalinda hizi kura,sioni jinsi watapona.
CDM+ACT Wazalendo wanayo hiyo base,andaeni mikakamikakati ya pamoja.Watanzania Wanataka mabadiliko,tutengeneze mikakati chanya maana ni wepesi kuliko.Wanajimwambafy ila wanafahamu nguvu ya Wananchi.
Nadhani hiyo base ilitakiwa iwepo mpaka sasa, kura milioni moja itawezekana but someone can prove vipi him/herself kwamba tayari huo mtaji wa milioni moja upo kibindoni?!

Issue hapa ni watu wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura, hiki ndio kitu CCM hawakipendi wanajua vzr kabisa majority ya wananchi hawako upande wao ndio maana siku zote wanaegemea msaada wa polisi na tume.

Hivyo, hapa kwa mtazamo wangu, ni kuhamasishana wakati wa kwenda kupiga kura, watu wajitokeze kwa wingi, tayari mchezo utakuwa umekamilika.

Uchache wa wapiga kura ndio unaosababisha CCM wafurahie km ilivyotokea kwenye serikali za mitaa, but this time, provided vyama vikubwa vimeshasema vitashiriki uchaguzi, situation will be completely very different compared to serikali za mitaa.

Haya makelele ya hamtatangazwa washindi yapuuzwe, ni kama wanacheza "mind games" kukatisha tamaa wapiga kura wasijitokeze kwa wingi kwenda vituoni hiyo siku ikifika, kwasababu wanapenda watu wachache wajitokeze vituoni.
 
CCM huwà wanawalisha wapiga kura yamini(nipo tayari kusahihishwa),nilikuwa nina maanisha kitu cha aina hiyo(Base) ya waadilifu wa mabadiliko.

Nakubaliana nawe kwamba hiyo base ilitakiwa iwepo tayari, sawa kabisa,tule yamini wapiga kura milioni moja wanaoenda kuupigia upinzani kura, hao milioni moja kila moja akahakikisha angalau wapiga kura kumi na hao kumi nao wakifanya hivyo,CCM itakuwepo?

Hivyo naungana nawe kuhusu kujitokeza kwa wingi siku ya upigaji kura,lakini tujipange kwa wingi wetu,bila hivyo tunaenda kufanya nini kama hatuna lengo?

Lengo letu ni kuwa "Tunaenda kumpiga mkoloni mweusi chini kwenye sanduku LA kura,tunazilinda na kuhakikisha zinatangazwa kihalali bila kutishiwa".

Tuone umahiri wao wa kuiba,hawawezi maana ni wepesi.Umoja ni Nguvu.
 
Hahahahah! Mnachekesha, kushiriki si ndo kuuhalalisha uchaguzi wenyewe
 
tindo , Salary Slip , Retired , Erythrocyte kama mna kumbukumbu nzuri huu ndiyo ulikuwa ushauri na msimamo wangu kamwe CHADEMA wasisusie uchaguzi na kuwapa washindani wao ushindi kwenye sahani ya fedha (not to give or serve CCM everything on a silver platter).

Kususia uchaguzi Tanzania ni sawa na kujimaliza kisiasa, matokeo tumesha yaona kule Zanzibar na huku Tanganyika kwenye chaguzi za kujaza nafasi kwenye majimbo na udiwani na kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa...

Labda watu waambiwe waende na silaha ili kulinda matokeo, maana tume ya uchaguzi na vyombo vya dola haviaminiki. Kinyume na hapo, vyama vya upinzani vishiriki ili kwenda kubariki huo uhuni, lakini sio kutegemea kutangazwa.
 
Chadema wanawaanda tu wafuasi wao ili wakishindwa wapate sababu
Kama unaona mazingira sio mazuri,usiingize timu,lakini ukiweka wagombea maana yake unaamini utashinda kwa tume hiyo.hiyo,tusidanganyane
Hawa siyo wa kuwaacha. Nchi siyo yao pekee yao. CHADEMA waingie kwenye uchaguzi. Anayeharibu process kwenye hatua yoyote, adhabu yake ipatikane hapo hapo alipo.

Ikifanyika hivyo, baada ya muda watazingatia taratibu.

Hata huko kuliko na demokrasia na haki, havikuletwa kwenye bakuli bali wadhulumaji walilazimishwa na wananchi.

Tuna wajibu wa kuilazimisha Tume ya Ucjaguzi itende haki. Tuna wajibu wa kuwalazimisha wakurugenzi wa Wilaya kuwatangaza walioshinda, wapende wasipende.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya maneno, natamani wayatimize. Makamanda wanaweza kuwa wanaongea tu
 
Hakuna chama Cha kuishinda CCM,hakuna wa kushinda uchaguzi zaidi ya mgombea wa CCM, hajazaliwa bado
 
Wanadai propaganda ni muhimu sana. Huyu bwana akifeli siasa akiwa motivation speaker atavuna mpunga hatare
 
Policcm wasisahau ku-update nyenzo zao za kupiga risasi juu halafu igeuke chini kama ilivyokuwa Kinondoni
 
Hatuna namna kwa hili, lazima watatungaza tu..wakileta za kuleta nikudeal na mtu Kama mtu (DED ) na ikibidi hadi ndg zao kokote waliko
Ni vema wakalijua hilo kungali mapema, wasije wakasema hawakujua.

Hii kazi wanayoifanya ni ya kufa na kupona, wasijifanye hawalijui hili. Kazi hii ni hatma ya Tanzania yote.
 
Nimemuelewa.

Kusubiri fadhila kutoka CCM ni kupoteza muda, na kususia uchaguzi hakusaidii kama ilivyoonekana kwenye serikali za mitaa.

Dawa ni kwenda kushindana nao huko huko kwenye vyumba vya majumuisho ya kura na kumtangaza mshindi, mbivu na mbichi zijulikane hukohuko, atakaekubali haki yake kunyan'ganywa afanye hivyo, but atleast not without a fight.

Sometimes haki inatafutwa, huletewi kwenye sahani.
Kama wapinzani wamelitambua hili, na wamedhamiria kulisimamia vyema, basi twende tukapige kura bila ya kinyongo.

Wale wote wanaoamini "Nikulipe mshahara, nikupe gari.....," ni muhimu zaidi kwao, itabidi pia watambue kuwa safari hii ni zaidi ya hivyo vitu wanavyoahidiwa.

Their actions will have consequences.
 


"Serikali inayoogopa watu, serikali inayoishi kwa uongo haiwezi kushinda kura. Na mimi niwaambie na hiyo meseji iwafikie, uchaguzi huu tunaenda hakuna wa kujitoa. Uchaguzi huu tunaenda, tunajua hakuna Tume Huru (ya Uchaguzi).

Tunajua wanatunga sheria zozote wanazotunga. Tumeamua tuache watunge sheria yoyote, kusiwe na Katiba, kusiwe na Tume Huru, uchaguzi tunakwenda kushindia kituoni. Wanataka hawataki, watatutangaza.

Nani anawadanganya kwamba hamtatangazwa? Toka lini CCM na serikali yake, toka lini walikuwa na mpango wa kuwatangaza wapinzani? Haijawahi kuwa nao, hawana, hawatakuwa nao. Tutawashida hivyo hivyo.

Ng'ombe huyu mara hii anachinjwa alivyolala, akilala kifudifudi, tunachinja kuanzia mgongoni. Akilala kiubavu, tunachinja kiubavu. Huyu tunachinja alivyolala. Tutawashinda wanapenda hawapendi."

Mhe. Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu Chadema, Bara.

Ni ujumbe mzito na sahihi na kwa wakati sahihi.
 
Serikali za mitaa hamkushiriki sababu hakuna tume huru, ila kwenye huu uchaguzi mnashiriki hivyohivyo?

Ng'ombe huyu mara hii anachinjwa alivyolala, akilala kifudifudi, tunachinja kuanzia mgongoni. Akilala kiubavu, tunachinja kiubavu. Huyu tunachinja alivyolala. Tutawashinda wanapenda hawapendi."- Benson Kigaila
 
Ng'ombe huyu mara hii anachinjwa alivyolala, akilala kifudifudi, tunachinja kuanzia mgongoni. Akilala kiubavu, tunachinja kiubavu. Huyu tunachinja alivyolala. Tutawashinda wanapenda hawapendi."- Benson Kigaila
Kigaila anajifanya mangi mkuu, Chadema wangeendelea kusimamia misingi wangefika mbali ila saiv hamna kitu
IMG-20200621-WA0001.jpg
 
Uchagyzi huu upinzani ni kutafuta ruzuku tu. Lakini hakuna mwaka ambao upinzani nilegelege kama 2020 . Oyaoya ilikuwa 2015 au kipindi cha Dr slaa au 1995 NCCR mageuzi ya Mrema labda wajipange 2025
 


"Serikali inayoogopa watu, serikali inayoishi kwa uongo haiwezi kushinda kura. Na mimi niwaambie na hiyo meseji iwafikie, uchaguzi huu tunaenda hakuna wa kujitoa. Uchaguzi huu tunaenda, tunajua hakuna Tume Huru (ya Uchaguzi).

Tunajua wanatunga sheria zozote wanazotunga. Tumeamua tuache watunge sheria yoyote, kusiwe na Katiba, kusiwe na Tume Huru, uchaguzi tunakwenda kushindia kituoni. Wanataka hawataki, watatutangaza.

Nani anawadanganya kwamba hamtatangazwa? Toka lini CCM na serikali yake, toka lini walikuwa na mpango wa kuwatangaza wapinzani? Haijawahi kuwa nao, hawana, hawatakuwa nao. Tutawashida hivyo hivyo.

Ng'ombe huyu mara hii anachinjwa alivyolala, akilala kifudifudi, tunachinja kuanzia mgongoni. Akilala kiubavu, tunachinja kiubavu. Huyu tunachinja alivyolala. Tutawashinda wanapenda hawapendi."

Mhe. Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu Chadema, Bara.
Kigaila atakuwepo mstari wa mbele wakati wa hayo mapambano au anataka kufanya wenzie wajinga!?
 
Back
Top Bottom