Uchaguzi 2020 CHADEMA: Tutaishinda CCM jinsi ilivyo. Ng'ombe huyu mara hii hageuziwi Kibla, anachinjwa alivyolala

Uchaguzi 2020 CHADEMA: Tutaishinda CCM jinsi ilivyo. Ng'ombe huyu mara hii hageuziwi Kibla, anachinjwa alivyolala

CCM huwà wanawalisha wapiga kura yamini(nipo tayari kusahihishwa),nilikuwa nina maanisha kitu cha aina hiyo(Base) ya waadilifu wa mabadiliko...
Kuhusu CCM kuwalisha wapiga kura wao yamini sifahamu, lakini tukitazama hali halisi field, kama hauna uungwaji mkono na walio wengi habari ya kulisha watu yamini inakuwa haina maana, ndio maana bado wanakimbilia msaada wa polisi na tume.

Hapo kwa Chadema hali ni tofauti, kama unaouungwaji mkono wa kutosha, ni suala tu lakuwahamasisha hao watu wajitokeze kwa wingi kwenda kuliga kura na wajue wanamchagua nani, baada ya hapo ndio inafuata part ngumu kidogo ya kuzihesabu kura na kumtangaza mshindi.

Hapa napaita pagumu kwasababu mpinzani akizubaa kidogo hata kama ana kura za kutosha anapotezwa, hili lilimtokea mgombea wa ubunge Chadema, Musoma Mjini - Vicent Nyerere, hivyo hapa ndipo mahala pa kujipanga zaidi.

The rest tuko pamoja.
 
Kama wapinzani wamelitambua hili, na wamedhamiria kulisimamia vyema, basi twende tukapige kura bila ya kinyongo.

Wale wote wanaoamini "Nikulipe mshahara, nikupe gari.....," ni muhimu zaidi kwao, itabidi pia watambue kuwa safari hii ni zaidi ya hivyo vitu wanavyoahidiwa.

Their actions will have consequences.
Sure.

Hapa ni vyema wapinzani wakafuta kwenye akili zao wazo la kutotangazwa washindi hata kama wameshinda, ile ni mbinu iliyotengenezwa kutuvunja moyo, na bahati mbaya wengi wetu tukaanza kuiimba kila siku kwamba hata kama tukishiriki tukashinda uchaguzi wataiba, hili sio kweli.

Let's give them a simple examination, twende tukapige kura za kutosha, halafu tuone jinsi watakavyogoma kumtangaza mpinzani mshindi, here, there must be pressure from different angles, to stop them performing their irregularities.

Lakini pia, huu uchaguzi wengi watakuwa majimboni kwao, hivyo lile suala la RC, DC, na RCO wote kujazana chumba cha kuhesabia kura halitakuwepo, hivyo chance ya wapinzani ipo kubwa tu, muhimu wajipange kikamilifu.
 
Yale Yale ya uongo uongo miaka yote wapinzani bungeni huwa wanafikafikaje? hizi siasa za majitaka ni Kama Msigwa alivyomchafua Kinana kisha akasema alikuwa amsingizia
 
Sure.

Hapa ni vyema wapinzani wakafuta kwenye akili zao wazo la kutotangazwa washindi hata kama wameshinda, ike ni mbinu iliyotengenezwa kutuvunja moyo, na bahati mbaya wengi wetu tukaanza kuiimba kila siku kwamba hata kama tukishiriki uchaguzi wataiba, hili sio kweli.

Let's give them a simple examination, twende tukapige kura za kutosha, halafu tuone jinsi watakavyogoma kumtangaza mpinzani mshindi, here there must pressure from different angles, to stop them performing their irregularities
Tujitokeze wapiga kura wenye sifa tukiwa na vichinjio vyetu,tunaenda kuwashangaza CCM. Hawawezi kuiba kura zetu tukizisimamia na kizilinda wanatoka na hivyo watupishe tumewachoka kama walivyotuchoka.Hawajali hata uhai wa raia na bado wanataka madaraka.
Uongozi umewashinda wamebakiwa na mabavu.Ole wao wasitangaze washindi halali waliochaguliwa na Wananchi.
 
Mwanamke umeolewa na ikifika usiku unaleta masharti. Ikifika usiku toa pichu na ulale watu wastarehe, Eti ngo'mbe atachinjwa atakavyo lala, sema burdani itapatikana tuu na wewe utachagua unalalaje. Chadema kweshnei 2020.
 
CCM itashinda milele na milele hata mwisho wa dunia,hamtuwezi mnatuogopa nyie ni wanaume ila sio vidumee poleni na mtajidai ili muonekane mmeshindwa kabla ya uchaguzi mkuu wenu freeman mbowe amelewa mpaka akadondoka chini akavunja mguu akiwa na watu ambao sio mke wake . Kalewa chakari hii ni aibu kwenu doa la uchaguzi eti ndio tumchague kuwa nani raisi au nani?

Tuambizane eti serikali ya sasa ni yauongo ipi mliwahi ona ni wakweli. Nanani kakuambia kuwa nyie wa kweli. Nyie sio wa kweli hata kidogo mbowe aliahidi watu wake katika jimbo lake huko moshi kuwa atawafanyia vitu na hadi leo imebaki tu empty hata wananchi hawajasaidiwa.
 
Jifariji bro

MÊmENtO HoMO

jamaa ana pointi, chadema haikubaliki hata kidogo, ukitaka kuprove hilo tafuta video yoyote ambayo magufuli yupo haswa ikiwa live stream, yaani cdm nawshauri mkajipange tu upya! Hata mbowe mwenyewe alishakataliwa jimboni kwaker kitambo!

 
Mwananchi gani wa kijijini ana shida na hayo masukari?

Hayo makitu mnayapapatikia nyie wa mjini kule kijijini wanajilia vyakula natural siyo hayo matakataka mnayobugia huko mjini na kuishia kulazwa muhimbili.
Bila Shaka Wewe Ni Mpumbavu kama wazee wako hawana haja na sukari na umeshndwa kuwanunulia.
 
Nimemuelewa.

Kusubiri fadhila kutoka CCM ni kupoteza muda, na kususia uchaguzi hakusaidii kama ilivyoonekana kwenye serikali za mitaa.

Dawa ni kwenda kushindana nao huko huko kwenye vyumba vya majumuisho ya kura na kumtangaza mshindi, mbivu na mbichi zijulikane hukohuko, atakaekubali haki yake kunyan'ganywa afanye hivyo, but atleast not without a fight.

Sometimes haki inatafutwa, huletewi kwenye sahani.

bora ata msiende khesabu kura maaana mtaaibika vibaya sana!
 
Hatuna namna kwa hili, lazima watatungaza tu..wakileta za kuleta nikudeal na mtu Kama mtu (DED ) na ikibidi hadi ndg zao kokote waliko
Madogo mnajuaga kutishia na kujiliwaza! Muda wenyewe ukifika, utasikia, oh, Serikali ilitumia nguvu kubwa! Pumbavu!
 
Quinine,
Mh, nachelea kusema kuwa akiamua kutangaza anayempenda unafanyaje? Tulifikirie kwa mapana na marefu! Watafanya hivyo kama serikali za mitaa. Quinine unalionaje hili?
Mara hii wakati wao wako kwenye kupika data sisi tunazizunguka nyumba zao wote wanaoshiriki ditectly au indirectly kwenye dhulma hii wakiwemo policcm!
 
Uko sahihi mheshimiwa. Naona mazingira yaliyotawala uchaguzi wa serikali za mitaa yatajirudia. Wagombea wa vyama vya upinzani makini hawatapitishwa na Tume ya Uchaguzi kwa visingizio mbalimbali.

La sivyo wakishinda kwenye sanduku la kura hawatatangazwa washindi. Hii tayari imesukwa ndani ya taratibu mpya ya maadili ya uchaguzi ambayo wapinzani walishurutishwa kutia saini (wawakilishi wa vyama kwenye kituo cha kupigia kura kutopewa nakala ya matokeo).
Mwenye akili timamu anajua ni namna gani CDM ilivyo na wakati mgumu kupata idadi kubwa ya viti bungeni mpaka kura za mgombea Urais, kwa sehemu kubwa Tundu Lissu atafufua mioyo ya watu lakini kwa sababu ulizozitaja hapo ni ngumu yeye kushinda.

Hamna namna ya kutiana moyo ktk hili.
 
tindo , Salary Slip , Retired , Erythrocyte kama mna kumbukumbu nzuri huu ndiyo ulikuwa ushauri na msimamo wangu kamwe CHADEMA wasisusie uchaguzi na kuwapa washindani wao ushindi kwenye sahani ya fedha (not to give or serve CCM everything on a silver platter).

Kususia uchaguzi Tanzania ni sawa na kujimaliza kisiasa, matokeo tumesha yaona kule Zanzibar na huku Tanganyika kwenye chaguzi za kujaza nafasi kwenye majimbo na udiwani na kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa...
Ubaya ni kuwa JF ukizungumza kitu negative utaonekana unatumiwa na CCM lakini kiuhalisia sivyo.

Kuna mambo yanayoendelea CHADEMA yaani mtu unaona kabisa huu ni uwendawazimu.

Wanaosema Mbowe aachie kiti wana sababu za msingi saana, chama kifight kwa ajili kuchukua dola na sio kutazama maslahi ya kifedha.
 
Mjitoe bana mbona serikali za mtaa mliweza kwa nini huku mkomae au ndo maslahi binafsi?!
Dah...nani ajitoe? Tumeisha sema safari hii ng'ombe anachinjwa jinsi alivyolala...hatumgeuzii kibla [emoji41]
 
Mawazo yako ni mazuri sana. You have a point to ponder! Kama Kigaila alivyosema jana Serengeti kuwa wataingi katika uchaguzi bila tume huru, Katiba etc kwa vile tangu 1995 hawajawahi kuingia kwenye uchaguzi na ridhaa ya watawala. Akataja very nicely and inspiring mafanikio waliyoyapata katika chaguzi hizo! Lakini kumbuka mazingira yakisiasa ya nyuma NI TOFAUTI KABISA NA SASA! Dictatorship huko nyuma ilikuwa 10% or less!

Leo dictatorship is almost 100%. Kuna uwezekano ikatoka amri kuwa DED wote wawatangaze wagombea wa CCM come whay may! Unafanyaje? Umepata 99% of votes anatangazwa wa NCCR/CCM! Unafanyaje? This is my concern! Unasemaje tindo Salary Slip Erythrocyte
Kuna mdau hapo amesema itatumika Samson option yani tukose wote itakula kwa wote watakaoshiriki hujuma na dhuluma ndugu wa hao maded wake zao na watoto wao watakuwa hatarini tusifike huku.
 
"Serikali inayoogopa watu, Serikali inayoishi kwa uongo haiwezi kushinda kura. Na mimi niwaambie na hiyo meseji iwafikie. Uchaguzi huu tunaenda hakuna wa kujitoa. Tunaenda tunajua hakuna Tume Huru ya Uchaguzi. Tunajua wanatunga sheria zozote wanazotunga," Mhe. Kigaila, NKMB

Tumeamua tuwaache watunge sheria yoyote. Kusiwe na Katiba au Tume Huru, uchaguzi tunakwenda kushindia kituoni. Wanataka hawataki, watatutangaza. Nani anawadanganya kwamba hamtatangazwa? Toka lini CCM na serikali yake walipanga kuwatangaza wapinzani?," Mhe. Kigaila Benson, NKMB.

"Haijawahi kuwa nao, hawana, hawatakuwa nao. Tutawashida hivyohivyo. Ng'ombe huyu mara hii anachinjwa alivyolala. Akilala kifudifudi tunachinja kuanzia mgongoni, akilala kiubavu tunachinja kiubavu. Huyu tunachinja alivyolala. Tutawashinda wanapenda hawapendi," Mhe. Kigaila, NKMB.
Miaka yote ishirini na tamo mnashiriki uchaguzi, mlikuwa mnashinda na kupata madiwani na wabunge. Leo 2020 ndio mlete kisingizio tume sio huru?
 
Back
Top Bottom