Tumejaza kwenye chama wafuasi na wanachama wahuni wahuni ambao wanamatusi na hawana uwezo wa kujenga hoja.
Tuwekeze kama ilivyokuwa Nccr mageuzi. Tuwe na wasomi na watu wenye vision kubwa.
Maana wasomi ni watu wenye busara. Sio kama hawa wahuni na wapayukaji.
Unaweza kuwa na hoja lakini namna ya kuiwasilisha kumeharibu maudhui nzima,
kwanini nasema hivyo?
1. Jiulize swali hili,je ni kweli wabunge na viongozi walioisaliti CDM na kujiunga ccm kwa ajili ya maslahi binafsi walikuwa si wasomi?
2. Je ni kweli watu wote wasio na elimu ya juu tulionao mitaani na makazini,wanatenda bila busara?
3. Yupi bora kati ya msomi msaliti na asiyesoma ila ana moyo wa kizalendo na ana uwezo wa kufanyia kazi kwa uaminifu maelekezo anayopewa?
Muda si rafiki nina mengi ya kuhoji ila niishie hapa.
Nimalizie kwa nukuu ya mwalimu Nyerere juu ya askari alisema '' Afadhari kuwa na taifa ambalo,lisilo na silaha za kisasa lakini,lenye moyo wa kishujaa kuliko kuwa na taifa lenye silaha za kisasa lakini vijana wake ni waoga''
Ningeishauri CDM kusajili vijana wenye moyo wa kishujaa wanaoelewa lengo la chama na uelekeo wake
kuliko wasaka tonge kwa mwavuli wa usomi.
HERI YA MWAKA MPYA 2022