CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

Hili Swali nilielekeze kwa Mzee Mwanakijiji maana anaweza kutupa maelezo ambayo yanaweza mwanga kidogo..

Ni kwanini Dr. Slaa alimkaribisha Lowassa Chadema?

Sidhani kama hili ni swali sahihi; kama nijibu nadhani alilitoa mwenyewe na linaeleweka. Lakini kwamba "alimkaribisha" inadhania mambo mengi sana. Rejea majibu yake jinsi gani Lowassa aliomba kuingia lakini pia usisahau kuwa ushahidi mkubwa uliopo ni kuwa tayari Lowassa alishaanza dili ya kutaka kuingia CDM mapema sana kabla ya kukatwa CCM na mtu mhusika mkubwa hakuwa Slaa katika hili. Kimsingi hata kile kinachoitwa "kupitishwa" kwa Slaa kugombea ilikuwa ni geresha tu kwani kuna waliokuwa wanajua mapema dili wanalotaka kuchezewa lichezwe vipi. Slaa alikuwa ni chaguo lao la pili; chaguo lao la kwanza tunalijua sasa.
 

Mzee Mwanakijiji;

Nilifuatilia maoni yako mara baada ya uteuzi wa Magufuli. Katika uchambuzi wako ulionyesha kuwa moja ya tatizo la UKAWA kukosa kumpata mgombea mapema lilikuwa CUF. Lakini kutokana na maendeleo ya sasa inaonyesha kuwa CDM yenyewe pia ilikuwa na mikakati ya kuchelewesha. Hivyo makubaliano ya nani agombee yalikuwa sio maamuzi ya Dr. Slaa, Prof. Lipumba na Makaidi, badi kama unavyosema mhusika mkuu.

Moja ya swali linalokuja ni hili. Lowassa hajawahi kufanya kampeni bila kutumia pesa. Hiki ni kitu kinachoeleweka. Je tiketi ya CDM aliipata bure? Kama hajaipata bure, inaonyesha kuwa watanzania tunapenda kubakwa kisiasa na wengine wanafurahia hicho kitendo.
 


Alinda;

Pesa na madaraka yanafanya watu wasalitiane. Nimemsikiliza Dr vizuri. Na kwa maoni yangu binafsi, watu wamezidiana. Hili sio swala la kumleta Lowassa ndani ya CDM. Kuna watu wamefaidika na siku zinavyokwenda tutakuja kuyasikia zaidi.
 
Mkuu sikuelewi kabisa unachotaka kusema. Unasema hakuna mahala Dr.Slaa amejadiliwa? hivi kweli una hakika na unayoyaandika au basi tu kutaka nifanya miye nmjinga saaana sijasoma hoja za watu kabla sijaandika hoja yangu. Mtu unaweza anzisha hoja maadam ipo katika misingi ile ile.

Nakuomba rudi nyuma page chache tu, utaona kila mtu anamzungumzia tukio hili la Dr.Slaa na maamuzi yake kukutana na waandishi wa habari na kusema UKWELI. Huo ukweli ndio hoja wapo walouchambua kwa mitazamo yao wengiine wakiunganisha hotuba ya Tundu Lissu ama walichokijua wao..Sasa imekuwaje kati ya watu woote hawa umechagua miye kuwa nilichoandika siko fair na sipingani kwa hoja! Nipingane na nani? ama ni vizuri kueleza nachokielewa mimi badala ya kupingana..

Mimi nilichoandika hapo juu ni UKWELI ambao watu kama wewe hamtaki watu wengine waujue kwa sababu ya interest zenu na hakuna mahala namzungumzia mtu ama mwandishi yeyote humu. Sijakutaja jina lako na wala sina sababu japo nakusoma mwendo wako wa kulazimisha watu wakufuate wewe kwa sababu tu ni mwanzilishi wa mafa.. Miye sio msulkule naandika nachokiona ni kwa faida ya Watanzania wenzangu wanaotaka kujua ukweli.

Wewe kazi yako kubwa siku zote ni kunichambua mimi ukaacha hoja. Sasa anayepingana bila hoja nani kama si wewe ulogeuza hoja kuwa ni mimi. Kuna mahala nimekuzungumzia wewe au mtu yeyote aloandika nikaacha hoja yake na kuanza mzungumzia yeye? tabia hii ni yako wewe na hujui kujadiliana na watu isipokuwa kwa wale wanaokuunga mkono. Ukipingwa kwa hoja utaanza kumjadili alokupinga!

Ukweli utabakia kwamba Chadema wamechemsha na uongo hautawafikisha popote wanazidi kujisiliba nya kwa sababu sisi wengine hufuatilia issues na sina sababu ya kufanya uchunguzi wa event ilokwisha tokea kwa sababu UKWELI haufanyiwi uchunguzi!. Mwezi July, kweli wapo walosema uamuzi wake uheshimiwe, lakini hawakumsoma mwenyewe akilalamika na kuomba Ulinzi twitter isipokuwa kudanganya watu kwamba yuko likizo!

Na hata alipotoa maelezo yake na kulalamika kule twitter kwa kutishiwa maisha yake Aug 3, akaomba Usalama ili alindwe hakutokea mtu yeyote hapa wala Chadema alosema kitu ama kukana habari ile isipokuwa wali hack ukurasa wake na kumweka Lowassa. Yericko Nyerere alinambia aloandia hayo sio yeye (Dr.Slaa) bali ni mkewe Josephine na watu wengi wakaamini hivyo. Je, mlifanya uchunguzi wakati ule? ama ni baada ya kujitokeza juzi kama alivyoahidi Twitter mwezi jana na UKWELI sasa tumeujua!..

Sasa haya ndio mafuriko nambayo hayawezi kuzuiwa kwa mikono na kama kawaida mafuriko ni kazi ya Mungu! Fitna, majungu na hiyana mwisho wake ndio kama huu..
 

Naomba turejee kwenye kauli ya leo ya Mbatia.
Kama Dr. Slaa alikuwa chaguo la pili kwanin alikataa kutangazwa na Mbatia ile siku waliowawekesha waandishi wa habari? Akataka asubiri mbwembwe?
Tundu lisu amesema wazi kuwa Dr. Slaa alikuwa ameshachaguliwa mwezi wa kwanza akathibitishwa na chama mwezi wa nne. Mwezi wa tano the same Slaa akaanzisha mazungumzo na Lowasa.
Sasa alianzisha mazungumo na Lowasa ili aje kuwa mwanachama wa kawaida au apeperushe bendera?
Hapa hatujapewa jibu.
 
hebu twende taratibu bila jazba.. Ni nani aliyemleta Lowassa Chadema? na kwanini?
Alomleta Lowassa Chadema siwezi kumjua zaidi ya mhusika mwenyewe isipokuwa nasema hawezi kuwa Dr.Slaa kwa maelezo ya Tundu Lissu kwa sababu katika maelezo yake uongo umejitenga wazi kabisa..

1. Mimi nilipokuwa Bongo mwezi November na December mwaka jana nilipata habari hizo sikutaka kuzizungumza hapa kijiweni kwa sababu zilikuwa tuhuma tu. Miezi ilivyopita nikasikia habari mpya kuwa ataenda ACT sio Chadema na ndiye mfadhili wa safari zao.. Nikayaacha kama yalivyo nikisubiri UKWELI ni upi.

2. Hapa hapa JF ilikuwepo mjadala kuhusu Lowassa kuhamia Chadema toka mwaka 2011 kama hatachaguliwa CCM tukazipuuza kwahiyo haikuwa habari mpya. Lissu anaposema kwamba ni Dr.Slaa aliyemleta Lowassa ni uongo kwa sababu nyingi tu za msingi na nimezisema hapo nyuma. a) Haiwezekani mtu alochaguliwa kugombea Urais na kamati kuu ama baraza kuu ajichukulie maamuzi binafsi ya kumtafuta mtu mwingine nje ya chama aje kugombea badala yake hali yeye kisha pitishwa! - Haiwezekani.. Hata wewe leo hii ukichaguliwa kuwa mbunge wa Ilala na umepitishwa huwezi tena kufanya maajabu aloyasema Tundu Lissu na zaidi ya hapo Dr.Slaa na Lowassa ni Mbwa na Chatu! Ningekubali tu kama Tundu Lissu angesema Dr.Slaa amechukia baada ya Kamati ya Chadema kumchagua, lakini ujio wa Lowassa tulimwambia akae pembeni Lowassa atasimama badala yake..

3. Muda aloutaja Tundu Lissu kwamba Dr.Slaa ndio alituma ujumbe, wakati huo Lowassa alikuwa bado hajatoswa CCM, Lowassa alikuwa tumaini la wajumbe wengi wa CCM kuliko mgombea mwingine yeyote na hata yeye mwenyewe alijua atashinda na hakuna wa kumzuia, leo iweje akubali mazungumzo ya kuhamia Chadema hata kabla ya uchaguzi wa ndani wa CCM? Kisha kwa sisi tunaomjua Lowassa huyu mtu ana guts za ajabu, anajiamini kupita kiasi na kwamba anachokifikiria ni lazima kipatikane kwa nguvu zozote zile. Kutoswa CCM ilikuwa pigo kubwa sana ambalo hakulitegemea kabisa. Lowassa alikataa ushauri wa wapambe wake ndani ya CCM kuweka Plan B ikiwa ataenguliwa. Na ndivyo alivyoingia UKAWA akaweka masharti kaa atajiunga Chadema awe mgombea na pasipo ushindani. hili ndio mimi nadhani lilowaondoa Dr.Slaa na Lipuymba UKAWA..

Ni hayo tu... siwezi kwenda taratibu mahala ambapo mnataka kunibana katika jambo ambalo hata nyie wenyewe hamjui nani alomleta Lowassa isipokuwa kwa kuwasoma waongo, wafitini wenye kuwa na kila sababu kila jambo bana wanapolifanya. Uongozi wa kamati kuu Chadema wamekuwa na maamuzi mabaya sana na haya yote yanatokana roho mbaya za vaadhi ya viongozi wenyewe.
 
Mkuu GalaxyS3

Ninashukuru kwa bandiko lako namba #448 kwa sababu limewakilisha kwa kiwango kikubwa fikra na mtazamo wangu.

Hoja za Dk. Slaa zinaonyesha hakutaka Lowassa awe mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA kutokana na masharti aliyoyatoa katika vikao. Ikumbukwe Lowassa asingejiunga CHADEMA au chama chochote ili awe mwanachama wa kawaida bali awe mgombea Urais.

Kama alivyosema GalaxyS3, masharti aliyoweka Dk. Slaa alifahamu Lowassa hawezi kuyatimiza na kwa msingi huo, angeshindwa na kama ingelazimishwa basi angejiudhuru.

Siwezi kufahamu kwa sasa kama aliweka masharti hayo kwa sababu ya kinyongo kwamba Lowassa atachukua nafasi aliyopewa yeye kama mgombea Urais kwa tiketi ya UKAWA lakini ninachofahamu, msingi wa ukuaji wa CHADEMA (ufisadi) na historia ya Lowassa na CHADEMA unabeba hoja/sababu ya uwepo wa masharti aliyotoa Dk. Slaa.

Hoja ya nani alianzisha mawasiliano na Lowassa ni vigumu kufahamu kwa kutumia hoja zilizoko kwa sasa mezani lakini nasaba na historia ya Dk. Slaa inanieleza hawezi kuanzisha mawasiliano kwa sababu ni mtu anayefanya siasa kama personal. Hata maelezo yake mengine kuhusu ''uozo'' wa Lowassa, Sumaye, Msindai na Masha yanaonyesha kimantiki alivyokuwa anapinga ujio wa Lowassa tokea mwanzo.

Gazeti la RaiaMwema la tarehe 12 Aug 2015 limegusia kuhusu ujio wa Lowassa uliopelekea kuchelewesha kumtangaza mgombea Urais kwa tiketi ya umoja wa UKAWA ambaye kwa maelezo ya Prof. Lipumba alikuwa ni Dk. Slaa kwa kumnukuu Dk. Emmanuel Makaidi akisema,
Kwa kiwango kikubwa pia ninaweza kukubaliana na fikra za Zakumi katika bandiko lake la #463 anaposema inawezekana Mbowe na Dk. Slaa walizidiana kimaslahi.

Mbowe aliposema Dk. Slaa yuko likizo alikuwa anatumia lugha ya kidiplomasia akifahamu labda Dk. Slaa atabadilisha uamuzi wake. Ndio maana tuliona jinsi ambavyo viongozi mbali mbali na wazee wakienda kuonana na Dk. Slaa ili kujaribu kumshawishi abadilishe uamuzi wake.

Nimalizie kwa kusema hili jukwaa kwa sasa kwa kiwango kikubwa limekuwa na hoja za kishabiki badala ya uhalisia wa hoja.

Hili suala la Dk. Slaa, CHADEMA na Lowassa kwa sasa linajadiliwa kiushabiki shabiki.

Kuna watu wameishajenga fikra, ukimzodoa Lowassa hata kwa kutumia ukweli unakuwa unabomoa UKAWA, na kwa matokeo hayo UKAWA hawawezi kushinda uchaguzi hasa kiti cha Urais. Hawa ni wale waliosema/wanasema CCM lazima iondoke hata kwa msaada wa shetani. Hawa ni wale wanafahamu Lowassa ana makandokando lakini kwa vile amepitishwa kuwa mgombea Urais, hawana choice nyingine katika njia ya kuitoa CCM madarakani bali kuunga mkono maamuzi hayo ingawaje dhamira zao zinawasuta kutokana na historia ya Lowassa.

Hawa wanaJF wanafahamu kwa vile kwa sasa Dk. Slaa amesema hajihusishi na siasa tena, kuendelea kumkumbatia hata kama ni katika msingi/misingi ya ukweli inakuwa haina mashiko wa kisiasa kwa sababu kazi iliyo mbele yao ni kuiondoa CCM kwa njia zozote zile. Kwa nini umkumbatie Dk. Slaa ambaye hoja zake zinazoofisha CHADEMA na mgombea Urais wakati Dk. Slaa kwa sasa hana mchango wowote katika uchaguzi huu zaidi ya kuwa liability.

Kuna wengine wanajificha kwenye suala la Prof. Lipumba wakisema Dk. Slaa angefanya kama alivyofanya Prof. Lipumba lakini wanasahau kama hawakutoa pongezi kwa Prof. Lipumba bali walimzodoa sana baada ya kusema alichokisema na kujiudhuru uongozi ndani ya CUF.

Kwa maoni yangu, nadhani hili jukwaa halitendewi haki!
 
Last edited by a moderator:
@Ng'wamapalala hapo juu. Kwanza karibu na tunashukuru kwamaoni yako

Yapo mengi ya kujadili, nianzie kwa ufupi tu paleulipomalizia. Ukiangalia mabandiko ya nyuma kidogo

JokaKuu bandiko 455 kasema ''
..Dr angetumia approachaliyofanya Prof.Lipumba sidhani kama tungekuwa tunamjadili yeye binafsi badalaya hoja zake.''

Nguruvi3 badiko 456 aliandika hivi '' He could simply borrow a leaf from Lipumba.Natofautiana sana na Lipumba lakini jambo zuri alilofanya ni kutoa statementambayo pamoja na mapungufu yake haikuonyesha ukakasi kama wa Slaa''

Tulichomaanishana nadhani JokaKuu atakubaliana nasi ni kuwa, approach ya Lipumba ilileng akuzungumzia hoja iliyopo.
Alisema ' Nafsi inamusta' kwa maana kuwa anaona moral values zake zinakuwa eroded kwa ujio.


Prof hakusema mambo mengine wala tofauti nyingine au mambo ya kiofisi. Alikiri kushiriki katika mchakato ambao mwisho nafasi inamsuta

Niliandikamahali kuwa Prof Lipumba alipokuwa anamkaribisha hakujua kuwa hilo ni tatizo?
Kwanini amefanya hivyo na mwisho akaondoka? Tulihoji


Tukirudikwa Dr Slaa, tumesema ilikuwa ni haki, ni sahihi kutoa maoni si kwa faida yak ebali sote. Haki ya kueleza upande wake ni ya asili

Tukasema,msimamo wake uheshimiwe, maamuzi yake yaheshimiwe

Tulipomfananishana na Prof tukaona mapungufu mengi.

Kwanza, hotuba yake ilikuwa katika hali isiyoeleweka inayoleta shaka.

Kwa mfano, baada ya kueleza kwa ufupi, moja kwamoja akaenda shule za kata, maji Monduli. T
ukauliza hilo lina uhusiano gani natatizo linalomkabili?


Dr alisema kaacha siasa July 28. Halafu kaelekeza mashambulizi kwa akina Sumaye,Guninita n.k. ambao hawakutajwa katika mawasiliano yake na mshenga Gwajima.Hawa wanaingiaje katika hoja iliyopo mezani?

Mambo yadini yanaingiaje?

Tukahitimishakuwa, Dr aliongozwa na hasira. Alikuwa na hoja ambazo wengine tupo katika rekodi kuzizungumzia kabla ya tarehe 28 kwa undani zaidi.

Tatizo lake, hasira ziliondoa busara


Kinachoonekana hotuba yake ilivuka mipaka, badala ya kuzungumzia tatizo, akaongelea matatizo mengine yasiyihusiana na tatizo

Kuna kitu ambacho pengine hukutuelewa. Neno approach halina maana sahihi. . Tunachopongezani approach si usahihi au upotofu wa hoja.

Nadhaniu takuwa umeelewa, na wala hakuna aliyejificha , si JokaKuu si Nguruvi3
 

HOwever ndugu yangu, kuna mapengo (gaps) nyingi sana ukisikiliza hotuba, ukamuangalia halafu kaa chini siku nzima urudie kukisikiliza alichosema au kukisoma...

KUna ile sensational reception kuwa kamwaga mboga. Lakini ukikaa chini na kuanza kupitia kila alichosema na kutafakari bila kukurupuka, unakutana na kauli za Nape "tunawajua hawa" lakini ni action au Mwakyembe "huyu atafunguliwa kesi" lakini ni Mwakyembe huyu huyu alisema kuna mengine hatuwezi kuyasema hadharani maana yangetikisa nchi!

Sasa kama leo Mwakyembe "aliinusuru" nchi kutikisika kutokana na kweli ya uchunguzi wake, atueleze alitunusuru kutokana na kitu gani? Maana kama alitunusuru usiasa wa nyadhifa na mamlaka ya mtu, kisa fulani ni fulani, basi anasahau kama Lowassa alivyokurukupa kulazimisha mkataba mbovu, yeye Mwakyembe "kuinusuru" nchi karuhusu nchi iingie hasara ya zaidi ya miaka minane ya kukosa umeme wa uhakika na kuilipa Dowans na kisha Symbion fedha za capacity charges na huku hakuna umeme wa kusukuma uzalishaji.

So who is worst of the worst?
 

Wakristo, tuna kauli moja ambayo ni ahadi tunaisema wakati tunajiandaa kula sakramenti ya bwana. Inasema "namkataa shetani na mambo yake yote na kazi zake zote"

Kitendo cha Dr. Slaa kuweka masharti kwa Lowassa wiki zile za kwanza za Lowassa kuhamia na leo kumuita "Shetani" ni kujikanyagakanyaga na kushindwa kusimama upande unaoeleweka.

Haijali orodha ya masharti, midhali alitoa masharti badala ya kumkataa Lowassa at get go, ina maana Lowassa alikuwa na manufaa ya namna fulani kwa Dr. Slaa.

Nikibadili mwelekeo na kusema ni suala la Ubaba Uchungaji, mwanadamu hana mamlaka ya kidini au kimungu hasa Wachungaji na Mapadiri kusema kutubu kwa mtu au kukiri dhambi kwa mtu kwa namna yeyote, hakutoshi na hakustahili kupokelewa kama kitubio au unyenyekevu wa ukosaji.

Kama leo Dr. Slaa anamshabikia Mwakyembe na hoja zake zote na hata kauli kuwa kuna mengine waliepuka kuyasema "kuinusuru" nchi, iweje akubali kauli ya Mwakyembe ya kutoa taarifa nusu nusu na si kuikubali kauli ya Lowassa ambayo tunajua pia kuwa nayo "inanusuru " nchi?

Kwa mtu anayejisifu kusimamia haki na kweli, hauwezi kuwa na selectiveness ya kipi unaona ni halali na kipi utakimezea na kipi utakipigia kelele za kulaani.

Ni dokezo tuu la kuweka sawa mambo na fikra zetu za kudai uwazi, ukweli na kuwajibika!
 
@Ng'wamapalala kuna hoja hapo, unaweza kutusaidia?

Pili, Alinda aliuliza haya

Je, Dr alimkaribisha Lowassa kama nani? Mgombea,mwanachama, au mtu atakayesaidia kampeni?

Mwalimu akaulizahivi ' Gwajima alipompigia simu Dr Slaa na kumwambia, Dodoma wamemkatatufanyeje ? Ina maana gan?

Kuna alihojia kuwa nani hasa alimwalika Lowassa kati ya pande mbili?
 
Swali la msingi ni Je, Lowassa ni Asset ama Liability kwa CHADEMA??

I will add, he is a political capital on hedging, or high risk volatility equity security.. is he Google, Apple, Ali Baba or Pfizer, its up to the investor to decide!

He could also be Chinese Yuan gaining and surging, or the stable Euro or the declining Tanzanian Shilling!

Its all about the market appetite and response!
 

Je Mchungaji Msigwa alipokuwa na Polepole na akasema kuwa yeye na Slaa walikuwa kwenye mchakato wa kumleta Lowassa Ukawa alikuwa anadanganya?

Mchungaji na Padiri....😛ray2::smokin:
 

Na wengine waliondolewa na kutuhumiwa kuwa mapandikizi na wasaliti (Zitto, Kitila nk)
 
Mkuu Rev. Kishoka

Katika bandiko 469 uliloninukuu, ile collosal damage sikumaanisha ya ufisadi peke yake.
Nilimaanisha unitended consequences zinazotokana na baadhi ya kauli zake na zinavyoweza kupokelewa katika jamii.

Katika bandiko 470, tukushukuru sana sana kwa ufafanuzi wako.
Kuna watu wasioelewa kwanini hoja zinaletwa na kuchambuliwa.


Ulichokifanya ni ku dissect hotuba ya Dr kama tunavyofanya

Kwamba ''no stone unturned'' Kwa mfano, Dr Slaa alipoongea na Gwajima na kuambiwa ‘amekatwa tufanyeje' hii ilimaanisha nini tukiangalia suala zima kwa mukatadha wa muda?

Huko nyuma tumeonyesha jinsi Dr Slaa alivyohoji mambo.

Kwa mfano, aliuliza wabunge wangapi wanakuja? Akataka hata majina na hadi tarehe za mwisho kabla ya kuacha siasa hakupewa.

Katika hotuba anaonekana mwiba sana kwa ufisadi, sasa ilikuwaje hapo akubali aste aste?

Kwamba, kuna nyakati alikuwa anajali ujio na mwisho ujio ukawa mbaya.

Alinda
aliuliza, kwanini mtu anayechukia ufisadi kama Dr asimwambie Mshenga Gwajima moja kwa moja?


Mwisho, ukisoma hotuba yake ukairudia vema inaonekana kama ni kauli fulani tunazosikia sikia.

Suala la shule za kata lilizungumzwa wakati wa kura za maoni za CCM kama lile la maji.

Chakujiuliza ilikuwaje mambo hayo yakaingia katika mgogoro wao ambao ni yeye na Mbowe/Lissu?


Halafu Dr amesema anaacha siasa. Katika hotuba anasema atazungumka kumpinga Lowassa.
Hapa inakuwaje, kwamba anakuwa na NGO au anampinga kama mtu binafasi au inakuwaje?


Haya ni mambo tunayotakiwa tuyajadili kwa upana wake
 

Nadhani hapa watu pia wanamiss ukweli mwingine; kama CDM walimpitisha Slaa mapema hivyo awe mgombea wao ni kwanini? Waliamini kuwa anawafaa kweli kweli au walifanya kama hadaa? Siyo kwamba walimpitisha kwa sababu waliamini anaweza kuwakilisha maslahi ya chama na harakati zao kwenye Uchaguzi Mkuu? Sasa watu wale wale ndani ya miezi michache wanabadili 360 halafu walitaka Slaa asimame na kusema ndio tu? Ukweli wangemkubalia pale pale aliporesign on principle.
 


Nguruvi, ukisoma vizuri kuna kitu ambacho hakijasemwa vizuri. Mazungumzo na Lowassa hayakuanza baada ya jina lake kukatwa. Gwajima alifanya kile alichotakiw akufanya na mhusika mkuu. Walijua kizuizi kikubwa kwa Lowassa kuja CDM ni Slaa, kwanza sababu ya nafasi yake (alikuwa tayari ni mgombea wao) na pili sababu ya msimamo wake ulio tofauti sana na Lowassa. Si unaona wakati mwingine hata ndani ya familia kuna mambo fulani mzazi anajua ili lifanyike lazima mzazi mwenzie ndio atoe "Ok". Hivyo, mtoto ataambiwa nenda kwa "babaako" au "mamaako" si kwamba yule mzazi mwngine hajaimbishwa bado!

Kuna watu walishaimbishwa kwa muda na ulipofika wakati akatumwa mshenga... "nenda kwa Slaa"... the rest is history.

Mzazi anayeulizwa anaweza kusema "Mamaako anajua" halafu mtoto anasema "ntaenda kumuuomba ila ukikubali najua hatakataa..." kumbe dili lilishachongwa muda!! Angalia simulizi hili kwa karibu utaona mchezo huu...
 

Ukiongezea na suala la kuhongwa maaskofu wa katoliki na kupigwa kwa waislamu mwembechai moja kwa moja unapata mwanga kwamba amecheza kwa mujibu wa script ya CCM iliyozoeleka kutoka kwa kina Nape. Wakati yeye anagombea 2010 chadema iliitwa chama cha wakatoliki lakini leo kwa ajili ya Lowasa kanisa hilo hilo linatupiwa tuhuma ya kuhongwa!

Ninaamini hata yeye mwenyewe sasa hivi kama kweli ni mnyoofu kama anavyotaka tuamini atakuwa anatazama replay ya press conference asiamini kwamba aliyekuwa anazungumza pale mbele ni yeye!
 

Dada yangu Alinda,

KUna kitu kinapingana hapa! Dr. Slaa alidai kwenye hotuba yake hakutaka kuwa Rais.

Lakini inaelekea wazi kuwa alikuwa tayari Lowassa aje. Aidha habari zisizothibitishwa, ujio wa Lowassa na wafuasi wake ulikuwa uongeze nguvu CDM na hata kumpa fursa mgombea wa CDM (Dr. Slaa) uwezo wa kunyakua Urais.

CDM waliweka sharti ndani ya UKAWA la kupewa Urais ambalo lilimshinda Lipumba (again, hizi ni habari za mizunguko na michepuko na hata udini pia unatajwa hasa Ukatoliki versus Uislamu).

Again, kutokana na maudhui ya mkutano wake na kiwango cha hisia (emotions), suala la yeye kusema hakuwa na nia ya Urais linaonekana kama ni uongo (aidha za michepukoni ni kuwa yeye na wapambe walitaka Lowassa aje aonegze nguvu, tatizo lilikuja Mbowe alipoona opportunity from another angle na kuamua kumwachia Lowassa agombee urais).

Kiukweli, hotuba nzima imeamsha maswali mengi ya credibility za wanasiasa wengi (not Lowassa, he is known thug, master of manipulation and opportunist that is not a secret at all) wazee wetu wiki hii hasa Sitta, Slaa na Mwakyembe.

Ukiangalia kauli za hawa wazee watatu, kila mmoja anatoa vitisho na blackmail kuwa ana mengi ya kumwaga mboga na kudai kama Lowassa na wenzake wnaa ubavu wathubutu kujibu hoja.

This is a mockery to good governance and transparency. It is absolute denial of justice and tarnish credibility of so called Wapiganaji au Wapambanaji.

Leo hii tukianza kusema wewe bwana tuna siri zao hebu nyamaza tusikuumbue, ilhali tunakutuhumu mwizi au tunakujua ni mhalifu bila kukufikisha pale panapostahili, hatuoni kuwa bado tunaendeleza utamaduni mchafu tunaoupiga vita wa mtandao, ufisadi, vificho, visasi na hata kupoteza credibility ya kusimamia haki na utu?

Inanikumbusha reaction ya watu nilipohoji kukiukwa kwa kanuni na katiba ya CCM kwenye mchakato wa kuchagua mgombea wa CCM, nilipohoji kufurahia kudhihkiwa na kunajisiwa demokrasia na kanuni ndani ya CCM, kisa Lowassa kakatwa mpaka nikatuhumiwa kukatiwa kitu.

Nikauliza, kama leo tunaruhusu na kufurahia CCM walichofanya ndani yao, kesho wakifanya kwenye uchaguzi mkuu na magoli ya mikono tutakuwaje na sauti za kulalamika au kukemea?

Natambua sisi ni binaadamu an tuna double standards. Lowassa is public enemy #1 , lakini pia ni kipenzi cha wengine wengi tuu pamoja na uanaharamu na uharamia wake wote.

Kama kweli tunataka mabadiliko, basi tuwe mstari wa mbele kuisimamia haki bila selectiveness au kufanya mambo ya mizengwe maana ugonjwa huu wa mizengwe tuliomlaumu Mwalimu Nyerere 1995, tumeuendeleza 2000, 2005, 2010 na leo hii 2015 tumeufurahia kutokana na Mizengwe kutoa goli la mkono kumkata Lowassa na wengine.

Kama tulishangilia uhuni wa CCM na safu ya viongozi wake kumkata Lowassa na wengine, iweje leo tumkasirikie Mbowe kwa kutumia fursa "kuleta" ushawishi wa mizengwe ambao Ukawa na CDM waliupigia kura ya ndio?

Ni aibu leo tunasema heri Magufuli ana ufisadi mdogo tunaweza kuishi nao, huku tunajua walimleta machoni petu tupige kura ni mafisadi wenye nguvu kubwa na kwa ushirika kama fisadi Lowassa!

We should not have double standards on anything, otherwise huo ni ushetani mkubwa kuliko machafu na madhaifu ya wale tunaowajua kuwa ni wahalifu.

Tuache unafiki na hizi selective justice na selective minds za kujenga upya nchi au hata kuchambua mambo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…