Jokakuu, huwezi kukaa na kutegemea tu kuwa kitu fulani kitatokea. Msingi aa kutegemea huko ni nini? Isipofutwa utalalamika? Kama watu hawatatataka kujua wanataka kufanya nini wasi poo ofanya wasichotakiwa tutaanza vipi kuwauliza? Hii pragmatism should have some basis.
Tatizo ambalo wengi bado hatutaki kulikubali - japo lipo linatukodolea macho - ni kuwa UKAWA siyo entity ambayo unaweza hata kuijadili bila kuonekana ni mtu wa kufikirika. UKAWA siyo chama cha siasa, siyo chombo chochote kinachoongozwa na vitu vinavyoeleweka. UKAWA hata siyo "umoja" kama wengi wanavyodhania - maana nasikia watu wanasema ni 'umoja wa upinzani'. UKAWA hata siyo "Muungano" ni ushirikiano tu. Simply put ni loose association ya watu ambao wana matamanio mamoja. Walikuwa na muda mrefu wa kuunganisha nguvu tangu wakati ule. Kwa mfano, tangu walipotoka kwenye Bunge la Katiba wangeweza kabisa kupanga kuua vyama vyao na kuanzisha chama kimoja chenye nguvu zaidi na chenye mfumo unaoeleweka kabisa kuelekea kuongoza. Lakini wangefanya hivyo bado kungekuwa na mgogoro mkubwa nani awe kiongozi ajaye wa chama hicho? Sidhani kama viongozi wa sasa wa hivi vyama wangekuwa tayari kusalimu amri na kuweka vyeo vyao pembeni ili kupata uongozi mpya wa chama. .
Mkuu Zakumi,Mag3:
Wewe kweli umeichoka CCM. Hivi walikupeleka JKT wakati ule wa zamani?
Mkuu hapo umenena .. people are projecting their expectations onto Ukawa .. huyo mgombea hata hajagusia katiba mpya and they are dreaming kuwa viongozi hawa wakiingia watabadili sheria. Inasikitisha kuwa safari ya matumaini is just that hope without basis or foundation. .
..lakini ukawa si unajulikana kwamba ni umoja wa katiba mpya, katiba ya Mzee Warioba?
..mpaka pale mgombea wa ukawa atakapokuja na msimamo mwingine basi there is a basis for us kuamini kwamba atasimamia matakwa ya katiba ya vyama vinavyounda ukawa.
..kama ambavyo kuna uwezekano wa ukawa kusambaratika huko mbele ya safari, uko uwezekano pia wa umoja huo kudumu na kutoa mchango mkubwa kwa mageuzi ambayo tumekuwa tukiyalilia kwa muda mrefu.
..binafsi nimeona niwape nafasi hawa ukawa tuone watafanya nini. naamini hata wakiboronga itakuwa rahisi kuwatimua.
..nina HOFU kubwa sana na hatma ya wapenda mageuzi nchi hii, ikiwa CCM ya Nape Nnauye, Paul Makonda, Ridhiwani Kikwete, January Makamba,.. itachukua madaraka.
cc Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, Mag3, Alinda
Mkuu,
Ninakubaliana na wewe kwa sababu siasa za Tanzania kwa sasa imekuwa kama ushabiki wa vilabu vya mpira.
Nakumbuka kuna wakati nilikuwa ninapitia makabrasha nikakutana na andiko la Mkenya anayeitwa Josh Maiyo ambaye alielezea kuhusu vyama vya siasa katika nchi za Kiafrika na wanachama wake ambapo alisema,
Kwa sasa kuna uwezekano wa kupata Rais wa Tanzania ambaye anawakirisha andiko la Josh Maiyo!
JokaKuu, that is the point. Kabla ya mwaka 1992 tulikuwa na chama kimoja CCM na ni wachache tu kama mimi ambao waliweza kujitenga na kukaa kando bila kujiunga na CCM toka iasisiwe mwaka 1977. Wengi wa wanamageuzi wa mwanzo ama walikuwa ni wana CCM hai au ambao walikuwa CCM mfu ikiwa na maana kwamba ni kwa mwili tu na si kwa moyo. Kujiunga na upinzani kulionekana na kuhesabika kwa baadhi ya watu kama uenda wazimu au usaliti. Wanamageuzi wa mwanzo waliogopwa kama ukoma na sehemu kubwa ya jamii.
Kupigania mabadiliko ya utawala kulitafsiriwa na sehemu kubwa ya jamii kama uroho wa madaraka wakati ukweli ni kwamba waroho wa madaraka ni wale walioyahatamia na kuyang'ang'ania. Ingawa upinzani umefanya kazi kubwa kuuelimisha umma lakini Watu kama hao bado tunao na wengi kama si wote ni wanachama wa CCM. Lakini pia wapo wachache ambao hawaungi mkono CCM kwa mambo mengi lakini wanalazimika kubaki humo kulinda maslahi yao.
Ni hawa ambao kitendo cha Lowassa kinaweza angalau kuwatoa hofu na ama kuwapa ujasiri wa kumfuata huko aliko au kumpigia kura kama atasimama kama mgombea Uraisi. Lakini pia tusisahau kwamba na huko upinzani tunao ambao watauona ujio wa Lowassa kama unahatarisha nafasi zao ndani ya UKAWA. Hapa ndipo natofautiana na wengi kwa sababu naamini kama mtu hasukumwi na ubinafsi, atamkaribisha yeyote na chochote kile mradi kinamuongezea nguvu katika mapambano kama tuliyo nayo kama upinzani.
Tukubali tusikubali ujio wa Lowassa kumeiongezea nguvu UKAWA na pia kuteuliwa kwake kama mgombea kumepunguza kwa kwango fulani sintofahamu (tension) iliyoanza kuota mizizi kuhusu yupi ashike usukani kati ya CUF, Chadema na NCCR. Katika hivi vyama vinavyounda UKAWA, wako wanachama ambao haingekuwa rahisi kwao kuafiki haraka haraka wateule wao wa awali kuenguliwa. Ujio wa mtu mpya ambaye anatoka nje ya watarajiwa kunaleta muafaka na kupunguza munkari ambao wangekuwa nao vinginevyo.
Binafsi nilimpenda Dr. Slaa apeperushe bendera hiyo, lakini ninaye rafiki yangu ambaye alimuona Prof. Lipumba kama anafaa zaidi...kwa bahati sote wawili tumeunga mkono pendekezo la Lowassa kuteuliwa. Nakiri uteuzi wa Lowassa yawezekana umewavunja mioyo watu wengine lakini kwa maslahi mapana ya UKAWA naamini jibu sahihi ni hilo kama lengo ni umoja katika kumuondoa mkoloni CCM. Ningefurahi zaidi kama walengwa wawili hao, Dr. Slaa na Prof. Lipumba wangeunga mkono hayo maamuzi na tusonge mbele.
Tatizo ambalo wengi bado hatutaki kulikubali - japo lipo linatukodolea macho - ni kuwa UKAWA siyo entity ambayo unaweza hata kuijadili bila kuonekana ni mtu wa kufikirika. UKAWA siyo chama cha siasa, siyo chombo chochote kinachoongozwa na vitu vinavyoeleweka. UKAWA hata siyo "umoja" kama wengi wanavyodhania - maana nasikia watu wanasema ni 'umoja wa upinzani'. UKAWA hata siyo "Muungano" ni ushirikiano tu. Simply put ni loose association ya watu ambao wana matamanio mamoja. Walikuwa na muda mrefu wa kuunganisha nguvu tangu wakati ule. Kwa mfano, tangu walipotoka kwenye Bunge la Katiba wangeweza kabisa kupanga kuua vyama vyao na kuanzisha chama kimoja chenye nguvu zaidi na chenye mfumo unaoeleweka kabisa kuelekea kuongoza. Lakini wangefanya hivyo bado kungekuwa na mgogoro mkubwa nani awe kiongozi ajaye wa chama hicho? Sidhani kama viongozi wa sasa wa hivi vyama wangekuwa tayari kusalimu amri na kuweka vyeo vyao pembeni ili kupata uongozi mpya wa chama.
Sasa kinachotokea leo na kitakachotokea baada ya uchaguzi ni rahisi sana kutabirika.
1. Kama CDM watashinda Urais (siyo UKAWA kwani siyo chama cha siasa chenye mgombea kwenye Uchaguzi huu) basi mgogoro utakaokuja utakuja kwenye kura za viti maalum. Je CUF ambao mwanachama wao amekubali kuwa makamu wa Rais nao watagiwiwa vipi hivyo viti - Tume ya Uchaguzi itasema imefungwa mikono kwani haiangalii kura za Makamu wa Rais bali za mgombea wa Urais basi viti hivyo vyote vitaenda CDM na kuipa wabunge wengi zaidi Bungeni. Huo mgogoro wa hapo hata kuufikiria naogopa. Makamu akijiuzulu kupinga hilo na kuamua kurudi kwenye chama chake, Lowassa atatakiwa atafute mwenza mwingine kutoka CDM Zanzibar?
2. CDM wakishindwa kura za Urais, ni vipi utawaona kina Duni na Lowassa wanabakia kukijenga chama chao cha kufikia (adopted party) badala ya Duni kurudi zake CUF na Lowassa kuamua kustaafu siasa? Au watu watakubali tena Mbowe aongoze chama kukijenga kuelekea 2020 ambako huko tena watasubiria mgombea mwingine wa CCM kuwasaidia kuing'oa CCM? Hawawezi kuwa na mgombea wao miaka mitano ijayo wakaaminika tena.
Kuna migogoro mingine tu inakuja ambayo sidhani kama tumeifikiria vizuri na maana yake katika demokrasia na siasa za Tanzania kwa miaka mitano ijayo.
Kuungana na kuwa chama kimoja chenye nguvu ni jambo jema, lakini tusisahau kujiuliza swali la msingi sana je hiki kitu kinawezekana? Na kama hakiwezekani je hawa wapinzani wafanye nini? Je waendelea kila chama kivyake au wajaribu kama wanavyojaribu katika Ukawa ingawaje kuna nguvu kubwa inayotumika usiku na mchana kuwavuruga?
Nilimsikiliza vizuri mgombea wa Ukawa kwenye speech yake Kunduchi, hakuna mahali alisema kilichomfanya akaachana na CCM ni katiba au hata ufisadi. Amehama Chama kwa sababu moja tu - jina lake lilikatwa! Lowassa hajasema ameondoka CCM kwa sababu hawana sera nzuri, au kwasababu yeye anataka Serikali tatu. Hajasema hayo. Na hata hansard za Bunge Maalum la Katiba inaonesha aliunga mkono serikali mbili.
Kwa kifupi, kuna maswali mengi sana juu ya hii 'fast track exercise' ya kumpata mgombea wa UKAWA. Najua Mbowe na Lissu wamekazana kusema kuwa wanapambana na mfumo. Lakini hawataki kusema 'mfumo' unajengwa na nani? Na je, mgombea wao anahusika kwa namna yeyote katika kujenga mfumo wanaoupinga?
Nilimsikiliza vizuri mgombea wa Ukawa kwenye speech yake Kunduchi, hakuna mahali alisema kilichomfanya akaachana na CCM ni katiba au hata ufisadi. Amehama Chama kwa sababu moja tu - jina lake lilikatwa! Lowassa hajasema ameondoka CCM kwa sababu hawana sera nzuri, au kwasababu yeye anataka Serikali tatu. Hajasema hayo. Na hata hansard za Bunge Maalum la Katiba inaonesha aliunga mkono serikali mbili.
Kwa kifupi, kuna maswali mengi sana juu ya hii 'fast track exercise' ya kumpata mgombea wa UKAWA. Najua Mbowe na Lissu wamekazana kusema kuwa wanapambana na mfumo. Lakini hawataki kusema 'mfumo' unajengwa na nani? Na je, mgombea wao anahusika kwa namna yeyote katika kujenga mfumo wanaoupinga?
Mwanakijiji na Alinda:
Timing ni kitu muhimu katika siasa. Katika moja ya hotuba zake baada ya uchaguzi wa mwaka 2010, JK alisema hatuwezi kubadili kanuni za mchezo wakati mchezo umeanza. Alikuwa na maana kanuni mpya (katiba) itapatikana kabla ya uchaguzi wa 2015.
Kama kungekuwa na uwezekano, UKAWA ungekuwa na juhudi moja kubwa. Timing ya katiba mpya kwenye uchaguzi wa 2015. Wapinzani wasingeshiriki kwenye uchaguzi wa aina yoyote mpaka katiba mpya ipatikane. Kwa maoni yangu naona wanatumia nguvu nyingi sana kutaka kushinda uchaguzi huu na baadaye kubadilisha kanuni wakiwa washindi. Kwa kushiriki kwao, inawalazimu kuyamezea mambo yasio sameheka.
..ccm wangeweza kuendelea na uchaguzi na vyama vya kina Dovutwa, Mziray, na Hamad Rashid.
..nyinyi mnacheza na CCM nyinyi. hakuna mabadiliko yatafanyika bila CCM kupokonywa ikulu na bunge.
JokaKuu, wapo watu kama mwenzangu Mzee Mwanakijiji ambao wameamua kuangalia kila tendo kwa jicho hasi mradi mhusika katika ufanikishaji wake ni mtu asiyekubalika machoni pao. Wanaamini kwamba motisha inayomsukuma mtu huyo ni maslahi binafsi na hawatoi nafasi kabisa kwa mtu kama huyo kufanikisha mabadiliko bila kutanguliza ubinafsi. They dont trust that person to willingly put the needs or wishes of others before their own...Because of this, Mzee Mwanakijiji has turned into a very predictable cynic...mimi ushindi wa ukawa siuangalii kwa kutumia "lens" ya migogoro itakayofuatia.
..naangalia ni mambo gani mazuri yanaweza kutokea.
..kwa mfano, ikiwa ukawa watashinda nategemea sheria inayovikwaza vyama vya siasa kuungana au kuunda coalitions kufutwa mara moja.
..pia sheria inayomzuia mbunge kuhama chama bila kupoteza ubunge wake nayo nategemea itafutiliwa mbali
Cc Mkandara, Nguruvi3 Alinda Mwalimu
Mzee Mwanakijiji said:Jokakuu, huwezi kukaa na kutegemea tu kuwa kitu fulani kitatokea. Msingi aa kutegemea huko ni nini? Isipofutwa utalalamika? Kama watu hawatatataka kujua wanataka kufanya nini wasi poo ofanya wasichotakiwa tutaanza vipi kuwauliza? Hii pragmatism should have some basis.
Cynic - who advocates the doctrines that virtue is the only good, that the essence of virtue is self-control, and that surrender to any external influence is beneath human dignity.
Zakumi, ndio maana nasema wengi wenu hamuijui CCM and what it is capable of. Je umesahau Bunge Maalum La Katiba? Kususa kwa wapinzani kulisaidia nini, si waliendelea tu kama vile hakuna upinzani! Take note: ni hivyo vyama vidogo ndivyo viliwapa CCM uhalali. Mbona nyumba zao hazikuchomwa?Vyama vidogo kama hivyo ni vya kuvifanyia utemi. Mnaviambia tu mkishiriki tu, tunachoma nyumba zenu moto.
Wakati wa kutoa manifesto bado, wakati wa kutoa ilani bado, wakati wa kujinadi bado, lakini wewe tayari unaihukumu UKAWA. Haulazimishwi kuipigia kura UKAWA lakini kwa nini usisubiri uonje chakula kilicho jikoni kabla ya kutoa hukumu, kwa nini hungoji kampeni zianze na ukiona maswali yako hayajibiwi uwanyime kura? Safari hii natumaini midahalo itakuwepo, sidhani kama wapo watakaoweka mpira kwapani kama safari iliyopita.
Mkuu JokaKuu,..wale hilo lisikupe shida.
..Dr.Mwakyembe amepata PhD yake kwa thesis ambayo inatetea muungano wa serikali 3.
..lakini kwasababu yuko kwenye CCM basi kwenye bunge la katiba akatetea serikali 2.
..Dr.Asha-Rose Migiro alikuwa mjumbe wa Tume ya Jaji Kisanga ambayo ilipendekeza serikali 3.
..lakini kwenye bunge la katiba Dr.Migiro akabadilika na kutetea serikali 2.
..mimi nadhani hansard haina maana hapa. kitu cha msingi ni Lowassa amejiunga na chama ambacho sera yake ni serikali 3.
cc MBEBA MAONO KAJA
Mkuu JokaKuu,
Hoja yako ni nini hapa?
Hii mifano ya wana CCM unayoitoa niya watu ambao walikataliwa na vikao vya CCM kuteuliwa kuwa wagombea Urais wa Tanzania, inawezekana moja ya kikwazo ni kuwa vigeugeu katika misimamo muhimu ya kitaifa.
Kwa sasa tunaongelea Rais wa Tanzania ambaye madaraka yake ndani ya Katiba yalishawahi kusemwa na Mwl. Nyerere yanaweza kumfanya kuwa dikteta kama ana hulka za kidikteta.
Katiba ya Tanzania (1977) kwa jinsi ilivyo mbovu, inahitaji Rais anayeaminika na ambaye siyo mtovu wa uadilifu.
Kwa maelezo ya Mzee Butiku, Lowassa ni mtetezi mkuu wa Serikali mbili kwa sababu ya madaraka na nguvu zitokanazo na Rais wa Tanzania katika serikali mbili. Ieleweke kuwa, Lowassa hakuingia CHADEMA kwa sababu amevutiwa na Sera za CHADEMA bali ameingia CHADEMA kwa sababu jina lake limekatwa na wazee wa CCM na kwa sababu hiyo, ndiyo maana alipoingia CHADEMA hakutaka kuwa wanachama wa kawaida bali alitaka kuwa mgombea Urais.
Mabere Marando ametueleza, CHADEMA walianza maongezi na Lowassa ya kuhusu kuhamia CHADEMA kabla hata ya vikao vya CCM vya kuteuwa wagombea Urais havijaanza.
Kitu kingine ninachokiona kwa sasa, Hata kama Lowassa atashinda Urais, kitu ambacho mpaka sasa sina uhakika, naamini hawezi kuachia nguvu na madaraka yatokanayo na serikali mbili ili awe Rais wa Tanzania katika serikali tatu. Ninaamini Rasimu ya Warioba ambayo imetoa masharti ya kipindi cha mpito kwa miaka minne ataiweka kabatini mpaka baada ya uchaguzi wa pili ili kuhakikisha anamaliza kipindi chake cha pili kwa mujibu wa Katiba akiwa Rais katika serikali mbili, kwa maana hii, Serikali tatu tutaziona mwaka 2025.