Sina kumbukumbu kama Lowassa aliwahi ongea chochote kuhusu katiba mpya/au serikali 2 3.. Kama kuna mtu mwenye andishi lake tunaomba aliweke hapa ili tufahamu nini msimamo wake kuhusu swala zima la katiba mpya..
Kama kuna mtu moja ndani ya CCM alikuwa
non-commital kwenye swala la Katiba pendekezwa ni Edward Lowassa lakini kwa watu ambao wako tayari kumvika taji la
mfalme wa mafisadi Tanzania dai kama hilo lilitegemewa. Edward Lowassa alianza hata kuzikosoa sera za CCM kabla ya hapo lakini kama walivyosema wahenga,
give a dog a bad name then hang him. Je Lowassa ndio mbuzi wa kafara katika kukitakasa chama cha mafisadi, CCM?
Lowassa hajawahi kuwa top leader nchi hii, kila wakati amekuwepo mtu mkubwa zaidi juu yake aliyeapa kwa msahafu kuilinda na kuitetea katiba ya nchi hii. Toka mwaka 2008 alipojiuzulu Uwaziri Mkuu na kukaa nje ya serikali, ufisadi umezidi kusitawi na kufikia kiwango cha kutisha. Ni baada ya kuwa nje ya serikali ndio kwa mara ya kwanza tukashuhudia serikali dhaifu ikikiri hadharani kuwa wapo wahalifu wenye nguvu wasiokamatika.
Wako watu kama Chenge wameita dola milioni moja kwenye account zao nje ya nchi vijisenti, wameshtakiwa kwa kuua na wamekuwa ndio washauri wakuu wa mikataba ya kifisadi awamu hadi awamu lakini wanaendelea kuaminika na kupewa heshima ya kutuandikia katiba mpya. Hivi sasa anagombea ubunge na kashinda kwa kura nyingi katika kura kura ya maoni lakini Edward Lowassa hapewi hata
benefit of doubt anapokanusha tuhuma.
Tunaye Kiongozi Mkuu wa nchi, kahusishwa na kila kashfa tuliloingia tangu akiwa ni Waziri wa Nishati hadi alipochaguliwa kuiongoza nchi mwaka 2005 kwa njia ya wizi lakini bado anapewa
benefit of doubt. Amewahi kuvunja katiba ya nchi aliyoapa kulinda na kuitetea alipoamua kuwasamehe wezi na kuwaomba warudishe walochoiba lakini bado anapewa
benefit of doubt licha ya kwamba kwa wenzetu wastaarabu,
the buck stops with the President.
Hivi sasa tunaye mgombea mteule wa Uraisi ambaye ripoti zipo zikimhusisha na kashfa ya upotevu wa mabilioni ya pesa iliyotokana na kodi za wanachi lakini anapewa
benefit of doubt. Amehusishwa na kashfa ya uuzwaji wa nyumba za serikali kiasi kwamba Mawaziri wanakosa makazi huku nyumba ambazo wangekaa zimegawiwa kiholela kwa washikaji wasiohusika, lakini maadam yuko CCM, anapewa
benefit of doubt na kutakaswa kuwa ni msafi.
Edward Lowassa mwenyewe, kwa kuhamia upinzani, ni kama amewafia mafisadi wote wa nchi hii na kuchukua dhambi zao na sasa ni wasafi waking'ara kama theluji. Maadam ameamua kujitetea akiwa nje ya CCM, yeye pamoja dhambi zote ndani ya serikali ya CCM, anatakiwa afungwe ndani ya sanduku na kutupwa baharini. Baada ya hapo ufisadi utabaki ni historia katika taifa hili, na Watanzania tutaishi raha mstarehe milele na milele!
Kwamba binadamu yeyote anaweza kutakasika isipokuwa moja anayeitwa Edward Lowassa? Kwamba dhambi zote zinasameheka isipokuwa za Edward Lowassa? Kwamba ufisadi wote sasa umehamia Chadema na kuiacha CCM ikiwa safi? Kwamba...
are you kidding me? Kwa nini hatuko tayari kumpa
benefit of doubt huyu mtu moja kama tumeweza kuwapa maelfu kwa maelfu mafisadi walio ndani ya CCM? Hii chuki inasababishwa na nini?