CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

MBINU NA CHANGAMOTO ZA CHAGUZI

Chaguzi huambatana na mbinu , mikakati na changamoto

Chaguzi huwa na makundi ya wapiga kura. Kwa hali ya kisiasa yapomakundi yafuatayo

(1) Kundi linalopiga kura ya hasira- hili ni lile lisilo naupande, lilichoshwa na hali iliyopo

(2)Kundi la wanachama watiifu, hili linachagua tu kutokanana vyama iwe ni CCM, UKAWA au kingine

(3) Kundi lenye mashaka- hili halina uhakika lisimame wapi namara nyingi huangalia hoja ingawa si jambo linalotazamwa sana ukilinganisha na personality

CCM inategemea makundi 2 na 3 kwasababu tayari ni mwathirika wa kundi la 1

Wapinzani wana ‘advantage' ya makundi yote. Ushindani upo kundi la 3 litakaloamua nani anashinda majimbo au dola

Wapinzani kama ilivyo kwa CCM, wana ‘disadvantage'.

Kwanza, uwezowa kufikia jamii una vikwazo tukijua CCM ina mtandao wa wakuu wa mikoa na wilaya na rasilimali za umma.

Pili,CCM wanaserikali inayomiliki vyombo muhimu.

Mfano, zipo taasisi za nishati zinazolalamikiwa kutotenda haki kwa maagizo ya serikali ili kuwanyima wananchi habari

Vyombo vya habari vinavyoegemea CCM, na vyombo vya dola kutumika vibaya

Ushindi hautaamuliwa kwa hesabu za kura, yapo mengine ambayo kama hayataangaliwa yatabadili mwenendo wa uchaguzi

Kwa mfano,hatujawahi kupata majibu ya kwanini watu wajiandikishe kwa asilimia 70 , wapiga kura wawe asilimia 30.

Kuna nini kinaendelea ambacho serikali au tume ya uchaguzi imeshindwa kubaini?

Mfumo wa pili , BVR, je, umehakikiwa kufanya kazi kamailivyokusudiwa?

Kukiwa na matatizo ya kifundi au ‘kufundwa' itakuwa ni kwa maumivu ya wapinzani

Lipo suala la ‘voters suppression' kusudio ni kuzuia watu wasitumie haki ya kura kwa udanganyifu kama ule wa 1995 watu walipoambiwa siku ya kwanza ni CCM na ya pili wapinzani

Au inaweza kuwa vitisho kwa wapiga kura (2010) kwa jeshi kutoa tamko, au kutumika nguvu za dola kwa namna yoyote.

CCM wanakiri hali ngumu inayowakabili. Istegemewe CCM itatoa dola au bunge au vyote katika kisahani cha dhahabu.

Itapigana hadi tone la mwisho ikitambua kuwa KANU imetoweka kama ilivyo UNIP

Kitakachosaidia wapinzani ni ushindi usio na shaka ‘decisive victory'.

Itawezekana wakijiweka vema kupambana na hila, kukabiliana na hoja, kujenga hoja na kujibu hoja.

Kuzuia uharibifu kwakushambulia na si kujilinda ni muhimu kwao.

Kuwepo na uthubutu ‘courage' ya kupambana na changamoto si chaguo ni lazima kwa wapinzani

Tusemezane
Wanajamvi tunalirudia bandiko hili kwa makusudi zaidi ilimjadala unaofuata punde ueleweke.

Yanayofuata, vyombovya dola na daftari la kura
 
VYOMBO VYA HABARI KATIKA UCHAGUZI

ITV NA RADIO ONE WAPEWA ‘KARIPIO'
UHAKIKI WA DAFTARI LA KURA

Sehemu ya I

Awali,bandiko #225 JokaKuu ameeleza kuhusu CCM kutenda jambolikawa halali.

Jambo hilo likitendwa na wapinzani linaundiwa uharamu na vyombo husika
Hoja yetu, ni vema CCM wakafanya kwanza kwani inafunguamilango kwa wapinzani.

Kwa mfano, Lowassa alipokuwa CCM alikusanya wadhamini laki 8, alikopita alisindikizwa na makundi makubwa

Magufuli alianza ziara za kujitambulisha. Kote alikopitaalipokewa na watu shughuli kusimama.

Ndivyo pia ilivyokuwa wakati anachukua fomu Eneo la Lumumba na jiji shughulizilifungwa kutoa nafasi

Lowassa wa UKAWA naye kafanya kama ilivyokuwa kwa Magufuli. Shughuli zake zilijaza watu , kama Magufuli

Naibu inspekta jenerali wa jeshi la Polisi amepiga marufukumaandamano wakati wa kurudisha fomu.
Hapa tunasisitiza wakati wa kurudishafomu za wagombea Urais

Kwa maneno mengine mikutano ya kujitambulisha ya UKAWAiendelee pamoja na kuwa inaathri shughuli. Kwanini?

Jibu ni rahisi CCM walifanya hivyo napengine kuna aibu yakunyooshewa vidole mbona UKAWA wakifanya inakuwa nongwa. Hapa kuna faida ya CCMkutangulia na ‘mambo yao''

Lakini pia ipo hoja. Mkutano wa UKAWA kuchukua fomu haukuwana tukio la uhalifu kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Polisi. Uchaguzi nisuala la msimu, kwanini naibu Inspekta anaona upo umuhimu wa kuzuia kwa sasa?

Na nyongeza ya hapo, je kampeni zitakapokuwa na idadi kubwa,naibu inspekta jenerali atapiga marufuku?

Kwa mbali tunaweza kuona hoja ya kuzuia mikutano bila kuwana sababu za msingi inajaengwa

Mikusanyiko ya kisiasa ni haki ya mtu au watukwa mujibu wa sheria za nchi ilimradi hakuna uvunjaji wa sheria.

Je, tangu sakata lianze ni wapi kuna tukio la uhalifu?

Kwanini Polisi wadhani ni muhimu kuanza kutekeleza agizo lao wakati wakurudisha fomu na si kuanzia sasa?

Inaendelea sehemu ya II
 
Sehem ya II

MATUKIO YANAYOHUSISHA TAASISI ZA UMMA NA ZA BINAFSI KATIKA HABARI

Upo msemo unaosema '' If one's an incident, two's a coincidence and three's a pattern''

Kwa lugha isiyo rasmi, ‘kama jambo moja ni tukio, la pili nimpangilio na la tatu ni mwendelezo''

Ina maana jambo la kwanzani tukio, likijirudia ni kama limepangwa na mara ya tatu inakuwa ni mwendelezo

Kauli ina maana kwa wakati huu. Yame kuwamalalamiko ya taasisi kama Tanesco kukata umeme katika nyakati kadhaa.

Ni matukio yanayojirudia rudia hasa wapinzani wanapokuwa na jambo mbele ya TV.Zipo hisia, hiyo ni pattern

Hisia kama hizo zipo katika vyombo vya habari vya umma.
Kwamba, habari zinazopoewa uzito ni zile zinazotakiwa kusikika na si zilezilizotokea.

Matumizi ya vyombo hivyo yana mwonekano wa upendeleo ikiegemea chama tawala. Haya tunayaona kila siku

Upo mswada uliotaka vyombo vya habari vijiungena TBC saa 2 (prime time) ili watu wote wasikilize habari ya TBC.

Hapa kuna tatizo kubwa sana. Hivi TBC inayoendeshwa kwa kodi za umma inawezaje kushindwa kutekeleza majukumu yake hadi kutaka nafasi kwa vyombovya watu binafsi?

Kinachoonekana ni kutaka kuzima habari za vyombo binafsi katika muda nyeti(prime time) ili wananchi wasikilize habari za TBC inayoshindwa ushindani licha ya fursa inazopata dhidi ya vyombo binafsi

Ikumbukwe ipo sheria ya kutoa habari za uchaguzi iliyoIpa tume ya uchaguzi ‘exclusivity' na si vinginevyo.

Na ipo sheria inayohusu matumizi ya takwimu inayoipa idara ya takwimu nguvu za kutoa takwimu pekee.

Na ipo sheria ya mitandao inayozuia na kubana kuhusu kupashana habari kwa kutumia vyombo hivyo

Sheria zote hizi zimeharakishwa kwa hati za dharura kuelekeauchaguzi, kwanini?

Mabadiliko ya kijamii yameleta msukumo kwa vyombo vyahabari.
Kwamba, wananchi wana uhuru na chaguo la nini wasikilize na kwa wakatigani wala si kuchaguliwa.

Vyombo binafsi vimekuwa mstari wa mbele kupasha ummanini kinatokea na si nini wananchi wanatakiwa wajue.

Kwa muda huu ambao hali ya CCM ni pumzi katika mashine,nguvu ya vyombo vya umma imepungua,
vimepoteza kuaminiwa na si chanzo cha habari. Chama tawala na serikali yake vimeingiwa na kiwewe.

Kiwewe ni, je, wapinzani wakiamua kutumia vyombo binafsi kwa kununua muda kama sehemu ya biashara nini kitatokea?

Je,vyombo binafsi vikisimama kuuhabarisha umma katika ukweli nini kitatokea? Kutakuwa na namna?

Ndio sasa tunaona taasisi za umma zikitumika kupiga rungu ili kutoa mfano kwa wengine.

Radio one na ITV wapewa karipio na kamisheni ya utangazaji

Inaendelea
 
Kinachoendelea Mwanza kama ni kweli basi ninaanza kuwa na wasi wasi na uchaguzi wa mwaka huu, endapo NEC wataamua kufanya uchakachuaji kama walivyozoea.

Picha: Mwanza usiku vijana wakikesha kumlinda Lowassa.

attachment.php

Sina uhakika kama hawa watu wanampenda Lowassa sana, si uhakika kama wanampenda Mbowe au viongozi wa Chadema/Ukawa sana na si kwamba Lowassa ua viongozi wa Ukawa wako kwenye hatari hivyo wanawajibu wao kuwalinda BALI kitu ambacho nina uhakika nacho ni kuwa hawa watu wanataka mabadiliko, hawa watu wamechoka na matusi, manyanyaso, kejeri, dharau, kuitwa ni wanywa viroba, kukosa thamani katika nchi yao, kuwa daraja la tatu katika nchi na nk. Hivyo wanachotaka ni mabadiliko nani alete mabadiliko na ni mabadiliko yapi kila mtu ana ndoto zake kichwani na kwa hizi ndoto zao hawako tayari kusubiri miaka 5 tena bali wanataka sasa..

Ni wajibu wa tume ya uchaguzi kusoma alama za nyakati, na kuandaa mazingirai mazuri ambayo yatatoa haki bin haki kwa pande zote mbili yaani chama tawala na vyama vya upinzani la sivyo tujiande kwa nchi yetu kumwaga damu.. Huu ndio ukweli ambao tunapaswa kuusema.
 
sehemu ya III

Inaendelea….

Kamisheni ya utangazaji imetoa karipio kali kwa Radio one naITV kwa ‘breaking news' kuhusu kuzuiwa kwa maandamano ya kuchukua fomu ya UKAWA

Hatuna maelezo ya kina ya pande zinazohusika, yaani ITV au mlalamikaji.
Tunachojua wametakiwa kuomba radhi siku mbili mfululizo katikataarifa ya habari ya saa 2 usiku (prime time)

Maelezo zaidi ya mamlaka ya mawasiliano yanasema, radio zisigeuzwe magenge ya watu kusema hovyo hasa kuipindi hiki cha kuelekeauchaguzi ili kulinda amani na utulivu

Ni kweli radio zimekuwa sehemu ya matatizo katika baadhi ya nchi hata kuchochea vurugu.

Ni kweli watangazaji wengine viwango vyao vya weledi vinatia shaka

Wasi wasi ni pale ambapo hatari inaonekana kuelekea uchaguzi na si wakati mwingine.

Hatujui amani na utulivu unahusu kauli gani na wala magenge ni watu wa aina gani.

Je, yule mtangazaji aliyesoma habari za magazeti kwa kuacha au kubadili hali iliyokuwepo ni sehemu ya ‘genge'?
Mamlaka iliona hali hiyo?

Kwa mantiki hiyo, kuna nafasi ya kutoa hukumu kwa vyombo binafsi kwa kutumia maneno ya jumla.

Sote ni wadau wa mani na utulivu. Amani na utulivu hupatikana penye haki.

Tatizo si vyombo binafsi tu, linaweza kuwa vyombo vya umma,kwa kushindwa kutoa taarifa kwa haki na ukweli

Kutisha wana habari haiwezi kuwa mbadala wa haki inayoleta amani

Vyombo binafsi hufanya kazi kibiashara, suala la habari ni muhimu kuliko habari inamhusu nani

Mamlaka ya mawasiliano isiishie tu kwa ITV na Radio , ni muhimu ikaangalia kama vyombo vya umma vinatumika kwa haki kila upande ukiwa na sehemu yake

Haki na Amani ni mapacha, huwezi kupata kimoja bila kingine.

Mamlaka ya mawasiliano ijiulize, kwanini TBC ya umma ikifanya biashara za ushindani haina wasikilizaji au watazamaj!

Kuelekea uchaguzi, wapinzani watambue,nafasi yao katika habari ni ndogo, wanapaswa kuwa wabunifu wa namna ya kuwasiliana na umma

Wana habari na vyombo vitakavyotishwa na kukaa kimya,vitakuwa vimekiuka maadili ya kazi yao na pengine kubeba lawama kwa kushindwa kuuleza umma ukweli

Inaendelea..
 
Sehemu ya Mwisho

Habari ifuatayo ni kwa hisani ya gazeti la Habari leo
http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/943-nec-wapambe-7-tu-ndio-watarejesha-fomu-za-urais

Hapo nyuma tulisema tutaongelea uandikishaji wa wapiga kura kwa kutumia BVR

Kabla hatujaenda huko habari iliyopo hapo juu inatia shaka.
Huko nyuma serikali ilisema kura ya maoni ya katiba pendekezwa ya CCM ipo.
Tume ikang'ang'ania hata pale walipokiwa hawana vifaa

Serikali ikaahidi kuleta vifaa zaidi ili kura ipigwe. Tume ikadai wimbo wakiwa wanajua kazi haiwezekani

Serikali ikasema kura ya maoni itachanganywa na uchaguzi mkuu, tume ikasema hilo ndilo litafanyika

Serikali ikaahirisha kura ya maoni, tume nayo ikaahirisha kama kawaida

Juzi naibu mkuu wa jeshi la polisi alitoa zuio la maandamano wakati wa kurudisha fomu.

Tume imekuja na kauli ya kuwataka wagombea waende na watu 7 tu, sababu ni kudhibiti wanachama watakaovuruga shughuli za wananchi

Tume ya uchaguzi imeenda mbali kwa kutoa ubashiri, utabiri na 'unajimu' wa kuwepo uvunjifu wa amani

Tunarudia tena, mikusanyiko halali ni haki ya wananchi kikatiba.

Si jukumu la Polisi au tume ya uchaguzi kuwachagulia wananchi lini washiriki na lini wasishiriki.

Si jukumu la Polisi au tume kuzungumzia shughuli za wananchi.

Ni jukumu la Mameya, wakuu wa mikoa na Wilaya kueleza malalamiko yao kama kweli inabidi kufanya hivyo

Si jukumu la tume ya uchaguzi kubashiri uvunjwaji wa amani bila vithibitisho

Jukumu la tume ni kusimamia shughuli za uchaguzi kwa amani.

si jukumu lao kuangalia watu wanafanya nini mitaani au wanaathirika vipi na shughuli za kisiasa kama hakuna uvunjifu wa amani

Tume ya uchaguzi ilitakiwa ikae kitako na kujiuliza, walioandikishwa majina yao yanaonekana katika data base yao?

Tume itafanya nini matatizo kama hayo yakijitokeza vituoni siku ya uchaguzi oktoba

Hayo ni mambo muhimu katika kuleta amani na kuzuia uvunjifu wa amani na si tume kusimamia shughuli zisizowahusu

Hapo juu tumesema . one's an incident, two's a coincidence, three's a pattern'

Ukifuatailia kwa undani, tume imekuwa inatoa maagizo baada ya kauli kutoka maeneo mengine

Tukumbuke hii ni tume huru ya uchaguzi, sasa inakuwaje utendaji kazi wake unakuwa wa kutiliwa shaka

Ni wakati tume iachane na kuangalia boda boda wanafanya nini katika shughuli zao za kila siku.

Pengine ni bora ieleze tuhuma zinazotolewa kuhusu idara ya IT kama inavyokaririwa kutoka mikutano ya siasa

Tume ya uchaguzi nichombo chenye hatima ya nchi.

Tunakumbuka kauli ya aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi KenyaKiviutu ilivyoleta simanzi, majonzi huzuni na misiba.

Mambo ya uchaguzi yanapaswa kuwa yenye heri na hivyo kila tahadhari ichukuliwe ili tubaki kuwa taifa lenye amani na utulivu.

Amani na utulivu ni zao la haki iliyotendeka na ikaonekana imetendeka bila shaka

Tusemezane
 
Alinda #244 hapo sijaelewa. Hiyo picha ni siku ya mikutano au ni mkesha baada ya mkutano? Ufafanuzi tafadhali maana kuna la kusema hapo.
 
Last edited by a moderator:
Kinachoendelea Mwanza kama ni kweli basi ninaanza kuwa na wasi wasi na uchaguzi wa mwaka huu, endapo NEC wataamua kufanya uchakachuaji kama walivyozoea.

Picha: Mwanza usiku vijana wakikesha kumlinda Lowassa.

Sina uhakika kama hawa watu wanampenda Lowassa sana, si uhakika kama wanampenda Mbowe au viongozi wa Chadema/Ukawa sana na si kwamba Lowassa ua viongozi wa Ukawa wako kwenye hatari hivyo wanawajibu wao kuwalinda BALI kitu ambacho nina uhakika nacho ni kuwa hawa watu wanataka mabadiliko, hawa watu wamechoka na matusi, manyanyaso, kejeri, dharau, kuitwa ni wanywa viroba, kukosa thamani katika nchi yao, kuwa daraja la tatu katika nchi na nk. Hivyo wanachotaka ni mabadiliko nani alete mabadiliko na ni mabadiliko yapi kila mtu ana ndoto zake kichwani na kwa hizi ndoto zao hawako tayari kusubiri miaka 5 tena bali wanataka sasa..

Ni wajibu wa tume ya uchaguzi kusoma alama za nyakati, na kuandaa mazingirai mazuri ambayo yatatoa haki bin haki kwa pande zote mbili yaani chama tawala na vyama vya upinzani la sivyo tujiande kwa nchi yetu kumwaga damu.. Huu ndio ukweli ambao tunapaswa kuusema.
Alinda , kinachotokea ni mtihani wa demokrasia ambao nchi yetu haijawahi kukumbana nao.

Ni mtihani utakaoamua hatma ya nchi si kwa miaka mitano bali mingi ijayo
Kwa wenyewe wanasema 'set a tone' kwamba, tunaendeleaje kama taifa

Kama ulivyosema, hali inaweza kuwa tete endapo Watanzania hawatajifunza kutokana na ishara alizoleta muumba.
Kuna kila dalili ya maelezo juu ya mtihani wa demokrasia nchini.

1. Tumeona ushiriki wa wananchi katika shughuli za siasa kwa kiwango kikubwa kuliko ilivyozoeleka

2. Tumeona na kusikia mitazamo tofauti ya hatma ya taifa kutoka kila kundi au makundi

3. Tumeona jinsi gani haki inavyoweza kuwa chachu au kichocheo cha hali ya kisiasa.

Hapa tunafafanua
CCM wametoa funzo kubwa. Kwamba, kwa muda mrefu wameishi kwa kutumia hila.

Tumesikia hila zikipewa misamiati kama kura hazikutosha, wasubiri muda wao, bado wanalelewa n.k.

Kwa muda wamelea wanachama wao na kuwajengea imani kwa wananchi.
Mwisho wa siku CCM wanakwenda kinyume na matakwa ya umma.

Hakuna wa kumlaumu kwani wao waliona hatua zote zikitendeka.

Kwa sababu ya kuishi kwa ghilba CCM ilidhani inaweza kuendelea na ghilba hiyo kama sehemu ya maisha yake.

Kumeguka tunakokuona ni kura ya kutokuwa na imani, ni ishara ya kukataa ghilba na kwamba sasa inatosha

Kwa namna yoyote iwavyo, CCM wakubali kuwa hawakufanya haki kwavile waliachia hali kuendelea wakitegemea ghilba

Pili, tumeona bunge la katiba. Maoni ya wananchi yametupwa kwa mtindo ule ule wa kuishi kwa ghilba.

CCM waliamini wanaweza kuandika katiba kuacha wananchi wajifurahishe wakijua ghilba ni nyenzo nzuri ya kuaminika.

Katiba mpya imeshindikana na wala wananchi hawajutii hilo kwavile kushindwa kwake ilikuwa kushindwa kwa ghilba

Hapa pana funzo, kwamba, umma ukiamua hakuna namna, kama heri inatakiwa ili kuepuka shari.

CCM kusitisha kura yao ya maoni ilikuwa kuepusha shari ikijua wananchi wamekataa ghilba, wapo tayari kuishi na katiba iliyopo kuliko kukumbatia ghilba

Mfano wa tatu, tumeona CCM ikiishi kwa kutumia tume za kubumba ili kuficha ukweli wa uhalifu.

Wananchi wamechukia na ndicho kinachoonekana sasa hivi.
Wanajua serikali imekuwa inafanya ghilba katika mambo yanayohusu maisha yao.

Kinachoendelea ni ishara nzuri kuwa kuna nyakati unaweza kudanganya baadhi ya watu, lakini huwezi kudanganya watu wote kwa nyakati zote. Kwamba, ghilba ina muda na kiwango

Mfano wa nne, tumeshuhudia mihimili ya umma ikifanya kazi kwa kusigishana.

Katika historia ya nchi hii, Rais amesusiwa katika shughuli za mambo nyeti ya kitaifa. Hiyo nayo ni ishara kuwa nyakati zimebadilika, watu wanasimama na kuhesabiwa na ule woga uliojengewa neno la kutisha 'amani na utulivu' umeondoka

Amani na utulivu si kauli mbiu kama wengi wanavyodhani. Huwezi kuhubiri amani na utulivu na ikatokea.
Amani na utulivu ni zao la uwepo wa haki. Kama haki haipo amani na utulivu haviwezi kudumu kama si kutoweka

Hapa ndipo penye kiini cha uchaguzi. Haki itendeke kwa kila mmoja. Asiwepo anayeonea au anayeonewa

Asihukumiwe mtu kwa hisia tu bila ushahidi. Hukumu tunayozungumzia hapa si dhana ya kutaka kuhukumu upande mmoja kwa vile historia inaonyesha abcd. Au kuhukumu upande mwingine kwavile tunadhani itakuwa abacd

Kinachotakiwa ni kusikiliza wananchi wanasema nini. Kitakachoamuliwa na wananchi ndicho kinachopaswa kufuatwa bila kujali ni kwa upande gani au sababu gani. Kwa maneno mengine wananchi waachwe waseme wanataka nini.

Ili kuwaacha wananchi waseme, vyombo husika visimame katika haki ili tuweze kupata uzao wa amani na utulivu

Kinyume chake, kanuni za asili zimeshatupa maono juu ya nguvu inayotokana na umma.

Ni nguvu ya ajabu kwasababu katika historia ya dunia, nguvu ya umma haijawahi kushindwa.

Tuheshimu umma na kuamini kuwa kauli ya wengi ni kauli ya umma.

Wengi ni wapi , ni swali la muda

Tusemezane
 
Mkuu Nguruvi3 nini matarajio yako kwa post namba 251 je tume itafanya yanayotegemewa? Yaani haki au itaendelea na staili yake ya kusikiliza aliewachagua?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nguruvi3 nini matarajio yako kwa post namba 251 je tume itafanya yanayotegemewa? Yaani haki au itaendelea na staili yake ya kusikiliza aliewachagua?
Mkuu hili swali ni gumu kwa kuzingatia kuwa hatujui nini kinaendelea na mapungufu ya habari

Tunachoweza kusema ni kuwa haki si itendeke tu bali ionekane inatendeka

Kutendeka kwa haki ni kusimamia misingi ya sheria kanuni na taratibu

Kuonekana inatendeka ni pamoja na process nzima kuwa ya uwazi , penye mashaka kufafanuliwa n.k.

Kazi ya tume ni kuhakikisha uchaguzi unakuwa fair and free na kwamba mshindi na aliyeshindwa wanakubaliana na maamuzi ya wananchi. Si kazi ya tume kupanga kazi za wananchi na kama uchaguzi utaingilia shughuli zao

Ili kuweza kuondoa mashaka miongoni mwa wana jamii, tume ihakikishe kila hoja inajibiwa kwa mantiki na weledi

Kwa mfano, kama tume imeamua kuchukua wataalam kadha kutoka eneo fulani, tume ina wajibu wa kueleza kwanini hatua hizo zimechukuliwa, zimelenga kufanikisha nini na kwa utaratibu gani, hili liyajenga imani na kuondoa mashaka yasiyo ya lazima

Kunapokuwa na hisia ni mwanzo wa kuondoka kwa imani. Imani isipokuwepo haki inaweza kuonekana haipo hata kama ipo

Kuna maswali yasiyo na majibu ya siku nyingi. Haya yanatia wasi wasi kwa wengine pengine kwa kutojua

1. Kwanini wananchi wajiandikishe kwa asilimia kubwa , wapige kura kwa asilimia chache

2. Je, data base ya BVR inafanya kazi kama ilivyokusudiwa? Majina ya wapiga kura yapo kama ilivyotarajiwa?

3. Inakuwaje hadi leo watu hawajui matokeo kamili ya uchaguzi wa 2010.
Maana tuliambiwa kuna maeneo yalikuwa bado yanafanyiwa kazi.
Mara tukasikia hata kama yangehesabiwa yasingeweza kubadili matokeo.

Hoja si kubadilisha matokeo, hoja kubwa ilikyokuwepo ni kuwa kila kura lazima ihsabiwe.
Je, za mwaka 2010 zilihesabiwa zote? Kama sivyo, ni kwanini

Tumeona chaguzi nyingi duniani zikitibuka kutokana na kukosekana kwa haki na tume za uchaguzi kutokuwa wazi na makini katika kazi zao. Tunao mfano mzuri sana wa Kenya uliopelekea mauji na taifa kuparaganyika

Lakini pia tuna mifano mizuri. Nigeria iliyokuwa na matatizo kwa miaka mingi, imefanya uchaguzi na kuduwaza dunia.
Rais mmoja akimpa kijiti mpinzani wake kwa amani na utulivu.

Tumeona Ghana ikiwa taifa lililofanikiwa sana katika uchaguzi. Ghana ilikuwa nchi ya kupinduana kila asubuhi.
Kwa miaka kumi iliyopita, Ghana imekuwa mfano wa uchaguzi wa haki barai Afrika

Tumeona sehemu nyingi pia kukiwa na utulivu. Dunia ya sasa imebadilika na watu hukaa kitako katika kuienzi demokrasia
Lakini pia tunaona misururu ya watu wa Libya, Syria wakipoteza maisha katika bahari

Japo tatizo si uchaguzi, tunaweza kuona mateso wanayopata wananchi kutokana na kuvurugika kwa amani na utulivu
Wanaolipa gharama ni akina mama , wazee na watoto

Tanzania tungependa tubaki kama mfano wa kuigwa. Kila mmoja awajibike kwa nafasi yake tukijua kuwa umoja na usalama wetu sote ni jukumu letu na si kikundi au kundi la watu.

Taasisi zilizopewa dhamana zitambue zinafanya kazi katika mazingira ya amani.

Kinyume chake matatizo hayachagui na tusije fika huko. Hatuna sababu ya kuwa na dua za kutakia taifa amani, tunasababu za kuwajibika kulitakia taifa amani. Njia nzuri ya kuwajibika ni kusimama pamoja katika njia ya haki na ukweli.

Haki na ukweli utatekelezwa na kila mmoja wetu. Hatupendi kuona taasisi za umma zenye masilahi mapana na majukumu mazito zikivutwa na kuingizwa katika mchezo wa siasa.

Tuache umma uamue na kauli ya umma iheshimiwe kwa vitendo

Kama kuna tatizo basi chanzo chake kitakuwa kuminywa kwa haki kwa kutumia ghilba
 
Je huoni kama vyama vya upinzani kwa kuchelewa kudai tume huru kama Kenya ni kosa? Kama ni kosa kwa muda huu tutarajie huruma au uwajibikaji usio egemea upande mmoja ambao ni ngumu. Nini ni way forward kwa hapa tulipo?
 
Kuhusu kudai tume huru ya uchaguzi, hili suala lina sura nyingi kidogo

1. Tuliwaeleza wapinzani baada ya uchaguzi 2005 na ule wa 2010 kuwa bila tume huru mambo yatakuwa mazito.

Kwa bahati mbaya hawakusikiliza wakajikita katika mambo mengine

2. CCM walijua karata waliyo nayo ni katiba ya sasa na tume huru ya sasa.

Walitumia wingi wao ku-block move yoyote ya kuwa na tume huru.

Tena hapa tuseme ukweli, hawa akina Lowassa na wenzake walikuwa sehemu ya tatizo hilo.

Leo tunaweza kusema 'chicken are coming home to roost' Kwamba kuku wanarejea nyumbani kutamia mayai waliyotaga

Hapa liwe funzo kwa wanasiasa kuwa hakuna hali ya kudumu katika maisha, that's no permanent situation.

Wanasiasa waliopinga tume huru na mgombe binafs na katiba wote ni waathirika wa wa kupelekeshwa mbio kwa jina la 'wingi'

3. Hata kama wapinzani wangevalia njuga bado CCM wangetumia wingi wao.

Hapa hakuna contradiction ya maelezo kwa maana kuwa wapinzani walipaswa kulianzisha na kutafuta kuungwa mkono na wananchi

4. Katiba mpya iliwapumbaza sana na kudhani ili mikutano ya siri magogoni ilikuwa na maana yoyote

Tuliwaeleza lazima wawe waangalifu, kuna ghilba. Mkuu wa CCM hawezi kutenda tofauti na falsafa ya udanganyifu ya chama chake

Way forward

Hakuna namna lazima kwanza mfumo uliopo wa ghilba na matumizi mabaya ya wingi uvunjwe kabisa

Wananchi wana nafasi hiyo katika njia tatu kuu

1. KKuchukua umiliki wa bunge ili kuzuia uhalifu uliotumia wingi kupitisha sheria kibabe

2. Kumiliki bunge na dola na kubadilisha mfumo kabisa

3. Kumiliki dola ili iwe na unfluence katika kubadili mfumo

Njia zipi watumie

Njia ya kwanza, ni kuwataka wapinzani waweke wazi, katika kipindi fulani watafuta sheria na kufumua mfumo huu wa CCM

Njia ya pili, kupeleka wawakilishi wengi ili kuchukua hatma ya bunge kabisa

Njia ya tatu, kuchukua umiliki wa vyombo vyote na kufumua mfumo

Hapa pressure si kwa CCM bali kwa wapinzani.

Lazima waonyeshe wananchi kuwa kweli wamedhamiria kubadili nchi katika mwelekeo na si kugawana vyeo.

Hawa UKAWA wa prove hilo wakati wa kampeni kuwa wanachokifanya kitatoa matokeo chanya.

Kinyume chake, itakuwa kuweka mvinyo wa zamani katika chupa mpya

All saidi and done, wananchi wana hati miliki ya nchi. Ni wakati wasimame na kusema enough is enough, tunataka mwelekeo mpya.

Tumechoka ghilba na maneno uyasiyo na vitendo. Tunataka kutoa fundisho kwa wanasiasa kuwa siasa ni kazi na si kiti cha enzi.
 
Alinda " Ni wajibu wa tume ya uchaguzi kusoma alama za nyakati, na kuandaa mazingirai mazuri ambayo yatatoa haki bin haki kwa pande zote mbili yaani chama tawala na vyama vya upinzani la sivyo tujiande kwa nchi yetu kumwaga damu.. Huu ndio ukweli ambao tunapaswa kuusema." Hivi ALINDA hii damu unayoisemwa tujiandae kuimwaga ni ya binadamu au mbuzi? tumwage damu sababu ya madaraka au,tufanye damu imemwagika watanzania wote wamekufa,wamebaki wanao ishi NJE YA Tanzania,itakua imekusaidia nini wewe na wenzako mnao tamani damu imwagike kisa madaraka,ishu ya amani ni ya vyama vyote,alianza Mbowe kusema uchaguzi mwaka huu hautafanyika,hivyo damu itamwagika,ajatuomba radhi mpaka sasa watanzania
UTANZANIA WETU NI BORA KULIKO VYAMA VYETU,vyama vyote na viongozi wao na wafuasi wao wajiepushe na kauli za uchochezi,upinzani na CHAMA tawala
Mungu ibariki Tanzania
 
Last edited by a moderator:
Alinda " Ni wajibu wa tume ya uchaguzi kusoma alama za nyakati, na kuandaa mazingirai mazuri ambayo yatatoa haki bin haki kwa pande zote mbili yaani chama tawala na vyama vya upinzani la sivyo tujiande kwa nchi yetu kumwaga damu.. Huu ndio ukweli ambao tunapaswa kuusema."

Hivi ALINDA hii damu unayoisemwa tujiandae kuimwaga ni ya binadamu au mbuzi?

tumwage damu sababu ya madaraka au,tufanye damu imemwagika watanzania wote wamekufa,wamebaki wanao ishi NJE YA Tanzania,itakua imekusaidia nini wewe na wenzako mnao tamani damu imwagike kisa madaraka,

ishu ya amani ni ya vyama vyote,alianza Mbowe kusema uchaguzi mwaka huu hautafanyika,hivyo damu itamwagika,ajatuomba radhi mpaka sasa watanzania

UTANZANIA WETU NI BORA KULIKO VYAMA VYETU

vyama vyote na viongozi wao na wafuasi wao wajiepushe na kauli za uchochezi,upinzani na CHAMA tawala
Mungu ibariki Tanzania
Adharusi , kwanza nimefikiria kwanini umekuja kwa njia uliokuja nayo, sijapata jibu
Nadhani Alinda atakuwa amekuwepo kukujibu kama ataona ipo haja au umuhimu.

Pili, sidhani kama unasoma mabandiko kwa kina au kuyaelewa.
Ningekushauri urudi nyuma kama mabadiko sita hivi ili upate weledi wa nini kinaongelewa

Tatu, nadhani una duku duku la pembeni zaidi ya mada.
Unapoingiza hisia, fikra , maoni au chuki bila kuongozwa na mada si kutendea haki mjadala na hilo linasikitisha

Nne, suala la amani na utulivu wengine tumelifafanua vizuri na mara nyingi .
Tumesema kuwa amani na utulivu si suala la kundi au kikundi cha watu, ni suala la kila mmoja wetu wewe na mimi
tukiwemo.

Tukaeleza, amani si neno au mashudu ya ng'ombe. Ni zao linalotokana na kile kinachoitwa haki.
Kwamba huwezi kutenga amani na haki , hawa ni mapacha

Tano, hujamtendea haki Alinda kwa mtazamo wangu. Ungesoma sentensi yake ya mwisho ungeleewa anazungumzia nini.

Alichosema ni maoni yake akisisitiza kuwa yapo mambo yanayopaswa kusemwa ili sote tuwe salama.

Hoja yake ni kuwa hakuna taboo ya kuongelea hatari inayoonekana, maana taboo inaweza kuficha tatizo.
Sijui kutoa kwake tahadhari kumekuudhi nini hadi kufikia mahali pa kumshambulia

Sita, kuhusu suala la Mbowe, ukumbi huu ni haki yako. Unaweza kuandika maoni yako iwe hapa au pengine ukizingatia sheria na watu wakasoma.

Unapomzungumzia Mbowe kama unamshtaki katika uzi huu hujatutendea haki.
Unategemea tufanye nini zaidi ya wewe unayeujua ukweli na hujauandikia kitu?

Saba, unaposema Alinda na wenzake, tungependa kujua hao wenzake ili tusoma nao wameandika nini.

Tutakapoona kile tusichokiona tutakushukuru sana na hakika atakayekuwa nje ya mstari tutamwambia.
Hadi hapo tusaidie hao wenzake Alinda na wapi tena?
Hapa tutakuomba utujibu maana ni mahali tunapohitaji kupajua, na tunadhani unawajua na si majungu. Ni wapi hao?

Nane, hakika nchi hii ni yetu sote na sote tunaipenda. Kuipenda ni pamoja na kuitakia mema.
Mema hayazungumzwi vichochoroni yanaongelewa barazani.

Sasa jema ni lipi na baya ni lipi hayo yapo katika jicho na masikio ya msikilizaji.

Hatudhani kama una haki ya kuchagulia watu lipi ni jema kwa mujibu wako.

Hata hivyo una haki ya kuzungumzia jema kwa maoni yako.

Tisa, tafadhali tungeomba usiingize hisia zako ili kuonyesha kuna tatizo katika mjadala.

Kama lipo liweke wazi na usimwekee mtu au watu maneno. Usichague maneno yako yakawa ya uzi au mada.

Tunaendelea wana jamvi
 
Last edited by a moderator:
Alinda " Ni wajibu wa tume ya uchaguzi kusoma alama za nyakati, na kuandaa mazingirai mazuri ambayo yatatoa haki bin haki kwa pande zote mbili yaani chama tawala na vyama vya upinzani la sivyo tujiande kwa nchi yetu kumwaga damu.. Huu ndio ukweli ambao tunapaswa kuusema." Hivi ALINDA hii damu unayoisemwa tujiandae kuimwaga ni ya binadamu au mbuzi? tumwage damu sababu ya madaraka au,tufanye damu imemwagika watanzania wote wamekufa,wamebaki wanao ishi NJE YA Tanzania,itakua imekusaidia nini wewe na wenzako mnao tamani damu imwagike kisa madaraka,ishu ya amani ni ya vyama vyote,alianza Mbowe kusema uchaguzi mwaka huu hautafanyika,hivyo damu itamwagika,ajatuomba radhi mpaka sasa watanzania
UTANZANIA WETU NI BORA KULIKO VYAMA VYETU,vyama vyote na viongozi wao na wafuasi wao wajiepushe na kauli za uchochezi,upinzani na CHAMA tawala
Mungu ibariki Tanzania

Hivi wewe uwe unasoma na kuelewa maana nzima ya mstari au maana mzima ya paragraf? au unasoma neno moja na kulitungia maana unayoelewa wewe?

Vijana (kwa maandishi nategemea kuwa wewe ni kijana) mstaki kukaririshwa kama watoto wadogo, jifunzeni kusoma na kuelewa nini dhana mzima ya andishi fulani, wakati mnasoma kitu/ jambo fulani jaribu kulinganisheni mnachokisoma/kiona na hali halisi ya maisha yako au maisha ya watanzania kwa ujumla ukifanya hivyo utaona mantiki nzima ya kitu au jambo linalosemwa.

Hivi kwa akili uliyojaliwa na mwenyezi Mungu kusema "kama haki hisipotendeka kuna uwezekano wa kumwaga damu ni uchochezi? Ni uchochezi wa nini na wa nani kwenda kwa nani?
Je ni kweli haki zinatendeka ktk changuzi zetu? na kama haki hazitendeki unachoshauri ni nini? watu wakae kimya wakiangalia baadhi ya wataule wakisigina haki zao? au watu wapaze sauti zao? na je unafahamu watu wakipaza sauti zao ni nini kinachotokea?

Labda nikupe mfn kidogo tu labda utaelewa ninachomaanisha:

Je unakumbuka 2010 "boss" wako Zitto alitiwa ndani baada ya kuilazimisha tume kutangaza matokeo kama yalivyo?

Je hapo kwa akili zako ni nani mchochezi ni Zitto aliyetaka haki itendeke au ni tume ya uchanguzi uliyotaka kutangaza matokeao jinsi watakavyo wao?

Pia kwani watanzania kumwaga damu ni mara ya kwanza? Si ulisikia kiongozi wako mkuu akisema "wakati wanakigoma wakipigwa mabomu watu wa Arusha Iringa walikuwa wanakumbatia watawala! Labda nikuulize je hiyo damu uliyomwagika miaka ya 1990 huko mkoani Kigoma ilikuwa ni damu ya Mbuzi au ya binadamu? Na je hii damu ilimwagika kwa ajili ya madaraka au kwa ajiri ya kutaka haki sawa?

Hakuna ninachochukia kuona kijana kama wewe mtu ambaye ungekuwa mstari wa mbele kutaka haki sawa, kupigania haki zako, haki za watoto wako, haki za mkeo, haki za wazazi wako, unalishwa propoganda tena propoganda unazolishwa unalishwa na mtu kama Nape na wewe hauhoji bali unazitafuna na kumeza huu ukigawia watoto wako(km unao).

Nitapenda ujibu hayo maswali maana wewe unafahamika kwa "kusepa"
 
Umenena vema Alinda

Kwa mujibu wa mwezentu huyu suala la umwagaji damu ni la wapinzani kina Mbowe pekee, sio la watawala wanaotumia vyombo vya dola kukong'ota watu kila siku hata pale wanapoamua kukusanyika kwa amani kwa mujibu wa haki yao kikatiba!
Kwa mujibu wa mwenzetu huyu suala la umwagaji damu sio la kina Pinda waliosema "wapigwe tu" au "liwalo na liwe".
Kwa mujibu wa mwenzetu huyu umwagaji wa damu sio kauli za kina Nape kwamba watashinda kwa njia yoyote hata kwa "goli la mkono" ila wakiongea kina Mbowe ndio inakuwa uchochezi na umwagaji damu!
 
Hivi wewe uwe unasoma na kuelewa maana nzima ya mstari au maana mzima ya paragraf? au unasoma neno moja na kulitungia maana unayoelewa wewe?

Vijana (kwa maandishi nategemea kuwa wewe ni kijana) mstaki kukaririshwa kama watoto wadogo, jifunzeni kusoma na kuelewa nini dhana mzima ya andishi fulani, wakati mnasoma kitu/ jambo fulani jaribu kulinganisheni mnachokisoma/kiona na hali halisi ya maisha yako au maisha ya watanzania kwa ujumla ukifanya hivyo utaona mantiki nzima ya kitu au jambo linalosemwa.

Hivi kwa akili uliyojaliwa na mwenyezi Mungu kusema "kama haki hisipotendeka kuna uwezekano wa kumwaga damu ni uchochezi? Ni uchochezi wa nini na wa nani kwenda kwa nani?
Je ni kweli haki zinatendeka ktk changuzi zetu? na kama haki hazitendeki unachoshauri ni nini? watu wakae kimya wakiangalia baadhi ya wataule wakisigina haki zao? au watu wapaze sauti zao? na je unafahamu watu wakipaza sauti zao ni nini kinachotokea?

Labda nikupe mfn kidogo tu labda utaelewa ninachomaanisha:

Je unakumbuka 2010 "boss" wako Zitto alitiwa ndani baada ya kuilazimisha tume kutangaza matokeo kama yalivyo?

Je hapo kwa akili zako ni nani mchochezi ni Zitto aliyetaka haki itendeke au ni tume ya uchanguzi uliyotaka kutangaza matokeao jinsi watakavyo wao?

Pia kwani watanzania kumwaga damu ni mara ya kwanza? Si ulisikia kiongozi wako mkuu akisema "wakati wanakigoma wakipigwa mabomu watu wa Arusha Iringa walikuwa wanakumbatia watawala! Labda nikuulize je hiyo damu uliyomwagika miaka ya 1990 huko mkoani Kigoma ilikuwa ni damu ya Mbuzi au ya binadamu? Na je hii damu ilimwagika kwa ajili ya madaraka au kwa ajiri ya kutaka haki sawa?

Hakuna ninachochukia kuona kijana kama wewe mtu ambaye ungekuwa mstari wa mbele kutaka haki sawa, kupigania haki zako, haki za watoto wako, haki za mkeo, haki za wazazi wako, unalishwa propoganda tena propoganda unazolishwa unalishwa na mtu kama Nape na wewe hauhoji bali unazitafuna na kumeza huu ukigawia watoto wako(km unao).

Nitapenda ujibu hayo maswali maana wewe unafahamika kwa "kusepa"
Wewe mwanamke sijui Zitto alikukosea nini daah!!!.

Uzi huu unasomeka "CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika".

Lakini nashangaa unamshambulia Zitto.

Chuki ni ugonjwa hatari sana weka maneno ya akiba bibie, zamani povu lilikuwa linakutoka kuhusu ufisadi wa Lowassa, leo hii umekuwa mateka wake unapambana kweli kweli mpaka unatoa angalizo kuwa damu itamwagika.
 
Last edited by a moderator:
HAYA NI MAJIBU KWA wafuatao Nguruvi3 Alinda Mwalimu
Maelezo yangu hayakua na mtazamo mbaya kwangu lengo kuifanya Tanzania salama ya bila Uhasama,wa kisiasa,nimeshangaa nimepigwa mande(kuchangiwa)
MAJIBU kwa Nguruvi3 ;
Mosi,usipate tabu kufikiri,huu uzi si Mara ya kwanza kuchangia Mimi,upitie utaona.
Pili,Uzi huu kila siku kabla ya kulala lazima niupitie,na penye kuchangia na nachangia,jaribu kuperuzi utaona.
Tatu,Sina dukuduku,mbona nimeshawai kuchangia katika uzi huu,nimemrekibisha Alinda na vyama vyote vya siasa (au hili la vyama siasa amkuliona katika andiko langu)
Nne,Nakubali Amani ni swala la wote,ndio maana Mimi nimetoa taadhari kwa Alinda mama yangu(km Ana mtoto wa miaka 30+ kama Mimi),na wale wa gori la Mkono,na yule aliesema atatangaza matokeo kabla ya Tume ya uchaguzi kutangaza(ndio mana nikasema vyama vya siasa).
Tano,Nimemsoma vizuri sana Alinda nimetenda Haki kwa Nchi yangu,na ndio mtazamo wangu,kauli ya kumwaga damu kwangu si kauli njema na wala si Afya kwa Nchi yetu.
Sita,Mbowe anapenda sana kuwa mnafiki,akiwa na watu wa CDM, aliwezaje kusema uchaguzi hautafanyika, wakati yeye sio NEC, na kudai damu itamwagika, Mbowe lazima atuombe Radhi kutuletea taharuki kwa kauli ya kumwaga damu, mpaka Leo mwana mama Alinda anaona jambo la kawaida kumwaga damu.
Saba,Wenzake kina Alinda ni kina Marando,Mbowe, Nape,Mnyika,Lema,Pinda wote wanaopenda kauli za kuleta vurugu.
Nane,Sote tunaipenda Nchi yetu,ndio mana pale nimemalizia Tanzania Yetu ni bora kuliko vyama vyetu,pia sijamchagulia mtu la kusema,Ila mtu akisemwa kauli za hatari kwa taifa,siwezi kunyamaza kamwe,ndio maana katika maelezo ya ALINDA nimemkosoa mwisho tu,nilikua na uwezo wa kumkosoa mwanzo tu wa maelezo yake,maana akua na uhakika na alishopost,anasema kabisa kama ni kweli hii picha,rejea maelezo yake katika ile picha, kwanini amalize na neno la umwagaji damu, kwa picha ambayo Hana uhakika.
Tisa,Sijamuwekea maneno Alinda, ndio maana nimemnukuu,si maneno yangu.

**Sehemu I
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom