Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #241
Wanajamvi tunalirudia bandiko hili kwa makusudi zaidi ilimjadala unaofuata punde ueleweke.MBINU NA CHANGAMOTO ZA CHAGUZI
Chaguzi huambatana na mbinu , mikakati na changamoto
Chaguzi huwa na makundi ya wapiga kura. Kwa hali ya kisiasa yapomakundi yafuatayo
(1) Kundi linalopiga kura ya hasira- hili ni lile lisilo naupande, lilichoshwa na hali iliyopo
(2)Kundi la wanachama watiifu, hili linachagua tu kutokanana vyama iwe ni CCM, UKAWA au kingine
(3) Kundi lenye mashaka- hili halina uhakika lisimame wapi namara nyingi huangalia hoja ingawa si jambo linalotazamwa sana ukilinganisha na personality
CCM inategemea makundi 2 na 3 kwasababu tayari ni mwathirika wa kundi la 1
Wapinzani wana ‘advantage' ya makundi yote. Ushindani upo kundi la 3 litakaloamua nani anashinda majimbo au dola
Wapinzani kama ilivyo kwa CCM, wana ‘disadvantage'.
Kwanza, uwezowa kufikia jamii una vikwazo tukijua CCM ina mtandao wa wakuu wa mikoa na wilaya na rasilimali za umma.
Pili,CCM wanaserikali inayomiliki vyombo muhimu.
Mfano, zipo taasisi za nishati zinazolalamikiwa kutotenda haki kwa maagizo ya serikali ili kuwanyima wananchi habari
Vyombo vya habari vinavyoegemea CCM, na vyombo vya dola kutumika vibaya
Ushindi hautaamuliwa kwa hesabu za kura, yapo mengine ambayo kama hayataangaliwa yatabadili mwenendo wa uchaguzi
Kwa mfano,hatujawahi kupata majibu ya kwanini watu wajiandikishe kwa asilimia 70 , wapiga kura wawe asilimia 30.
Kuna nini kinaendelea ambacho serikali au tume ya uchaguzi imeshindwa kubaini?
Mfumo wa pili , BVR, je, umehakikiwa kufanya kazi kamailivyokusudiwa?
Kukiwa na matatizo ya kifundi au ‘kufundwa' itakuwa ni kwa maumivu ya wapinzani
Lipo suala la ‘voters suppression' kusudio ni kuzuia watu wasitumie haki ya kura kwa udanganyifu kama ule wa 1995 watu walipoambiwa siku ya kwanza ni CCM na ya pili wapinzani
Au inaweza kuwa vitisho kwa wapiga kura (2010) kwa jeshi kutoa tamko, au kutumika nguvu za dola kwa namna yoyote.
CCM wanakiri hali ngumu inayowakabili. Istegemewe CCM itatoa dola au bunge au vyote katika kisahani cha dhahabu.
Itapigana hadi tone la mwisho ikitambua kuwa KANU imetoweka kama ilivyo UNIP
Kitakachosaidia wapinzani ni ushindi usio na shaka ‘decisive victory'.
Itawezekana wakijiweka vema kupambana na hila, kukabiliana na hoja, kujenga hoja na kujibu hoja.
Kuzuia uharibifu kwakushambulia na si kujilinda ni muhimu kwao.
Kuwepo na uthubutu ‘courage' ya kupambana na changamoto si chaguo ni lazima kwa wapinzani
Tusemezane
Yanayofuata, vyombovya dola na daftari la kura