CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

Nitakusahihisha jambo moja na ambalo labda halikueleweka. Katika andiko langu lile nilieleza jinsi gani ilivyo ngumu kuchakachua kura za Ubunge. Nilieleza na sheria haijabadilika kuwa kura za Ubunge zinahesabiwa na kutangazwa kituoni; hata kura za Urais ni hivyo hivyo na ndivyo ilivyotokea mwaka 2010. Kitu ambacho kilitokea ni kuwa agizo/amri haikutolewa kuzuia kutangazwa matokeo ya kura za Urais hadi yapelekwe NEC. Amri iliyotolewa ni kwa vyombo vya habari kutokutangaza matokeo ya Urais hadi yatakapotangazwa "rasmi" na NEC. Kwa maneno mengine, matokeo ya Urais yalitangazwa majimboni kama sheria inavyotaka - wasingeweza kutuma bila kuyatangaza ila vyombo vya habari havikuweza kutangaza hadharani kabla ya NEC. Hivyo, maripota wa TV au radio kina Ufoo Saro, George Marato na wenzao walipopewa nafasi ya kutangaza matokeo walikuwa na matokeo ya Urais mkononi lakini mabosi wao wa ITV waliwaambia wasiwaambie yale ya Urais bali yale ya Ubunge kwanza..

Kwahiyo mpaka hapo unaona pamoja na kuwepo sheria ya kutangaza matokeo vituoni, bado serikali hakuruhusu matoke hayo yatangaze na vyombo vya habari maana walijua kuwa kama vyombo vya habari vingetangaza basi wasingeweza kuchakachua. Na kilichofanyika Tume ya uchaguzi walitangaza matokeo ambayo ni ya uongo kwani kulikuwa hakuna tena kitu cha kuwafanya wasifanye hivyo. Na ninakumbuka mgombea wa urais kupitia Chadema yaani Dr. Slaa alilalamikia tume kutangaza matokeo ambayo hayakuwa ya kweli. Hivyo basi kusema kuwa CCM hawawezi kuchakachua kwa vile matokeo yanatangwa vituoni hali vyombo vya habari hawaruhusiwi kuyatangaza ni kujidangaya maana watakachuchua maeneo ambayo ni ya vijijini, wananchi hawana umeme, Tv za kuweza kuona kama klichotangazwa katika vituo vyao vya kupigia kura ndicho kinachotangazwa na tume!

Kwenye Ubunge nako ni vile vile pamoja na kutangaza matokeo vituoni bado kulikuwa na udangayifu mkubwa na uvunjwaji wa sheria rejea mbunge aliyekimbia na masanduku ya kura na tume limtangaza kuwa ni mshindi.au ucheleweshaji wa matokeo kwa maeneo yalioshinda wapinzani mf.Mwanza, Arusha na maeneo mengine, umwagikaji wa damu sehemu ambazo wapinzani walifanya vizuri na nk. Hivyo basi hatuwezi kuja hapa kujipa matumini kuwa tume itafanya tofauti na miaka ya nyuma.

Kikubwa wananchi wahimizwe baada ya kupiga kura basi walinde kura zao maana naona njia hii inasaidia kwa kiasi fulani.

Kwanini? kwa sababu matokeo ya awali ya Urais yaliyokuja kutoka sehemu ambayo tayari yalikuwa yametangazwa na yale ya Ubunge yalionesha Dr. Slaa alikuwa anaongoza. Ilibidi wazuie hadi mikoa ya Lindi, Mtwara, Tabora na Tanga ilipoanza kuleta kura zake ndiyo Tume ilipokuwa inatangaza kura za Urais ikaanza na mikoa ile ya ngome ya CCM. Hawakuanza na kura ambazo tayari wengine walikuwa nazo za mikoa ambayo wapinzani (CDM) walikuwa tayari wamepata kama Arusha, Musoma Mjini, Mbeya mjini n.k.

Ukilielewa hili utaelewa kwanini walijitahidi sana kupitisha sheria ya Cybercrime na kudhibiti takwimu. Kama siyo rasmi siyo sahihi hata kama ni sahihi.

Hiki si kweli kama ingekuwa ni kweli, na kama wangekuwa wanajiamini kuwa mikoa hiyo kuna kura nyingi za CCM basi wangeacha TV/redio sikakusanya matokeo na kuyaleta kama yalivyo na kwa jinsi hiyo watu wangeona wenyewe jinsi kura za CCM zinavyoongezeka kutoka katika mikoa hiyo. Walichofanya baada ya kuona Dr. Slaa anaongoza, na kupata matokeo ya hiyo mikoa kulikuwa hakuna jinsi zaidi ya kuchakachua tu..

Leo hii nikikuuliza Mkoa wa Mbeya vijijini CCM walipata kura ngapi za urais si dhani kama kunajibu la ukweli kilichopo (kama kipo) ni namba za kubumba.
 
Kwahiyo mpaka hapo unaona pamoja na kuwepo sheria ya kutangaza matokeo vituoni, bado serikali hakuruhusu matoke hayo yatangaze na vyombo vya habari maana walijua kuwa kama vyombo vya habari vingetangaza basi wasingeweza kuchakachua.

Ndio maana ni muhimu sana kufikiria namna gani matokeo yataweza kutangazwa regardless ya kutotangazwa na vyombo vya habari. Tulikuwa na mkakati mzuri sana this year lakini ujio wa Lowassa umevuruga kila kitu.

Na kilichofanyika Tume ya uchaguzi walitangaza matokeo ambayo ni ya uongo kwani kulikuwa hakuna tena kitu cha kuwafanya wasifanye hivyo. Na ninakumbuka mgombea wa urais kupitia Chadema yaani Dr. Slaa alilalamikia tume kutangaza matokeo ambayo hayakuwa ya kweli. Hivyo basi kusema kuwa CCM hawawezi kuchakachua kwa vile matokeo yanatangwa vituoni hali vyombo vya habari hawaruhusiwi kuyatangaza ni kujidangaya maana watakachuchua maeneo ambayo ni ya vijijini, wananchi hawana umeme, Tv za kuweza kuona kama klichotangazwa katika vituo vyao vya kupigia kura ndicho kinachotangazwa na tume!

Hilo wala halina ubishi; lakini nalo si makosa ya CCM ni makosa ya upinzani wenyewe kujipanga. Nimeeleza hapo juu sijui kama umeona. Mwaka 2010 siku ya Uchaguzi viongozi wote wakuu wa chama walikuwa wamebanwa majimboni mwao - hakuna aliyekuwa anasimamia au kupigania kura za urais wote walikuwa wanapigania kura za ubunge maana wangetoka kidogo tu wangelia. Mwaka huu kuna tofauti? Nope. Viongozi wale wale wameenda tena majimboni halafu wanamtegemea Lowassa kushinda kwa mapenzi ya Mungu.

Kwenye Ubunge nako ni vile vile pamoja na kutangaza matokeo vituoni bado kulikuwa na udangayifu mkubwa na uvunjwaji wa sheria rejea mbunge aliyekimbia na masanduku ya kura na tume limtangaza kuwa ni mshindi.au ucheleweshaji wa matokeo kwa maeneo yalioshinda wapinzani mf.Mwanza, Arusha na maeneo mengine, umwagikaji wa damu sehemu ambazo wapinzani walifanya vizuri na nk. Hivyo basi hatuwezi kuja hapa kujipa matumini kuwa tume itafanya tofauti na miaka ya nyuma.

Hapa sidhani kama umeelewa. Tume haitangazi matokeo ya Ubunge yanatangazwa majimboni. Sasa kama jimboni hamkujipanga ndo itakula kwenu! Mgombea mwingine akikimbia na sanduku la kura tatizo siyo tume; wakichelewa kutangaza matokeo wakati tayari yameshakamilika huilii tume. Nitakumbusha kitu kimoja kama umesahau; wakati Nassari anagombea Arumeru Mashariki zilifanyika jitihada kubwa kuvuruga matokeo; nilitumia vyanzo vyangu kutangaza ushindi wa Nassari hapa JF, hakukuwa na jinsi isipokuwa kumtangaza Nassari ushindi. Sasa, kama huna wawakilishi wa kuaminika kura zako zinaweza kuchezewa; huwezi kutegemea huruma ya CCM kushinda. CDM wanataka kushinda "by any means necessary"? CCM wanataka kubakia madarakani "by all means necessary".

Kikubwa wananchi wahimizwe baada ya kupiga kura basi walinde kura zao maana naona njia hii inasaidia kwa kiasi fulani.

Hakuna kulinda kura per se bali kuhakikisha matokeo yanatangazwa. Kura huwezi kuzilinda zaidi ya zilivyo kwenye maboksi; la maana ni kuhhakikisha kura zote halali zimehasabiwa na kuandikwa zilivyo na kutangazwa mbele ya wajumbe na kubandikwa nje. Hiki ndicho watu wanatakia kugombania.

Hiki si kweli kama ingekuwa ni kweli, na kama wangekuwa wanajiamini kuwa mikoa hiyo kuna kura nyingi za CCM basi wangeacha TV/redio sikakusanya matokeo na kuyaleta kama yalivyo na kwa jinsi hiyo watu wangeona wenyewe jinsi kura za CCM zinavyoongezeka kutoka katika mikoa hiyo. Walichofanya baada ya kuona Dr. Slaa anaongoza, na kupata matokeo ya hiyo mikoa kulikuwa hakuna jinsi zaidi ya kuchakachua tu..

Ni kujidanganya sana kudhania kuwa hakuna watu wanaipenda kweli CCM na wako tayari kuona inatawala tena. Kufikiria kuwa ushindi wa upinzani unaporwa tu na kuwa hawashindwi kweli nalo siyo sahihi. Tanzania ina watu wenye kuipenda CCM kweli na wapinzani hawajaweza kuwashawishi wote. Na yapo maeneo ambayo ni ngome ya CCM, kama vile yapo maeneo ambayo ni ngome ya upinzani. Kudhania vinginevyo ni kutokuwapa credit Watanzania. Wapo watu wanaamini kabisa kuwa CCM haipendwi ila inashinda kwa hila tu. Hili si kweli. Siyo Watanzania wote wanaipenda CHADEMA.

Leo hii nikikuuliza Mkoa wa Mbeya vijijini CCM walipata kura ngapi za urais si dhani kama kunajibu la ukweli kilichopo (kama kipo) ni namba za kubumba.

Unajua ni namba za kubumba kama wewe mwenyewe huna namba za kuonesha vinginevyo? Huwezi kudhania tu bila kuwa na ushahidi usiopingika - irrefutable evidence- (tangazo la Msimamizi wa Uchaguzi akitangaza matokeo ya kura hizo na nakala za wawakilishi wako zikikubaliana na tangazo hilo) to the contrary.
 
Alinda

Hapa kuna hoja moja. CCM wakinuia kuchakachua hawawezi kualumiwa kwasababu ndiyo nia na dhamira yao
Utamlaumu vipi mwzi kwa kuiba ikiwa wizi ndio dhamira na nia yake?

Tume ya uchaguzi inapotumia mwanya ulioachwa wazi na wapinzani, nayo hailaumiwi kwasababu tunajua ni 'dugu moja'

Wapinzani wanaposhindwa kusimama kutetea kura zao, hapo kuna kosa.

Ina maana wameshindwa na kutoa loop hole ya kutendewa ubaya.

Kwa mfano, Filikunjombe katangazwa kupita bila kupingwa

Kuna hoja hapa

1. Ilitokeaje ikiwa UKAWA walitumia miezi na miezi kufanya vetting ya wagombea na tukasikia wamegawana

2. Ni nani amekwenda kuthibitisha kuwa lipo tatizo na kwanini limetokea

3, Ni nani atahakiki matokeo, ataongoza usimamizi ikiwa wote wamekwenda majimboni

4. Ni nani kati ya Watanzania atakayekwenda jimbo hilo la Filikunjombe kuhakiki kura za Urais

In fact Mzee Mwanakijiji huenda akawa ndio amewafungua macho kuwa jimbo hilo bado lina maana kwao

Sasa inapotokea mambo ya namna hii, ni lazima kuwaambia ukweli kuwa hawajajipanga.

Na huo ni ukweli wanaotakiwa waishi nao ili siku za mbeleni waubaini kama hawataki kuuzuia
 
Hawakujipanga vizuri huo ndio ukweli, na kikubwa zaidi hata pale walipokua wamejipanga vizuri ujio wa Lowassa UKAWA umewavuruga sana kiasi sasa wamekua hawajajipanga kabisa, nimesikitika suala kama la wagombea walotoka CCM wasioaminika kama Nkumba eti nao wanapewa nafasi ya kugombea na kuwafanyia yaliyotokea, nadhani hili ni funzo kwao, sana.

Ni kweli wengi watakua majimboni, the only solution hapa naiona kama wakitaka angalau kuounguza mianya ya wao kuchakachuliwa kwa namna yoyote, muda kwao sio rafiki, kama wanao watumishi na makada waaminifu toka makao makuu hao inabidi waende wakapamabane kwa kura za Urais maeneo yale ambayo hawajasimamisha wabunge.

Leo nimeangakia taarifa ya habari nikasikitika, kiongozi wa CDM eti anafurahia Filikunjombe kupita bila kupingwa, sasa kama hawa ndio mawakala wa CDM huko majimboni, basi tegemea maafa makubwa sana kwenye kura za urasi maana wanaonekana hawapo honest kwa chana chao na hawajui ni nn wanakiamini.

Kiukweli kabisa UKAWA wana mambo mengi sana ya kuyashughulikia ili kukabiliana na CCM, na kwa namna nionavyo muda sio rafiki kwao kabisa, sijui watawapata wapi watu waaminifu wa kuwasaidia kupambana na hila zozote za wapinzani wao.

kimsingi nawaona kama vile hawakujipanga vema na kuna ukurupukaji mwingi huku wakitegemea huruma za wanachi, kitu ambacho Nguruvi3 amepambana nacho sana kule duru za Siasa kwenye nyuzi za kuelekea uchaguzi mkuu na kuwakemea viongozi wao kutegemea hilo bali inabidi waweke mikakati ya kushinda na sio kutegemea huruma, sasa sijui wao walikua wanawaza tu habari za mafuriko badala ya kufikiria namna bora na kujipanga.

Kwa hakika uchaguzi huu upinzani ukishindwa kukamata moja ya mihili ya dola wajilaumu wenyewe, maana upepo ulikua upande wao na nyota njema ilikua inawaangukia wao, ila jeuri, kiburi cha kupendwa na ubinafsi bila kuwa na mipangilio mizuri na mikakati ya ushindi ni vitu ambavyo naviona vinawakwamisha.
Naungalia uchaguzi huu kipekee sana, na kila nikafikiria makosa ya wapinzani na kuchokwa kwa chama tawala, nabaki nikiduwaa tu kwamba mbona hawa watu wahaoni hii fursa kwao, tutafakari tuone nchi yetu itafika wapi.
 
Mimi naona watu hapa mnawapa 'pass' CCM na tume yao na kuwananga zaidi watu wa upinzani ilhali the cards are stacked against them no matter how you spin it.

Kilicho cha muhimu zaidi ni kubadili kabisa namna ambavyo tume ya uchaguzi inapatikana na kubadili pia jinsi ambavyo matokeo ya uchaguzi yanavyotangazwa na kuziba loopholes zinginezo zinazotoa upenyo kwa uchakachuzi kufanyika.

Mimi bado sijashawishika kwamba kwa mazingira ya sasa upinzani unaweza kushinda wingi wa wabunge pamoja na urais.

Tume ya uchaguzi inayoteuliwa na mwenyekiti wa CCM si tu haileti picha nzuri bali inanifanya nikose kabisa imani nayo.

Hivi kuna hata mmoja kati yenu humu aliye na imani na hiyo tume iliyoteuliwa na mwenyekiti wa CCM?

Mwenyekiti wa CCM kweli anaweza kuteua tume ambayo haiko beholden kwake na CCM wenzake?

Really?
 
NN Suala la tume ya uchaguzi sijui kama kuna anayesema itakuwa fair hata siku moja
.Imeteuliwa na M/Kiti wa CCM bila kuwa confirmed na authority yoyote

Mwenyekiti wa tume anafuta maagizo ya serikali. Ukisoma mabandiko ya nyuma tumeorodhesha mambo ambayo serikali ikisema, tume inadakia na kutekeleza

Hadithi iliyopo ni ya kuku na yai. Kipi kimeanza? Kwamba wapinzani wamiliki mhimili mmoja ili walazimishe au wamiliki dola

Jaribio la kudai tume huru lilifanyiwa mizengwe na wapinzani wakaingia mkenge

Tuliwaambia kile walichokuwa wanazungumza magogoni kisiwe siri. Wakapuuza tukawaona wakinywa Juisi

Tuliwaeleza magogoni hakuaminiki, leo Lowassa anaweza kuthibitisha

Kuhusu kupata wabunge, kama wameweza kupata 80 wanashindwaje kupata 130?

Maana hesabu zao ni za kuzuia 2/3 inayotumiwa na CCM kama sikushika dola au bunge

Wananchi wamechoka, lakini je, zipo mbinu za kukabiliana naCCM?

Kumbuka CCM hata wakipumulia mashine bado wana ‘manesi'wengi kama tume ya uchaguzi

King Suleiman kasema yote, tumewambia wasitegemee huruma za wananchi

Uchaguzi si kura ni zaidi ya hapo. Mikutano na mikusanyiko haitoshi kuwapeleka wanapotaka lazima wawe na mbinu nyingine za kuzuia nakushambulia Huu mchezo wa off side trick wakisubiri wananchi wafunge hauwasaidii

Kama unadhani tuna wananga, hebu jiulize vikao vya UKAWA miezi na miezi vimesihia kwa jimbo kutokuwa na mpinzani.

Hakuna sababu zozote za maana kwasababu kama wanaweza kutumia helkopta kufanya kampeni, wangeweza kutumia helkopta kuhakikisha wanasheria wanatua kila jimbo kuhakiki fomu na kuzuia hujuma

Leo hakuna maelezo ya kwanini majimbo kadhaa yameshapotea

Huwezi kupoteza majimbo ukategemea tume itakupa mwanya ukijua ni ya upande mwingine

Tumeuliza katika majimbo waliyopoteza kuna mtu wa kusimamia kura za Urais?
Kuna sababu gani wamepoteza majimbo hayo?

Kazi ya kugawana ililenga nini? Ni chama gani kimepoteza majimbo hayo?

Mbowe alipata exhaustion au fatigue kutokana na maandaliziya mgombea kuchukua fomu.

Ningemuelewa kama leo angekuwa na exhaustion kueleza kwanini wamepoteza Ludewa!

Wapinzani wana karata azote mkononi, ushindi si wingi wakarata bali watazicheza vipi
 
Nikufikiria kwa mara nyingine "Fursa" ya ujio wa Lowassa ilivyochezewa kama shilini cho cha shimo, nashindwa kuelewa munkari uliotokea Ukawa mpaka wakapoteza mwelekeo.

Nafikiri kukosekana kwa kuwa na timu maalum zenye kufanya ground work (kutokuaminiana) na walio wenyeviti kung'ang'ania na kutaka kushikilia kila kitu kwa sababu wanazozijua ndiko kutakako waangusha Ukawa.

HIvi Lowassa si tunajua alikuwa na timu iliyojisuka vizuri kabisa ndani na nje ya CCM na walijiandaa vizuri kabisa? je hao wadhamini laki nane si walipatikana kutokana na yeye kujijenga na kuielewa vita na kuuelewa ugumu wa kazi yake ndani ya CCM?

Je Ukawa kabla ya "Rizki" Lowassa kuwaangukia, walikuwa wamejipanga vipi ki-oganaizesheni kuingia uchaguzi huu? je walitarajia suala la hoja tuu kutokana na atakayeteuliwa kuwa mgombea wa CCM?

Walipoanza Tongozana viongozi, wale watendaji (technocrats, organizers, lawyers, finance managers, Campaign strategist) kwa nini nao hawakuanza kwa kasi kuunganisha nguvu kama walikuwa wameshasomana tangu awali kama maadui?

i am totally lost in the amount of disorganization ya kuingia uchaguzi mkuu na tunajiandaa kisaikolojia kuwa goli la mkono ndio litawapa CCM ushindi huku tunaona wazi kuna madhaifu ya wazi!

May be I am too naive or have too much expectations after all these years of bashing and demanding strategic planning kwa Ukawa (Wapinzani), hoping watakuwa wasikivu na waelewa.
 
Rev. Kishoka:

Nina swali. Hivi Lowassa kujiunga CDM/UKAWA lilikuwa jambo la dharura au lilikuwa limepangwa? Kwa kasi aliyopokelewa inaonyesha CDM walisubiri hili au baadhi ya viongozi wa juu walisubiri hili.

Vilevile CDM kama chama pekee au ndani ya UKAWA hawakuwa na uhakika na ushindi wowote hule. Inawezekana expectations zako zilikuwa kubwa. Lakini wenyewe pamoja na juhudi za kampeni walizofanya toka 2010 walikuwa wanajua kuwa hawana nafasi.

Tukuridi kwenye mada kamili. Kwa sisi tuliohamua kuwa watazamaji, nadhani itakuwa bora kama mshindi wa uchaguzi wa uraisi ashinde kwa utata. Ashinde kwa asilimia 1% au 2%. Hili utokee mvutano unaweza kuleta serikali ya mseto, na mabadiliko ya haraka ya kikatiba. Hila naomba damu zisimwagike.
 
Zakumi

Kwamba ujio ulikuwa unasubiriwa au ulitokea tu, hilo ni swali gumu na majibu wanayo wenyewe.
Ukiangalia kutoka angle tofauti ni kama vile lilikuwa jambo la kupangwa. Vipo viahiria kama vitatu hivi. Tuachie hapo

Kwamba, mshindi kwa asilimia 50.01 au 51 atalamisha serikaliya mseto, hilo litategemea bunge likoje.
Kumbuka uchaguzi wetu Rais anachaguliwa moja kwa moja na si kutoka bungeni

Rais atakayeshinda hata kwa 0.001 bado atakuwa na nguvu iwapo atakuwa na majority katika bunge na hilo halite mlazimisha kuunda serikaliya mseto

Kwa upande mwingine, Rais atakayeshinda kwa asilimia 60 na kupoteza bunge atalazimika kuunda serikali ya mseto kwasababu hatakuwa na bunge wala wziri mkuu

Ndio maana tunawaambia wapinzani, kuacha majimbo watu wapite bila kupingwa ni hasara kubwa sana.

Kupoteza kiti kimoja cha bunge kunaweza kubadili sura ya utawala kabisa.

Kama unakumbuka bunge la katiba CCM hawakuwa na viti vya kutosha isipokuwa vya Sam six alivyounda unda na laana ikamwangukia

Tatizo ni kuwa ushindi wa asilimia 1 au chini unaweza kutuweka mahali pagumu. Mungu asaidie!
 
Last edited by a moderator:
Nikufikiria kwa mara nyingine "Fursa" ya ujio wa Lowassa ilivyochezewa kama shilini cho cha shimo, nashindwa kuelewa munkari uliotokea Ukawa mpaka wakapoteza mwelekeo.

Nafikiri kukosekana kwa kuwa na timu maalum zenye kufanya ground work (kutokuaminiana) na walio wenyeviti kung'ang'ania na kutaka kushikilia kila kitu kwa sababu wanazozijua ndiko kutakako waangusha Ukawa.

HIvi Lowassa si tunajua alikuwa na timu iliyojisuka vizuri kabisa ndani na nje ya CCM na walijiandaa vizuri kabisa? je hao wadhamini laki nane si walipatikana kutokana na yeye kujijenga na kuielewa vita na kuuelewa ugumu wa kazi yake ndani ya CCM?

Je Ukawa kabla ya "Rizki" Lowassa kuwaangukia, walikuwa wamejipanga vipi ki-oganaizesheni kuingia uchaguzi huu? je walitarajia suala la hoja tuu kutokana na atakayeteuliwa kuwa mgombea wa CCM?

Walipoanza Tongozana viongozi, wale watendaji (technocrats, organizers, lawyers, finance managers, Campaign strategist) kwa nini nao hawakuanza kwa kasi kuunganisha nguvu kama walikuwa wameshasomana tangu awali kama maadui?

i am totally lost in the amount of disorganization ya kuingia uchaguzi mkuu na tunajiandaa kisaikolojia kuwa goli la mkono ndio litawapa CCM ushindi huku tunaona wazi kuna madhaifu ya wazi!

May be I am too naive or have too much expectations after all these years of bashing and demanding strategic planning kwa Ukawa (Wapinzani), hoping watakuwa wasikivu na waelewa.
Naweza kusema mipango yao ilikuwa mizuri tu.

Tatizo lilijitokeza pale akina Lipumba walipoanza kuvuta miguu. Kulikuwa na mivutano isiyo ya lazima.

Kuhusu timu ya Lowassa, tuliwahi kusema katika uzi wa 'kuelekea uchaguzi'
Tuliuliza, hivi hawa UKAWA wamejiandaaje kuhusu huo ujio.Wanawezaje ku accommodate na si ku receive huo ujio.

Wana mpango gani waku-merge hizo timu kwa muda mfupi?

Tulihoji iwapo kulikuwa na analysis ya jambo hilo kwa kina,kuangalia merits au demerits zake.
Kwamba, ilikuwa sahihi na kwa muda sahihi?

Sasa kunakuwepo na timu Ukawa na timu Lowassa halafu majimbo yanapotea, kuna maswali mengi kuliko majibu.

Tuliambiwa utafiti umeonyesha hivyo, Mbowe akisema fursa imejitokeza.
Tulihoji sana kama Mbowe ana uhakika na anachokifanya

Ukisema kuna( technocrats, organizers au lawyers nastrategist) naweza kusema pengine wapo.

Lakini haitoshi kuwa na timu, muhimu ni kuwa na leadership na formation ya timu.
It does matter una wachezaji wazurikiasi gani

Ukitaka kujua kuna tatizo, hadi sasa suala la Ludewa limekaliwa kimya.

Hakuna communication na public nini kimetokea.
Hilo litajenga hali ya kukataa tamaa na ku encourage CCM kuendeleza ubabe kama si uhuni

Tunasikia eti fomu namba 10 ya mgombea haikuwekwa makusudi ingawa ilijazwa.
Kwamba Mkurugenzi alifanya mbinu za kuinyofoa.

Well, hilo linaweza kuwa kweli kabisa kwani CCM wanaweza kufanya lolote ilimradi washinde.

Kwa upande mwingine, kuna maswali ya kujiuliza. Ilikuwaje mtu akabidhi fomu na kuondoka bila kuwa evidence.
Hapo ndipo tume ya chauzi itacheza mchezo maridhiwa

Wakati huo huo kuna mgombea wa CCM amejaza umri wa siku 6.Tume imekaa kimya

Katika hali ya kuwa organized haya yalitakiwa yawekwe hadharani mapema sana.

Tunasikia wa Ludewa kakata rufaa. Kilichotakiwa ni timu nzito ya wanasheria kufika mahali husika na si vijbarua.
Tume hawatishiki na barua wanajua kazi yao

Sasa uongozi mzima sijui upo bize na maandalizi ya kuzindua kampeni au vipi

Wanasema tunawananga, ukweli ni kuwa lazima waonyeshwe mambo wanayofanya.
 
Hapa sidhani kama umeelewa. Tume haitangazi matokeo ya Ubunge yanatangazwa majimboni. Sasa kama jimboni hamkujipanga ndo itakula kwenu! Mgombea mwingine akikimbia na sanduku la kura tatizo siyo tume; wakichelewa kutangaza matokeo wakati tayari yameshakamilika huilii tume. Nitakumbusha kitu kimoja kama umesahau; wakati Nassari anagombea Arumeru Mashariki zilifanyika jitihada kubwa kuvuruga matokeo; nilitumia vyanzo vyangu kutangaza ushindi wa Nassari hapa JF, hakukuwa na jinsi isipokuwa kumtangaza Nassari ushindi. Sasa, kama huna wawakilishi wa kuaminika kura zako zinaweza kuchezewa; huwezi kutegemea huruma ya CCM kushinda. CDM wanataka kushinda "by any means necessary"? CCM wanataka kubakia madarakani "by all means necessary".

Kura za ubunge huko majimboni je zinatangaza na Tume ya uchanguzi au zinatangazwa na chombo gani? hapo tuelewashane.
Mojawapo ya kazi ya tume ya uchaguzi ni kuhakikisha matokeo yanatangazwa pindi yanapomalizika kuhesabiwa, ni kuhakikisha amani, ukweli na uwazi vinatawala wakati wote wa upigaji wa kura mpaka kura zinapohesabiwa na kutangazwa mshindi. Sasa basi inakuwaje mbunge mtarajiwa au hata mwananachi wa kawaida akimbie na masanduku ya kura na tume ya uchanguzi bado itangaze mshindi katika jimbo ilo? Je ni kazi ya vyama vya siasa kulinda mabox yasikwapuliwe, Je ni kazi ya vyama vya siasa kutangaza matokeo kipindi uhesabuji wa kura umalizapo? Jibu ni hapana bali ni kazi ya tume ya uchaguzi.

Kwa msingi huo nashindwa kuelewa unapotupia lawama vyama vya upinzani pale masaduku yanaponyakuliwa au utangazaji wa matokeo kucheleweshwa kwa makusudi.

Kuhusu Arumeru ulifanya kitu kizuri ambacho mimi binafsi ninakupongeza kwa kufanya hivyo. Ila pamoja na hayo ulichokifanya kilitakiwa kunywa na tume ya uchaguzi. Tunategemea hii Tume itende haki kwa pande zote na pale tunapoona tume haitendi haki ni wajibu wetu kuwambia ukweli tusibebeshe mapungufu ya tume kwa vyama vya siasa.

Hakuna kulinda kura per se bali kuhakikisha matokeo yanatangazwa. Kura huwezi kuzilinda zaidi ya zilivyo kwenye maboksi; la maana ni kuhhakikisha kura zote halali zimehasabiwa na kuandikwa zilivyo na kutangazwa mbele ya wajumbe na kubandikwa nje. Hiki ndicho watu wanatakia kugombania.

Ninaposema kulinda kura simaanishi kulinda kwa mitutu ya bunduki na mapanga.. Ni wananchi kutotoka katika vituo vya kupigia kura na hii inafanya hata wale wasimamizi wa vyama vya upinzani kupata nguvu, kutokuwa wanyonge, kutojisikia wapweke, kutoogopa maana wanafahamu kuna watu nje ambao wanawapata nguvu ya kuendelea kuhakikisha kinachotendeka ni haki kwa pande zote mbili au zaidi. Ila kama tungekuwa na tume uhuru basi kusingekuwa na haja ya kukaa kituoni bali unapiga kura na kuondoka na jioni unapata matokeo.

Ni kujidanganya sana kudhania kuwa hakuna watu wanaipenda kweli CCM na wako tayari kuona inatawala tena. Kufikiria kuwa ushindi wa upinzani unaporwa tu na kuwa hawashindwi kweli nalo siyo sahihi. Tanzania ina watu wenye kuipenda CCM kweli na wapinzani hawajaweza kuwashawishi wote. Na yapo maeneo ambayo ni ngome ya CCM, kama vile yapo maeneo ambayo ni ngome ya upinzani. Kudhania vinginevyo ni kutokuwapa credit Watanzania. Wapo watu wanaamini kabisa kuwa CCM haipendwi ila inashinda kwa hila tu. Hili si kweli. Siyo Watanzania wote wanaipenda CHADEMA.

Ninafahamu kuwa kuna watu wanaipenda CCM tena hawa huwambii kitu chochote kuhusu vyama vya upinzani, na hii ni haki yao na kama Taifa lazima tutofautiane bila kuwepo na hizi tofauti hakuna Taifa. Ila ninachokataa ni pale unaposema walitoa amri ya vyombo vya habari kutotangaza matokeo ili wasubiri mikoa fulani ambayo walikuwa wamepata kura nyingi. Na ndio maana nikawambia kama walikuwa wanafahamu kuwa baadhi ya mikoa fulani kuna kura nyingi basi wangeacha vyombo vya habari wakatangaza matokea kadri yanavyoletwa na kama yangeanza kuja yale matokeo ya mikoa yao pendwa basi tungeona jinsi kura za Rais Kikwete zinavyoongezeka...

Unajua ni namba za kubumba kama wewe mwenyewe huna namba za kuonesha vinginevyo? Huwezi kudhania tu bila kuwa na ushahidi usiopingika - irrefutable evidence- (tangazo la Msimamizi wa Uchaguzi akitangaza matokeo ya kura hizo na nakala za wawakilishi wako zikikubaliana na tangazo hilo) to the contrary.[/QUOTE]

Nafahamu kuwa ni No. za kubumba maana no. ya NEC zilitofautiana na kura halisi zilizopigwa. Rejea lalamishi la Dr. Slaa kuhusu tume kutangaza matokeo ya uongo.
 
Alinda

Hapa kuna hoja moja. CCM wakinuia kuchakachua hawawezi kualumiwa kwasababu ndiyo nia na dhamira yao
Utamlaumu vipi mwzi kwa kuiba ikiwa wizi ndio dhamira na nia yake?

Tume ya uchaguzi inapotumia mwanya ulioachwa wazi na wapinzani, nayo hailaumiwi kwasababu tunajua ni 'dugu moja'

Wapinzani wanaposhindwa kusimama kutetea kura zao, hapo kuna kosa.

Ina maana wameshindwa na kutoa loop hole ya kutendewa ubaya.

Kwa mfano, Filikunjombe katangazwa kupita bila kupingwa

Kuna hoja hapa

1. Ilitokeaje ikiwa UKAWA walitumia miezi na miezi kufanya vetting ya wagombea na tukasikia wamegawana

2. Ni nani amekwenda kuthibitisha kuwa lipo tatizo na kwanini limetokea

3, Ni nani atahakiki matokeo, ataongoza usimamizi ikiwa wote wamekwenda majimboni

4. Ni nani kati ya Watanzania atakayekwenda jimbo hilo la Filikunjombe kuhakiki kura za Urais

In fact Mzee Mwanakijiji huenda akawa ndio amewafungua macho kuwa jimbo hilo bado lina maana kwao

Sasa inapotokea mambo ya namna hii, ni lazima kuwaambia ukweli kuwa hawajajipanga.

Na huo ni ukweli wanaotakiwa waishi nao ili siku za mbeleni waubaini kama hawataki kuuzuia

Sikatai kuwa vyama vya upinzani kuna sehemu vinafanya uzembe maana lalamishi la tume ya uchaguzi tumelisikia tangu mwaka 1995 kwa Nccr lakini baada ya uchanguzi hakuna jitihada zozote zilizofanyika ili kuhakikisha walao hii tume inakuwa na huru. Mwaka 2000-2005 kwa Cuf lakini baada ya uchanguzi viongozi wetu wakasahau kabisa kuwa kunahitaji la tume huru, mwaka 2010 kwa Chadema ila baada ya uchaguzi wakajikita katika mambo mengine na wakasahau umuhimu wa tume huru, Sisi kama wadau wa mageuzi tumejaribu kila mara kukumbushia hitaji la tume huru lakini hakuna aliyetilia maanani na mpka sasa hivi unaona vyama vya siasa havina shida na tume, hakuna anayelalamikia tume wameridhika kabisa na hii kitu, Ila subiri uchaguzi umalizike au wakati wa kutangaza matokeo ndio utasikia kilio chao

Ila ninachopinga na nyie ni kitendo cha kuchukua madudu ya tume na kuyabebesha vyama vya siasa, ilo ndilo sielewi, mapungufu ya tume tuyabebeshe tume nyewe na mapungufu ya vyama vya siasa tuvibebeshe vyama vya siasa.
 
Katika mazingira yaliyopo ya bunge kutawaliwa na CCM na kuendeshwa kibabe na Spika kupitisha hoja zao hata kama zina maslahi huku zile za upinzani zikipigwa chini, nini Upinzani walipaswa kufanya kushinikiza Serikali ikubali tume huru ya uchaguzi? Kufanya mikutano na maandamano pekee? Nini cha ziada walipaswa kufanya? Tumeshuhudia kilichotokea kwenye bunge la katiba walivyotumia wingi wao kupitisha mambo kibabe...

Ni kitu gani haswa wapinzani wangeweza kufanya kuishinikiza serikali isalimu amri kwenye jambo hili ambalo kwa vyovyote hawako tayari kulibadili sababu lina maslahi kwao? Rais ndie mwenyekiti wa chama tawala mwenye nguvu juu ya mihimili yote ya dola wanapledge loyalty kwake!

Nakubaliana na Nyani Ngabu kwamba wakati mwingine tunawatwisha mzigo mzito kuliko uwezo wao wapinzani kwenye hili. Shinikizo la kweli litakaloifanya serikali kuzibua masikio litatoka kwetu wananchi na sio vyama vya upinzani peke yao.
 
Tume huru hata CCM wanakiri kuwa tume iliyopo si huru, na ndio maana hata Mh. Kikwete wakati wa kikao na viongozi wa vyama vya siasa (rejea katika sakata la bunge la katiba)alikiri mwenyewe kuwa kwa sasa wafanye marekebisho ya tume ya uchaguzi, na baadhi ya vitu vingine na mambo ya katiba mpya yangeendelea mwakani baada ya uchaguzi.

Na kwa bahati mbaya sana vyama vya upinzani ambao ni waanga wakubwa wa hii tume hawakufanya chochote cha kuibana serikali ii itekeleze takwa lao.

Pia ninapokuja swala la kurudisha fomu za uchaguzi ninategemea kuwa tume ya uchaguzi hiko pale kuwapa maelezo wachukuaji fomu wote jinsi ya kujaza hizo fomu na pale fomu zinaporudishwa ni wajibu wa hao watu wa tume kuhakikisha kuwa fomu zimejazwa jinsi inavyotakiwa na pale kwenye makosa ya kibinadamu basi wana wajibu wa kuwambia wagombea kurekebisha hizo kasoro ndogo ndogo.

Ni upuuzi mtu kuenguliwa kwa vile amekosea herufi moja au tarehe, au amesahau fomu moja tu,kukosea mhuri na nk Jamani haya ni makosa ambayo yanaweza kubadilishwa ndani ya lisaa moja.

Nategemea mgombe kuenguliwa pale panapokuwepo tuhuma nzito kama ni mwizi, kifungo, makosa ya kutolipa kodi, kama mtu si raia wa watanzania na nk.

Tume si sehemu ya machinjio si sehemu ya kuwanyima haki wananchi kuchangua mtu wanayeona wanafaa si sehemu ya kukaa na kuviziana bali ni sehemu ya kutoa haki, kuhakikisha kuwa raia wanapata haki yao ya kuchagua na kuchanguliwa.

Hivi katika karne hii bado tume hajaona umuhimu wa kuweka utaratibu kwa wale watu wanapita bila kupingwa walau wapingiwe kura zandiyo na hapana?
Hivi katika karne hii kuna mtu anatembea vifua mbele na kutamba kuwa yeye ni kiongozi wakati anafahamu watu katika jimbo lake wamenyimwa haki yao ya msingi waliyoisubiri kwa miaka 5? hii ni aibu kwa tume na ni aibu kwa viongozi wote wapenda kupita bila kupingwa na katika demokrasia ya kweli hakuna neno kupita bila kupigwa.
 
Na kwa bahati mbaya sana vyama vya upinzani ambao ni waanga wakubwa wa hii tume hawakufanya chochote cha kuibana serikali ii itekeleze takwa lao.

Uko sahihi lakini swali ninalojiuliza bado ni kwamba wapinzani walipaswa waibane serikali kivipi? Kwa njia zipi? Kupitia Bungeni? Kupitia maandamano na migomo nchi nzima?

Ni njia ipi ambayo ingekuwa effective kuishinikiza serikali hii "SIKIVU" ili iweze kufanya mabadiliko hayo ambayo pengine yangeweza kuwaumiza wao wenyewe?
 
Kama kuna eneo ambalo UKAWA wamekuwa disorganised ni usimamizi wa wagombea wa ubunge. Matukio ya baadhi ya wagombea wao either kushindwa kabisa kurejesha fomu au kurejesha fomu zenye kasoro ni uzembe mkubwa unaoweza kuwagharimu. Sina hakika baada ya kuondoka Slaa na Lipumba who is in charge haswa kwenye vyama vyao katika suala zima la kusimamia mchakato wa wagombea ubunge. Inaonekana kama waliobaki wako busy na kampeni zao wenyewe za ubunge na uraisi!
 
Uko sahihi lakini swali ninalojiuliza bado ni kwamba wapinzani walipaswa waibane serikali kivipi? Kwa njia zipi? Kupitia Bungeni? Kupitia maandamano na migomo nchi nzima?

Ni njia ipi ambayo ingekuwa effective kuishinikiza serikali hii "SIKIVU" ili iweze kufanya mabadiliko hayo ambayo pengine yangeweza kuwaumiza wao wenyewe?

Serikali ilichoweza kukifanya ni kuweka uoga mioyoni mwa watu kiasi kwamba hawana uwezo wa kuorganise chochote na kikafanikiwa. Mwisho wa siku wananchi wanaishi kwa ile dhana ya 'business as usual' au ni upepo tu utapita hata katika mambo ya msingi.
Nadhani kuna wakati serikali inatakiwa kuonyeshwa na wananchi kuwa haiogopeki.
Mimi sio muumini wa fujo au maandamano ila kuna wakati inabidi tu pale unapoona haki zako zote zimebanwa na huna njia nyingine.
Tume ya uchaguzi pamoja na vyombo vya dole vinafanya kazi kwa maelekezo ya CCM, unategemea Ukawa watapumulia wapi? Na mbaya zaidi hadi Nape anakuja kutuambia wananchi watashinda kwa bao la mkono. Kweli? Is this fair!?
Hata kama watanzania tuna hulka ya upole this is too much, tunaelekea ujingani. Hakuna jinsi amabayo wananchi tutakuja kupata uchaguzi huru na wa haki kwasababu wao ndio wameshika mpini.
Hapa yanahitajika maandamano ya amani usiku na mchana kuwatoa hawa watu madarakani hata kama sanduku la kura limeshindikana.
Ni kwamba uchaguzi huu ukipita na CCM wakishinda basi tegemeeni uozo mkubwa na wa hatari zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya Tanzania.
 
Mkuu Nguruvi3 na wadau wa great thinkers, ombi maalaumu, tuchepuke kdg. Naomba mada mbili zinanisumbua sana moyo wangu

Naomba uje na mjadala kuhusu zuio la polisi kutembea kwenye daladala nakutembelea maeneo ya kijamii kama sokoni au mahospitali, maana kwa mtazamo wangu naona kama hakuna uvunjifu wowote wa kisheria na pia kila mgombea anayo haki ya kikatiba ya kuwa popote, naona itaibua sintofaham kubwa sana kwamba polisi kama wanaegemea upande fulani na kutaka kulinda headlines za mgombea mwingine zisikike.

Pili, ni kuhusu haya mapingamizi ya NEC na wagombea kupita bila kupingwa, kuna mapingamizi jamani yanahuzunisha sana, mara muhuri mara sijui jina au sahihi mtu anaondolewa kugombea, is ths a democracy we need?? Mm nadhani ifike mahali NEC baadhi ya vitu wich can be amended wasiwe wanawadisqualfy wagombea, kwa kweli ni huzuni sana.

Kweli tunawalaumu wagombea hasa wa wapinzani kwa uzembe, bt mara nyingine human error can prevail na sio sahihi kudisqualfy kwa makosa kama hayo.
Kwakweli Tume huru ya uchaguzi need reform kwa hili

Pole kwa kuwahamisha, nakuomba uje na bandiko tulijadili kama haitakwaza
 
Mwalimu kama utakuwa umemsoma vema Alinda katika bandiko ameeleza vema uzembe wa wapinzani

Ni muda mrefu tumewaeleza kuwa hakuna tume huru na hakuna namna ya wao kujinasua isipokuwa kushinikiza

Ni kweli bunge lisingefanya chochote cha maana. Hata hivyo, unakumbuka agenda ya katiba ilikuwa ya wapinzani na serikali ilipogundua ni tatizo wakaamua kuichukua ili kupitisha muda.

Tuliwaonya wapinza katika uzi wa 'Juisi ya maembe'' Yaliyotokea ni hadithi

Tume huru ingepatikana kwa shinikizo la vyama vya siasa. Unajua , wananchi hawana platform bali wana nguvu ya kutumia platform katika kusukuma agenda.

Vyama vya upinzani vingegomea uchaguzi huu kushinikiza tume huru ya uchaguzi.

Hilo lingewezekana kwa kutambua lilikuwa na nguvu ya umma nyuma yake

Alinda kuhusu kubebesha lawama wapinzani, hapa kuna sehemu mbili

1. Ni kweli tume si huru na yote yanayoendelea ni mashaka matupu. Hata tume yenyewe inajua hilo
2. Kuna uzembe wa wapinzani ambao hujikuta wanaingia katika mitego ya tume kwa uzembe. Hilo ndilo tunalooongelea

Nimetoa mfano, kama helkopta inatumika katika kampeni, si ingekuwa bora ikatumiwa na wanasheria kuhakiki fomu?
Hoja si kuwa kuna makosa, ni katika kutegua mitego ya tume ya uchaguzi unaoendelea

Pili, wapinzani lazima wawe mstari wa mbele kuujuza umma kuhusu mawenge wenge yanayoendelea

Leo tume ina kigugumizi kuhusu Nsunzagwanko wa siku 6 kwa umri.

Kwa upande wa wapinzani tume ipo mbele na haraka sana kuondoa majina yao.

Hili lilitakiwa liwe ubaoni ili wananchi na dunia ielewe nini kinaendelea... Wapinzani wapo wapi?

Tatu, ni lazima awepo mtendaji wa chama asiye na shughuli za ubunge ili aweze kuratibu shughuli nyingine

Hilo halikufanyika hata pale mtendaji alipoondolewa. Dr Slaa aliachishwa ubunge kwa sababu hizo.
Je sababu hizo hazina mashiko leo hii?

Nne, ina maana vetting ya wanachama haikuzingatiwa? Said Nkumba alipewa vipi kugombea

Tano, Je vyama husika viliweka mkakati wa kuzuia wagombea kulaghaiwa ? Kama hakuna nini watu watarajie

Kwa ufupi kila upande una mizigo yake, hata hivyo mizigo ya wapinzani ni yao na si lazima ihusishwe na tume.

Tume inajulikana inafanya kazi zipi, si makosa wakitimiza azma yao kwani ''wanatekeleza''

Ni makosa wapinzani wakiacha tu kila jambo liende kwa mionzi ya jua. Lazima wasimame kidete kutetea haki zao
 
Mkuu Nguruvi3 na wadau wa great thinkers, ombi maalaumu, tuchepuke kdg. Naomba mada mbili zinanisumbua sana moyo wangu

Naomba uje na mjadala kuhusu zuio la polisi kutembea kwenye daladala nakutembelea maeneo ya kijamii kama sokoni au mahospitali, maana kwa mtazamo wangu naona kama hakuna uvunjifu wowote wa kisheria na pia kila mgombea anayo haki ya kikatiba ya kuwa popote, naona itaibua sintofaham kubwa sana kwamba polisi kama wanaegemea upande fulani.

Pili, ni kuhusu haya mapingamizi ya NEC na wagombea kupita bila kupingwa, kuna mapingamizi jamani yanahuzunisha sana, mara muhuri mara sijui jina au sahihi mtu anaondolewa kugombea, is ths a democracy we need?? Mm nadhani ifike mahali NEC baadhi ya vitu wich can be amended wasiwe wanawadisqualfy wagombea, ninahuzuni sana.

Kweli tunawalaumu wapinzani kwa uzembe, bt mara nyingine human error can prevail na sio sahihi kudisqualfy kwa makosa kama hayo.
Kwakweli Tume huru ya uchaguzi need reform kwa hili

Pole kwa kuwahamisha, nakuomba uje na bandiko tulijadili kama haitakwaza

Hivi ni kweli polisi wamezuia wagombea urais wasipande dala dala au ni propogana kama zilivyo propogana nyingine??

Maana siamini kuwa Polisi wanaweza kuzuia mtu kutumia usafiri anaotaka. Hivi kesho Lowassa akipanda baiskeli na kwenda Kariakoo kufanya manunuzi yake utamzuia? ni sheria ipi waliyotumia kutoa zuio hili??
 
Back
Top Bottom