Alinda
Platinum Member
- Jun 26, 2008
- 1,695
- 2,149
Nitakusahihisha jambo moja na ambalo labda halikueleweka. Katika andiko langu lile nilieleza jinsi gani ilivyo ngumu kuchakachua kura za Ubunge. Nilieleza na sheria haijabadilika kuwa kura za Ubunge zinahesabiwa na kutangazwa kituoni; hata kura za Urais ni hivyo hivyo na ndivyo ilivyotokea mwaka 2010. Kitu ambacho kilitokea ni kuwa agizo/amri haikutolewa kuzuia kutangazwa matokeo ya kura za Urais hadi yapelekwe NEC. Amri iliyotolewa ni kwa vyombo vya habari kutokutangaza matokeo ya Urais hadi yatakapotangazwa "rasmi" na NEC. Kwa maneno mengine, matokeo ya Urais yalitangazwa majimboni kama sheria inavyotaka - wasingeweza kutuma bila kuyatangaza ila vyombo vya habari havikuweza kutangaza hadharani kabla ya NEC. Hivyo, maripota wa TV au radio kina Ufoo Saro, George Marato na wenzao walipopewa nafasi ya kutangaza matokeo walikuwa na matokeo ya Urais mkononi lakini mabosi wao wa ITV waliwaambia wasiwaambie yale ya Urais bali yale ya Ubunge kwanza..
Kwahiyo mpaka hapo unaona pamoja na kuwepo sheria ya kutangaza matokeo vituoni, bado serikali hakuruhusu matoke hayo yatangaze na vyombo vya habari maana walijua kuwa kama vyombo vya habari vingetangaza basi wasingeweza kuchakachua. Na kilichofanyika Tume ya uchaguzi walitangaza matokeo ambayo ni ya uongo kwani kulikuwa hakuna tena kitu cha kuwafanya wasifanye hivyo. Na ninakumbuka mgombea wa urais kupitia Chadema yaani Dr. Slaa alilalamikia tume kutangaza matokeo ambayo hayakuwa ya kweli. Hivyo basi kusema kuwa CCM hawawezi kuchakachua kwa vile matokeo yanatangwa vituoni hali vyombo vya habari hawaruhusiwi kuyatangaza ni kujidangaya maana watakachuchua maeneo ambayo ni ya vijijini, wananchi hawana umeme, Tv za kuweza kuona kama klichotangazwa katika vituo vyao vya kupigia kura ndicho kinachotangazwa na tume!
Kwenye Ubunge nako ni vile vile pamoja na kutangaza matokeo vituoni bado kulikuwa na udangayifu mkubwa na uvunjwaji wa sheria rejea mbunge aliyekimbia na masanduku ya kura na tume limtangaza kuwa ni mshindi.au ucheleweshaji wa matokeo kwa maeneo yalioshinda wapinzani mf.Mwanza, Arusha na maeneo mengine, umwagikaji wa damu sehemu ambazo wapinzani walifanya vizuri na nk. Hivyo basi hatuwezi kuja hapa kujipa matumini kuwa tume itafanya tofauti na miaka ya nyuma.
Kikubwa wananchi wahimizwe baada ya kupiga kura basi walinde kura zao maana naona njia hii inasaidia kwa kiasi fulani.
Kwanini? kwa sababu matokeo ya awali ya Urais yaliyokuja kutoka sehemu ambayo tayari yalikuwa yametangazwa na yale ya Ubunge yalionesha Dr. Slaa alikuwa anaongoza. Ilibidi wazuie hadi mikoa ya Lindi, Mtwara, Tabora na Tanga ilipoanza kuleta kura zake ndiyo Tume ilipokuwa inatangaza kura za Urais ikaanza na mikoa ile ya ngome ya CCM. Hawakuanza na kura ambazo tayari wengine walikuwa nazo za mikoa ambayo wapinzani (CDM) walikuwa tayari wamepata kama Arusha, Musoma Mjini, Mbeya mjini n.k.
Ukilielewa hili utaelewa kwanini walijitahidi sana kupitisha sheria ya Cybercrime na kudhibiti takwimu. Kama siyo rasmi siyo sahihi hata kama ni sahihi.
Hiki si kweli kama ingekuwa ni kweli, na kama wangekuwa wanajiamini kuwa mikoa hiyo kuna kura nyingi za CCM basi wangeacha TV/redio sikakusanya matokeo na kuyaleta kama yalivyo na kwa jinsi hiyo watu wangeona wenyewe jinsi kura za CCM zinavyoongezeka kutoka katika mikoa hiyo. Walichofanya baada ya kuona Dr. Slaa anaongoza, na kupata matokeo ya hiyo mikoa kulikuwa hakuna jinsi zaidi ya kuchakachua tu..
Leo hii nikikuuliza Mkoa wa Mbeya vijijini CCM walipata kura ngapi za urais si dhani kama kunajibu la ukweli kilichopo (kama kipo) ni namba za kubumba.