CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

CCM kwa hulka yake ime declare an all out war against wananchi wasioipenda kwa kutumia silaha yoyote ile na zozote zile na moja wapo katika silaha hiyo ni vulnerable Dr. Slaa. He will soon wake up out of his slumber and slowly realize kwamba Watanzania wa sasa si wale wa 2010, this is a completely new breed. Bila kujua Dr. Slaa anaijeruhi CCM kuliko Lowassa or UKAWA for that matter, mark my words.
Mkuu nashukuru hili umeliona kutoka angle nyingine .

CCM walitambua Lowassa ni ‘asset' kushinda uchaguzi.
Walimkata kwasababu CCM na serikali yake iligubikwa na tuhuma nyingi za ubadhirifu, uzembe, wizi na ufisadi

Kumuondoa Lowassa ilikuwa kupunguza nguvu za hoja za matatizo yanayowakabili na si kukabiliana na tatizo

Katika mambo CCM isiyotaka yazungumziwe ni ufisadi n.k. kwasababu yatafumua vidonda na vitaanza kuvuja damu upya

Ukifuatilia kwa makini, ilani na sera pamoja na hoja za mgombe wa CCM zinajaribu sana kulikwepa suala la ufisadi , umasikini na mateso mengine.

Ni ilani iliyojaa matumaini hata kama hayajawahi kuwepo, hayatekelezeki au hayawezi kutetewa

Kwa bahati mbaya sana, kwavile mtumbwi unakaribia kujaa maji , kila abiria anakamata chochote ili kunusu chombo.

Wametokea watu wawili ambao kihistoria wana tatizo na Lowassa.

Tunakumbuka timbwili la Richmond na utatu wa Lowassa-Sitta-Mwakyembe

Ipo hofu ya kibaindamu tu kuwa , hivi ikitokea vile majaaliwa yetu ni nini?
Je, kuna kisasi kitakachofuata? Ni hofu tu ya kawaida
ya kibinadamu

Hapa ndipo karata ya Dr ikaanza kutumika. Dr Slaa akapewa nondo za Richmond ili kukabiliana na tishio, si la kundi la CCM kwa ujumla bali kwa nafsi moja moja. Hofu imetenda

Wasichokitambua ni kuwa hoja ya ufisadi ikirudi tena katika majukwaa, CCM watarudi kule kule wasikotaka.

Maana yake, EPA, escrow na taarifa za CAG, Nyumba za serikali, Mabehewa mabovu, pesa za wizara ya ujenzi kuhamishwa bila idhini n.k. yatarudi katika ‘stage'

Mengine Dr Saal hana uwezo nao. Kwasasa anaweza kuonekana ni mshumaa, baada ya nusu saa mshumaa huo utaangaza kwa wengine wenyewe ukiteketea

Ndio maana nimewaambia UKAWA, mbona hoja zinazungumzika? Ni kupata watu wa kuzizungumza vizuri tu.

Dr Slaa anaweza kuwa msaada kwa UKAWA wakimtumia vizuri maana anategeneza platform

Kwa CCM atawasadia kwa muda na kuwaletea matatizo kwa muda mrefu, anafumua vidonda
 
..I took the worst case scenario kwamba Lowassa siyo Ukawa.

..lakini baada ya kutafakari, hata katika mazingira ambayo Lowassa siyo ukawa, bado nimeangukia kwenye kwenye scenario namba 1.

..I like ur strategy ya kutokuweka "mayai yote ktk kikapu kimoja." It is something I have toyed with for some time. lakini ktk kampeni hizi, CCM inaendelea kufanya mambo yanayozidi kunitibua, na ndiyo maana nimeshawishika kuwapumzisha kila mahali.

..Tangu Magufuli aanze kufanya kampeni kwa nia ya kupotosha waziwazi, nimepoteza hata ile heshima ndogo niliyokuwa nayo kwake. Hivi kweli miaka 20 aliyokaa serikalini, na exposure aliyoipata, hafahamu tofauti ya kilichotokea Libya, Iraq, Zaire, na hiki kinachoendelea hapa Tanzania?

NB:

..unaweza kutuletea uzi wa hii theory yako ya kutokuweka mayai yote ktk kikapu kimoja.

..choice ya kwanza itakuwa ni Lowassa Raisi, Waziri Mkuu toka CCM, chama cha kikuu cha upinzani CDM/UKAWA.

..choice ya pili itakuwa ni Raisi Magufuli, Waziri Mkuu toka CDM/UKAWA, chama kikuu cha upinzani CCM.

..choice ya tatu ni Raisi na waziri mkuu kutoka chama kimoja, lakini chama tawala kina very slim majority.

cc Rev. Kishoka, Zakumi, Nguruvi3, NasDaz
JokaKuu, za miaka mkuu!

Nikirudi kwenye mnakasha, kwanza siungi mkono kauli ya kwamba EL ataleta mabadiliko... kama lengo ni kuitoa CCM, sawa lakini kwamba eti kuleta mabadiliko; sioni ni namna gani mabadiliko hayo yanaweza kuletwa na mtu kama EL unless kama tunaota ndoto za mchana kwamba EL akiingia madarakani, ataharakisha mchakato wa katiba mpya (mchakato mwingine) na kuleta katiba inayopunguza nguvu za rais... sioni uwezekano huo na kama hakuna, sitarajii mabadiliko yoyote, labda mabadiliko ya kuileta Tanganyika!

MABADILIKO TOWARDS TANGANYIKA! Hapa EL ameshafahamu kwamba Watanzania ni rahisi kuwateka akili! Narudia, EL hana ubavu wa ku-engineer mabadiliko ya katiba itakayojali maslahi mapana ya wananchi na kupunguza nguvu dola! Ili kuwateka zaidi CHADEMA na CUF, sana sana ninachoona anaweza kufanya ni ku-revive tu Rasimu ya Katiba Ya Jaji Warioba na kurudisha suala la serikali tatu ambalo sichelei kulisema hata kidogo kwamba ndio pekee ambalo linaimarisha ushirikiano huu wa UKAWA, husani kati ya CHADEMA na CUF... huku CHADEMA wanataka Tanganyika yao, na kule CUF wanataka Zanzibar yao yenye mamlaka kamili!

Kwangu mimi, Lipumba anaaminika maradufu kumlinganisha na Maalim Seif! Sioni makubaliano ya msingi kati ya Maalim Seif na Mbowe zaidi ya ikiwa CUF wataiunga mkono CHADEMA na EL, basi EL akiingia madarakani, waiachie Zanzibar mamlaka kamili... sioni lingine zaidi ya hili na katika hili, Maalim Seif yupo tayari kwa lolote!

Hili likifanyika, wote tutapiga vigelegele kwamba tayari tumepata mabadiliko as if rushwa, ufisadi, ukosefu wa uwajibikaji, ukiukwaji wa haki za raia na mambo mengine yote ya hovyo yanatokea kv hatuna Tanganyika!
 
Hili la kuweka mayai yote kapu moja linaweza kutokea.

Huko nyuma katika mijadala tuliwahi kuzungumza na JokaKuu . Tulisema hivi

Plan ya UKAWA , Plan A1 kushinda dola na bunge, Plan A2 kushinda kimoja kati ya dola au Bunge.
Hakuna Plan A na B

Kwa hali iliyopo inaonekana linawezekana kwasababu hizi

UKAWA wanaweza kushinda Bunge na Serikali

CCM wanaweza kushinda bunge na Serikali

Kwa bahati mbaya UKAWA wameacha jukumu la kuwa ‘power broker'

Ukitazama kwa jicho pevu attention yao imeondoka katika suala la bunge

Kwahiyo wameamua kucheza karata moja kubwa! Ni hatari isiyoonekana lakini ipo

Kwa maana kuwa meli ikizama izame na mzigo

Mkuu,

Nukta yangu ya msingi katika bandiko langu kwa JokaKuu ni kuwa, hizo plan A1, plan A2 zote ziko kwenye interest UKAWA. Swali ni kuwa what is best for Tanzania. Kwa maoni yangu ni kuwa UKAWA hii ya Lowasa haiwezi kuleta yale mabadiliko yaliyo kwenye fikra za mtanzania wa kawaida (najua utakuwa na opionion yako kwenye hili).

Swali ni je, kutokana na tuliyojifunza katika miaka 10 iliyopita kwenye accountable government. Is it in the best interest ya Mtanzania kuweka mayai yake yote kwenye kapu moja?

Najua inawezekana niko nje kidogo ya mjadala wa Dr. Slaa unaoendelea sasa hivi ila nadhani kwenye hoja kuu ya original bandiko nadhani bado niko. Naomba radhi kama sipo.
 
Hii kasi ya kujiadhirisha mbele ya kadamnasi inamfuta kabisa kutoka kuwa mtu mahiri na mwenye busara.

Inaelekea baada ya Serena, kafuata interview ya Tido na sasa Star TV kujitetea mno na kuendelea kutoa hoja ambayo ni kutwanga ngumi kwenye maji.

Lakini pia hii ni mbinu ya kuondoa wanahabari kufuatilia kampeni za Ukawa. Propaganda za CCM ni distortation na mis-information.

Dr. Slaa anajitangaza kana kwamba kaonewa haki ya kuwa mgombea wa Chadema/Ukawa (his tone and choice of words says it in plain english despite his continuous refusal kuwa hautaki Uraisi) hivyo anatafuta sympathy ya wananchi ambao wanahamasishwa kuanza maandamano ya kumuaga na yeye eti anaanza kampeni ya kuaga wananchi kutembelea mikoa.

Go figure mtu anayedai kuwa na roho safi kabisa!

Na hapo amekuambia ameacha siasa, shangaa mwenyewe.
Prof. Lipumba aliondoka kwenye uongozi wake kwa amani na wala hakuna anayemlaumu.
Amekuwa wiser kuliko Dr. Slaa.
 
Hivi ni akina nani wanaunda 'Genge' la Lowassa?...

Kuna yeyote anaweza kunisaidia kuwataja kwa majina?...

Pia si vibaya mkuu wangu ukaanza na hao aliowaacha CCM...

..kila mtu ana dhana yake kuhusu "genge" la Lowassa.

..kwa mtizamo wangu sehemu ya "genge" hilo ni wabunge, wenyeviti wa mikoa wa CCM, na wajumbe wa NEC-CCM waliokuwa wakimuunga mkono.

..kwa mfano kuna waliojitokeza hadharani kumuunga mkono kama Sophia Simba, Dr.Nchimbi, Alhaji Kimbisa, Mzee Madabida, Bwana Msukuma, Iddi Azzan Zungu, Mzee Ngombale Mwiru, Nazir Karamagi, Andrew Chenge, Mghana Msindai, Hamisi Mgeja, John Guninita, etc etc.

..inasemekana Lowassa alikuwa na support kubwa sana kwenye CCM-NEC kiasi kwamba jina lake lingefikishwa kwenye ngazi hiyo angepata ushindi wa Tsunami.

..ilitegemewa kuwa kutakuwa na mass exodus ya vigogo wa CCM na Lowassa kwenda CDM. That did not happen ndiyo maana mimi na-conclude kwamba "genge" sasa limehamia kwa Magufuli.
 
JokaKuu, za miaka mkuu!

Nikirudi kwenye mnakasha, kwanza siungi mkono kauli ya kwamba EL ataleta mabadiliko... kama lengo ni kuitoa CCM, sawa lakini kwamba eti kuleta mabadiliko; sioni ni namna gani mabadiliko hayo yanaweza kuletwa na mtu kama EL unless kama tunaota ndoto za mchana kwamba EL akiingia madarakani, ataharakisha mchakato wa katiba mpya (mchakato mwingine) na kuleta katiba inayopunguza nguvu za rais... sioni uwezekano huo na kama hakuna, sitarajii mabadiliko yoyote, labda mabadiliko ya kuileta Tanganyika!

MABADILIKO TOWARDS TANGANYIKA! Hapa EL ameshafahamu kwamba Watanzania ni rahisi kuwateka akili! Narudia, EL hana ubavu wa ku-engineer mabadiliko ya katiba itakayojali maslahi mapana ya wananchi na kupunguza nguvu dola! Ili kuwateka zaidi CHADEMA na CUF, sana sana ninachoona anaweza kufanya ni ku-revive tu Rasimu ya Katiba Ya Jaji Warioba na kurudisha suala la serikali tatu ambalo sichelei kulisema hata kidogo kwamba ndio pekee ambalo linaimarisha ushirikiano huu wa UKAWA, husani kati ya CHADEMA na CUF... huku CHADEMA wanataka Tanganyika yao, na kule CUF wanataka Zanzibar yao yenye mamlaka kamili!

Kwangu mimi, Lipumba anaaminika maradufu kumlinganisha na Maalim Seif! Sioni makubaliano ya msingi kati ya Maalim Seif na Mbowe zaidi ya ikiwa CUF wataiunga mkono CHADEMA na EL, basi EL akiingia madarakani, waiachie Zanzibar mamlaka kamili... sioni lingine zaidi ya hili na katika hili, Maalim Seif yupo tayari kwa lolote!

Hili likifanyika, wote tutapiga vigelegele kwamba tayari tumepata mabadiliko as if rushwa, ufisadi, ukosefu wa uwajibikaji, ukiukwaji wa haki za raia na mambo mengine yote ya hovyo yanatokea kv hatuna Tanganyika!
NasDaz ahlan wasahalan!!

..nafurahi kusikia toka kwako baada ya kimya kirefu.

..bila kuleta mabadiliko EL atapoteza support ya political base iliyomuingiza ikulu.

..sitegemei kama Lowassa atakuwa mjinga kiasi kwamba afanye mambo ambayo yatawatibua UKAWA. Unless ana mipango ya kurudi CCM.

..zaidi kama wananchi wakiweza kuiondoa CCM ujue kwamba EL atakuwa ana-deal na MAZOEA MAPYA. Itakuwa vigumu sana kwa mtawala[chama/raisi/wabunge] yeyote yule kuendelea kukaa madarakani bila kutekeleza matakwa ya wapiga kura waliomuingiza madarakani.

NB:

..mimi nataka ile IMANI kwamba ukipitishwa na CCM wewe moja kwa moja ni Raisi wa Tanzania ifutike ktk vichwa vya wa-Tanzania.

..pia napenda kusiwe na chama chenye 66% ya kupitisha miswada na sheria ktk bunge la muungano.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,

Nukta yangu ya msingi katika bandiko langu kwa JokaKuu ni kuwa, hizo plan A1, plan A2 zote ziko kwenye interest UKAWA. Swali ni kuwa what is best for Tanzania. Kwa maoni yangu ni kuwa UKAWA hii ya Lowasa haiwezi kuleta yale mabadiliko yaliyo kwenye fikra za mtanzania wa kawaida (najua utakuwa na opionion yako kwenye hili).

Swali ni je, kutokana na tuliyojifunza katika miaka 10 iliyopita kwenye accountable government. Is it in the best interest ya Mtanzania kuweka mayai yake yote kwenye kapu moja?

Najua inawezekana niko nje kidogo ya mjadala wa Dr. Slaa unaoendelea sasa hivi ila nadhani kwenye hoja kuu ya original bandiko nadhani bado niko. Naomba radhi kama sipo.
Mkuu GLAxyS3

Upo katika mada kabisa. Ukisoma kwa ukaribu bandiko na kule tulikolitoa suala lamabadiliko ni muhimu sana.
Na hapo wengi tumetofautiana sana

Kwa mfano, sisi wengine tunaamini mbadiliko yaliyotoka katika wanachama waliojenga vyamavya upinzani wenyewe ni real and sustainable.

Huu ndio msingi wa kusema upo uwezekano wa Plan A1 na A2 kupitia wanachama waliopigania mabadiliko ya dhati

Kwa upande mwingine, watu kama JokaKuu Alinda @Ma3 wanasema, nilazima kukata kichwa cha joka kwanza, ili kupata nafasi ya kuhangaika na mijusi au vinyoka mbele ya safari (chase thefox to the bush first..)

Ni wazi tunataka mabadiliko, sote tunataka hili dudu lililodumu miaka 50 sisi tukidumaa
liondoke. Hilo ndilo linasukuma watu wengi kukubali chochote ilimradi tu kuiondoa CCM.

Kuna mambo mawili kutokana na hali hiyo

Immediate measure ambazo ni hizi tunazoona za kukukmbatiakila kitu

Sustainable measure ambazo kwa sasa wengine hawaoni kamani kipaumbele na wewe unasomeka kuwa pro

Katika hili kuna wale wanaosema ujio wa Lowassa utasaidiakatika harakati za kupambana na tembo sitting room.

Wapo wanaosema kuna tatizo na ujio kwasababu hakukuwa na maadalizi na political base ipo paralysed muda ukiwa hautoi nafasi ku recuperate from the drastic changes

Pengine Mag3 atakaporudi ataweza kutusaidia kupambanua kamaujio wa Lowassa ambao ni immediate measure unaweza kuwa msaada na kwamba ni asset na denominator

Kwa upande mwingine GalaxyS3 utusaidie kama tunaweza kuwa na sustainable changes tembo akiwa amejaa sitting room , if not, how long we've to wait

Sasa umeeliza what is best kwa mwananchi. Tunaweza kusemathe best thing ni CCM kuondoka madarakani.

Rearrangement of the system siyo task ngumu kama kuiondoa CCM.

Namwananchi atakuwa bora bila CCM hata kama mbadala utakuwa mbovu
 
Nguruvi3, ni kweli nilisema nitarudi na mathalani nimepata ka muda kidogo naomba nianze kwa kuwapa changamoto kidogo wachangiaji wanaofuatilia kwa haya maswali;

  1. Hivi hali ingekuwaje upinzani ungegomea kupitishwa kwa mswada wa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 hadi sheria kandamizi kama zilivyooanishwa na marehemu Jaji Nyalali zifutwe?
  2. Hivi hali ingekuwaje kama upinzani ungegoma kushiriki uchaguzi wa kwanza uliohusisha vyama vingi mwaka 1995 hadi katiba mpya ipatikane?
  3. Hivi hali ingekuwaje kama katika chaguzi zilizofuatia miaka ya 2000, 2005 na 2010 upinzani ungegoma kushiriki hadi tume huru ya uchaguzi iundwe?
  4. Hivi hali ingekuwaje upinzani ungegomea mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya mwaka 2013 hadi hoja zao zote za msingi kwa Raisi Kikwete zijibiwe?
Na katika msingi huo huo naomba niulize swali muhimu kwa wakati huu nalo ni je hali ingekuwaje ndani ya UKAWA kama Lowassa asingepokelewa na kuteuliwa kuwa mgombea wa Uraisi? Hapa maswali mengine ya nyongeza yanayofuatia hilo ni je hali ingekuwaje kama, kwa mfano, Prof, Lipumba wa CUF ndiye angeteuliwa? Na je Dr. Slaa wa Chadema ? Na mwisho je Dr. George Kahangwa wa NCCR Mageuzi?

Lakini tukiachana na hayo maswali kuna swali lazima tulizingatie kwani linasemekana pia liliulizwa na Dr. Slaa, je Edward Ngoyai Lowassa alikuwa anakuja kama asset au liability kwa UKAWA? Je, kwa ujio wa Lowassa, nafasi ya UKAWA kushinda uchaguzi ujao mwezi Oktoba umeongezeka ama umepungua? Nikijibu nasema kama nafasi hiyo itakuwa imeongezeka hata kwa kiasi kidogo basi kwangu ni jambo jema lakini kama itapungua hata kwa kura moja, basi UKAWA imepoteza.

Dalili zote mpaka sasa zinaonesha kwamba UKAWA wamecheza karata zao vizuri ingawa yawezekana kukawepo na hali kidogo ya sintofahamu. Ninachokataa ni watu kuwa tayari kuamini kwamba wapo binadamu sugu wasioweza kubadilika, hawa nawaambia kuwa kisichoweza kubadilika ni maiti pekee kisicho na uhai. Pamoja na kwamba Lowassa kaweza kuitosa CCM bado wanataka kutuaminisha kwamba hata akiwa Raisi matendo yake hayawezi kubadilika, yatabakia yale yale akiwa CCM!

Ujio wa Lowassa hata kama wengine hawauafiki lakini umeleta changamoto upinzani na kwa mara ya kwanza chama tawala, CCM, kimeingiwa na woga mkuu. Kwa mara ya kwanza CCM imepigwa na bumbwazi na kubaki ikihaha ikitafuta namna ya kujinusuru. Jana nilipomwangalia mgombea Magufuli akimshika mkono na kuanmza kumnadi Prosper Mbena wa Ikulu ambaye mke wake alituhumiwa kuchota sh. 2,000,000,000,000/= za ESCROW kupitia Stanbic Bank, nilijiuliza maswali mengi sana!
 
NasDaz ahlan wasahalan!!

..nafurahi kusikia toka kwako baada ya kimya kirefu.

..bila kuleta mabadiliko EL atapoteza support ya political base iliyomuingiza ikulu.

..sitegemei kama Lowassa atakuwa mjinga kiasi kwamba afanye mambo ambayo yatawatibua UKAWA. Unless ana mipango ya kurudi CCM.

..zaidi kama wananchi wakiweza kuiondoa CCM ujue kwamba EL atakuwa ana-deal na MAZOEA MAPYA. Itakuwa vigumu sana kwa mtawala[chama/raisi/wabunge] yeyote yule kuendelea kukaa madarakani bila kutekeleza matakwa ya wapiga kura waliomuingiza madarakani.

NB:

..mimi nataka ile IMANI kwamba ukipitishwa na CCM wewe moja kwa moja ni Raisi wa Tanzania ifutike ktk vichwa vya wa-Tanzania.

..pia napenda kusiwe na chama chenye 66% ya kupitisha miswada na sheria ktk bunge la muungano.
Mkuu JokaKuu, Ahlan bīk
Nikirejea kwenye mada yako kuhusu suala la mabadiliko, hapa inategemea ni mabadiliko ya aina gani mwananchi wa kawaida anayahitaji! Kama ni mabadiliko ambayo mwananchi wa kawaida anayahitaji, sioni ni namna gani EL administration inaweza kuyaleta hayo! EL atahitaji support ya UKAWA administration zaidi kuliko support ya wananchi na ndio maana nikatangulia kusema kwamba, akiweza kui-release Zanzibar kwa matakwa ya CUF; hapo CUF hawatakuwa ni kingine cha maana zaidi wanachohitaji zaidi ya Zanzibar yenye mamlaka kamili no matter how corrupt the government will be... hii kwao haiwezi kuwa priority agenda compared to Zanzibar yenyewe mamlaka kamili! Na kwa upande mwingine, ikipatikana Tanganyika, hapa CHADEMA leadership itakuwa imelogwa kwa 100% na kuona mabadiliko yenyewe ndo haya bila kujali how corrupt and irresponsible the government is.

Kwa upande mwingine, tusisahau UKAWA ikishinda EL ndo rais wa nchi... rais dola; mwenye maguvu yote kuanzia kikatiba, kisheria na kwa tafsiri zingine zote tutakazoweka! Wakati tunahoji hofu ya EL kupoteza support ya UKAWA ikiwa atawatibua, kwa upande mwingine tunatakiwa kuhoji ikiwa CHADEMA watakuwa na ubavu wa kumvua uanachama pindi wakiona anashindwa kufikia yale waliyotarajia! Yaani hapa tunatakiwa kuangalia chama ambacho kilishindwa kumvua uanachama Shibuda kwa hofu tu ya kupoteza ruzuku ya ubunge wake, leo hii kitakuwa na ubavu wa kumvua uanachama rais na ku-jeopardize the whole system upwards down!

To answer the question ikiwa anaweza kuwatibua UKAWA, the answer is YES and not necessarily kwamba arudi CCM! Ingawaje sipendi kuzungumzia maradhi ya mtu na hii ikiwa ni mara yangu ya kwanza kabisa kuzungumzia afya ya EL; kwa jinsi ninavyomuona EL sioni kama anahitaji second term! Na hata akihitaji second term, bado atakuwa na some alternatives ikiwa atazinguana na UKAWA! Mosi, UKAWA wasipokuwa makini wanaweza kujikuta ndani ya mvuragano mkubwa sana especially matumaini yao yasipofikiwa! So, after first term na ikiwa atakuwa amezinguana sana na UKAWA, basi anaweza kutumia the same route Mwai Kibaki and Augustine Mrema used!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mag3, ingawaje hoja umeielekeza kwa Nguruvi3, wacha na mimi nidakie kipengele kimoja tu nacho ni:
Na katika msingi huo huo naomba niulize swali muhimu kwa wakati huu nalo ni je hali ingekuwaje ndani ya UKAWA kama Lowassa asingepokelewa na kuteuliwa kuwa mgombea wa Uraisi? Hapa maswali mengine ya nyongeza yanayofuatia hilo ni je hali ingekuwaje kama, kwa mfano, Prof, Lipumba wa CUF ndiye angeteuliwa? Na je Dr. Slaa wa Chadema ? Na mwisho je Dr. George Kahangwa wa NCCR Mageuzi?
Mosi, kwa suala la kutompokea EL, sina sababu ya kumung'unya maneno kusema kwamba endapo UKAWA wasingempokea EL ingekuwa wamefanya kosa kubwa sana la kisiasa kwa sababu, pamoja na yote yanayosemwa, bado ukweli unabaki pale pale kwamba EL ni tishio kwa CCM.

Tukija na hoja ya whether he's an asset or liability! Kwangu mimi, unlike Dr. Slaa, EL is a balance sheet with one side shown assets and another side liabilities! Binafsi, Dr. Slaa alipozungumzia suala la EL kuwa ama asset or liability, ni kama nimemwelewa tofauti... kwamba issue sio EL as a balance sheet with assets and liabilities but the issue is the number and value of items making the asset side of a balance sheet coz' no matter what, a balance sheet will remain a balance sheet with assets and liabilities sides and so for EL!

Now you have items making the asset side of a balance sheet... now you make use of these assets to outweigh the liability side of a balance sheet for the better of the company UKAWA though a balance sheet will remain there with assets and liabilities sides. Hizi assets ndizo zile Dr. Slaa alizitaja kama idadi ya wabunge aliotarajia kuhama nao, idadi ya wenyeviti wa CCM wa Mkoa, Wilaya n.k! Lakini hata kama angehama nao wote, the liability side ingebaki constant though ingekuwa outweighed but not wiped off na UKAWA as a company ingenufaika!

Baada ya hapo tunahamia kwenye kipengele cha pili! Kuja na hizi assets hakumaanishi kwamba you're no longer liability and you can now run for presidential post! Kama kweli lengo la EL ni kuleta mabadiliko na si kutaka urais, sasa hapa ndo angetakiwa ku-release assets zake zitumike kuimaliza CCM! The question is who'd to control the utilization of these resources? Dr. Slaa, Lipumba or Dr. George Kahangwa?

Kwanza swali ambalo hadi sasa sijapata jibu ni how come mtu kama Lipumba alitaka yeye ndo awe mgombea wa UKAWA! Si tu kwamba hana ushawishi wowote kwa kumlinganisha na Dr. Slaa, bali hata hiyo legitimacy ilishatoweka pindi Maalim Seif walipomtangaza kuwa ndie mgombea wa CUF (UKAWA?) kule Zanzibar! Isingewezekana na wala kuleta maana yoyote kutaka na huku Bara asimame mtu wa CUF unless kama huyo mtu wa CUF angekuwa na ushawishi mkubwa maradufu kumzidi wa CHADEMA! Tukirudi kwa Dr. Kahangwa, this's not all about someone from UKAWA allies but someone with political muscles... na huyo Kahangwa hana muscles za kumzidi japo Mbatia not mentioning Lipumba achilia mbali Dr. Slaa. Kutokana na hayo, ni Dr. Slaa peke yake ndie alikuwa na legitimacy as compared to Lipumba or Kahangwa!

So, to sum up... kwanza kama nilivyosema ingekuwa ni kosa kubwa UKAWA kutompokea EL! But basing on assets and liabilities issue kama nilivyomwelewa Dr. Slaa, ujaji huo wa EL na assets zake ungebaki kuwa ni kwa nia ya kuja kuingozea nguvu UKAWA sawa na alivyofanya Sumaye! Na endapo bendera ingepeperushwa na Dr. Slaa, UKAWA ingebaki much more intact than it's hata kama CUF na NCCR wangesusia umoja kwa kutoteuliwa wagombea wao! Sana sana kususia huko naona kungekuwa na manufaa zaidi kwa CHADEMA kuliko ilivyo sasa; WHY? Generally speaking, over 75% ya majimbo waloyosimamishwa watu wa CUF, NCCR na NLD ni kwamba yameshapotelea mikononi mwa CCM! Msidhani Lipumba alifanya kazi ndogo kupata majimbo mawili mkoani Lindi! I doubt ikiwa masihara masihara yale ya Juma Duni Haji yanaweza kuleta matokeo!
 
Last edited by a moderator:
NasDaz, tofauti kubwa kati ya mimi na wewe ni moja tu; wakati unaamini kwamba wapo binadamu who are born destined to be evil mimi, on the other hand, sikubaliani na falsafa hiyo. Mimi naamini kwamba hakuna kitu kama hicho na badala yake ni mazingira tunayokulia na jamii tunayoishi kama sehemu yake is what shapes our destiny. Mdahalo wa kama yawezekana binadamu akazaliwa akiwa muovu umefanyika kwa karne nyingi na matokeo yake kwa ufupi ni kwamba siku zote wanaosema hapana wameshinda.

NasDaz, humans are just born, humans are nor Evil nor Good. Humans are just human, and the only reason for them to become Evil, is if the environment they are surrounded by, encourages bad behaviors. Humans when they are born don't have a sense of what is going on, so how could we tell if they are born Evil? They don't even have any memory. Everything comes into their life as the grow older.

Kinachonishangaza katika huu mjadala ni namna tulivyo tayari kuwagawa viongozi wetu katika makundi mawili, wale ambao tunaweza kuyafumbia macho makosa yao na wale ambao hatuko tayari kuwapa nafasi hata wakitubu. Mimi sikumtaka Lowassa katika mazingira ya awali alokuwemo na hivyo hivyo nilikuwa upande wa Dr. Slaa katika mazingira alokuwemo awali lakini sasa nimebadilisha msimamo.

I believe that neither of these two guys was born evil but that it is the environment that influenced what they turned out to be each in his own way. With the wind of change now blowing, Dr. Slaa apparently appears decided to build a wall to stop it while Lowassa has decided to build a windwill to utilize it...guys, to exist is to change, to change is to mature, to mature is to go on creating oneself endlessly.

Kila kitu kinachosemwa kuhusu namna Lowassa atakavyondesha serikali akiwa Raisi kinasukumwa na hisia na kwa bahati mbaya hisia hizo zinaongozwa na vitu vitatu; chuki, mashaka na woga. Ni kweli yawezekana wapo wengi wasio na imani na lengo la Lowassa tofauti na mimi niliye tayari kumpa faida ya shaka kama nilivyo tayari kumpa faida ya shaka mtu yeyote atakayeunga mkono mabadiliko.

Faida ya kuingia timu mpya katika utawala wa nchi hii ni nyingi lakini kubwa kuliko zote ni ustaarabu wa kupokezana kijiti. Aina hii ya ustaarabu hujenga uvumilivu ndani ya jamii na kupunguza hofu na mashaka inayoandamana na kiu ya mabadiliko. Tukifanikiwa katika hili tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana katika kujenga utawala unaowajibika na kuondoa kabisa ulaghai na kiburi katika kuwatumikia wananchi.
 
JokaKuu , NasDaz anahofu ya mwanahistoria waUingereza Lord Acton inayosema ‘absolute power corrupts absolutely'

Kwa mfano,mtandao ndio ulimwingiza JK madarakani. Baada ya kupata nguvu , JK kaurudi mtandao.
Hapo ndipo naiona hofu ya NasDaz ilipo na ni legit

NasDaz , JokaKuu anasema ni lazima kuwepo na mahali pa kuanzia ili tuwe na mwanzo mpya(new norm)

Kauli hiyoinaungwa mkono na Mag3 anayesema bila kuwa na mahali pa kuanzia tutacheza mdumange mpake machweo.

Anauliza kama tumetoa doubt kwa CCM kwa miaka 20+kwanini tusitoe doubt kwa abiria aliyeshuka na kuamua kulisukuma gari , kinyumena wale walioko ndani wanaoamini wanalisukuma wakiwa ndani?

GalaxyS3anauliza, mabadiliko yanayotafutwa ni ya muda au ya kudumu!
Yeye anasimama katika maabadiliko ya kudumu hata kama itachukua miaka mingine mingi

Rev. Kishoka anasema, mabadiliko ni muhimu na lazima.
Wasi wasi wake ni jinsi gani yakufikia mabadiliko hayo. Je, upo umakini katika kufikia malengo au imekuwa`stampede``

Mambo mazito

Tuendelee
 
NasDaz, tofauti kubwa kati ya mimi na wewe ni moja tu; wakati unaamini kwamba wapo binadamu who are born destined to be evil mimi, on the other hand, sikubaliani na falsafa hiyo. Mimi naamini kwamba hakuna kitu kama hicho na badala yake ni mazingira tunayokulia na jamii tunayoishi kama sehemu yake is what shapes our destiny. Mdahalo wa kama yawezekana binadamu akazaliwa akiwa muovu umefanyika kwa karne nyingi na matokeo yake kwa ufupi ni kwamba siku zote wanaosema hapana wameshinda.

NasDaz, humans are just born, humans are nor Evil nor Good. Humans are just human, and the only reason for them to become Evil, is if the environment they are surrounded by, encourages bad behaviors. Humans when they are born don't have a sense of what is going on, so how could we tell if they are born Evil? They don't even have any memory. Everything comes into their life as the grow older.

Kinachonishangaza katika huu mjadala ni namna tulivyo tayari kuwagawa viongozi wetu katika makundi mawili, wale ambao tunaweza kuyafumbia macho makosa yao na wale ambao hatuko tayari kuwapa nafasi hata wakitubu. Mimi sikumtaka Lowassa katika mazingira ya awali alokuwemo na hivyo hivyo nilikuwa upande wa Dr. Slaa katika mazingira alokuwemo awali lakini sasa nimebadilisha msimamo.

I believe that neither of these two guys was born evil but that it is the environment that influenced what they turned out to be each in his own way. With the wind of change now blowing, Dr. Slaa apparently appears decided to build a wall to stop it while Lowassa has decided to build a windwill to utilize it...guys, to exist is to change, to change is to mature, to mature is to go on creating oneself endlessly.

Kila kitu kinachosemwa kuhusu namna Lowassa atakavyondesha serikali akiwa Raisi kinasukumwa na hisia na kwa bahati mbaya hisia hizo zinaongozwa na vitu vitatu; chuki, mashaka na woga. Ni kweli yawezekana wapo wengi wasio na imani na lengo la Lowassa tofauti na mimi niliye tayari kumpa faida ya shaka kama nilivyo tayari kumpa faida ya shaka mtu yeyote atakayeunga mkono mabadiliko.

Faida ya kuingia timu mpya katika utawala wa nchi hii ni nyingi lakini kubwa kuliko zote ni ustaarabu wa kupokezana kijiti. Aina hii ya ustaarabu hujenga uvumilivu ndani ya jamii na kupunguza hofu na mashaka inayoandamana na kiu ya mabadiliko. Tukifanikiwa katika hili tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana katika kujenga utawala unaowajibika na kuondoa kabisa ulaghai na kiburi katika kuwatumikia wananchi.

Mag3;

Ni kiongozi gani ambaye ametubu na watu wakaendelea kumsakama na makosa yake? Dr. Slaa hajafanya kosa lolote. Lowassa hajasema chochote kile kuhusu shutuma zinazotolewa dhidi yake.

Ninapobeba mabox tunashushulisha na mambo ya management. Utafiti wa studies nyingi katika management zinaonyesha kuwa maendeleo ya mtu binafsi, taasisi, au ya jamii mara nyingi hayashuki kutoka mbinguni. Ni matokeo ya watu yaliyopangwa (deliberate actions).

Deliberately, you decided to venture in maths, computers and electronics. Deliberately, Lowassa decided to accumulate wealth. Na tunapojikita katika deliberate actions zinazobadilisha maisha yetu tunajenga characters ambazo ni vigumu sana kwa sisi wenyewe kuzifuta.

Ni vigumu kwako kubadilisha characters ambazo zimekufikisha ulipo. Vilevile ni vigumu kwa Lowassa kubadilisha characters zilipomfikisha alipo. Kitendo cha Lowassa kujiunga na CDM sio ufunio aliuona Paulo ambao ulimfanya kuacha kuwatesa wafuasi ya Yesu na baadaye kujiunga nao. Hivyo usitegemea kuwa atabadilika.
 
Lakini, si Dk Slaa alikuwa CCM. Yeye liwezajekubadilika

Wengi tu walikuwa CCM wamebadilika

Usisahau mwananchi aliyeipigia CCM kura miaka 50 anaweza kupigia upinzani. Je, hajabadilika!

Kwa hoja yako hii, watakaobadilisha Tanzania lazim awatoke nchi jirani kama si mbinuni

Senti sumuni tu
 
Lakini, si Dk Slaa alikuwa CCM. Yeye liwezajekubadilika

Wengi tu walikuwa CCM wamebadilika

Usisahau mwananchi aliyeipigia CCM kura miaka 50 anaweza kupigia upinzani. Je, hajabadilika!

Kwa hoja yako hii, watakaobadilisha Tanzania lazimawatoke nje ya nchi kama si mbinuni

Senti sumuni tu

Itabidi uanze kujikita kwenye madesa ya management. Kubadilisha kadi ya chama ni sawa na
kubadilisha shati. Hakubadilishi tabia za mtu za kiutendaji. Utendaji wa kazi wa Dr. Slaa hakutegemea chama.

Kitendo cha kupiga kura hakisukumwi na talents au behaviors za mtu. Kinasukumwa na mahitaji binafsi na ya kijamii. Watu wote wanaotaka kumchagua Lowassa, wana sababu kwanini wanataka hivyo.
 
..Dr.Slaa sasa hivi yuko karibu na Dr.Mwakyembe na Mwigulu Nchemba.

..kwa mtizamo wangu Dr anapaswa kuwa makini sana na hawa marafiki zake wapya.

cc Rev. Kishoka, Nguruvi3, Alinda, ZeMarcopolo

Unaweza kuwa sahihi, lakini unapoona Mbowe na Lissu ni sawa kuwa na urafiki mpya na Lowassa unaweza vipi kuona Slaa kuwa karibu na Mwigulu na Mwakyembe ni tatizo?
 
Ombi kwa ndugu yangu Nguruvi3kama utaweza tunaomba uchambuzi wa wagombea urais hasa Lowassa na Magufuli maana kati yao mmoja wapo ndiye rais..

Ningependa kuwafahamu kwa undani zaidi wa hawa wagombea katika mambo ya maamuzi magumu lakini ambayo si hasara kwa Taifa, maono yao katika kumsaidia mtanzania wa hali ya chini, utendaji wao, mapenzi yao kwa mama yetu Tanzania, Ilani zao, je zinatekelezeka? na mwisho katika maono yao wanataka kuona Tanzania ya aina gani katika miaka 5 ijayo..

Na nafikri kama itawezekana basi tunaomba Invisible apeleke ombi wa hawa wagombea kwa ajili ya mahojiano humu JF inaweza kuwa kama ilivyokuwa kwa Mh. Kagesheki (video) au maandishi kama iliyokuwa kwa Mh. Zitto..
 
Last edited by a moderator:
Mag3;
Lowassa hajasema chochote kile kuhusu shutuma zinazotolewa dhidi yake.

Kwa mujibu wa Tundu Lisu, Lowasa alijieleza mbele ya kamati kuu kuhusiana na tuhuma zinazomkabili hususan Richmond ambapo alimtaja mhusika mkuu. Ukiondoa Dr Slaa hatujasikia mjumbe mwingine yoyote wa kamati kuu alieonyesha kutoridhika na maelezo ya Lowasa.

Bado swali la msingi linabaki kwa Dr Slaa kwamba pingamizi lake kwa Lowasa linatokana na tuhuma za ufisadi au kutotimiza "masharti" ikiwemo kuingia na wabunge na wenyeviti wa CCM wa mikoa?
 
Mwalimu,

Lowasa alishutumiwa kwa hard evidence, zikiwemo barua and memo zinazoonesha involvement yake kwenye Richmond. CDM ilitangaza jina lake kuwa ni fisadi ikidai ina hard evidence za ushiriki wake. Kusema alijielezea kwenye kamati kuu bila kutoa specifics sio fair kwa kweli. Hii habari eti somebody told him, that some on top said he should proceed, does not make any sense.

Tuseme tu kuwa, hata CCM wako mafisadi and that should not be an agenda kwa Lowasa ila tusidanganye kuwa Lowasa alitoa maelezo. Kama kungekuwa kuna maelezo ya maana tusingekuwa tunazungumzia Richmond leo. Tukianza kukubali haya mambo ya eti alijieleza kwenye kamati kuu, kwani aliowafanyia ufisadi ni kamati kuu. Slippery Slope.

Mimi ndio nasema sitaki kuweka mayai yangu kwenye kapu moja, tutarudi kule kwa CCM, maswali yanapewa majibu marahisi halafu tunakubali. Kama upande mmoja utapewa serikali, it is in the best interest ya Tanzania upande huo usipewe na bunge. Tutaepusha haya mambo ya alijieleza kwenye kamati kuu ya chama wakati tunazungumzia nation interest.
 
Mag3,

Nimekusoma vizuri sana na nimekuelewa vizuri vile vile! Kwanza niseme jambo moja... I consider no one as an evil; neither EL or else! Kwanza kwa bahati mbaya, I don't trust majority of politicians. Hata hivyo, shaka yangu ipo kama alivyoeleza Nguruvi3! Sina hofu na EL kama EL bali nina hofu na EL kutokana na watu waliomzunguka! Kama ulivyoongea, hakuna anayezaliwa akiwa shetani bali mazingira na watu waliomzunguka ndiyo yanayoweza kumbadilisha mtu au kumfanya adumu kwenye his/her existing state! Unfortunately, bado sijaona ni namna gani mtu kama Mbowe, Lema, Tundu Lissu, Mzee Baregu na wengine kama wao wanavyoweza kuwa na ushawishi mbele ya EL sawa na ushawishi walio nao watu kama akina RA, Chenge, Kalamagi na wengineo kama wao! Hofu yangu ni kwamba namtofautisha EL na Lyatonga Mrema! Ingawaje both Mrema (wa 1995) na EL wana ushawishi mkubwa kwa wananchi lakini tofauti na Mrema, ushawishi wa EL umevuka toka kwa wananchi wa kawaida hadi kwa influential people ndani ya CCM yenyewe hadi serikalini! I doubt ikiwa Mrema alikuwa nayo haya! Majority ya hawa influential ni corrupts na conservatives kwenye maeneo yao ya kujidai. Hawa ndio watu ambao EL amedumu nao hadharani na sirini kwa miaka kadhaa tofauti na akina Mbowe aliokutana nao barabarani ambao ingawaje nikiri pia sifahamu uhusiano wao behind the scene!

Sasa basi, je hao watu waliomzunguka EL wana hiyo kiu ya mabadiliko tunayoyaimba? Hivi kweli leo hii EL anaweza kuwa na uwezo wa kusema viongozi wote wa CCM wafirisiwe kwavile ukwasi wao umepatikana kwa njia isiyo halali wakati majority ni watu wake wa karibu? By the way, hiyo moral authority ataitoa wapi? Na endapo atafikiria kufanya hivyo; je ataanzia wapi? Viongozi waliokuwa kwenye Nyerere Administration? Mwinyi administration? Mkapa administration? Au JK administration? From any of those administrations; kwanini na yeye mwenyewe asiwe included? Watu wanadai ametubu... ametubu wapi? Kwenda Jerusalem ndo kutubu? Kama huko ndiko kutubu kwenyewe; ni kiongozi gani basi nchi hii ni mchafu? Waislam wana mwezi unaitwa mwezi wa toba... majority including viongozi wa CCM na serikali yake ambao ni waislamu huwa wanafunga kutafuta toba! Nani basi mchafu? Hao akina JK wenyewe huwa wanaenda Makka kuhiji... je, na wao tuwaite wasafi? Na kwavile watu wengi wanazungumzia suala la kutubu, basi bila shaka tunakubaliana kwa upande wake kulikuwa na tatizo na ndio maana tunaamini kwamba the guy might be not the same guy anymore... ametubu! Kama ndivyo, tangu lini shughuli za umma mtu akaenda kutubu Jerusalem au Makka kama hizo sio issue zake mtu binafsi na Mungu wake!?

Lakini kama alivyoandika Mzee Mwanakijiji; hivi ni kweli EL ndie amebadilika au ni sisi ndio tumebadilika? What's so special alichofanya EL hadi tuamini huyu anaweza kuwa chachu ya mabadiliko?Hivi ni mabadiliko tuyatakayo wananchi ambayo EL anayeweza kuyafanya bila kuwa na direct effect ama kwake mwenyewe binafsi au kwa watu wake wa karibu? Hivi kweli tunaamini kabisa kwamba EL anaweza kuwa engine ya mabadiliko kwenye nchi hii? Ina maana tumeshasahau ni miezi michache tu iliyopita wakati akitafuta tiketi ya CCM, timu ya EL ilikuwa inaundwa na RA, Karamagi na Chenge?

Kama ambavyo nilivyosema hapo awali; nakubaliana kimantiki (sio kwa kuangalia rationality) na dhana ya kwamba hoja ni kuitoa CCM lakini kutarajia mabadiliko; I don't see it anywhere! Binafsi naamini kwamba mtu mabadiliko anaishi nayo na anachofanya ni kutafuta nafasi tu atekeleze azma yake... hili tuliliona kwa watu kama akina Mikhail Gorbachev na Frederik de Klerk... EL hajayaishi mabadiliko na wala hakuwahi kuyawaza na ndio maana hata kwenye kampeni zake anapozungumzia suala la mabadiliko anakimbilia kwenye kusema "anachukia umasikini!" Huwezi kuondoa umasikini ikiwa hujafanya mabadiliko ya msingi; mabadiliko ambayo hana ubavu wa kuyafanya!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom