Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #561
Mkuu nashukuru hili umeliona kutoka angle nyingine .CCM kwa hulka yake ime declare an all out war against wananchi wasioipenda kwa kutumia silaha yoyote ile na zozote zile na moja wapo katika silaha hiyo ni vulnerable Dr. Slaa. He will soon wake up out of his slumber and slowly realize kwamba Watanzania wa sasa si wale wa 2010, this is a completely new breed. Bila kujua Dr. Slaa anaijeruhi CCM kuliko Lowassa or UKAWA for that matter, mark my words.
CCM walitambua Lowassa ni ‘asset' kushinda uchaguzi.
Walimkata kwasababu CCM na serikali yake iligubikwa na tuhuma nyingi za ubadhirifu, uzembe, wizi na ufisadi
Kumuondoa Lowassa ilikuwa kupunguza nguvu za hoja za matatizo yanayowakabili na si kukabiliana na tatizo
Katika mambo CCM isiyotaka yazungumziwe ni ufisadi n.k. kwasababu yatafumua vidonda na vitaanza kuvuja damu upya
Ukifuatilia kwa makini, ilani na sera pamoja na hoja za mgombe wa CCM zinajaribu sana kulikwepa suala la ufisadi , umasikini na mateso mengine.
Ni ilani iliyojaa matumaini hata kama hayajawahi kuwepo, hayatekelezeki au hayawezi kutetewa
Kwa bahati mbaya sana, kwavile mtumbwi unakaribia kujaa maji , kila abiria anakamata chochote ili kunusu chombo.
Wametokea watu wawili ambao kihistoria wana tatizo na Lowassa.
Tunakumbuka timbwili la Richmond na utatu wa Lowassa-Sitta-Mwakyembe
Ipo hofu ya kibaindamu tu kuwa , hivi ikitokea vile majaaliwa yetu ni nini?
Je, kuna kisasi kitakachofuata? Ni hofu tu ya kawaida ya kibinadamu
Hapa ndipo karata ya Dr ikaanza kutumika. Dr Slaa akapewa nondo za Richmond ili kukabiliana na tishio, si la kundi la CCM kwa ujumla bali kwa nafsi moja moja. Hofu imetenda
Wasichokitambua ni kuwa hoja ya ufisadi ikirudi tena katika majukwaa, CCM watarudi kule kule wasikotaka.
Maana yake, EPA, escrow na taarifa za CAG, Nyumba za serikali, Mabehewa mabovu, pesa za wizara ya ujenzi kuhamishwa bila idhini n.k. yatarudi katika ‘stage'
Mengine Dr Saal hana uwezo nao. Kwasasa anaweza kuonekana ni mshumaa, baada ya nusu saa mshumaa huo utaangaza kwa wengine wenyewe ukiteketea
Ndio maana nimewaambia UKAWA, mbona hoja zinazungumzika? Ni kupata watu wa kuzizungumza vizuri tu.
Dr Slaa anaweza kuwa msaada kwa UKAWA wakimtumia vizuri maana anategeneza platform
Kwa CCM atawasadia kwa muda na kuwaletea matatizo kwa muda mrefu, anafumua vidonda