Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 790
- 1,316
Moja ya hoja ambayo hivi karibuni CHADEMA wamekuwa wakiitumia kama kete muhimu kujitofautisha na CCM ni uwazi waliokuwanao nao katika uchaguzi mkuu wao. Uwazi wa kiwango kile hata mm ningelipenda kuuona kwenye chaguzi zote za nchi yetu. Ni imani yangu, kwamba kama chaguzi zetu zingekuwa na uwazi wa namna ile, hata makelele ya "no reform no election" tusingalikuwa nayo.
Hata hivyo ukomavu huu kwenye siasa za ndani ya chama cha CHADEMA, umekuwa ni adimu sana inapokuja kwenye siasa za ushindani nje ya chama chao. Wanachadema ni wepesi sana kushabikia serikali inapokosolewa, lakini inapotokea taarifa ya kazi nzuri zilizofanywa na serikali inatolewa, humshambulia mtoa taarifa kwa lugha zisizokuwa na staha. Hii ni tabia mbaya, inayopaswa kukemewa na kila mpenda demokrasia.
Tunaposema mema yaliyofanywa na serikali huo sio uchawa, bali tunatimiza wajibu wetu wa kiraia wakuwatia moyo viongozi kufanya vizuri zaidi. Kadhalika tunapoikosoa serikali pale inapofanya vibaya, hatufanyi hivyo kwakuwa tunawachukia viongozi wetu, la hasha! Tunawakosoa kutimiza wajibu wa kiraia wakuwasimamia viongozi wetu, ili waweze kujisahihisha.
Kuikosoa au kuipongeza serikali hakutakiwi kufanyika kwa misingi ya itikadi za kichama. Ni wajibu wa kila mtanzania kwa kuzingatia utashi wake bila kujali chama chake. Tusipojenga utamaduni wa namna hii tutaishia kuwa na upinzani unaopinga kila kitu na CCM wanaopongeza kila kitu.
Upo ubaya gani kwa mwanachadema kueleza furaha yake ya kupata maji, umeme, barabara, shule, soko, kituo cha afya na akaipongeza serikali kwa kutekeleza miradi hiyo? Kutokushukuru ni dhambi, ni dalili ya wivu na roho mbaya. Kama ambayo hatufurahishwi na mwenendo wa serikali kushughulikia mambo yahusuyo demokrasia na haki za binadamu, ndivyo hivyo hivyo ambavyo hatufurahishwi na tabia ya wanachadema kuwavunjia heshima watanzania wenzao wenye maoni tofauti.
Nguvu ile ile tunayoitumia kuikosoa serikali inapofanya vibaya, ndio nguvu ile ile itumike kuipongeza serikali inapofanya vizuri. Haingii akilini mtanzania mwemzetu, ambaye umekuwepo Dar 2010 mpaka sasa utuaminishe kuwa huoni maendeleo yaliyofanyika. Maneno kama haya sio tu ni upotoshaji bali yanawakatisha tamaa viongozi katika jitihada zao za kutuletea maendeleo.
Tunapoelekea uchaguzi mkuu, Mwenyezi Mungu atusaidie kuwa na ustahimilivu na uvumilivu wa kutuwezesha kushiriki siasa za kistaarabu.