CHADEMA, ukomavu wa kisiasa ni pamoja na kuyakubali mazuri ya CCM

Hapo unatumia barabara maji na umeme pamoja na ulinzi wako ambacho ni sera ya ccm
Taja serikali yoyote duniani ambayo haitoi huduma hizo. Hapo ni sawa na kumsifia babako kwa kukuzaa.
 
Moja ya hoja ambayo hivi karibuni CHADEMA wamekuwa wakiitumia kama kete muhimu kujitofautisha na CCM ni uwazi waliokuwanao nao katika uchaguzi mkuu wao. Uwazi wa kiwango kile hata mm ningelipenda kuuona kwenye chaguzi zote za nchi yetu. Ni imani yangu, kwamba kama chaguzi zetu za zingekuwa vile makelele tusingalikuwa nayo.

Hata hivyo ukomavu huu kwenye siasa za ndani ya chama cha CHADEMA, umekuwa ni adimu sana inapokuja kwenye siasa za ushindani nje ya chama chao. Wanachadema ni wepesi sana kushabikia serikali inapokosolewa, lakini inapotokea taarifa ya kazi nzuri zilizofanywa na serikali inatolewa, humshambulia mtoa taarifa kwa lugha zisizokuwa na staha. Hii ni tabia mbaya, inayopaswa kukemewa na kila mpenda demokrasia.

Tunaposema mema yaliyofanywa na serikali huo sio uchawa, bali tunatimiza wajibu wetu wa kiraia wakuwatia moyo viongozi kufanya vizuri zaidi. Kadhalika tunapoikosoa serikali pale inapofanya vibaya, hatufanyi hivyo kwakuwa tunawachukia viongozi wetu, la hasha! Tunawakosoa kutimiza wajibu wa kiraia wakuwasimamia viongozi wetu, ili waweze kujisahihisha.

Kuikosoa au kuipongeza serikali hakutakiwi kufanyika kwa misingi ya itikadi za kichama. Ni wajibu wa kila mtanzania kwa kuzingatia utashi wake bila kujali chama chake. Tusipojenga utamaduni wa namna hii tutaishia kuwa na upinzani unaopinga kila kitu na CCM wanaopongeza kila kitu.

Upo ubaya gani kwa mwanachadema kueleza furaha yake ya kupata maji, umeme, barabara, shule, soko, kituo cha afya na akaipongeza serikali kwa kutekeleza miradi hiyo? Kutokushukuru ni dhambi, ni dalili ya wivu na roho mbaya. Kama ambayo hatufurahishwi na mwenendo wa serikali kushughulikia mambo yahusuyo demokrasia na haki za binadamu, ndivyo hivyo hivyo ambavyo hatufurahishwi na tabia ya wanachadema kuwavunjia heshima watanzania wenzao wenye maoni tofauti.

Nguvu ile ile tunayoitumia kuikosoa serikali inapofanya vibaya, ndio nguvu ile ile itumike kuipongeza serikali inapofanya vizuri. Haingii akilini mtanzania mwemzetu, ambaye umekuwepo Dar 2010 mpaka sasa utuaminishe kuwa huoni maendeleo yaliyofanyika. Maneno kama haya sio tu ni upotoshaji bali yanawakatisha tamaa viongozi katika jitihada zao za kutuletea maendeleo.

Tunapoelekea uchaguzi mkuu, Mwenyezi Mungu atusaidie kuwa na ustahimilivu na uvumilivu wa kutuwezesha kushiriki siasa za kistaarabu.
Sifa ni hisani isiyodaiwa, viongozi wakitekeleza wajibu, sifa yao halisi ni mshahara wanaopata. Wakikosea kelele inakuwa kubwa maana huo sio wajibu wao. Hawalipwi mshahara ili wakosee ama watende uovu. Hii imekaa sawa kwako?
 
Yaani CCM kama ni haki wanapaswa kuuwawa wooote wanayoyafanya ata Mimi darasa la saba naweza kuyafanya!!sasa kujenga vyoo,vituo vya afya nani atashindwa??shida nikuteua wajinga kuongoza jahazi ambalo limezama.kama sisi ni masikini tuna kila kitu alafu unawasifu CCM si utakuwa chizi.
 
Moja ya hoja ambayo hivi karibuni CHADEMA wamekuwa wakiitumia kama kete muhimu kujitofautisha na CCM ni uwazi waliokuwanao nao katika uchaguzi mkuu wao. Uwazi wa kiwango kile hata mm ningelipenda kuuona kwenye chaguzi zote za nchi yetu. Ni imani yangu, kwamba kama chaguzi zetu za zingekuwa vile makelele tusingalikuwa nayo.

Hata hivyo ukomavu huu kwenye siasa za ndani ya chama cha CHADEMA, umekuwa ni adimu sana inapokuja kwenye siasa za ushindani nje ya chama chao. Wanachadema ni wepesi sana kushabikia serikali inapokosolewa, lakini inapotokea taarifa ya kazi nzuri zilizofanywa na serikali inatolewa, humshambulia mtoa taarifa kwa lugha zisizokuwa na staha. Hii ni tabia mbaya, inayopaswa kukemewa na kila mpenda demokrasia.

Tunaposema mema yaliyofanywa na serikali huo sio uchawa, bali tunatimiza wajibu wetu wa kiraia wakuwatia moyo viongozi kufanya vizuri zaidi. Kadhalika tunapoikosoa serikali pale inapofanya vibaya, hatufanyi hivyo kwakuwa tunawachukia viongozi wetu, la hasha! Tunawakosoa kutimiza wajibu wa kiraia wakuwasimamia viongozi wetu, ili waweze kujisahihisha.

Kuikosoa au kuipongeza serikali hakutakiwi kufanyika kwa misingi ya itikadi za kichama. Ni wajibu wa kila mtanzania kwa kuzingatia utashi wake bila kujali chama chake. Tusipojenga utamaduni wa namna hii tutaishia kuwa na upinzani unaopinga kila kitu na CCM wanaopongeza kila kitu.

Upo ubaya gani kwa mwanachadema kueleza furaha yake ya kupata maji, umeme, barabara, shule, soko, kituo cha afya na akaipongeza serikali kwa kutekeleza miradi hiyo? Kutokushukuru ni dhambi, ni dalili ya wivu na roho mbaya. Kama ambayo hatufurahishwi na mwenendo wa serikali kushughulikia mambo yahusuyo demokrasia na haki za binadamu, ndivyo hivyo hivyo ambavyo hatufurahishwi na tabia ya wanachadema kuwavunjia heshima watanzania wenzao wenye maoni tofauti.

Nguvu ile ile tunayoitumia kuikosoa serikali inapofanya vibaya, ndio nguvu ile ile itumike kuipongeza serikali inapofanya vizuri. Haingii akilini mtanzania mwemzetu, ambaye umekuwepo Dar 2010 mpaka sasa utuaminishe kuwa huoni maendeleo yaliyofanyika. Maneno kama haya sio tu ni upotoshaji bali yanawakatisha tamaa viongozi katika jitihada zao za kutuletea maendeleo.

Tunapoelekea uchaguzi mkuu, Mwenyezi Mungu atusaidie kuwa na ustahimilivu na uvumilivu wa kutuwezesha kushiriki siasa za kistaarabu.
Uko Sahihi kabisa,sasa vaa viatu vya familia ya Mzee Kibao,Lisu,Mdude,Soka na Father Kitima. Halafu uende kwao ukawajengee maksri na kuwapa fedha. Halafu subiri wakusifie.
 
Giza haliwezi kufukuza giza, nuru pekee yaweza kufukuza giza
 
Back
Top Bottom