Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 790
- 1,316
Si kweli, tuweni na kiasi, usinene ukamala,yapo mengi sana ambayo chama cha mapinduzi kimeyafanya.Hakuna zuri hata moja lililofanywa na ccm. Labda uwe huelewi mambo.
Taja moja tu, ili tukusaidie kuondoka kutu kichwaniSi kweli, tuweni na kiasi, usinene ukamala,yapo mengi sana ambayo chama cha mapinduzi kimeyafanya.
Yapo mengi sana kuanzia kwenye elimu, afya maji, miundo mbinu ya barabara nk, maendeleo ni kuangalia ulipo kuwepo, ulipo na unapotaka kwenda, unafikiri tulipo hapa leo ndio tulikuwepo 1961 wakati nchi hii inapata uhuru? Maendeleo ni gradual process, tafadhali kaa kwa kutulia, kama una hoja tafadhali karibu kwa mnakasha.Taja moja tu, ili tukusaidie kuondoka kutu kichwani
Bahati mbaya kswahili kina upungufu wa misamiati. Kiingereza kina maneno mawili:-Yapo mengi sana kuanzia kwenye elimu, afya maji, miundo mbinu ya barabara nk, maendeleo ni kuangalia ulipo kuwepo, ulipo na unapotaka kwenda, unafikiri tulipo hapa leo ndio tulikuwepo 1961 wakati nchi hii inapata uhuru? Maendeleo ni gradual process, tafadhali kaa kwa kutulia, kama una hoja tafadhali karibu kwa mnakasha.
Bahati nzuri development or underdevelopment is there depending na vigezo ulivyoset before, tuanzie hapa, maendeleo kulingana na mazingira yetu ili taifa lionekane lime endelea au halijaendealea tuangalie nini? Literacy ratio, infant mortality rate, accessible roads throughout the year nk nk au nini? Karibu kwa mjadala, plz don't just jump to the conclusion.Bahati mbaya kswahili kina upungufu wa misamiati. Kiingereza kina maneno mawili:-
A. Underdevelopment.
B. Development.
Kwa taarifa yako ccm imeleta A hapo juu
Akili kama za Heche hizi😂Hakuna zuri hata moja lililofanywa na ccm. Labda uwe huelewi mambo.
Ambacho hatukubaliana nao hawa ni kusema ccm haijanya kitu, hii nchi ni kubwa sana, kwa tulioitembelea nchi ni mashahidi wa maendeleo makubwa tuliyonayo na tunayoendela kuyapata chini ya ccm, ccm ina mapungufu yake mengi tu lakini huwezi kubeza maendeleo makubwa yaliyoletwa na Serikali ya chama cha mapinduzi.Akili kama za Heche hizi😂
SAWA SAWA kwani nani anakataa mazuri ya CCM. Nchi inajengwa vizuri ila doa la no reform no election inashika hatamu, hamuoni au? DahhhMoja ya hoja ambayo hivi karibuni CHADEMA wamekuwa wakiitumia kama kete muhimu kujitofautisha na CCM ni uwazi waliokuwanao nao katika uchaguzi mkuu wao. Uwazi wa kiwango kile hata mm ningelipenda kuuona kwenye chaguzi zote za nchi yetu. Ni imani yangu, kwamba kama chaguzi zetu za zingekuwa vile makelele tusingalikuwa nayo.
Hata hivyo ukomavu huu kwenye siasa za ndani ya chama cha CHADEMA, umekuwa ni adimu sana inapokuja kwenye siasa za ushindani nje ya chama chao. Wanachadema ni wepesi sana kushabikia serikali inapokosolewa, lakini inapotokea taarifa ya kazi nzuri zilizofanywa na serikali inatolewa, humshambulia mtoa taarifa kwa lugha zisizokuwa na staha. Hii ni tabia mbaya, inayopaswa kukemewa na kila mpenda demokrasia.
Tunaposema mema yaliyofanywa na serikali huo sio uchawa, bali tunatimiza wajibu wetu wa kiraia wakuwatia moyo viongozi kufanya vizuri zaidi. Kadhalika tunapoikosoa serikali pale inapofanya vibaya, hatunafanyi hivyo kwakuwa tunawachukia viongozi wetu, la hasha! Tunawakosoa kutimiza wajibu wa kiraia wakuwasimamia viongozi wetu, ili waweze kujisahihisha.
Kuikosoa au kuipongeza serikali hakutakiwi kufanyika kwa misingi ya itikadi za kichama. Ni wajibu wa kila mtanzania kwa kuzingatia utashi wake bila kujali chama chake. Tusipojenga utamaduni wa namna hii tutaishia kuwa na upinzani unaopinga kila kitu na CCM wanaopongeza kila kitu.
Upo ubaya gani kwa mwanachadema kueleza furaha yake ya kupata maji, umeme, barabara, shule, soko, kituo cha afya na akaipongeza serikali kwa kutekeleza miladi hiyo? Kutokushukuru ni dhambi, ni dalili ya wivu na roho mbaya. Kama ambayo hatufurahishwi na mwenendo wa serikali kushughulikia mambo yahusuyo demokrasia na haki za binadamu, ndivyo hivyo hivyo ambavyo hatufurahishwi na tabia ya wanachadema kuwavunjia heshima watanzania wenzao wenye maoni tofauti.
Nguvu ile ile tunayoitumia kuikosoa serikali inapofanya vibaya, ndio nguvu ile ile itumike kuipongeza serikali inapofanya vizuri. Haingii akilini mtanzania mwemzetu, ambaye umekuwepo Dar 2010 mpaka sasa utuaminishe kuwa huoni maendeleo yaliyofanyika. Maneno kama haya sio tu ni upotoshaji bali yanawakatisha tamaa viongozi katika jitihada zao za kutuletea maendeleo.
Tunapoelekea uchaguzi mkuu, Mwenyezi Mungu atusaidie kuwa na ustahimilivu na uvumilivu wa kutuwezesha kushiriki siasa za kistaarabu.
Hapo unatumia barabara maji na umeme pamoja na ulinzi wako ambacho ni sera ya ccmTaja moja tu, ili tukusaidie kuondoka kutu kichwani
Mazuri ya ccm yanakua obscured na hulka ya ccm ya ubaguz kwenye miradi ya maendeleo, ukandamizaji wa democrasia, utekaji, mauwajiMoja ya hoja ambayo hivi karibuni CHADEMA wamekuwa wakiitumia kama kete muhimu kujitofautisha na CCM ni uwazi waliokuwanao nao katika uchaguzi mkuu wao. Uwazi wa kiwango kile hata mm ningelipenda kuuona kwenye chaguzi zote za nchi yetu. Ni imani yangu, kwamba kama chaguzi zetu za zingekuwa vile makelele tusingalikuwa nayo.
Hata hivyo ukomavu huu kwenye siasa za ndani ya chama cha CHADEMA, umekuwa ni adimu sana inapokuja kwenye siasa za ushindani nje ya chama chao. Wanachadema ni wepesi sana kushabikia serikali inapokosolewa, lakini inapotokea taarifa ya kazi nzuri zilizofanywa na serikali inatolewa, humshambulia mtoa taarifa kwa lugha zisizokuwa na staha. Hii ni tabia mbaya, inayopaswa kukemewa na kila mpenda demokrasia.
Tunaposema mema yaliyofanywa na serikali huo sio uchawa, bali tunatimiza wajibu wetu wa kiraia wakuwatia moyo viongozi kufanya vizuri zaidi. Kadhalika tunapoikosoa serikali pale inapofanya vibaya, hatufanyi hivyo kwakuwa tunawachukia viongozi wetu, la hasha! Tunawakosoa kutimiza wajibu wa kiraia wakuwasimamia viongozi wetu, ili waweze kujisahihisha.
Kuikosoa au kuipongeza serikali hakutakiwi kufanyika kwa misingi ya itikadi za kichama. Ni wajibu wa kila mtanzania kwa kuzingatia utashi wake bila kujali chama chake. Tusipojenga utamaduni wa namna hii tutaishia kuwa na upinzani unaopinga kila kitu na CCM wanaopongeza kila kitu.
Upo ubaya gani kwa mwanachadema kueleza furaha yake ya kupata maji, umeme, barabara, shule, soko, kituo cha afya na akaipongeza serikali kwa kutekeleza miradi hiyo? Kutokushukuru ni dhambi, ni dalili ya wivu na roho mbaya. Kama ambayo hatufurahishwi na mwenendo wa serikali kushughulikia mambo yahusuyo demokrasia na haki za binadamu, ndivyo hivyo hivyo ambavyo hatufurahishwi na tabia ya wanachadema kuwavunjia heshima watanzania wenzao wenye maoni tofauti.