CHADEMA waendelea na ajenda yao ya maandamano ya amani. Wapeleka barua Polisi kuomba ulinzi

CHADEMA waendelea na ajenda yao ya maandamano ya amani. Wapeleka barua Polisi kuomba ulinzi

Familia ya mbowe na ya lisu ni raia wa nchi nyingine kwa hiyo hawawezi kushiriki maandamano kwenye nchi ya kigeni. Inawezekana pia mbowe na lisu wenyewe hawatakuwa mstari wa mbele kwenye maandamano. Wao watakuwa mahali wanakula kiyoyozi wakisubiri kutoa taarifaya maandamano. Makapuku ndiyo watawekwa frontline.
Uongo
 
Asante sana, kwa taarifa na barua hii kumbe ni Maandamano ya Kanda ya Pwani, tulidhani ni ya kitaifa!.
Barua zote za kiofisi zinatakiwa kuwa na ref number na kusainiwa na office bearers zikiwa signed na stamped. Barua hiyo haina any ref, ofisa habari sio office bearers hawezi kusaini barua ya Ofisi, anasaini kwa niaba!.

All and all, ni muhimu sana, inaonyesha Chadema sasa ni chama makini kinachofuata katiba, sheria taratibu na kanuni.

This is very good news and a good move, ombi kwa uongozi wa Chadema, uwe tayari kupokea majibu yao kesho, wakikataliwa wasiandamane.

P
Mkuu hivi unajua polisi wote ni wafuasi wa Chadema, kama huamini utaona polisi ndio watakuwa wa kwanza kufungua pazia la maandamano!!!
 
Bwana Mayalla kwani ni lini CHADEMA waIiwahi kutokufuata katiba ,Sheria taratibu na kanuni ?
Naomba usikumbushie tukayafukua madudu ya Chadema!, tuendelee kujipanga kwa Maandamano
Tukutane trh 23 kwenye maandamano hi fursa sio ya kukosa
Bila kukosa nitakuwa front row tena mimi sio tuu ni muandamanaji bali pia ni mhamasishaji!. Kufuatia Umuhimu wa Maandamano ya UKUTA: Nimehamasika, Nitashiriki, Tujitokeze kwa Wingi! Ila...!
P
 
Safi sana, jeshi linalotumia kodi zetu halina budi kutoa ulinzi kwa ajili ya maadamano ambayo ni haki ya msingi katika katiba ya Tanzania.

Kinyume na hapo ni kukandamiza sauti za watanzania walipa kodi ambao ndiyo wamewapa ajira vigogo hawa wa Polisi, na pia viongozi wote wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Ikumbukwe kuwa katiba inataamka wananchi wa Tanzania ndiyo wenye mamlaka yote juu ya nchi yao iendeje.

1726867435643.png

20 September 2024 amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ambaye ni Rais Samia Hassan alipowaita IGP Camilius Wambura na viongozi wakuu waandamizi wa jeshi la Polisi katika Ikulu ya Dar es Salaam.

1726867724771.png

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. Samia S. Hassan akiwa ktk picha ya pamoja, mara baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Camillus Wambura pamoja na Makamishna wa Jeshi hilo kumaliza mkutano uliyo fanyika Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 20 Septemba, 2024.
 
Familia ya mbowe na ya lisu ni raia wa nchi nyingine kwa hiyo hawawezi kushiriki maandamano kwenye nchi ya kigeni. Inawezekana pia mbowe na lisu wenyewe hawatakuwa mstari wa mbele kwenye maandamano. Wao watakuwa mahali wanakula kiyoyozi wakisubiri kutoa taarifaya maandamano. Makapuku ndiyo watawekwa frontline.
Watoto wa makapuku ndio haki zao zinaminywa so huoni ina make sense wakiandamana mstari wa mbele??watoto wa lisu na mbowe wana shida gani ili waandamane??wana elimu bora,miundombinu mizuri,.sababu nyingine ya kuandamana umetupa...
 
ombi kwa uongozi wa Chadema, uwe tayari kupokea majibu yao kesho, wakikataliwa wasiandamane.
Umesema ninanukuu

“ombi kwa uongozi wa Chadema, uwe tayari kupokea majibu yao kesho, wakikataliwa wasiandamane.,,
✍️
Chadema Kwenye barua yao na kwenye vyombo mbali mbali vya habari wamesisitiza kuwa maandamano yao yatakua ya AMANI.

Je, kwanini unahisi watakataliwa ikiwa kuandamana ni haki yao kikatiba?

Je, ni kweli kuwa “utawala,, huu haufuati sheria, kanuni na kwamba hauzingatii katiba inavyo elekeza?
 
Familia ya mbowe na ya lisu ni raia wa nchi nyingine kwa hiyo hawawezi kushiriki maandamano kwenye nchi ya kigeni. Inawezekana pia mbowe na lisu wenyewe hawatakuwa mstari wa mbele kwenye maandamano. Wao watakuwa mahali wanakula kiyoyozi wakisubiri kutoa taarifaya maandamano. Makapuku ndiyo watawekwa frontline.

..watoto wa Mama, Abduli, Wanu, na Mchengerwa, watasaidiana na vyombo vya dola kutoa ulinzi wakati wa maandamano.
 
Ndani ya Taarifa yao wameonyesha Maandamano yao yatakapoanzia na kuishia, pamoja na Njia ambazo Maandamano hayo yatakamopita.

Taarifa yao hii hapa

View attachment 3101505

Mungu Ibariki Chadema.
Hii barua mbona haina uandishi mahiri? Hadi napata wasiwasi huenda sio halisi. Kisarufi na kimuundo wa barua naona haijakidhi.

Anyways, natumai nchi itaenda kwenye hatua mpya kupitia maandamano haya.

Ova
 
Umesema ninanukuu

“ombi kwa uongozi wa Chadema, uwe tayari kupokea majibu yao kesho, wakikataliwa wasiandamane.,,
✍️
Chadema Kwenye barua yao na kwenye vyombo mbali mbali vya habari wamesisitiza kuwa maandamano yao yatakua ya AMANI.
Kusema ni Maandamano ya amani ni jambo moja na kitendo cha kuandamana kwa amani ni jambo jingine.

Kumewahi kutokea watu kwa mbele wanahubiri amani, huku wamekunjua mikono ya ishara ya amami, huku nyuma wameficha mapanga migongoni mwao!. Polisi wana jicho refu linaloona yaliyofichika!.

Chadema kama chama wana haki ya kikatiba kuandamana na kufanya mikutano, ila dhamana ya amani na usalama haiko mikononi mwa Chadema, mwenye dhamana ya kuhakikisha ni Maandamano ya amani ni Jeshi la Polisi, ndio maana ni takwa la kisheria, kikanuni na kiutaratibu kutoa taarifa kwa maandishi na lazima ujibiwe kwa maandishi kupewa kibali cha kuandamana.
Je, kwanini unahisi watakataliwa ikiwa kuandamana ni haki yao kikatiba?
Sio nahisi watakataliwa Jeshi letu ssfi na makini la polisi zinazo taarifa za kinteligensia, hadi Maza ana taarifa, hivyo wameisha yapiga marufuku Maandamano hayo.

Ni kweli Maandamano ni haki ya Chadema, ila hakuna haki bila wajibu, kupata barua ya kibali cha Maandamano ni wajibu wa jeshi la polisi kuyalinda, Chadema ikinyimwa kibali ni wajibu wake kusitisha hayo maandamano.
Je, ni kweli kuwa “utawala,, huu haufuati sheria, kanuni na kwamba hauzingatii katiba inavyo elekeza?
Si kweli. Ukkweli nikuwa “utawala,, huu unafuata katiba, sheria, taratibu na kanuni na kwamba unazingatiia sana katiba inavyo elekeza.
p
 
Mwenyezi Mungu asipotuongoza tutakuwa miongoni mwa watu waliopotea.
It is not in the interests of Chadema to make the demonstration violent.
Lakini watu sijui wanahangaishwa na nini.
Pale City Center siyo rahisi kuzuia rioting ikitokea.
Maybe I should just rest. I can think about this in the morning.
Sasa hivi nilikuwa nasoma Muwatta ya Imam Malik.
Napenda jinsi ambavyo Muhammad anaitwa "Messenger of Allah"
"Messenger", maana yake taarishi tu analeta habari za Mungu.
 
Back
Top Bottom