CHADEMA waendelea na ajenda yao ya maandamano ya amani. Wapeleka barua Polisi kuomba ulinzi

Maneno ya hivi huwa naona kama vile mnakaririshwa kama kasuku, bila ya kutafakari. Jamani sio lazima familia nzima ifanane misimamo. Mbona baadhi ya watoto wa Warioba sio wanasiasa kabisa?

Hata Makongoro Nyerere alikuwa Chadema na huku baba yake ni gwiji wa CCM. Sio lazima watoto wa Mbowe na Lissu nao ni wanaharakati za kisiasa, nao wana maamuzi yao kama binadamu.

Usikariri ndugu yangu, ndiyo maana hata wewe hauko hapa JF na ukoo wako wote, wengine wako busy huko hata na kucheza ngoma zenu za kitamaduni, JF wanaona kama vile ni kijiwe cha kupoteza muda.

Ova
 
Ndani ya Taarifa yao wameonyesha Maandamano yao yatakapoanzia na kuishia, pamoja na Njia ambazo Maandamano hayo yatakamopita.

Taarifa yao hii hapa

View attachment 3101505

Mungu Ibariki Chadema.
Ndani ya taarifa hiyo, sijaona mahali popote panapoonyesha maandamano ni ya vurugu, uvunjaji amani, n.k..

Kama polisi wanadhani hivyo, ni wajibu wao kuonyesha kifungu kinacho chochea ghasia kabla hawajazuia maandamano.

Na je, polisi bado waking'ang'ania kuzuia maandamano kwa shari; nini plani B waliyo nayo CHADEMA?

Ushauri wangu juu ya hilo ni kuachana na kichaa. Ujumbe wao utakuwa umewasilishwa kikamilifu.

Lakini, kutopenda kupigana mieleka na kichaa siyo kwamba ni uoga; ni kupisha shari tu ipite ili kujenga nguvu zaidi ambayo hata kichaa hataweza kuizuia siku za usoni (karibuni); hasa wakati wa chaguzi zote mbili. Hapo hata kichaa akitupa nguo zote na kubaki uchi wa mnyama, ni kumkabili tu.
 
Hivi kwenye barua hiyo kuna mahali popote ilipo omba ruhusa ya kuandamana?
 
Walishakataliwa labda kwa taarifa hii mpya. Ambayo haina mashiko.

Najiuliza, hawa wachaga hawstaki tufunguwe biashara zetu kutwa nzima siku ya mwanzo wa wiki?

Mimi nashauri msimamo wa polisi uwe uleule wa marufuku kwa maandamno, kabisa tena. Wakikaidi wafinywe tu.
 
Chadema vituko haviishagi 😀
Jambo linalo nishangaza sasa hivi baada ya kukufahamu vizuri ni jinsi wewe na mwenzako aitwae Paskal Njaa mnavyo fanana kitabia!
Tofauti kati yenu ni ndogo sana. Paskal hupenda kuandika matakataka marefu sana; huku wewe ukiishia tu kuweka vimaneno vichache vya mipasho kwenye michango yako. Lakini mwelekeo wa maudhui ni yale yale.

Mnaishi nyumba moja, au ofisi zenu ndizo zimeunganishwa?
 
Inaonyesha ni kiasi gani akili zilivyo waruka kichwani, toka huko kwa 'Chura', ambaye sasa anasikia hadi kwenu chawa.
'Screw' zitaendelea kukazwa tu, hampati pa kutokea tena.
 
Unaomba ulinzi kwa unaemfanyia maandamano kuwa hafanyi kazi yake?

Ni kama unamwambiya "dereva wewe hujuwi kuendesha gari" halafu unamwomba akufikishe safari yako?

Kama si ujinga ni nini huo?
 
Utakuwepo kwenye MAAANDAMANO; ? au wewe ni muumini wa TANU…. Zidumu fikra za mwenyekiti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…