Kutoka Arusha!
Wanajamvi, Amani iendelee kudumu Tanzania!
Wale wafuatiliaji wenzangu wa siasa, mtakuwa mmeshabaini kuwa siasa za Tanzania kwenye upande wa mgombea wa Urais kutoka CCM sasa zimeshika kasi kuu!
CCM inagombewa na kila mwanachama wa chama hiki anayejihisi kuwa ana sifa na anatamani ateuliwe kupeperusha bendera ya chama kwenye ngazi hiyo kuu!
Edward Ngoyai Lowassa ni mmoja wa wagombea hao!
Huyu anatajwa sana kuwa anaweza kupitishwa na chama kugombea nafasi hiyo kutokana na ushawishi mkubwa alionao kuliko mgombea yeyote yule kati ya hawa waliokwisha kujitanganza mpaka sasa! Kutokana Na historia yake iliyotukuka kiutendaji!
Lowassa Kesho tarehe 30.05.2015 atatangaza nia hapa Sheikh A.A.STADIUM Arusha!
Wachambuzi wa duru za siasa mjini hapa wanabainisha kuwa Iwapo
Mh.E.N.Lowassa atateuliwa na Chama cha Mapinduzi kugombea nafasi ya juu kabisa katika nchi hii, Na Wananchi wengi wa Arusha wameonyesha support kubwa sana kwa chama cha mapinduzi, hakuna namna yeyote ile chama kingine cha upinzani kama CHADEMA kinaweza kujipenyeza na kuingia tena kwenye siasa za Arusha.
Wananchi wote wa Arusha mjini na majimbo mengine wote wameonyesha nia ya dhati ya kumuunga mkono Ndg.Edward .N. Lowassa. That means wabunge, Madiwani, etc wote watatoka CCM, Vyama vya upinzani havina nafasi tena Arusha! Hii ni bahati mbaya sana kwa LEMA na CHADEMA, bila kusahau umoja wao wa UKAWA.
CCM na wagombea wake ndio watakao shika upande huu!
Idadi kubwa ya wananchi wanamsapoti Lowassa na CCM, hakuna namna yeyote ambapo
Godbless J Lema anaweza kujitutumua tena kwenye siasa za Arusha!
Kidumu cha cha mapinduzi!
VIVA LOWASSA, VIVA CCM!