CHADEMA wakumbushwe: Mungu si mfuasi wa vyama na hana kadi ya chama

Plsm

Senior Member
Joined
Aug 19, 2021
Posts
177
Reaction score
266
Mandiko yanasema, Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa, Hivi mandiko yanaposema hivyo huwa inamaanisha nini?

Mambo yanayohitaji utumie nguvu zako kuyakabili na inawezekana kufanya hivyo, fanya, yale yanayohitajika kuyafanya kutumia akili zako na upo upenyo wa aina hiyo fanya, Mungu ni Mungu wa yasiyoaezekana,

Unauchungu na jambo lako, usimfanye Mungu awe mwanasiasa, Unamvalia na gwanda zako na bendera zako kumshawishi awe mwana siasa na kamela juu, 😂 jamani mjue mnafanya vituko kweli kweli, Nani alowaambia kwamba Mungu anaweza kuwa sehemu ya siasa zenu?

Unaweza ukawa na jambo jema la kumwambia Mwenyezi Mungu, lakini ukajikuta umekosea namba ya kumwendea

Tukiacha kukumbushana, tutajikuta tukipoteza muda mwingi ambapo muda huo ungeweza kutusaidi kutufanya tukaingiza chochote kitu

Kama ilivyo kwa Simba na Yanga, ndivyo ilivyo kwa Chadema ama CCM kuwa, Mwenyezi Mungu hana chama na wala hana kadi ya chama chochote, Mungu anachokifanya ni kuweka ulinzi wake katika mechi ili watu wake wasiumie ila hawezi kuwa sababu ya Yanga wala simba kushinda mechi siku hiyo!

Mambo ya Sheria yafanyike kwa sheria zilezile ambazo kama nchi tulipatana kuwa kukitokea hivi, kutafanyika hivi, likitokea jambo hili, basi kifanyike kile

Tunamwendea Mwenyezi Mungu tukiwa na dhana ya kishabiki kwamba Mungu naye awe sehemu ya ushabiki huo? tunafanya maombi kwa sare na kurekodi maombi yetu kwa faida ya nani? Kwani Mwenyezi Mungu ndio hao mnaopenda waone sare zenu, jinsi mnavyoomba ama Mwenyezi Mungu kama anavyosema katika Neno lake ameketi mahali pa siri?

Chadema acheni utoto.
 
Ni wajinga sana hawa watu!

Magufuli aliposema tufunge na kuomba ili atuepushe na janga la corona, wenyewe wakawa wanamkejeli eti Mungu ana kazi nyingi za kufanya! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Machadema ni kama hayana vichwa!
 
Nahisi toka nijiunge JF wewe ndio nimekuona mtu wa kwanza unayejifanya unamfahamu mungu
Tunaomfahamu Mwenyezi Mungu kupitia mandiko yake mkuu, hata wewe unamfahamu kwa njia hiyohiyo
 
Vipi yule Mungu mliemkejeli wakati wa corona ndio huyo huyo mnaetaka awasikie sasa hivi?
 
Tunaomfahamu Mwenyezi Mungu kupitia mandiko yake mkuu, hata wewe unamfahamu kwa njia hiyohiyo
Acha ujinga kilaza wa ccm wewe,kwahiyo unamjua mungu kupitia maandiko ya binadamu wenzako.Kwanini huyo mungu asikufanye na wewe umjue bali anapitia kwa wengine ili wewe umjue.
 
Kumbe nabishana na kilaza? jinga kabisa wewe!
 
Naandika nafuta nafuta Tena hata hapa nimekosea Ila mleta mada pole sana, jiandae Yesu anarudi kuchukua kanisa
 
Ya Chadema yanakuhusu nini wewe?

Habari leo mujini, katiba mpya sikia,
Yadaiwa kama deni, Mdaiwa kakimbia,
Mapolisi kulikoni, wadai kuwazuia?
Enyi msiohusika, hoho vipi ziwawashe?
 
Kama ni utoto bsi wewe ndio utoto wenyewe!
Andika yote utoto
Mawazo utoto
Akili utoto😡
Mimi nawakumbusha tu, Mungu sio wa kumagawishi awe sehemu ya siasa, mnamvalia magwanda na kamera zikiwamulika, nani kawaambia Mwenyezi Mungu ana kadi ya Chadema ama ya chama chochote?
 
Kumbe nabishana na kilaza? jinga kabisa wewe!
Mimi nadhani wewe ndio kilaza,kwasababu huwezi nipa logic ya nilichokuuliza,umo ndani ya kichwa chako nadhani kuna mizizi tu ya mikaratusi
 
Mimi nawakumbusha tu, Mungu sio wa kumagawishi awe sehemu ya siasa, mnamvalia magwanda na kamera zikiwamulika, nani kawaambia Mwenyezi Mungu ana kadi ya Chadema ama ya chama chochote?
Huyu mungu unayemtetea ndio amekupa akili za hovyo hivyo haya ni maajabu.
 
Kinachonishangaza kingine, Chadema hamjawahi kuamini uweza wa Mungu, rejea maombi ya korona, sasa kinachowafanya mkimbilie kwake leo ni kipi sasa?
 
Mandiko yanasema, Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa, Hivi mandiko yanaposema hivyo huwa inamaanisha nini?

Mambo yanayohitaji utumie nguvu zako kuyakabili na inawezekana kufanya hivyo, fanya, yale yanayohitajika kuyafanya kutumia akili zako na upo upenyo wa aina hiyo fanya, Mungu ni Mungu wa yasiyoaezekana,

Unauchungu na jambo lako, usimfanye Mungu awe mwanasiasa, Unamvalia na gwanda zako na bendera zako kumshawishi awe mwana siasa na kamela juu, [emoji23] jamani mjue mnafanya vituko kweli kweli, Nani alowaambia kwamba Mungu anaweza kuwa sehemu ya siasa zenu?

Unaweza ukawa na jambo jema la kumwambia Mwenyezi Mungu, lakini ukajikuta umekosea namba ya kumwendea

Tukiacha kukumbushana, tutajikuta tukipoteza muda mwingi ambapo muda huo ungeweza kutusaidi kutufanya tukaingiza chochote kitu

Kama ilivyo kwa Simba na Yanga, ndivyo ilivyo kwa Chadema ama CCM kuwa, Mwenyezi Mungu hana chama na wala hana kadi ya chama chochote, Mungu anachokifanya ni kuweka ulinzi wake katika mechi ili watu wake wasiumie ila hawezi kuwa sababu ya Yanga wala simba kushinda mechi siku hiyo!

Mambo ya Sheria yafanyike kwa sheria zilezile ambazo kama nchi tulipatana kuwa kukitokea hivi, kutafanyika hivi, likitokea jambo hili, basi kifanyike kile

Tunamwendea Mwenyezi Mungu tukiwa na dhana ya kishabiki kwamba Mungu naye awe sehemu ya ushabiki huo? tunafanya maombi kwa sare na kurekodi maombi yetu kwa faida ya nani? Kwani Mwenyezi Mungu ndio hao mnaopenda waone sare zenu, jinsi mnavyoomba ama Mwenyezi Mungu kama anavyosema katika Neno lake ameketi mahali pa siri?

Chadema acheni utoto.
Utoto aliokuwa anaufanya mwenyekiti wenu wa kwenda kuhutubia madhabahuni umeusahau?
 
Back
Top Bottom