CHADEMA wamesema hawatoshiriki katika uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Muhambwe

CHADEMA wamesema hawatoshiriki katika uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Muhambwe

Nawaunga mkono.

CCM ni ile ile na Tume ni ile ile huku Mama akiwa bado kazungukwa na watu wenye mentalily za Magu.

Kingine:Katika hizi chaguzi ndogo, wanaweza kuwaacha wapinzani washinde/demokrasia itawale ili wawapumbaze waamini sasa Tume inatenda haki chini ya Mama Samia,halafu waje wawageuzie kibao kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.

Ogopa nyoka na CCM.
Ccm ni sawa na nyoka
 
We unatakaje?
Yan tuache kufanya mambo ya msingi tuwe busy kutaka kuwaridhisha chadema?

Wakina mnyika na Mbowe walikuwa wabunge kwa tume gani?

Mbona kipindi huko hawakugomea?
Punguza hasira hizo kutesa kwa zamu nyinyi MATAGA zamu yenu ya kulia na kusaga meno ndiyo imefika.
 
Yes.

Wananchi waachwe wachague wawakilishi wao sio tume ya uchaguzi na watendaji wake wawateulie wananchi watu wanaowataka wao, hizo zama zimepita.
Inawezekana mwendazake akawa ameondoka na huo mchezo?
 
Hata wakishiriki watagalagazwa tu kama walivyogalagazwa mwenyekiti wao na makamu mwenyekiti ktk uchaguzi mkuu uliyofanyika mwaka jana. Ikiwa mwenyekiti aligalagazwa ni nani mungine anaweza kushinda nafasi ya ubunge ktk chama chao. Big up chadema kwa kusoma alama za nyakati
Majizi mliobobea
 
Halafu mnashangaa kwanini watu wanafurahia watu wengine wanapopatwa na matatizo kumbe kisa ni kauli na matendo yenu na ya viongozi wenu
Wasitegemee kamwe tuwaunge mkono hata siku moja.

Kama kulia walie pekee yao na kucheka wacheke kivyao
 
Nawaunga mkono.

CCM ni ile ile na Tume ni ile ile huku Mama akiwa bado kazungukwa na watu wenye mentalily za Magu.

Kingine: Katika hizi chaguzi ndogo, wanaweza kuwaacha wapinzani washinde/demokrasia itawale ili wawapumbaze waamini sasa Tume inatenda haki chini ya Mama Samia,halafu waje wawageuzie kibao kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.

Ogopa nyoka na CCM.

Tuendelee kudai Katiba Mpya/Tume Huru ya Uchaguzi
Naunga mkono hoja 100%, bamoja na maridhiano KWA Sasa kipaumbele kwanza ni tume huru,katiba mpya, mengine badae,
 
Inawezekana mwendazake akawa ameondoka na huo mchezo?
Huyu aliekuja anaonekana ana dalili za kulegeza, lakini haitakiwi Chadema ishiriki uchaguzi kwa kutegemea fadhila au matakwa ya mwenyekiti wa CCM, inatakiwa ishiriki uchaguzi ikiamini nguvu zake yenyewe na uungwaji mkono wao kwa wananchi ndivyo vitakavyowapa ushindi, sio ushindi wao utokane na utashi wa mwenyekiti wa CCM.
 
Chama cha CHADEMA kimesema hakitashiriki uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Muhambwe lililopo wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma.

Jimbo la Muhambwe liko wazi baada ya aliyekuwa mbunge Atashasta Nditiye kufariki dunia Februari 12, 2021 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari iliyotokea Februari 10, 2021 eneo la Nane Nane, mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili mosi, 2021 naibu katibu mkuu wa CHADEMA, Benson Kigaila amesema baada ya kikao cha kamati kuu kilichofanyika Machi 31, 2021 kwa njia ya mtandao wameazimia kutoshiriki uchaguzi huo kutokana na mazingira ya tume ya uchaguzi kutotenda haki.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeshatangaza kuwa uchaguzi katika jimbo hilo utafanyika Mei 2, 2021.

Tayari Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemteua Florence Samizi kuwa mgombea wa nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.

Chanzo: Mwananchi
Naungana na CHADEMA maana hakuna uchaguzi hapo ni maigizo tupu
 
Huyu aliekuja anaonekana ana dalili za kulegeza, lakini haitakiwi Chadema ishiriki uchaguzi kwa kutegemea fadhila au matakwa ya mwenyekiti wa CCM, inatakiwa ishiriki uchaguzi ikiamini nguvu zake yenyewe na uungwaji mkono wao kwa wananchi ndio vitakavyowapa ushindi, sio ushindi wao utokane na utashi wa mwenyekiti wa CCM.
Good
 
Back
Top Bottom