Uchaguzi 2020 CHADEMA: Wanachama 11 wachukua fomu za kugombea nafasi ya Urais wa Tanzania

Uchaguzi 2020 CHADEMA: Wanachama 11 wachukua fomu za kugombea nafasi ya Urais wa Tanzania

Ni jambo jema!
CCM wanawasubiri kwa hamu.
Maendeleo hayana vyama!
Hapana umekosea, CCM haiwasubiri kwa hamu.

Wanaowasubiri kwa hamu ni wananchi wazalendo, waaminifu, wapinga uonevu, wadai wa haki, usawa na uhuru, wapinga udikteta, wanaoheshimu utawala wa sheria, wanaotii na kutetea Katiba na Watanzania wote ambao kwa asili yao ni wakarimu na wasio na chuki wala ubaguzi.

CCM inawasubiri kwa hofu ikiwa imejikunyata nyuma ya vyombo hivi...Polisi, TAKUKURU, TRA, Tume ya Uchaguzi, Usalama wa Taifa, Msajili wa Vyama, Mahakama, Jeshi la Wasiojulikana, Watekaji wa Kitaifa, Watesaji wa Kitaifa, Wauaji wa Kitaifa na serikali inayovisimamia vyombo hivi.
 
Kasubiri CCM Magu kachukua fomu leo
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli amechukua fomu ya kuwania kinyang'anyiro cha Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Magufuli amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally, Makao Makuu ya CCM, Dodoma.

View attachment 1481048

Maendeleo hayana vyama!
Yes nimemuona live kupitia TBC rais Magufuli akichukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM.

Kule tuu kuonyeshea live kupitia TBC ni kitu kizuri kwa kuonyeshea transparency ya zoezi hili zima, na kwa vile TBC ni public broadcasting station yaani TV ya umma, imetimiza wajibu wake kikamilifu kututangazia live, na natoa wito kwa vyama vyote vya siasa vitakavyo simamisha wagombea urais, kutoa ushirikiano kwa TBC ili TBC iwatangazie live Watanzania wagombea wao na kuwapa fursa Watanzania kuwaona wagombea wote wakipewa haki sawa kwenye vyombo vya habari vya umma.

Pili nimemnote rais Magufuli akitumia usafiri wa gari lenye number binafsi. This is very good thing kwasababu rais Magufuli ametenganisha shughuli za chama na shughuli za serikali. Rais Magufuli hakutumia gari za serikali, wala hakutembea na msafara ikiwemo battalion, rais Magufuli ametumia gari moja tuu yenye number za kiraia.

Hatua hii ni hatua yenye essence kubwa sana kwenye mustakabali wa usawa wa kidemokrasia na usawa wa uwanja wa mapambano kujenga uwanja sawa, the level playing field, hivyo ni hatua muhimu kuifuta ile dhana ya kugombea urais Tanzania kufananishwa na kugombea kisu cha makali kuwili huku mgombea mmoja ameshika mpini na kuwashikisha wapinzani wake upande wa makali kuwili
P
 
Yes nimemuona live kupitia TBC rais Magufuli akichukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM.

Kule tuu kuonyeshea live kupitia TBC ni kitu kizuri kwa kuonyeshea transparency ya zoezi hili zima, na kwa vile TBC ni public broadcasting station yaani TV ya umma, imetimiza wajibu wake kikamilifu kututangazia live, na natoa wito kwa vyama vyote vya siasa vitakavyo simamisha wagombea urais, kutoa ushirikiano kwa TBC ili TBC iwatangazie live Watanzania wagombea wao na kuwapa fursa Watanzania kuwaona wagombea wote wakipewa haki sawa kwenye vyombo vya habari vya umma...
Is this normal lakini kwa CCM mtia nia kuwa mmoja tu!?

(Swali la ufahamu).
 

Meya ya Jiji la Dar es salaam Mh. Isaya Charles Mwita ametangaza rasmi nia yake ya kuwania nafasi ya kugombania Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA

Je atawezana !!!!!!!
 
Chadema wanafanya maigizo sana kwenye sehemu nyeti

Ajaribu ubunge kwanza , Uraisi sio lelemama

Lowassa na Mvuto wote alipata kura million 6,

Hawa wagombea wa sasa ,sidhan hata kama watapata kura laki 1
 

Meya ya Jiji la Dar es salaam Mh. Isaya Charles Mwita ametangaza rasmi nia yake ya kuwania nafasi ya kugombania Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA

Je atawezana !!!!!!!
Mbona kwenye uenyekiti hamkufanya hivi mgemtambua yule aliyenunua ile nafasi yake!
 
Chadema wanafanya maigizo sana kwenye sehemu nyeti

Ajaribu ubunge kwanza , Uraisi sio lelemama

Lowassa na Mvuto wote alipata kura million 6,

Hawa wagombea wa sasa ,sidhan hata kama watapata kura laki 1

Na Jiwe ambaye hakuwa na mvuto Kabisa aliyepenyeza Bahati Mbaya akapata kura mil 8
 

Meya ya Jiji la Dar es salaam Mh. Isaya Charles Mwita ametangaza rasmi nia yake ya kuwania nafasi ya kugombania Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA

Je atawezana !!!!!!!
Ile issue ya Makonda kumng'oa kwenye umeya iliishia wapi ?
 

Meya ya Jiji la Dar es salaam Mh. Isaya Charles Mwita ametangaza rasmi nia yake ya kuwania nafasi ya kugombania Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA

Je atawezana !!!!!!!
Demokrasia
 
Yes nimemuona live kupitia TBC rais Magufuli akichukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM.

Kule tuu kuonyeshea live kupitia TBC ni kitu kizuri kwa kuonyeshea transparency ya zoezi hili zima, na kwa vile TBC ni public broadcasting station yaani TV ya umma, imetimiza wajibu wake kikamilifu kututangazia live, na natoa wito kwa vyama vyote vya siasa vitakavyo simamisha wagombea urais, kutoa ushirikiano kwa TBC ili TBC iwatangazie live Watanzania wagombea wao na kuwapa fursa Watanzania kuwaona wagombea wote wakipewa haki sawa kwenye vyombo vya habari vya umma....
I am failing to get good words to describe you!
1. Eti ameonyesha transparency.. Tangu 2015 todate TBC imekuwa ikimtangaza yeye peke yake, He has been making himself tranparent at the expense of other parties, leo eti amekuwa transparent! Umelogwa! Unadhani wapinzania hawataki kuonekana? akili imehama , imehama kabisa kabisa!!

2. Eti usafiri binafis! Unajuaje kama kabadilsha namba? Kama amedirki kuchota 1.5 triloni, kujenga uwanja wa ndege bila ruhusa ya bunge, kugawa hela barabarani, leo ashindwe kuchukua gari ya serikali kuchukua fomu . You must be crazy!

3. Eti uswa wa demokrasia, eti makali ya kusu etc . Amefanya siasa peke yake na chama chake for 5 yrs, leo ndiyo ameona kuna demokrasia! "amewanyonga" wapinzani leo eti demokrasia
You are nuts!
 
Mungu ibariki chadema na mungu ibariki kamati kuu ya chadema ikaje na majina matatu ya watu ili mkutano mkuu ukawaletee watanzania chaguo sahihi kwenye uchaguzi wa mwaka huu...nikiwa Kama Mjumbe wa mkutano mkuu na Mjumbe wa baraza kuu nasema lazima tuje na jina ambalo ni ndoto ya kila mtanzania kwenye uchaguzi wa mwaka huu...

Msituangushe tunaomba Lissu
 
Ni kupoteza muda kujipa matumaini kwa mambo usiyoyaweza!
Wenye akili wanahangaika Magufuri aoongezewe muda , nyinyi mnahangaika na kutafuta wagombea?

Una maana gani?

Hii kauli itolee ndani ya CCM kwa sbb kwenu Magufuli anayosha na hakuna mwingine kum - challenge.

Nje ya CCM atakutana na wanaume watakaomchambua kama karanga za mboga.

Magufuli hatoshi, hafai kuendelea na tayari alishaanza kulia lia.
 


Ikumbukwe kwamba waliotia nia ni wengi lakini ni wachache waliojitangaza hadharani , Sasa leo tega sikio ili usikie ni akina nani wengine Wazito sana waliotia nia ya kuomba Urais wa Tanzania kupitia Chadema .

Mungu ibariki Chadema

=======

----UPDATE----

Ndugu wanahabari

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinapenda kuutarifu Umma wa Watanzania kupitia mkutano huu kuwa jumla ya wanachama 11 wamejitokeza kutia nia ya kuwania uteuzi wa kupeperusha bendera, kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba, mwaka huu, ambao utahusisha pia nafasi za udiwani, uwakilishi na ubunge.

Wanachama hao ambao idadi yao na majina yao yanatangazwa rasmi kwa umma kupitia taarifa hii kwa vyombo vya habari, wamejitokeza, kila mmoja kwa wakati wake, ndani ya muda uliowekwa, kutangaza nia hiyo kwa kutekeleza Kifungu cha (1) cha Mwongozo wa Chama wa Kutangaza Kusudio la Kuwania Nafasi za Uongozi Kwenye Vyombo vya Uwakilishi Serikalini, kipengele cha (g), ambacho kinatamka;

"Kwa nafasi ya Uongozi wa Kitaifa ndani ya Chama na Urais taarifa za walio na kusudio la kugombea nafasi hizo zitawasilishwa kwa Katibu Mkuu na kujadiliwa na Kamati Kuu na kutolewa uamuzi kwa hatua zinazofuata."

Mtakumbuka kuwa mnamo, Juni 3, mwaka huu, Chadema kupitia tamko lililotolewa na Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. John Mnyika, kilifungua rasmi mlango kwa mwanachama yeyote anayetaka kutia nia ya nafasi ya urais, kuandika barua ya kusudio lake Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama.

Hadi mlango huo wa kutia nia unafungwa rasmi Juni 15, mwaka huu, saa 10.00 jioni, ikiwa ni jumla ya siku 12 baada ya kufunguliwa, wanachama waliotekeleza kanuni hiyo ni hawa wafuatao;

 Charles, Mwita Isaya
 Lissu, Tundu A.M
 Dkt. Majinge, Mayrose Kavura
 Manyama, Leonard Toja
 Mbowe, Freeman Aikaeli
 Mch. Msigwa, Peter Simon
 Adv. Mwanalyela, Gasper Nicodemus
 Nalo, Opiyo G.O.M
 Adv. Neo, Simba Richmund
 Nyalandu, Lazaro Samuel
 Shaban, Msafiri

Ndugu wanahabari

Ofisi ya Katibu Mkuu pia ilipokea barua iliyokuwa imeandikwa na vijana wa makundi mbalimbali ya waendesha bodaboda, kwa niaba ya mwanachama mmoja ambaye wao waliona anafaa kutia nia ya kuwania urais, lakini kwa kuwa barua hiyo haijakidhi matakwa ya kifungu hicho cha 1(g) cha mwongozo uliotajwa hapo juu, haijazingatiwa na hivyo hata jina la mwanachama huyo halijawekwa katika orodha ya watia nia wala hajatajwa hapa katika taarifa hii.

Hivyo basi, kufungwa rasmi kwa mlango huo wa kutia nia, kunaruhusu kuendelea kwa hatua zingine kwa mujibu wa taratibu za Chadema, kwa kuzingatia Katiba, Kanuni na Miongozo mbalimbali. Kwa mujibu wa mwongozo ulionukuliwa hapo juu, kwa sasa majina ya watia nia wote yatawasilishwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Chama, ambayo nayo itatekeleza wajibu wake kwa hatua mbalimbali katika mchakato huu kwa kuzingatia ibara ya 7.7.16 ya Katiba ya Chadema.

Ni vyema pia tukawakumbusha wanahabari na wananchi wote wanaofuatilia mchakato huu kuwa, hatua hii ya kutia nia ilihusisha kuandika barua kwa Katibu Mkuu na si kuchukua na kurudisha fomu. Hatua nyingine zinazofuata zitatangazwa baadae.

Imetolewa leo, Jumatano, Juni 17, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema


CHADEMA, please....please and please kupitia utaratibu wenu wowote na vikao vyenu vyote, watanzania tulio mamilioni kwa mamilioni tunamhitaji TUNDU A. M. LISSU apambane na CCM....

there's no way mkatuletea mtu mwingine na kumpa nafasi kuwania Urais wa JMT kwa tiketi ya chama chenu kisha watanzania tunaowaunga mkono tukawaelewa.....

Msifanye kosa la mwaka 2015 lililozaa yote haya. TUNAWAUNGA MKONO, FANYENI MAAMUZI SAHIHI....
 
Hakuna hata Jina lialoanza na Dr? Si ndiyo Chama cha wasomi hichi, au nimechanganya?
 
Siku moja tu baada ya Lisu kutumia masaa 4 akiwahutubia watanzania na kuwapa sababu za kwa nini anatangaza nia ya kuwania urais wa Tanzania, huku nyuma Mbowe akaibuka na igizo la kuvamiwa na watu wasiojulikana, kisha kukanyagwa kanyagwa na kuvunjwa mguu wa kulia bila mtoto wake James aliyekuwa ndani kusikia chochote ,badala yake akasikia Joyce Mkuya aliyekuwa umbali wa kilomita 5!!
Lengo la hili igizo ilikuwa ni kufunika habari ya Lisu kuandikwa na vyombo vya habari.

Kana kwamba haitoshi Mbowe baada tu ya kuruhusiwa kutoka hospitali ,huku akichechemea akatangaza nia ya kugombea urais wa Tanzania!

Yani watanzania wakiwa na hamu ya kusikia report kutoka kwa Mbowe mwenyewe kwamba alivamiwaje, ilikuwaje ,badala ya kujibu hizo hoja ,yeye akaja na igizo jingine la kwamba kuna wazee wameenda nyumbani kwake kumshawishi awanie urais wa Tanzania!!.

Hivi Lisu unataka ufanyiwe nini ndiyo ujue kwa sasa hauhitajiki Chadema?
Haya maigizo ya mwenyekiti wako wa chama kufunika utangazaji wako nia hayajakuamsha tu?.

Shituka
Mbona mnamuogopa sana Lissu? Huko ccm mnamuona tu kama Messi baada ya lile jaribio lenu dhidi ya uhai wake kubaunz.
 
hawa nao. wasije wakawafukuza uanachama wengine kisa kugombea nafasi pamoja na mwenyekiti wao
 
Sawa CHEDEMA tupeni list yenu, na wana Lumumba tunaisubiri ya kwenu... Hiki ndicho kipimo sahihi cha demokrasia ndani ya vyama vyenu.
Kwa bahati mbaya ccm hawana Presidential Candidate ila wana "The Warlord disguising as a Presidential Candidate"..
 
Back
Top Bottom