Uchaguzi 2020 CHADEMA: Wanachama 11 wachukua fomu za kugombea nafasi ya Urais wa Tanzania

Je Ile dhana ya Chama cha wasomi inajifia?

Ila katika kuangalia kiongozi Bora Swala la elimu linaweza likawa pendekezo la pili ingawa elimu ni mhumu (baada ya lile mtu mwenye uwezo)
Unachagua sura au matendo ya mtu?.... Unaangalia sifa au hoja/sera za mgombea?
 
Ikumbukwe kwamba waliotia nia ni wengi lakini ni wachache waliojitangaza hadharani , Sasa leo tega sikio ili usikie ni akina nani wengine Wazito sana waliotia nia ya kuomba Urais wa Tanzania kupitia Chadema .

Mungu ibariki Chadema

=======

----UPDATE----

Ndugu wanahabari

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinapenda kuutarifu Umma wa Watanzania kupitia mkutano huu kuwa jumla ya wanachama 11 wamejitokeza kutia nia ya kuwania uteuzi wa kupeperusha bendera, kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba, mwaka huu, ambao utahusisha pia nafasi za udiwani, uwakilishi na ubunge.

Wanachama hao ambao idadi yao na majina yao yanatangazwa rasmi kwa umma kupitia taarifa hii kwa vyombo vya habari, wamejitokeza, kila mmoja kwa wakati wake, ndani ya muda uliowekwa, kutangaza nia hiyo kwa kutekeleza Kifungu cha (1) cha Mwongozo wa Chama wa Kutangaza Kusudio la Kuwania Nafasi za Uongozi Kwenye Vyombo vya Uwakilishi Serikalini, kipengele cha (g), ambacho kinatamka;

"Kwa nafasi ya Uongozi wa Kitaifa ndani ya Chama na Urais taarifa za walio na kusudio la kugombea nafasi hizo zitawasilishwa kwa Katibu Mkuu na kujadiliwa na Kamati Kuu na kutolewa uamuzi kwa hatua zinazofuata."

Mtakumbuka kuwa mnamo, Juni 3, mwaka huu, Chadema kupitia tamko lililotolewa na Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. John Mnyika, kilifungua rasmi mlango kwa mwanachama yeyote anayetaka kutia nia ya nafasi ya urais, kuandika barua ya kusudio lake Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama.

Hadi mlango huo wa kutia nia unafungwa rasmi Juni 15, mwaka huu, saa 10.00 jioni, ikiwa ni jumla ya siku 12 baada ya kufunguliwa, wanachama waliotekeleza kanuni hiyo ni hawa wafuatao;

 Charles, Mwita Isaya
 Lissu, Tundu A.M
 Dkt. Majinge, Mayrose Kavura
 Manyama, Leonard Toja
 Mbowe, Freeman Aikaeli
 Mch. Msigwa, Peter Simon
 Adv. Mwanalyela, Gasper Nicodemus
 Nalo, Opiyo G.O.M
 Adv. Neo, Simba Richmund
 Nyalandu, Lazaro Samuel
 Shaban, Msafiri

Ndugu wanahabari

Ofisi ya Katibu Mkuu pia ilipokea barua iliyokuwa imeandikwa na vijana wa makundi mbalimbali ya waendesha bodaboda, kwa niaba ya mwanachama mmoja ambaye wao waliona anafaa kutia nia ya kuwania urais, lakini kwa kuwa barua hiyo haijakidhi matakwa ya kifungu hicho cha 1(g) cha mwongozo uliotajwa hapo juu, haijazingatiwa na hivyo hata jina la mwanachama huyo halijawekwa katika orodha ya watia nia wala hajatajwa hapa katika taarifa hii.

Hivyo basi, kufungwa rasmi kwa mlango huo wa kutia nia, kunaruhusu kuendelea kwa hatua zingine kwa mujibu wa taratibu za Chadema, kwa kuzingatia Katiba, Kanuni na Miongozo mbalimbali. Kwa mujibu wa mwongozo ulionukuliwa hapo juu, kwa sasa majina ya watia nia wote yatawasilishwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Chama, ambayo nayo itatekeleza wajibu wake kwa hatua mbalimbali katika mchakato huu kwa kuzingatia ibara ya 7.7.16 ya Katiba ya Chadema.

Ni vyema pia tukawakumbusha wanahabari na wananchi wote wanaofuatilia mchakato huu kuwa, hatua hii ya kutia nia ilihusisha kuandika barua kwa Katibu Mkuu na si kuchukua na kurudisha fomu. Hatua nyingine zinazofuata zitatangazwa baadae.

Imetolewa leo, Jumatano, Juni 17, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema

Hivi si hata zile za uenyekiti wa taifa na kanda walichukua wengi tu? Maamuzi ya ni nani apitiswe yalifanya na mwenye chama, sijui kama maamuzi ya nain apite kuwa mgombea wa uras yatafanana na yale
 
Tarehe ya kikao cha kamati kuu vipi?
Au hakijapangwa????
Tusubiri tuone kamati kuu ambayo wenyeviti wote ni wagombea watakavyozichanga karata mezani!
 
Kwanza je watafanyi kwa njia ya video? Maaana wanasema corona bado ipo.
 
Nadhani atakuwa huyu bwana
JamiiForums1858942893.jpg

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Kitafanyika nyumbani kwa Mbowe chini ya Heche,Mdee na Mnyika.hawa eti ndo wapewe nchi!!.hovyo kabisa hawa jamaa.
 
Mpaka sasa vyama vimetoa fomu kwa wanachama mbalimbali katika nafasi ya kiti cha Urais

CCM Zanzibar zaidi ya wagombea kumi

CCM Tanzania Bara mgombea mmoja tu kachukua fomu mpaka sasa

CHADEMA zaidi ya wagombea kumi wamejitokeza

TLP fomu ya kiti cha Urais inamsubiri mgombea wa CCM kwenda kuchukua mana chama kilimpitisha mgombea wa chama kingine

NCCR MAGEUZI mgombea mmoja mpaka sasa kachukua fomu
 
Kwanza ikumbukwe kuwa CCM ni chama Dola na kwamba mgombea urais wa JMT anakwenda kuwa mkuu wa vyombo vya dola tofauti na rais wa TFF au CWT.

Pili, uchaguzi mkuu katika ngazi ya chama kuna wagombea urais wawili yule wa JMT na yule wa Zanzibar na wawili hawa wana majukumu tofauti

Nirudi kwenye mada, Rais wa JMT ndiye mkuu wa vyombo vya dola nchini na mihimili yake kwahiyo mgombea wa nafasi hiyo ni lazima awe na sifa za kukubalika kidola.
Je, miongoni mwa wagombea wale 11 wa Chadema kuna yoyote mwenye sifa za kustahili kuwa mkuu wa vyombo vya dola?

Nawatakia Dominica yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
Ikumbukwe kwamba waliotia nia ni wengi lakini ni wachache waliojitangaza hadharani , Sasa leo tega sikio ili usikie ni akina nani wengine Wazito sana waliotia nia ya kuomba Urais wa Tanzania kupitia Chadema .

Mungu ibariki Chadema

=======

----UPDATE----

Ndugu wanahabari

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinapenda kuutarifu Umma wa Watanzania kupitia mkutano huu kuwa jumla ya wanachama 11 wamejitokeza kutia nia ya kuwania uteuzi wa kupeperusha bendera, kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba, mwaka huu, ambao utahusisha pia nafasi za udiwani, uwakilishi na ubunge.

Wanachama hao ambao idadi yao na majina yao yanatangazwa rasmi kwa umma kupitia taarifa hii kwa vyombo vya habari, wamejitokeza, kila mmoja kwa wakati wake, ndani ya muda uliowekwa, kutangaza nia hiyo kwa kutekeleza Kifungu cha (1) cha Mwongozo wa Chama wa Kutangaza Kusudio la Kuwania Nafasi za Uongozi Kwenye Vyombo vya Uwakilishi Serikalini, kipengele cha (g), ambacho kinatamka;

"Kwa nafasi ya Uongozi wa Kitaifa ndani ya Chama na Urais taarifa za walio na kusudio la kugombea nafasi hizo zitawasilishwa kwa Katibu Mkuu na kujadiliwa na Kamati Kuu na kutolewa uamuzi kwa hatua zinazofuata."

Mtakumbuka kuwa mnamo, Juni 3, mwaka huu, Chadema kupitia tamko lililotolewa na Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. John Mnyika, kilifungua rasmi mlango kwa mwanachama yeyote anayetaka kutia nia ya nafasi ya urais, kuandika barua ya kusudio lake Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama.

Hadi mlango huo wa kutia nia unafungwa rasmi Juni 15, mwaka huu, saa 10.00 jioni, ikiwa ni jumla ya siku 12 baada ya kufunguliwa, wanachama waliotekeleza kanuni hiyo ni hawa wafuatao;

 Charles, Mwita Isaya
 Lissu, Tundu A.M
 Dkt. Majinge, Mayrose Kavura
 Manyama, Leonard Toja
 Mbowe, Freeman Aikaeli
 Mch. Msigwa, Peter Simon
 Adv. Mwanalyela, Gasper Nicodemus
 Nalo, Opiyo G.O.M
 Adv. Neo, Simba Richmund
 Nyalandu, Lazaro Samuel
 Shaban, Msafiri

Ndugu wanahabari

Ofisi ya Katibu Mkuu pia ilipokea barua iliyokuwa imeandikwa na vijana wa makundi mbalimbali ya waendesha bodaboda, kwa niaba ya mwanachama mmoja ambaye wao waliona anafaa kutia nia ya kuwania urais, lakini kwa kuwa barua hiyo haijakidhi matakwa ya kifungu hicho cha 1(g) cha mwongozo uliotajwa hapo juu, haijazingatiwa na hivyo hata jina la mwanachama huyo halijawekwa katika orodha ya watia nia wala hajatajwa hapa katika taarifa hii.

Hivyo basi, kufungwa rasmi kwa mlango huo wa kutia nia, kunaruhusu kuendelea kwa hatua zingine kwa mujibu wa taratibu za Chadema, kwa kuzingatia Katiba, Kanuni na Miongozo mbalimbali. Kwa mujibu wa mwongozo ulionukuliwa hapo juu, kwa sasa majina ya watia nia wote yatawasilishwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Chama, ambayo nayo itatekeleza wajibu wake kwa hatua mbalimbali katika mchakato huu kwa kuzingatia ibara ya 7.7.16 ya Katiba ya Chadema.

Ni vyema pia tukawakumbusha wanahabari na wananchi wote wanaofuatilia mchakato huu kuwa, hatua hii ya kutia nia ilihusisha kuandika barua kwa Katibu Mkuu na si kuchukua na kurudisha fomu. Hatua nyingine zinazofuata zitatangazwa baadae.

Imetolewa leo, Jumatano, Juni 17, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema

ALL THE BEST!
 
Utasikia MEMBE ametia nia kupitia CHADEMA
Nadhani masharti aliyotoa Membe huko CHADEMA yamewashinda. Hakutaka kushindanishwa na yeyote, alitaka lipite jina lake tu na aungwe mkono na hiyo anayo ita "grand coalition". Hii ni kwa sababu anajua yeye mwenyewe au hata na akina ACT - Wananchi na wengine HAWEZI NA HATOSHI!
 
Ikumbukwe kwamba waliotia nia ni wengi lakini ni wachache waliojitangaza hadharani , Sasa leo tega sikio ili usikie ni akina nani wengine Wazito sana waliotia nia ya kuomba Urais wa Tanzania kupitia Chadema .

Mungu ibariki Chadema

=======

----UPDATE----

Ndugu wanahabari

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinapenda kuutarifu Umma wa Watanzania kupitia mkutano huu kuwa jumla ya wanachama 11 wamejitokeza kutia nia ya kuwania uteuzi wa kupeperusha bendera, kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba, mwaka huu, ambao utahusisha pia nafasi za udiwani, uwakilishi na ubunge.

Wanachama hao ambao idadi yao na majina yao yanatangazwa rasmi kwa umma kupitia taarifa hii kwa vyombo vya habari, wamejitokeza, kila mmoja kwa wakati wake, ndani ya muda uliowekwa, kutangaza nia hiyo kwa kutekeleza Kifungu cha (1) cha Mwongozo wa Chama wa Kutangaza Kusudio la Kuwania Nafasi za Uongozi Kwenye Vyombo vya Uwakilishi Serikalini, kipengele cha (g), ambacho kinatamka;

"Kwa nafasi ya Uongozi wa Kitaifa ndani ya Chama na Urais taarifa za walio na kusudio la kugombea nafasi hizo zitawasilishwa kwa Katibu Mkuu na kujadiliwa na Kamati Kuu na kutolewa uamuzi kwa hatua zinazofuata."

Mtakumbuka kuwa mnamo, Juni 3, mwaka huu, Chadema kupitia tamko lililotolewa na Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. John Mnyika, kilifungua rasmi mlango kwa mwanachama yeyote anayetaka kutia nia ya nafasi ya urais, kuandika barua ya kusudio lake Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama.

Hadi mlango huo wa kutia nia unafungwa rasmi Juni 15, mwaka huu, saa 10.00 jioni, ikiwa ni jumla ya siku 12 baada ya kufunguliwa, wanachama waliotekeleza kanuni hiyo ni hawa wafuatao;

 Charles, Mwita Isaya
 Lissu, Tundu A.M
 Dkt. Majinge, Mayrose Kavura
 Manyama, Leonard Toja
 Mbowe, Freeman Aikaeli
 Mch. Msigwa, Peter Simon
 Adv. Mwanalyela, Gasper Nicodemus
 Nalo, Opiyo G.O.M
 Adv. Neo, Simba Richmund
 Nyalandu, Lazaro Samuel
 Shaban, Msafiri

Ndugu wanahabari

Ofisi ya Katibu Mkuu pia ilipokea barua iliyokuwa imeandikwa na vijana wa makundi mbalimbali ya waendesha bodaboda, kwa niaba ya mwanachama mmoja ambaye wao waliona anafaa kutia nia ya kuwania urais, lakini kwa kuwa barua hiyo haijakidhi matakwa ya kifungu hicho cha 1(g) cha mwongozo uliotajwa hapo juu, haijazingatiwa na hivyo hata jina la mwanachama huyo halijawekwa katika orodha ya watia nia wala hajatajwa hapa katika taarifa hii.

Hivyo basi, kufungwa rasmi kwa mlango huo wa kutia nia, kunaruhusu kuendelea kwa hatua zingine kwa mujibu wa taratibu za Chadema, kwa kuzingatia Katiba, Kanuni na Miongozo mbalimbali. Kwa mujibu wa mwongozo ulionukuliwa hapo juu, kwa sasa majina ya watia nia wote yatawasilishwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Chama, ambayo nayo itatekeleza wajibu wake kwa hatua mbalimbali katika mchakato huu kwa kuzingatia ibara ya 7.7.16 ya Katiba ya Chadema.

Ni vyema pia tukawakumbusha wanahabari na wananchi wote wanaofuatilia mchakato huu kuwa, hatua hii ya kutia nia ilihusisha kuandika barua kwa Katibu Mkuu na si kuchukua na kurudisha fomu. Hatua nyingine zinazofuata zitatangazwa baadae.

Imetolewa leo, Jumatano, Juni 17, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema

Update ya mchakato?.
P
 
Back
Top Bottom