CHADEMA wananukuu kila kitu kutoka Ujerumani ambako habari ya kubadilishana madaraka ni nadra sana

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,019
Reaction score
6,825
Kiongozi wa Ujerumani Angela Merkel amekuwa chancellor wa Ujerumani toka 2005
Jakaya Kikwete kamkuta kamuacha
John Pombe Magufuli kamkuta kamuacha
Samia Suluhu Hassan kamkuta

Huko duniani kafanya kazi na:-
Marais 4 wa Marekani,
Mawaziri Wakuu 2 wa Canada,
Mawaziri Wakuu 3 wa Japan,
Marais 4 wa Ufaransa
Mawaziri 5 wa Uingereza na
Mawaziri 10 wa Italia

NA MWENYEKITI MMOJA WA CHADEMA KAMANDA MBOWE
 
Angela Markel sio kiongozi wa Ujerumani, Ujerumani inayo Rais ambaye ndiye mkuu/Kiongozi wa nchi. Markel ni kiongozi wa Serikali kama alivyo Netanyahu, alivyo Johnson.
Tafakari kidogo. Katika nchi hizo rais si "kiongozi wa taifa". (halafu mama yule wa Ujerumani anaitwa MErkel, si MArkel). Malkia wa Uingereza anasoma bungeni hotuba iliyo andikwa na waziri mkuu (hivyo ameshasoma: Uingereza inajiunga na Ulaya , baadaye: Uingereza inaondoka Ulaya, kodi juu, kodi chini...).
Pale Ujeruani ni chansela (=waziri mkuu) anayeamuru mwelekeo wa siasa. Raisi hana neno katika siasa. Anaangalia tu, kama katiba inafuatwa, anamteua mwanasiasa kama chansela tu kama wabunge wanashindwa kufikia suluhisho.
 
Mbona unazunguka sana mkuu. Labda nisaidie Frank-Walter Steinmeier ana wadhifa gani Ujerumani? Na Angela Merkel naye ana wadhifa gani?
 
Kiongozi wa Ujerumani Angela Merkel amekuwa chancellor wa Ujerumani toka 2005
Jakaya Kikwete kamkuta kamuacha
John Pombe Magufuli kamkuta kamuacha
Samia Suluhu Hassan kamkuta

Huko duniani kafanya kazi na:-
Marais 4 wa Marekani,
Mawaziri Wakuu 2 wa Canada,
Mawaziri Wakuu 3 wa Japan,
Marais 4 wa Ufaransa
Mawaziri 5 wa Uingereza na
Mawaziri 10 wa Italia

NA MWENYEKITI MMOJA WA CHADEMA KAMANDA MBOWE
Huyu hajamuacha Markel, kaondoshwa na Mungu, bila hivyo angelikuwa wa maisha
 
Hivi kwa nini wamarekani hawawakemei Ujerumani kwenye hilo la katiba kubadilishwa ili kumuongezea yule kikongwe muda wa kuongoza
 
L

Katiba ya Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani haijawahi kubadilishwa ili kumuongezea Chancellor Merkel muda.
Kwa kifupi mchakato wa kupata Chancellor:-
Kila baada ya miaka minne wajerumani wanapiga Kura kuwachagua wawakilishi wao katika bunge lao (bundestag), bunge hilo ndilo linaloamua nani awe kiongozi wa serekali (Chancellor).
Baada ya kushauriana na kila kundi bungeni, raisi wa shirikisho atapeleka pendekezo la mgombea wa nafasi ya u-Chancellor wa shirikisho la Ujerumani bungeni. Bunge litapiga kura ya kumchagua Chancellor bila kujadili pendekezo lililoletwa na raisi wa shirikisho la Ujerumani, baada ya kupata kura zaidi ya asilimia hamsini za wawakilishi bungeni Chancellor ataapishwa na raisi wa bunge.

Angela Merkel aliamua kustastaafu kukiongoza chama chake cha CDU mwaka 2018 hivyo ni wazi kuwa atastaafu u-chancellor baada ya uchaguzi ujao mwezi wa 9 mwaka huu
 
Mbona unazunguka sana mkuu. Labda nisaidie Frank-Walter Steinmeier ana wadhifa gani Ujerumani? Na Angela Merkel naye ana wadhifa gani?
Frank-Walter Steinmeir ni Raisi wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani
Mamlaka:-
*Kumpendekeza waziri mkuu (chancellor) bungeni,
*Kumteua na kumtengua Chancellor pamoja na mawaziri wa wizara nyingine,
*Kulivunja bunge,
*Kutangaza hali ya dharura bungeni katika hali fulani
*kuitisha bunge
*Kusaini na kutangaza sheria au kupiga kura ya turufu (veto) katika hali fulani
*Kuteua na kufukuza kazi majaji wa shirikisho, wafanyikazi wa serikali, na maafisa walioamriwa na wasioamriwa wa Jeshi
*Mamlaka ya kutangaza msamaha kwa wafungwa kwa niaba ya Shirikisho
*Kutoa tuzo kwa niaba ya Shirikisho
* Na kuiwakilisha Ujerumani nje na ndani ya nchi
Kwa lugha nyepesi raisi anasimamia sheria na katiba ya nchi

Angela Merkel ni waziri mkuu wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani
Mamlaka:-
# Mkuu wa serekali
# Mtendaji mkuu wa Ujerumani
# Amiri jeshi mkuu wa vikosi vya kijeshi vya Ujerumani wakati wa vita
Katiba ya Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani imeweka mamlaka mapana kwa Chancellor kuanzisha sera ya serekali. Kwa sababu hio baadhi ya waangalizi huuita mfumo wa kisiasa wa Ujerumani kama 'demokrasia ya Chancellor'.
 
Nani ni Mkuu wa dola/nchi/taifa la Ujerumani? ndilo swali naona unatoa job descriptions.
 
Mbona unazunguka sana mkuu. Labda nisaidie Frank-Walter Steinmeier ana wadhifa gani Ujerumani? Na Angela Merkel naye ana wadhifa gani?
Kaka unatumia kompyuta, Umewahi kufungua Wikipedia au Google search?
Rais wa Ujerumani ni mkuu wa dola katika Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani.
Kazi yake ni kuwa alama ya umoja wa taifa, lakini katika mfumo wa serikali ya kibunge nchini Ujerumani hana madaraka mengi. Madaraka muhimu ya kisiasa ni kama yafuatayo
  • rais anapaswa kutia sahihi kwa kila sheria iliyopitishwa bungeni. Hapa anaweza kukataa akiona sababu muhimu ya kwamba sheria hailingani na katiba. Akikataa bunge ina njia ya kusahihisha sheria au kumshtaki rais mbele ya mahakama kuu. Tangu 1949 maraisi wa Ujerumani walikataa mara 9 kutia sahihi wakalazimisha serikali na bunge kubadilisha sheria.
  • rais anaamua kama bunge inavunjwa baada ya chansella kushindwa katika swali la imani katika serikali; chansella kama kiongozi wa serikali anaweza kudai kura ya bunge kama ina imani katika serikali. Kama swali hili linakataliwa na wabunge wengi chansella anaweza kumwomba rais kuvunja bunge na uchaguzi wa bunge jipya. Lakini azimio liko mkononi mwa rais anayeweza kumteua kiongozi mwingine atakaye jaribu kuunda serikali mpya.
 
Frank-Walter Steinmeir ni Raisi wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani
Mamlaka:-
*Kumpendekeza waziri mkuu (chancellor) bungeni,
*Kumteua na kumtengua Chancellor pamoja na mawaziri wa wizara nyingine,
*Kulivunja bunge,
*Kutangaza hali ya dharura bungeni katika hali fulani
*kuitisha bunge
*Kusaini na kutangaza sheria au kupiga kura ya turufu (veto) katika hali fulani
*Kuteua na kufukuza kazi majaji wa shirikisho, wafanyikazi wa serikali, na maafisa walioamriwa na wasioamriwa wa Jeshi
*Mamlaka ya kutangaza msamaha kwa wafungwa kwa niaba ya Shirikisho
*Kutoa tuzo kwa niaba ya Shirikisho
* Na kuiwakilisha Ujerumani nje na ndani ya nchi
Kwa lugha nyepesi raisi anasimamia sheria na katiba ya nchi

Angela Merkel ni waziri mkuu wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani
Mamlaka:-
# Mkuu wa serekali
# Mtendaji mkuu wa Ujerumani
# Amiri jeshi mkuu wa vikosi vya kijeshi vya Ujerumani wakati wa vita
Katiba ya Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani imeweka mamlaka mapana kwa Chancellor kuanzisha sera ya serekali. Kwa sababu hio baadhi ya waangalizi huuita mfumo wa kisiasa wa Ujerumani kama 'demokrasia ya Chancellor'.
Asante, umejitahidi lakini katika tafsiri yako kuna makosa kidogo. Rais wa Ujerumani hawezi
* "Kumteua na kumtengua Chancellor pamoja na mawaziri" - si azimio lake; rais anampendekeza kiongozi bungeni akiona ana wabunge wa kutosha, baadaye bunga linachagua na rais anapaswa kumteua, pia kumtengua KAMA bunge limeamua dhidi yake.
*Kulivunja bunge ni haki kwa hali maalum pekee kama bunge limeshindwa kumchagua chansela
*kuitisha bunge hapa hana mamlaka
*Kuteua na kufukuza kazi majaji wa shirikisho, wafanyikazi wa serikali, na maafisa walioamriwa na wasioamriwa wa Jeshi Hawezi kufukuza watu. Anatia sahihi kwenye hati za kuteua na kutengua, lakini haamui. Maazimio ni ya watu wengine kufuatana na sheria mbalimbali na katiba.

Mamlaka kuu ya raisi wa Ujerumani ni wakati asilimia 51 za wabunge hazipatikani kumchagua chansela. Hapa ni azimio la rais kama anamkubali chansela mwenye kura nyingi (lakini chini ya nusu ya wabunge) au kama anaamuru uchaguzi mpya wa bunge. haikutokea bado tangu mwanzo wa Jamhuri mwaka 1949.
 
Kaka unatumia kompyuta, Umewahi kufungua Wikipedia au Google search?
Rais wa Ujerumani ni mkuu wa dola katika Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani.
Kazi yake ni kuwa alama ya umoja wa taifa, lakini katika mfumo wa serikali ya kibunge nchini Ujerumani hana madaraka mengi. Madaraka muhimu ya kisiasa ni kama yafuatayo
  • rais anapaswa kutia sahihi kwa kila sheria iliyopitishwa bungeni. Hapa anaweza kukataa akiona sababu muhimu ya kwamba sheria hailingani na katiba. Akikataa bunge ina njia ya kusahihisha sheria au kumshtaki rais mbele ya mahakama kuu. Tangu 1949 maraisi wa Ujerumani walikataa mara 9 kutia sahihi wakalazimisha serikali na bunge kubadilisha sheria.
  • rais anaamua kama bunge inavunjwa baada ya chansella kushindwa katika swali la imani katika serikali; chansella kama kiongozi wa serikali anaweza kudai kura ya bunge kama ina imani katika serikali. Kama swali hili linakataliwa na wabunge wengi chansella anaweza kumwomba rais kuvunja bunge na uchaguzi wa bunge jipya. Lakini azimio liko mkononi mwa rais anayeweza kumteua kiongozi mwingine atakaye jaribu kuunda serikali mpya.
Yote haya sipingani nayo wala sijui yanahusiana nini na nilichokisema. Nilichosema mimi ni kuwa Frank ndiye Head of the State na Angela ni Head of the government.
 
Asante, umejitahidi lakini katika tafsiri yako kuna makosa kidogo. Rais wa Ujerumani hawezi
* "Kumteua na kumtengua Chancellor pamoja na mawaziri" - si azimio lake; rais anampendekeza kiongozi bungeni akiona ana wabunge wa kutosha, baadaye bunga linachagua na rais anapaswa kumteua, pia kumtengua KAMA bunge limeamua dhidi yake.
*Kulivunja bunge ni haki kwa hali maalum pekee kama bunge limeshindwa kumchagua chansela
*kuitisha bunge hapa hana mamlaka
*Kuteua na kufukuza kazi majaji wa shirikisho, wafanyikazi wa serikali, na maafisa walioamriwa na wasioamriwa wa Jeshi Hawezi kufukuza watu. Anatia sahihi kwenye hati za kuteua na kutengua, lakini haamui. Maazimio ni ya watu wengine kufuatana na sheria mbalimbali na katiba.

Mamlaka kuu ya raisi wa Ujerumani ni wakati asilimia 51 za wabunge hazipatikani kumchagua chansela. Hapa ni azimio la rais kama anamkubali chansela mwenye kura nyingi (lakini chini ya nusu ya wabunge) au kama anaamuru uchaguzi mpya wa bunge. haikutokea bado tangu mwanzo wa Jamhuri mwaka 1949.
Ahsante sana kwa kutoa maelezo ya kina, sijakosea ila nilifupisha maelezo. Kila kitu nilichoandika kipo sawa ila katika mamlaka hayo Kuna mazingira yake na sio jumlajumla. Mgawanyo wa madaraka Ujerumani ni mzuri sana, Chancellor ana mamlaka mapana kuliko raisi, lakini kiprotokali Raisi ni wa kwanza akifwatiwa na raisi wa bunge ndo aje Chancellor.

Mfano
*Tofauti na Seneti ya Merikani, Bundestag haishiriki katika mchakato wa uteuzi wa Mawaziri wa Shirikisho. Wanateuliwa na Rais wa Shirikisho juu ya pendekezo la kisheria aliloletewa na Kansela wa Shirikisho

*Bundestag pia inashiriki katika uchaguzi wa Rais wa Shirikisho, ambaye ni mkuu wa nchi na anawakilisha Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani nyumbani na nje ya nchi. Rais wa Shirikisho anachaguliwa na bunge la Shirikisho kwa kura nyingi. Bunge la Shirikisho linakusanyika tu kumchagua Rais wa Shirikisho na linajumuisha washiriki wa Bundestag na idadi sawa ya wanachama waliochaguliwa na serikali za majimbo ya Ujerumani

*Mara tu sheria inapopitishwa na Bundestag ya Ujerumani, Serikali ya Shirikisho huipeleka kwa Rais wa Shirikisho kwa saini yake na kuchapishwa katika Gazeti la Sheria za Shirikisho. Sheria hiyo itaanza kutekelezwa tarehe iliyoainishwa katika sheria hio au, ikiwa hakuna tarehe iliyoainishwa, siku kumi na nne baada ya kuchapishwa kwenye Gazeti la Sheria la Shirikisho.
na mifano mingine mingi...
 
Jukumu muhimu la uongozi katika Bundestag ya Ujerumani inashikiliwa na Rais wa Bundestag

Rais wa Bundestag anawakilisha Bundestag (bunge la Ujerumani) ndani na nje ya nchi. Jukumu moja kuu ni kuhakikisha utunzaji wa utaratibu wa bunge wakati Bunge likiwa kwenye kikao.

Baada ya uchaguzi mkuu, katiba inaamuru kwamba Bundestag mpya la Ujerumani linapaswa kukusanyika kabla ya siku ya thelathini baada ya uchaguzi. Katika kipindi hicho, mazungumzo ya muungano hufanyika ili kuunda serikali ikiwa hakuna chama chochote kilichopata kura nyingi. Serikali ya sasa ya Ujerumani ina muungano mkubwa (grand coalition) wa vyama vya CDU / CSU na SPD

Katika siasa za sasa za Ujerumani, muungano mkubwa (Kijerumani: Große Koalition) unaelezea muungano unaosimamia vyama vya CDU / CSU na SPD, kwani kihistoria wamekuwa vyama vikuu katika chaguzi nyingi za majimbo na za shirikisho tangu 1949

Chama cha CDU ndio chama anachotoka Kiongozi wa sasa wa serekali (Chancellor) Angela Merkel, ambaye alichaguliwa mnamo 2005 na akachaguliwa tena mnamo 2009, 2013 na 2018. Ndiye mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa kansela.
Alihudumu kama kiongozi wa Upinzani kutoka 2002 hadi 2005 na kama kiongozi wa Christian Democratic Union (CDU) kutoka 2000 hadi 2018.
 
Back
Top Bottom