CHADEMA wananukuu kila kitu kutoka Ujerumani ambako habari ya kubadilishana madaraka ni nadra sana

CHADEMA wananukuu kila kitu kutoka Ujerumani ambako habari ya kubadilishana madaraka ni nadra sana

Kiongozi wa Ujerumani Angela Merkel amekuwa chancellor wa Ujerumani toka 2005
Jakaya Kikwete kamkuta kamuacha
John Pombe Magufuli kamkuta kamuacha
Samia Suluhu Hassan kamkuta

Huko duniani kafanya kazi na:-
Marais 4 wa Marekani,
Mawaziri Wakuu 2 wa Canada,
Mawaziri Wakuu 3 wa Japan,
Marais 4 wa Ufaransa
Mawaziri 5 wa Uingereza na
Mawaziri 10 wa Italia

NA MWENYEKITI MMOJA WA CHADEMA KAMANDA MBOWE
Pilipili usiyoila yakuwashani? Waachie wanachama na chama chao. Wao ndiyo waamuzi. Shughulika na chama chako.
 
ANGELA DOROTHEA MERKEL, kazaliwa mwaka 1954.

Merkel anaonekana kama ndiye kiongozi wa ukweli (de facto) wa Jumuiya ya Ulaya na mwanamke mwenye nguvu zaidi ulimwenguni. Kufuatia kuchaguliwa kwa Donald Trump mwaka 2016, vyombo mbalimbali vya habari vilimtaja Merkel kama "kiongozi mpya wa ulimwengu huru".

Angela Dorothea Kasner, ndilo jina lake la kuzaliwa, ni mtoto wa mchungaji wa kanisa la Kilutheri. Angela, msomi wa kweli mwenye PhD ya Quantum Chemistry aliyotunukiwa mnamo mwaka 1986 katika chuo kikuu cha sayansi cha kijerumani, Berlin (German Academy of Sciences at Berlin). Jina la Merkel ni la aliekuwa mumewe Ulrich Merkel ambaye walikutana katika chuo kikuu cha Leipzig (wakati huo kikiitwa chuo kikuu cha KARL MARX) wote wakisoma Physics, wakaoana mwaka 1977 na kuachana mwaka 1982.

Alijiunga na chama cha CDU mwaka 1990

Ifuatayo ni makala ya CNN imuhusuyo Merkel, toleo la tarehe 07 June, 2021.

Mwanzo...

Ni somo gumu wanasiasa wengi - haswa wanaume - wamejifunza kwa miaka 15 iliyopita: Kamwe, usimchukulie poa Angela Merkel

Kansela wa Ujerumani anajiandaa kuachia ngazi baadaye mwaka huu, baada kuweka heshima yake kwa muda kirefu kama mmoja wa viongozi wa kisiasa waliofanikiwa zaidi ulimwenguni.

Katika muda wake ofisini, ameshughulika na mawaziri wakuu watano wa Uingereza, marais wanne wa Ufaransa na mawaziri wakuu saba wa Italia. Wakati Rais mteule Joe Biden alipoingia madarakani, alikuwa kamanda mkuu wa nne wa Marekani ambaye atafanya naye kazi.

200430132306-angela-merkel-press-conference-germany-0430-large-169.jpg


Lakini licha ya rekodi yake, Merkel, kiongozi wa taifa la nne kwa uchumi mkubwa ulimwenguni, ametumia muda mwingi wa kazi yake ya kisiasa kujidhihirisha.

Viongozi wenzake wamejaribu kumshinda nguvu au hata kumdhalilisha. Vladimir Putin wakati flani alikuja na mbwa aina ya labrador kwenye mkutano wake na Kansela ambaye anaogopa mbwa sana. Donald Trump aliwahi kumwambia Kansela kuwa yeye ni mjinga. Silvio Berlusconi aliwahi kumwacha akingoja kikao kwa dakika 15 huku yeye (Berlusconi) akiongea na simu.

Alipokuwa mwanamke wa kwanza kuchukua kazi ya juu kabisa ya Ujerumani mnamo 2005, wengi walimwona kuwa hana uzoefu na hana haiba hivyo hatadumu.

Bild, gazeti la Ujerumani linalosomwa zaidi, liliashiria hafla hiyo kwa picha ya ukurasa wa mbele yenye kichwa cha habari kilichosema "Miss Germany!" Hata ndani ya chama chake mwenyewe, aliitwa "das Mädchen," kijerumani cha neno "binti/ msichana."

Lakini wakati viongozi wengine wamekuja na kupita katika miaka kadhaa ya hapa kati, Merkel amevumilia, akifurahia umaarufu usio na kifani. "Das Mädchen" akapewa jina la utani "die Mutti," MAMA na ishara ya utulivu (symbol of stability).

Mwanasayansi ya siasa Joyce Mushaben, anasema Merkel alionekana kama kiongozi "wa muda tu" wakati alipopanda kwa mara ya kwanza katika chama cha Christian Democratic Union (CDU).

Wapinzani wake wengi wa kiume walikuwa wamejaa kashfa, kukawa na hisia kwamba "angekuwa anashikilia mahali hapo hadi watakapopata mtu halisi wa CDU kuchukua nafasi yake," Mushaben anasema. "Walidharau kabisa uwezo wake wa kujifunza."

Merkel aliishia kuongoza chama kwa miaka 18, akiachia madaraka mwishoni mwa 2018. Hivi karibuni ikawa wazi kuwa ni jinsi gani itakuwa ngumu kuchukua nafasi yake. Mrithi mteule wa Merkel, Annegret Kramp-Karrenbauer alidumu kwa zaidi ya mwaka mmoja, akihangaika kuweka sawa makundi ya majimbo ndani ya chama.

Mwishoni mwa juma hili, chama kilimchagua Armin Laschet kama mrithi wake. Laschet, mshirika wa muda mrefu wa Merkel anayefanya kazi kama Waziri-rais wa jimbo la Shirikisho la Kaskazini-Rhine Westphalia, alishinda kwa 52.79% (kura 521), akimshinda Friedrich Merz, wakili wa makampuni, ambaye alipata 47.21% (kura 466).

Laschet ataongoza chama hicho katika uchaguzi wa shirikisho utakao fanyika mwezi Septemba mwaka huu. Uchaguzi wake (ndani ya chama) uliashiria kuwa ni kura ya wazi inayounga mkono kuendeleza siasa za wastani za Merkel.

Mushaben, mwandishi wa biografia wa Merkel na profesa wa siasa za kulinganisha (comparative politics) na masomo ya kijinsia katika chuo Kikuu cha Missouri-St. Louis, anasema ufunguo wa mafanikio ya Merkel ulikuwa kwenye mchanganyiko wa kipekee wa asili yake na uwezo wake.

Uzoefu wake wa kukua kama binti wa mchungaji katika Ujerumani Mashariki ya Kikomunisti umeathiri sana uamuzi wake wa kisiasa, na kama mwanasayansi wa zamani mwenye udaktari katika kemia ya quantum (PhD in quantum chemistry), mara nyingi hupambana na matatizo kwa njia ile ile kama alivokuwa akipambana na hesabu tata (complex calculations), anasema Mushaben.

Wakati mshauri wake wa kisiasa Helmut Kohl alipoingiliwa na kashfa ya ufisadi mnamo 1999, alimlaani hadharani na kumwomba aondoke, licha ya kuwa alikuwa mwanafunzi wake (protégé) kwa muda mrefu.

201209095710-01-germany-coronavirus-1209-merkel-large-169.jpg


"Watu walimwona kama mtu mwenye uadilifu, mtu ambaye hakuchukua tu kipaza sauti na kuanza kuropoka mdomoni mwake, lakini mtu ambaye alisubiri hadi awe na kitu cha kusema," Mushaben anaongeza.

Pamoja na kuwa mwanamke wa kwanza kuwa kansela, Merkel pia alikuwa mwanasiasa wa kwanza kutoka Ujerumani Mashariki ya zamani kuchukua wadhifa huo kufuatia kuanguka kwa Ukuta wa Berlin.

Merkel alirejea kumbukumbu hii ya asili yake hivi karibuni, wakati akishinikiza vizuizi zaidi kwenye janga virusi vya corona, akikubali kuwa yeye ni mtu anayeona kwamba uhuru wa kusafiri ni kama haki iliyoshindwa kwa bidii, hakuwa na raha juu ya sheria mpya, lakini alielezea ni kwanini zinahitajika.

Corinna Hoerst, mwandamizi mwenzake na naibu mkurugenzi katika Mfuko wa Marshall wa Ujerumani huko Brussels, anasema Merkel amekuwa aina mpya ya kiongozi.

"Anaonyesha uelewa, utulivu na uaminifu," Hoerst anasema. "Hiyo ni ya kipekee na imetafsiri upya, kwa kiwango flani, kile kitu watu wanatafuta kutoka kwa kiongozi, kwa sababu ni kinyume kabisa na aina yoyote ya ubaguzi wa kiume ambao tulikuwa nao."......inaendelea

1623408291164.png


1623408306412.png
 
210106115849-20210106-merkel-page-top-illo-large-169.jpg


MDHIBITI WA MAJANGA DUNIANI

Hata wakosoaji wake wakubwa wanakubali kwamba Merkel ana uwezo wa kipekee linapokuja suala la kushughulikia migogoro na majanga, baada ya kuivusha Ujerumani katika janga la kifedha la ulimwengu (2008/9), janga la deni la Eurozone, na janga la uhamiaji; ikiwa imesalia miezi kadhaa kabla hajaondoka madarakani, bado yuko mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya janga la virusi vya corona.

Yeye mara nyingi alijifanya kuwa mtu mwenye mwenye sauti ya sababu, na kama mtengenezaji wa mikataba. Wanasayansi wa siasa (political scienctists) wanamuelezea kuwa ni mtu "mtulivu," "mwenye busara," na "mwanadiplomasia." Wengine wanaweza hata kuongeza "kuchosha" ("booring") kwenye mchanganyiko huo.

"Hakuna kitu cha kupendeza (glamour) juu yake," anasema Gabriele Abels, profesa wa siasa za kulinganisha (competitive politics) katika chuo kikuu cha Tübingen, Ujerumani. "Yeye ni ... jambo la kweli, mwenye busara sana na watu hawawezi kumfikiria kama fisadi."

Abels anasema Merkel anajumuisha kile kitu wajerumani wengi wanatafuta kutoka kwa kiongozi: "Wakati sisi katika nyakati mbalimbali tunaangalia nchi zingine ambazo zina viongozi wengi wenye haiba (charisma), hatuitaki hii kwetu, tumekuwa nayo ya kutosha katika historia yetu (mf. Hitler)."

181105153008-angela-merkel-life-29-large-169.jpg


Hoerst anasema nguvu haswa ya Merkel katika miaka ya hivi karibuni imekuwa katika kujenga makubaliano na kuongoza kutoka katikati (leading from the middle).

"Ni jambo la kuchekesha kuwa wanawake wanaonekana kama, unajua, 'Ah, ana hisia nyingi (too emotional),' lakini kwa kweli, wanaume ndio ambao wameonekana kuwa na hisia kali, iwe ni Boris Johnson au Rais Trump, wakati Kansela Merkel amekuwa mwanadiplomasia na aliyeamua sio tu kusonga mbele lakini kumleta kila mtu karibu na wazo husika, "anasema.

Uamuzi wa Merkel kutafuta makubaliano umelipa wakati wa mizozo mikubwa zaidi katika muongo mmoja uliopita. Aliweza kufanya makubaliano (broker a deal) kati ya Eurozone na Ugiriki, na akawashawishi Urusi na maafisa wakuu wa Ukraine wazungumze.

Kama mwanasayansi wa zamani na waziri wa mazingira, pia aliweka swala la hali ya hewa katikati tangu mwanzo wa uongozi wake. Aliongoza Mkutano wa kwanza kabisa wa hali ya hewa wa UN huko Berlin na kuwashawishi viongozi wengine wa G8 kukubali hitaji la kupunguza uzalishaji wa gesi chafu (green house gas emittions). "Alimfanya hata George Bush akubali kuwa kulikuwa na shida ya mabadiliko ya hali ya hewa; alikuwa mpatanishi mzuri," Mushaben anasema.

Lakini kuongoza kwa makubaliano hakufanyi kazi kila wakati. Mwishoni mwa mwaka jana, alipambana sana kuwashawishi viongozi wa majimbo ya shirikisho la Ujerumani kutekeleza vizuizi vikali vya coronavirus nchi nzima wakati viwango vya maambukizo vilipoanza kuongezeka. Na kama Rais anayejirudiarudia (rotating president) wa Baraza la Jumuiya ya Ulaya katika miezi sita iliyopita, amejitahidi kupata makubaliano na Hungary na Poland juu ya kufuata kwao sheria ya Jumuiya ya Ulaya.

"Tunaweza kulisimamia hili"

Kulikuwa pia na nyakati ambazo Merkel hakuenda kutafuta maelewano, haswa mnamo 2015 wakati alipowakaribisha wakimbizi waliokimbia mizozo huko Syria na kwingineko.

"Watu wanaoteswa kisiasa wana haki ya kupata hifadhi. Tunaweza kujivunia ubinadamu wa Sheria yetu ya Msingi (katiba) ... pia tunatoa ulinzi kwa wale wote wanaotukimbilia kutoka kwenye vita," aliwaambia watu wa Ujerumani msimu huo wa joto.

"Ninaiweka kwa urahisi: Ujerumani ni nchi yenye nguvu. Nia ambayo tunafanya mambo haya lazima iwe: Tumefanikiwa sana - tunaweza kuyafanya!," Merkel alisema.

"Kwangu huo ndio wakati wake wa kukumbukwa zaidi, kipindi hicho cha wiki tatu mnamo 2015 ambapo alifanya uamuzi wa kupingana na watu wote katika baraza lake la mawaziri na mkuu wa jeshi la polisi la shirikisho na walinzi wa mipaka, wote walisema usifanye hivyo, yeye akasema, "Ikiwa tunaweza kuokoa mabenki, tunaweza pia kuokoa wanadamu," Mushaben anasema.

Hoerst anakubali kwamba uamuzi huo utakuwa sehemu kubwa ya urithi (legacy) wa Merkel.

190719131042-01-angela-merkel-0719-large-169.jpg


"Ilikuwa jambo la kibinadamu kufanya na ilikuwa jambo la haki kufanya," anasema. "Aliwawezesha raia wa Ujerumani ambao walihisi kuelewa hali (empathy) za wakimbizi lakini labda hawakufanya bidii yoyote, na aliwapa utambulisho na msaada ili wajipange ndani ya jamii na kufungua nyumba zao."

Wengi walikosoa hatua hiyo, haswa baada ya watu wanaokadiriwa kuwa milioni 1.2 kuwasili Ujerumani ndani ya mwaka mmoja na nusu uliofuata.

Utitiri huo mkubwa mwanzoni ulisababisha matatizo kadhaa, na kuviongezea nguvu vyama vya mrengo wa kulia vinavyopambana na wahamiaji kama kile cha Alternative für Deutschland (AfD). Lakini maoni hayo yanaonekana kuwa ya muda mfupi - AfD tangu wakati huo kimekuwa kikififia katika uchaguzi, na sera ya kuwakaribisha wakimbizi na wahamiaji inaanza kulipa kiuchumi.

Kama nchi nyingine nyingi za Ulaya, Ujerumani inakabiliwa na bomu la idadi ya watu (demographic time bomb), ikiwa na wastaafu wengi na wafanyikazi wachache.

Kulingana na Taasisi ya Ujerumani ya Soko la Ajira na Utafiti wa Kazini, 49% ya wakimbizi wenye umri wa kufanya kazi ambao wamewasili nchini tangu 2013 waliajiriwa mnamo Februari mwaka jana. Zaidi ya nusu yao walikuwa katika kazi zinazohitaji ujuzi (skilled works) na zaidi ya theluthi mbili walikuwa na kazi kamilfu (full time job).

Wengine 17% walikuwa katika mipango ya mafunzo ya kulipwa (paid training programs) na 3% walikuwa katika mafunzo ya kulipwa (internships). Kulingana na utafiti, wengi wa waliosalia walikuwa wanasoma, wakitafuta kazi kikamilifu au kwenye likizo ya uzazi (maternity) au ya wazazi (parental leave). Karibu 85% wamechukua kozi za lugha ya Kijerumani

1623414983368.png
 
Mwisho...

200921123236-trump-merkel-g7-file-large-169.jpg


Nini kinafuata?

Merkel amekataa mara kadhaa wazo la kugombea kwa muhula wa tano na wafafanuzi wengi wanaamini atashikilia ahadi hiyo.

"Hata uamuzi wake wa kuwania muhula wa nne ulisita sana, lakini alimuona Putin akifanya vibaya (behaving badly) na aliona uchaguzi wa Trump ndipo akasema," Sawa, mimi ndiye mtu mzima pekee aliyebaki kwenye ngazi hii, "Mushaben anasema .

Wakati huu, Merkel anaonekana ameamua kurudi nyuma.

"Sidhani kama atachukua nafasi nyingine yoyote, nadhani atastaafu na kufurahia kufanya mambo ambayo ameshindwa kuyafanya katika miaka 20, 30 iliyopita," Abels anasema.

Kulingana na Mushaben, Kansela anayemaliza muda wake hapo awali alisema kuwa anatarajia kutumia wakati mwingi kupika keki za matunda na supu yake maarufu ya viazi, akiashiria kuwa hapangi kufaya ziara kubwa za kuzungumza (speakings tour) au kuchukua nafasi nyingine (other positions).

Lakini hata kama atastaafu kabisa, ataendelea kuushawishi (influence) ulimwengu kwa muda mrefu ujao.

"Katika siku za usoni, itakuwa ngumu sana kusema kwamba mwanamke hawezi kuwa kiongozi mwenye mafanikio, na huo ni ujumbe muhimu sana," Abels anasema.

=========
 
Mashirika ya Ujasusi Ujerumani.

Likiwa ni taifa la 4 kwa uchumi mkubwa duniani, Ujerumani imejipanga vyema sana katika swala zima la ujasusi.

Kuna mashirika makuu mawili ya Ujasusi nchini ujerumani, BND na BfD. BND linahusika na ujasusi wa nje ya nchi wakati BfD likihusika na ujasusi wa ndani ya nchi.
Shirika la Bfd linashirikiana kwa ukaribu sana na shirika dogo la ujasusi ka LfV linalofanya ujasusi wa ndani ya jimbo, Ujerumani ikiwa ni nchi yenye majimbo 16 ndani yake.


1.) BfV - Ofisi ya Shirikisho ya Ulinzi wa Katiba [ Federal Office for the Protection of the Constitution]

220px-Emblem_of_the_BfV.png


(Kwa kijerumani: Bundesamt für Verfassungsschutz au BfV)
Ni shirika la ujasusi la mambo ya ndani ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani.
Likifanya kazi pamoja na Landesämter für Verfassungsschutz (LfV) {shirika la ujasusi katika ngazi ya majimbo}, ofisi hiyo imepewa jukumu la kukusanya ujasusi juu ya vitisho kuhusu utaratibu wa kidemokrasia, uwepo na usalama wa shirikisho au moja ya majimbo yake, na kuishi kwa amani kwa watu; kwa kukabiliana na Ujasusi (counter-intelligence); na usalama wa kinga (protective security/ "mabodigad") na kukabiliana na hujuma (counter-sabotage).
BfV inaripoti kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Shirikisho.
Kiongozi mkuu ni rais wa shirika, rais wa sasa wa BfV ni Thomas Haldenwang aliyeteuliwa mwaka 2018.

Maswala makuu BfV wanayohusika nayo ni:-

*Wanasiasa wenye siasa kali za mrengo wa kushoto, majukwaa yao, harakati zao na vyama vyao, haswa vikundi kadhaa ndani ya Die Linke, pamoja na vyama vingine vidogo na vikundi vinavyohubiri ukomunisti.

*Wanasiasa wenye siasa kali za mrengo wa kulia (haswa Wanazi-mamboleo, pamoja na chama cha kisiasa cha NPD, vikundi ndani ya Alternative für Deutschland ~chama cha AfD, na vikundi vidogo vinavyohubiri unazi, ufashisti, ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni).

*Mashirika yenye msimamo mkali ya wageni wanaoishi Ujerumani (magaidi wa kiislamu wakiwa ndio maarufu zaidi).

*Mashirika tata ya dini (Cults ~kwa kijerumani 'Sekten') kama vile Scientology (linalotambuliwa na serikali ya Ujerumani kama shirika la kibiashara la kimabavu, linalopinga demokrasia badala ya kufanya kazi Kama dini).

*Uhalifu wa kupanga (Organized Crime) pia unatajwa kama tishio kwa demokrasia, sheria na utulivu, na biashara huru katika mfumo wa uchumi wa biashara wa nchi hiyo. Hata hivyo, uhalifu wa kupanga ni kwa kiwango kidogo tu, kama utashughulikiwa na BfV, kwani unaangukia katika majukumu ya kawaida ya polisi wa kawaida, haswa BKA


2.) BND - Shirika la Shirikisho la Huduma ya Ujasusi [ Federal Intelligence Service ]

330px-BND_Logo.svg.png


Huduma ya Ujasusi ya Shirikisho ~Kwa kijerumani: Bundesnachrichtendienst;
BND ni shirika la ujasusi wa kigeni la Ujerumani, lipo chini ya Ofisi ya Kansela. Makao makuu ya BND ipo katikati ya jiji la Berlin na ndio makao makuu makubwa zaidi kwa eneo kuliko makao makuu yote ya ujasusi duniani.

220px-Zentrale_des_Bundesnachrichtendienst,_Berlin.jpg


BND ina ofisi 300 nchini Ujerumani na nchi za nje. Mnamo 2016, iliajiri watu karibu 6,500; 10% kati yao ni wanajeshi ambao wameajiriwa rasmi na Ofisi ya Sayansi za Kijeshi. BND ndio shirika kubwa la Jumuiya (mashirika yote) ya Ujasusi ya Ujerumani.

*BND ilianzishwa wakati wa Vita Baridi mnamo 1956 kama shirika rasmi la ujasusi wa kigeni la Ujerumani Magharibi, ambalo lilijiunga na NATO , kwa ushirikiano wa karibu na CIA.
Lilikuwa mrithi wa Shirika la mapema la Gehlen, ambalo mara nyingi lilikuwa likijulikana tu kama "Shirika" au "The Org", shirika la ujasusi la Ujerumani Magharibi lililoshirikiana na CIA ambalo uwepo wake haukutambulika rasmi.
Mtu mkubwa kabisa katika historia ya BND alikuwa Reinhard Gehlen, kiongozi wa Shirika la Gehlen na baadaye rais wa kwanza na mwanzilishi wa BND, ambaye alifahamika kama "mmoja wa majasusi mashuhuri zaidi wa Vita vya Cold."
Tokea kipindi cha mwanzo chaa Vita Baridi Shirika la Gehlen na baadaye BND lilikuwa na ushirikiano wa karibu na CIA, na mara nyingi ndio lilikuwa macho na masikio ya jamii nzima (mashirika yote) ya ujasusi wa nchi za kimagharibi katika ardhi ya kambi ya mashariki ( Eastern Block).
BND pia inachukuliwa kama moja wapo ya mashirika yenye taarifa nyeti kabisa za kijasusi zinazohusu Mashariki ya Kati kutoka miaka ya 1960. BND ilianzishwa haraka kama shirika la pili la ujasusi la magharibi mwa ulimwengu, la kwanza likiwa CIA.
Urusi na Mashariki ya Kati kwa ujumla ndio wamebaki kuwa walengwa wakuu muhimu wa shughuli za BND, pamoja na kufuatilia vikundi vya waasi duniani.

*Siku hizi shirika la BND linafanya kazi kama mfumo wa kutoa onyo mapema ili kuitahadharisha serikali ya Ujerumani juu ya vitisho kutoka nje kwa masilahi ya Ujerumani.
Linategemea sana utafuatiliaji wa mawasiliano ya simu (wiretapping) na ufuatiliaji wa kielektroniki (electronic surveillance) wa mawasiliano ya kimataifa (international communications).
Linakusanya na kutathmini habari juu ya maswala mbalimbali kama vile ugaidi wa kimataifa ambao sio wa jimbo (non-state terrorism), silaha za kuangamiza umati (weapons of mass destruction) na uhamishaji haramu wa teknolojia (illegal transfer of technology), uhalifu wa kupanga (organized crime), silaha na biashara ya dawa za kulevya, utakatishaji fedha (money laundering), uhamiaji haramu (illegal migration) na vita vya habari (information warfare).
Kama shirika la ujasusi wa nje ya Ujerumani, BND inakusanya taarifa za kijasusi za kijeshi na za raia. Japo Kamandi ya Kimkakati ya Upelelezi (KSA) ya Bundeswehr (Jeshi la Ujerumani) inafanya kazi hii pia, sio shirika la ujasusi. Ila kuna ushirikiano wa karibu kati ya BND na KSA.

*Washirika wa ndani ya nchi wa maswala ya ujasusi kwa BND ni Ofisi ya Shirikisho ya Ulinzi wa Katiba (Bundesamt für Verfassungsschutz, ama BfV) na washirika 16 katika ngazi za majimbo ~ Ofisi za Majimbo za Ulinzi wa Katiba (Landesämter für Verfassungsschutz au LfV),
pia kuna shirika tofauti la ujasusi wa kijeshi, shirika la Kupambana na Ujasusi wa Kijeshi (Militärischer Abschirmdienst, MAD).



3.) LfV - Ofisi ya Jimbo ya Ulinzi wa Katiba [State Office for the Protection of the Constitution]

Ofisi ya Jimbo ya Ulinzi wa Katiba (Kijerumani: Landesbehörde für Verfassungsschutz; LfV) ni shirika la ujasusi kwa ngazi ya jimbo nchini Ujerumani.
Hili linafanya kazi sawa na zinazofanywa na BfD lakini katika ngazi Jimbo.

Ujerumani ina majimbo kumi na sita (16).

images.png


Katika majimbo saba ya shirikisho la Ujerumani, LfV inafanya kazi kama shirika huru ndani ya jimbo na inaripoti kwa wizara ya mambo ya ndani ya jimbo. Katika majimbo tisa ya shirikisho yaliyosalia, LfV inaendeshwa kama kitengo tu ndani ya wizara ya mambo ya ndani ya jimbo.

*Majimbo yafuatayo, haswa Magharibi mwa Ujerumani, kila Jimbo lina shirika la LfV (Landesämter für Verfassungsschutz) iliyo huru:-

1. Landesamt für Verfassungsschutz Baden-Württemberg.

images (74).jpeg

images (75).jpeg

images (77).jpeg


2. Bayerisches Landesamt für Verfassungsschutz. Hii ni LfV ya Jimbo la Bavaria (kijerumani~Bayern).

images (78).jpeg

Polizeipraesidium_Oberbayern.JPG

640px-Coat_of_arms_of_Bavaria.svg.png

images (81).jpeg

images (80).jpeg


3. Landesamt für Verfassungsschutz Bremen.

4. Landesamt für Verfassungsschutz der Freien na Hansestadt Hamburg.

5. Landesamt für Verfassungsschutz Hessen.

6. Landesamt für Verfassungsschutz Saarland.

7. Landesamt für Verfassungsschutz Sachsen.


*Na katika majimbo tisa yafuatayo, LfV ni kitengo tu katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya jimbo husika,.:-


1. Verfassungsschutz Berlin.

2. Verfassungsschutz Brandenburg.

3. Verfassungsschutz Mecklenburg-Vorpommern.

4. Verfassungsschutz Niedersachsen.

5. Verfassungsschutz Nordrhein-Westfalen.

6. Verfassungsschutz Rheinland-Pfalz.

7. Verfassungsschutz Sachsen-Anhalt.

8. Verfassungsschutz Schleswig-Holstein.

9. Amt für Verfassungsschutz Thüringen.

==========
 
Hata huijui katiba ya ujerumani

Kwanza Chancellor anachaguliwa na Bunge Kuu la Ujerumani (Bundestag) na wala sio wananchi

Wananchi kazi yao ni kuchagua wabunge tu

Rais mpaka achaguliwe na wabunge apite ni atakua na uwezo mkubwa na ni harder kuliko kutoka kwa wananchi directly.

Chancellor wa Ujeruman anakoma kua Chancellor iwapo tu:

1)Anakufa
2)Ameamua ku-resign
3)Iwapo wabunge hawaridhiki na utendaji wake muda wowote na tarehe yeyote wanapojisikia na kumtoa madarakani dakika hiyo hiyo kwa kupiga kura kwenye box

Hakuna cha term limits wala nini

Merkel mwenyewe hajatawala kiivyo,kuna Helmut Kohl katawala miaka 16

Hii system inaitwa Chancellorship Democracy

Ni ngumu kuliko hii ya kudanganya wananchi kwa tisheti unaiba na kura machakani huko na ni ngumu kukutoa madarakani mpaka miaka 5 iishe

Wakati Chancellorship ni unachaguliwa among the best people waliochaguliwa na wananchi tayari na wapiga kura ni the best people tayari kutoka kwa wananchi na huwezi wadanganya kwa tisheti plus wakiamka asubuhi kama hawakufagilii wakutolea mbali huko uende Chattle mavini huko
Kweli mkuu, mfumo huu ni mzuri sana kwani una uwazi na uwajibikaji makini.
naomba niongeze kidogo katika maelezo yako hapo kwamba Chancellor anakaa madarakani kwa miaka 4 kama ilivyo kwa wabunge wengine, rais wa shirikisho ndio anakaa kwa miaka 5 lakini mwisho wa kugombea ni awamu 2 tu kwa mfululizo wakati Chancellor hana kikomo.
 
Kiongozi wa Ujerumani Angela Merkel amekuwa chancellor wa Ujerumani toka 2005
Jakaya Kikwete kamkuta kamuacha
John Pombe Magufuli kamkuta kamuacha
Samia Suluhu Hassan kamkuta

Huko duniani kafanya kazi na:-
Marais 4 wa Marekani,
Mawaziri Wakuu 2 wa Canada,
Mawaziri Wakuu 3 wa Japan,
Marais 4 wa Ufaransa
Mawaziri 5 wa Uingereza na
Mawaziri 10 wa Italia

NA MWENYEKITI MMOJA WA CHADEMA KAMANDA MBOWE
Kwahiyo ulitaka watie wapi? Mbona CCM mnatoa China mnajifanya marafiki wa Mao? Bullshit
 
Kwahiyo ulitaka watie wapi? Mbona CCM mnatoa China mnajifanya marafiki wa Mao? Bullshit
Nilitaka mtoke povu kama hivi- inapendeza- mdemke tu ila ndo Sabaya kesha mtoa bungeni hivyo
 
Nawaza na kuamini kwamba kushangilia kifo cha mtu yeyote ni laana.
Mfano wale Nyani walioshangilia kifo cha mkulima wa mahindi aliyelima kwa juhudi na kuzuia Nyani wasiibe walimuona ni mbaya lakini alipofariki hakuna aliyelima shamba la mahindi nao hawakupata fursa ya kuiba.

Mwendazake ameondoka naona kama ajenda za kisiasa zitafifia mnaweza mkapewa RUHUSA ya kuandamana,katiba mpya haki ya kutukana lakini msikidhi mahitaji mliyoyakusudia kwasababu MUNGU anafahamu fika nia yenu.
 
Mwaka 1967 CCM iliamua kuiga mfumo wa kisiasa wa Jamhuri ya Watu wa China, tukiwa bado tupo kwenye mfumo wa chama kimoja CCM ikajenga urafiki wa kudumu na CCP, chama cha kikomunisti cha China.
Leo hii China ni taifa la kwanza kwa uchumi mkubwa duniani lakini Tanzania ni taifa lenye hali mbaya sana, tatizo ni nini wakati tumekuwa na mfumo unaofanana wa kuongoza nchi?

WanaCCM karibuni tuyajadili haya
Cc comte, Katali
 
Katiba ya Ujerumani katika muundo wa picha
Imewekwa wazi, dunia nzima inaona. Haihitaji elimu kubwa ili uielewe, Kama ilivyo katiba ya yetu ya kisaniisanii na kiuiziuizi na mafichomaficho.

640px-PoliticalSystemGermany.png


Mwaka 2020, kitengo cha Ujasusi wa Kiuchumi Duniani "Economic Intelligence Unit" kiliiweka Ujerumani katika kiwango cha demokrasia kamili "full democracy"
 
Ikiwa Serikali ya China,ni Udikteta...Basi ni bora tuwe na Serikali mfano wao.
CCM Hawawezi kuwa na mfano huo wa serekali, kamwe!. Wanaiga tembo kunya tu ila mziki wake wanaujua.
China kiongozi wa serekali akipatikana na rushwa ananyongwa! Huku tunapishana nao mitaani wanatutimulia vumbi na kutumwagia maji machafu ya kwenye madimbwi wakiwa ndani ya mavieite yao kwenye full ac.

Mtu Kama Chenge aliefanya madudu ya kutisha eti bado alikuwa mbunge, hapo ndo China wenyewe wanapotushangaa. Wakati Lisu akimuita magufuli dikteta uchwara nadhani ulimuelewa
 
Asante, umejitahidi lakini katika tafsiri yako kuna makosa kidogo. Rais wa Ujerumani hawezi
* "Kumteua na kumtengua Chancellor pamoja na mawaziri" - si azimio lake; rais anampendekeza kiongozi bungeni akiona ana wabunge wa kutosha, baadaye bunga linachagua na rais anapaswa kumteua, pia kumtengua KAMA bunge limeamua dhidi yake.
*Kulivunja bunge ni haki kwa hali maalum pekee kama bunge limeshindwa kumchagua chansela
*kuitisha bunge hapa hana mamlaka
*Kuteua na kufukuza kazi majaji wa shirikisho, wafanyikazi wa serikali, na maafisa walioamriwa na wasioamriwa wa Jeshi Hawezi kufukuza watu. Anatia sahihi kwenye hati za kuteua na kutengua, lakini haamui. Maazimio ni ya watu wengine kufuatana na sheria mbalimbali na katiba.

Mamlaka kuu ya raisi wa Ujerumani ni wakati asilimia 51 za wabunge hazipatikani kumchagua chansela. Hapa ni azimio la rais kama anamkubali chansela mwenye kura nyingi (lakini chini ya nusu ya wabunge) au kama anaamuru uchaguzi mpya wa bunge. haikutokea bado tangu mwanzo wa Jamhuri mwaka 1949.

Mkuu, rejea katiba yao!

640px-PoliticalSystemGermany.png
 
Back
Top Bottom