Mashirika ya Ujasusi Ujerumani.
Likiwa ni taifa la 4 kwa uchumi mkubwa duniani, Ujerumani imejipanga vyema sana katika swala zima la ujasusi.
Kuna mashirika makuu mawili ya Ujasusi nchini ujerumani, BND na BfD. BND linahusika na ujasusi wa nje ya nchi wakati BfD likihusika na ujasusi wa ndani ya nchi.
Shirika la Bfd linashirikiana kwa ukaribu sana na shirika dogo la ujasusi ka LfV linalofanya ujasusi wa ndani ya jimbo, Ujerumani ikiwa ni nchi yenye majimbo 16 ndani yake.
1.) BfV - Ofisi ya Shirikisho ya Ulinzi wa Katiba [ Federal Office for the Protection of the Constitution]
(Kwa kijerumani: Bundesamt für Verfassungsschutz au BfV)
Ni shirika la ujasusi la mambo ya ndani ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani.
Likifanya kazi pamoja na Landesämter für Verfassungsschutz (LfV) {shirika la ujasusi katika ngazi ya majimbo}, ofisi hiyo imepewa jukumu la kukusanya ujasusi juu ya vitisho kuhusu utaratibu wa kidemokrasia, uwepo na usalama wa shirikisho au moja ya majimbo yake, na kuishi kwa amani kwa watu; kwa kukabiliana na Ujasusi (counter-intelligence); na usalama wa kinga (protective security/ "mabodigad") na kukabiliana na hujuma (counter-sabotage).
BfV inaripoti kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Shirikisho.
Kiongozi mkuu ni rais wa shirika, rais wa sasa wa BfV ni Thomas Haldenwang aliyeteuliwa mwaka 2018.
Maswala makuu BfV wanayohusika nayo ni:-
*Wanasiasa wenye siasa kali za mrengo wa kushoto, majukwaa yao, harakati zao na vyama vyao, haswa vikundi kadhaa ndani ya Die Linke, pamoja na vyama vingine vidogo na vikundi vinavyohubiri ukomunisti.
*Wanasiasa wenye siasa kali za mrengo wa kulia (haswa Wanazi-mamboleo, pamoja na chama cha kisiasa cha NPD, vikundi ndani ya Alternative für Deutschland ~chama cha AfD, na vikundi vidogo vinavyohubiri unazi, ufashisti, ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni).
*Mashirika yenye msimamo mkali ya wageni wanaoishi Ujerumani (magaidi wa kiislamu wakiwa ndio maarufu zaidi).
*Mashirika tata ya dini (Cults ~kwa kijerumani 'Sekten') kama vile Scientology (linalotambuliwa na serikali ya Ujerumani kama shirika la kibiashara la kimabavu, linalopinga demokrasia badala ya kufanya kazi Kama dini).
*Uhalifu wa kupanga (Organized Crime) pia unatajwa kama tishio kwa demokrasia, sheria na utulivu, na biashara huru katika mfumo wa uchumi wa biashara wa nchi hiyo. Hata hivyo, uhalifu wa kupanga ni kwa kiwango kidogo tu, kama utashughulikiwa na BfV, kwani unaangukia katika majukumu ya kawaida ya polisi wa kawaida, haswa BKA
2.) BND - Shirika la Shirikisho la Huduma ya Ujasusi [ Federal Intelligence Service ]
Huduma ya Ujasusi ya Shirikisho ~Kwa kijerumani: Bundesnachrichtendienst;
BND ni shirika la ujasusi wa kigeni la Ujerumani, lipo chini ya Ofisi ya Kansela. Makao makuu ya BND ipo katikati ya jiji la Berlin na ndio makao makuu makubwa zaidi kwa eneo kuliko makao makuu yote ya ujasusi duniani.
BND ina ofisi 300 nchini Ujerumani na nchi za nje. Mnamo 2016, iliajiri watu karibu 6,500; 10% kati yao ni wanajeshi ambao wameajiriwa rasmi na Ofisi ya Sayansi za Kijeshi. BND ndio shirika kubwa la Jumuiya (mashirika yote) ya Ujasusi ya Ujerumani.
*BND ilianzishwa wakati wa Vita Baridi mnamo 1956 kama shirika rasmi la ujasusi wa kigeni la Ujerumani Magharibi, ambalo lilijiunga na NATO , kwa ushirikiano wa karibu na CIA.
Lilikuwa mrithi wa Shirika la mapema la Gehlen, ambalo mara nyingi lilikuwa likijulikana tu kama "Shirika" au "The Org", shirika la ujasusi la Ujerumani Magharibi lililoshirikiana na CIA ambalo uwepo wake haukutambulika rasmi.
Mtu mkubwa kabisa katika historia ya BND alikuwa Reinhard Gehlen, kiongozi wa Shirika la Gehlen na baadaye rais wa kwanza na mwanzilishi wa BND, ambaye alifahamika kama "mmoja wa majasusi mashuhuri zaidi wa Vita vya Cold."
Tokea kipindi cha mwanzo chaa Vita Baridi Shirika la Gehlen na baadaye BND lilikuwa na ushirikiano wa karibu na CIA, na mara nyingi ndio lilikuwa macho na masikio ya jamii nzima (mashirika yote) ya ujasusi wa nchi za kimagharibi katika ardhi ya kambi ya mashariki ( Eastern Block).
BND pia inachukuliwa kama moja wapo ya mashirika yenye taarifa nyeti kabisa za kijasusi zinazohusu Mashariki ya Kati kutoka miaka ya 1960. BND ilianzishwa haraka kama shirika la pili la ujasusi la magharibi mwa ulimwengu, la kwanza likiwa CIA.
Urusi na Mashariki ya Kati kwa ujumla ndio wamebaki kuwa walengwa wakuu muhimu wa shughuli za BND, pamoja na kufuatilia vikundi vya waasi duniani.
*Siku hizi shirika la BND linafanya kazi kama mfumo wa kutoa onyo mapema ili kuitahadharisha serikali ya Ujerumani juu ya vitisho kutoka nje kwa masilahi ya Ujerumani.
Linategemea sana utafuatiliaji wa mawasiliano ya simu (wiretapping) na ufuatiliaji wa kielektroniki (electronic surveillance) wa mawasiliano ya kimataifa (international communications).
Linakusanya na kutathmini habari juu ya maswala mbalimbali kama vile ugaidi wa kimataifa ambao sio wa jimbo (non-state terrorism), silaha za kuangamiza umati (weapons of mass destruction) na uhamishaji haramu wa teknolojia (illegal transfer of technology), uhalifu wa kupanga (organized crime), silaha na biashara ya dawa za kulevya, utakatishaji fedha (money laundering), uhamiaji haramu (illegal migration) na vita vya habari (information warfare).
Kama shirika la ujasusi wa nje ya Ujerumani, BND inakusanya taarifa za kijasusi za kijeshi na za raia. Japo Kamandi ya Kimkakati ya Upelelezi (KSA) ya Bundeswehr (Jeshi la Ujerumani) inafanya kazi hii pia, sio shirika la ujasusi. Ila kuna ushirikiano wa karibu kati ya BND na KSA.
*Washirika wa ndani ya nchi wa maswala ya ujasusi kwa BND ni Ofisi ya Shirikisho ya Ulinzi wa Katiba (Bundesamt für Verfassungsschutz, ama BfV) na washirika 16 katika ngazi za majimbo ~ Ofisi za Majimbo za Ulinzi wa Katiba (Landesämter für Verfassungsschutz au LfV),
pia kuna shirika tofauti la ujasusi wa kijeshi, shirika la Kupambana na Ujasusi wa Kijeshi (Militärischer Abschirmdienst, MAD).
3.) LfV - Ofisi ya Jimbo ya Ulinzi wa Katiba [State Office for the Protection of the Constitution]
Ofisi ya Jimbo ya Ulinzi wa Katiba (Kijerumani: Landesbehörde für Verfassungsschutz; LfV) ni shirika la ujasusi kwa ngazi ya jimbo nchini Ujerumani.
Hili linafanya kazi sawa na zinazofanywa na BfD lakini katika ngazi Jimbo.
Ujerumani ina majimbo kumi na sita (16).
Katika majimbo saba ya shirikisho la Ujerumani, LfV inafanya kazi kama shirika huru ndani ya jimbo na inaripoti kwa wizara ya mambo ya ndani ya jimbo. Katika majimbo tisa ya shirikisho yaliyosalia, LfV inaendeshwa kama kitengo tu ndani ya wizara ya mambo ya ndani ya jimbo.
*Majimbo yafuatayo, haswa Magharibi mwa Ujerumani, kila Jimbo lina shirika la LfV (Landesämter für Verfassungsschutz) iliyo huru:-
1. Landesamt für Verfassungsschutz Baden-Württemberg.
2. Bayerisches Landesamt für Verfassungsschutz. Hii ni LfV ya Jimbo la Bavaria (kijerumani~Bayern).
3. Landesamt für Verfassungsschutz Bremen.
4. Landesamt für Verfassungsschutz der Freien na Hansestadt Hamburg.
5. Landesamt für Verfassungsschutz Hessen.
6. Landesamt für Verfassungsschutz Saarland.
7. Landesamt für Verfassungsschutz Sachsen.
*Na katika majimbo tisa yafuatayo, LfV ni kitengo tu katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya jimbo husika,.:-
1. Verfassungsschutz Berlin.
2. Verfassungsschutz Brandenburg.
3. Verfassungsschutz Mecklenburg-Vorpommern.
4. Verfassungsschutz Niedersachsen.
5. Verfassungsschutz Nordrhein-Westfalen.
6. Verfassungsschutz Rheinland-Pfalz.
7. Verfassungsschutz Sachsen-Anhalt.
8. Verfassungsschutz Schleswig-Holstein.
9. Amt für Verfassungsschutz Thüringen.
==========