CHADEMA wanazungumza na waandishi wa habari kutoka makao makuu

CHADEMA wanazungumza na waandishi wa habari kutoka makao makuu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Maandalizi ya kikao maalum cha Kamati Kuu ya CHADEMA yamekamilika katika Edwin Mtei House, Makao Makuu ya Chama, Mikocheni, Dar es Salaam.

Kikao hicho kinafanyika leo, Jumamosi, Agosti 29, 2026, na kitaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche.

"Mzee Warioba kwa umri wake hana kitu anachohitaji—hahitaji ubunge, udiwani wala Urais—lakini anaposimama katikati ya wazee waliokata kauli wakati nchi inaenda shimoni, anakuwa sauti ya Watanzania."

"Kushinikiza serikali ifuate sheria, utaratibu na demokrasia ndio wajibu wa wananchi kwa mujibu wa Ibara ya 8 ya Katiba. Wananchi ndio msingi wa mamlaka na madaraka yote."

"Wasituletee mambo ya CCM ya kuchinjana usiku kama kuku kisha asubuhi mtu ameondolewa kichwa. Sisi ni chama cha demokrasia na wajibu wetu demokrasia isipofuatwa ni kushinikiza."

"Kuna watu wanafanya biashara ya udarali wa siasa na kutumia fedha kuvuruga Baraza Kuu; fedha hizo zitaishia kuliwa tu maana CHADEMA inalindwa na wananchi na ndio tumaini pekee la nchi."

"Historia inatuambia kuwa mambo ya kuua, kuteka na kuwinda wanaosema ukweli yatashindwa tu. Huwezi kumlaumu mtu anayeteswa wala kumlaumu Tundu Lissu anayefunguliwa kesi ya uongo."

 
HQgT1r8WEAAQizI.jpg
 
Zamani ITV walikuwa wanarudha live lakini siku hizi hakuna hata chombo kimoja kinarusha habari za watu wanaopendwa na watanzania.
 
Back
Top Bottom