Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 40,476
- 26,173
Ndugu zangu watanzania,
Wiki iliyopita niliumia sana kuona mkutano wa CHADEMA kule kanda ya ziwa ukigeuka jukwaa la kuwatukana, kuwadhalilisha,kuwatweza na kuwavunjia heshima askari wetu ambao kila mmoja wetu anatambua kazi kubwa wanayoifanya usiku na mchana kuwalinda watanzania na mali zao.
Jambo hili lilifanywa na Sugu ambaye alitumia lugha chafu na matusi kwa askari wetu . Ikumbukwe ya kuwa kazi ya askari wetu mikutanoni ni kuangalia na kuimarisha usalama ,ulinzi na utulivu mikutanoni. Hao hao CHADEMA ikitokea wamevamiwa ,kufanyiwa fujo watakuwa ni wa kwanza kuanza kulalamika kukosa ulinzi ama watakuwa wa kwanza kupiga kelele kuomba msaada wa polisi hao hao ambao wanawatukana matusi na kuwadhalilisha.
Polisi licha ya kula kiapo cha uvumilivu na kudhibiti hisia zao katika utekelezaji wa majukumu yao lakini ni lazima ikumbukwe ya kuwa nao ni Binadamu wanaohitaji kuheshimiwa na siyo kuvunjiwa heshima na kudhalilishwa. Wana moyo wa nyama kama tulivyo wengine ,wana damu na hisia kama tulivyo sote. Tusije kushangaa askari akashindwa kuvumilia matusi na udhalilishaji na kuamua kufyatua risasi za moto kwa muhusika .tusije anza kulaumiana na kupiga makelele na mayowe wakati leo hii tunaona sawa na kukaa kimya.
Kazi ya chama cha siasa jukwaani ni kujenga na kutetea hoja ,kueneza sera na itikadi zake ,misimamo yake ,mitizamo yake , Muelekeo wake ,Dira yake na imani yake . ni juu ya falsafa yake katika mambo mbalimbali. Jukwaani siyo mahali na sehemu ya kutukana askari wetu,siyo sehemu ya kuwavunja moyo askari wetu. Ni sehemu ya kuwatia moyo ,kuwapa nguvu ,kuwapongeza na kuwapatia matumaini juu ya kutambua mchango na kazi yao njema ya kutetea Taifa letu.
Ikumbukwe ya kuwa askari hawa wamekula kiapo cha kulinda ,kutetea na kupigania Taifa letu hata ikibidi kupoteza Maisha na kumwaga Damu zao kwa ajili yetu watanzania. Ndio Maana hadi leo kuna askari wetu wengi sana wamefia kazini wakipigana na kupambana usiku na majambazi kwa ajili ya kutulinda watanzania. Kuna askari wamebakia na ulemavu wa kudumu kwasababu ya kutekeleza majukumu yao ya kulinda usalama wa Taifa letu.
Siyo sawa hata kidogo kuwatukana na kuwadhalilisha watu hawa ambao wamesaini viapo vya vifo vyao kupigania na kutetea Taifa letu. CHADEMA wasivyo na akili wanafikiri wanaweza kuungwa mkono na askari hawa ambao kutwa nzima wanawatukana na kuwadhalilisha,.Ikumbukwe ya kuwa askari hawa wana ndugu ,familia na jamaa zao ambao wanaumizwa kuona ndugu zao wakitukanwa na kudhalilisha ndugu zao.
Ni muda na wakati muafaka wa Mkuu wa Jeshi la polisi Nchini kutoa onyo kali sana kwa CHADEMA pamoja na kuwakemea kuacha mara moja kuwatukana na kuwadhalilisha Askari wetu katika majukwaa yao ya kisiasa.
IGP asimame imara na kusema sasa basi na kwa yeyote atakaye fanya na kutenda jambo hilo atakutana na Mkono Wa sheria. Ni lazma awajibishwe yeye kama yeye haraka sana mara baada ya kushuka tu jukwaani .apewe funzo na kushikishwa adabu .
Kama mtu hana hoja au kalewa mipombe yake au kavuta mibangi yake haina sababu ya kulazimisha kupanda jukwaani kuanza kutukana askari wetu.hiyo haikubaliki na haitakubalika wala kuvumiliwa. Askari wetu ni lazima waheshimiwe.
Polisi acheni unyonge. Simameni kujitetea wenyewe na kukataa udhalilishaji na utwezaji wa utu wenu ,kataeni kuvunjwa moyo ilihali mmejtoa muhanga na sadaka kwa ajili ya watanzania.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.